Biblia ni Maandiko Matakatifu ya Mungu yaliyoandikwa, yaliyotolewa kwa kuvuviwa wanadamu aliowachagua Mungu ambao walinena na kuandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.
Katika Neno hilo, Mungu amewapatia wanadamu ujuzi muhimu kwa wokovu.
02. Utatu Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, umoja wa Nafsi tatu za milele. Mungu mwenye uwezo wote, aliye juu ya yote, na aliyepo daima. Yu astahili
kuabudiwa, kusujudiwa na kutumikiwa na viumbe vyote milele zote.
03. Mungu Baba
Mungu Baba wa milele ni Mwumbaji, Chimbuko, Mtegemezaji, na Mfalme wa viumbe vyote. Ni mwenye haki na mtakatifu, mwingi wa huruma, mwenye fadhili,
si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na upendo na kweli.
04. Mungu Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanyika mwili katika Yesu Kristo. Katika Yeye vitu vyote viliumbwa,
tabia ya Mungu imefunuliwa katika Yeye, wokovu wa jamii yote ya mwanadamu unakamilishwa na ulimwengu unahukumiwa.
Aliteswa na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, alifufuka na akapaa.
Atakuja tena kwa utukufu mwingi kwa ukombozi wa watu wake.
05. Mungu Roho Mtakatifu
Mungu Roho Mtakatifu wa milele alikuwa mtendani pamoja na Baba na Mwana katika Uumbaji, katika Yesu kufanyika mwili na katika ukombozi.
Aliwavuvia waandishi wa Maandiko Matakatifu. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu; na wale wanaoitikia
huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu.
06. Uumbaji
Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote, na amefunua katika Maandiko Matakatifu uhalisi wa tukio la utendaji wake wa uumbaji.
Katika siku sita Bwana alifanya “mbingu nan chi” na vitu vyote vilivyo hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Mwanamume na mwanamke wa kwanza waliumbwa kwa mfano wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kuumbwa, ulikuwa “(mw)ema ukitangaza utukufu wa Mungu.
07. Mwanadamu na Asili Yake
Mwanamume na mwanamke waliumbwa wakiwa na sura ya Mungu binafsi wakiwa na uwezo na uhuru wa kufikiri na kutenda. Wakati wazazi wetu walipomkaidi Mungu,
sura ya mwumbaji iliharibiwa na wakawa watu wa kufa. Uzao wao hushiriki hali hii ya mwanadamu aliyeanguka na matokeo yake yote. Lakini Mungu katika Kristo, aliupatanisha ulimwengu kwa nafsi yake na kwa roho yake akarejeza
kwa watu wenye hali ya kufa taswira ya Mwumbaji.
08. Pambano Kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa imo katika pambano kuu baina ya Kristo na Shetani kuhusu tabia ya Mungu, Sheria yake na Utawala wake juu ya ulimwengu wote.
Mapigano haya yalianzia mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua , kwa kujiinua akawa Shetani, mpinzani wa Mungu na akaongoza sehemu
ya malaika katika maasi. Katika pambano hili, Kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuwaongoza kuwalinda na kuwategemeza katika njia ya wokovu
09. Maisha, Kifo na Ufufuo wa Kristo
Katika maisha ya Kristo ya utii kamili kwa mapenzi ya Mungu, mateso yake, kifo chake na ufufuo, Mungu aliandaa tayari
njia pekee ya upatanisho kwa dhambi ya mwanadamu, ili kwamba wale ambao kwa imani watapokea upatanisho huu wapate uzima wa milele,
na ulimwengu wote uweze kuelewa vema upendo mtakatifu usio na kikomo wa Muumbaji. Kafara hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya Mungu na neema ya tabia yake;
kwa sababu hufanya vyote kuhukumu dhambi yetu na kutoa njia ya msamaha wetu. Kifo cha Kristo ni badala na hufidia, kikipatanisha na kubadilisha. Ufufuo wa Kristo
hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya majeshi ya uovu, na kwa wale wanaipokea kafara hiyo
huhakikishiwa ushindi hatimaye dhidi ya dhambi na mauti. Inatangaza ukuu wa Yesu Kristo ambaye mbele zake kila goti mbinguni na duniani litapigwa
10. Uzoefu wa Wokovu
Kwa upendo usio na kifani na rehema, Mungu alimfanya Kristo asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu,
kusudi katika Yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu, tunatambua hitaji letu, na kukiri hali yetu ya dhambi,
tunatubia uasi wetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo, kuwa mbadala na Kielelezo chetu. Imani hii inayopokea
wokovu huja kupitia uwezo wa kimbingu kwa Neno nan i karama ya neema ya Mungu. Kupitia Kristo tunahesabiwa haki, kufanywa wana na binti wa Mungu,
na kuokolewa kutoka katika mamlaka ya dhambi. Kupitia Roho Mtakatifu tunazaliwa upya na kutakaswa; Roho hufanya upya nia zetu,
huandika sheria ya Mungu ndani ya mioyo yetu, na tunapewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu.
Tukikaa ndani Yake tunakuwa washirika wa hali ya asili ya uungu na kuwa na hakika ya wokovu sasa na katika siku ya hukumu.
11. Kukua Katika Kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo wachafu wakati wa huduma yake hapa
duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi
dhidi ya nguvu za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, fyraha, na uhakika wa upendo wake.
Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu. Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu
tunawekwa huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya nguvu za uovu, ujinga,
na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika
kufanana na tabia yake, tukiongea naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa
ajili ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo wale wanaotuzunguka na
kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho.
12. Kanisa
Kanisa ni jumuiya ya waumini waliokubali kumkiri Yesu kama mwokozi na Bwana wao. Kwa kuunganika na watu wa Mungu katika
Agano la Kale, tumeitwa kutoka ulimwenguni na tunaungana pamoja kwa ibada, ushirika, kufundisha Neno, kusherehekea Meza
ya Bwana, katika utumishi kwa wanadamu na katika kutangaza injili duniani kote. Kanisa ni familia ya Mungu iliyotengenezwa kwa agano. Kanisa ni mwili wa Kristo, jumuia ya imani ambayo Kristo mwenyewe ndiye Kichwa (Kiongozi).
13. Masalio na Utume Wake
Kanisa la ulimwenguni linajumuisha wale wote ambao kwa kweli wanaoamini katika Kristo lakini katika siku za mwisho
wakati wa kuenea kwa uasi, watu wa masalio wameitwa watoke wazitunze amri za Mungu na imani ya Yesu. Hawa masalio
wanatangaza saa ya kuja kwa hukumu, wakihubiri wokovu katika Kristo, na kupiga mbiu ya kukaribia kuja kwake mara ya pili.
Tangazo hilo linawakilishwa na mfano wa malaika watatu wa Ufunuo 14; linaambatana na kazi ya toba na
matengenezo duniani. Kila muumini anatakiwa binafsi kuwa na sehemu katika ushuhuda huu wa ulimwenguni mwote.
14. Umoja Katika Mwili wa Kristo
Kanisa ni mwili moja wenye viungo vingi, vilivyoitwa kutoka katika kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Katika Kristo tu uumbaji mpya;
tofauti za rangi, utamaduni, elimu na utaifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu na ya chini, tajiri na maskini,
mwanamume na mwanamke miongoni mwetu visitugawanye. Sisi sote ni sawa katika Kristo, ambaye kwa Roho mmoja,
ametungamanisha katika ushirika mmoja pamoja Naye na sisi kwa sisi; yatupasa tutumike na kutumikiwa bila upendeleo au usetiri.
15. Ubatizo
Kwa ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, na kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa uzima.
Hivyo tunamtambua Kristo kama Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tupokelewa kama washiriki na kanisa lake.
Ubatizo ni mfano wa muungano wetu na Kristo msamaha wa dhambi zetu, na kumpokea kwetu Roho Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa majini na
unategemea uthibitisho wa imani katika Yesu na ushuhuda wa toba ya dhambi.
Unafuata mafundisho katika Maandiko Matakatifu na ukubali wa mafundisho yake
16. Meza ya Bwana
Meza ya Bwana ni kushiriki katika mfano wa mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa imani katika Yeye, Bwana na Mwokozi wetu.
Katika uzoefu huu wa ushirika, Kristo anakuwepo kukutana na kuwaimarisha watu wake. Tunapotwaa (mkate na divai) kwa furaha
tunatangaza mauti ya Bwana hata arudipo tena. Maandalizi ya Meza ya Bwana hujumuisha kujihoji nafsi, toba na ungamo.
Bwana aliagiza huduma ya kutawadhana miguu ili kukumbusha utakaso mpya, kuonyesha nia ya kutumikiana sisi kwa sisi katika unyenyekevu unaofanana na wa Kristo,
na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya Meza ya Bwana ni ruhusa kwa waumini wote Wakristo.
17. Karama za Roho na Huduma
Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya
upendo kwa ajili ya ustawi wa wote kanisani na wa wanadamu.
Wakati washiriki wanapozitumia karama hizi za Roho kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi
ya mivuto ya uharibifu wa mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuzi utokao kwa Mungu, na kujengwa imara katika imani na upendo.
18. Karama ya Unabii
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii. Karama hii ni alama inayolitambulisha Kanisa la Masalio na ilidhihirika katika huduma
ya Ellen G. White. Kama mjumbe wa Bwana, maandishi yake yanaendelea kuwa chanzo madhubuti cha ukweli yanayotoa kwa kanisa:
faraja, uongozi, mafundisho, na maonyo. Pia yanaweka wazi kwamba Biblia ndiyo kanuni ambayo kwayo mafundisho yote na uzoefu lazima vipimwe.
19. Sheria ya Mungu
Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimeunganishwa katika Amri Kumi na zilifuatishwa katika maisha ya Kristo. Hizi zinadhihirisha
upendo wa Mungu, makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu, na mahusiano. Amri hizi ni sharti kwa watu wote katika kila kizazi. Humsaidia mwanadamu kujipima utii wake kwa Mungu. Ni udhihirisho wa uwezo wa Kikristo katika kubadilisha maisha, na hivyo kuimarisha ushuhuda wa Kikristo.
20. Sabato
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za Uumbaji, alipumzika siku ya saba na akaanzisha Sabato kwa ajili ya watu wote kama
ukumbusho wa Uumbaji. Amri ya nne ya sheria za Mungu zisizobadilika inaagiza kuadhimishwa kwa Sabato hii ya siku ya saba
kama siku ya mapumziko, ibada, na huduma kulingana na mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa Sabato.
21. Uwakili
Sisi tu wmawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa na Yeye wakati, fursa, uwezo, na mali na mibaraka ya dunia na rasilmali zake.
Tunawajibika kwake kwa matumizi yake mazuri. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa kutoa utumishi mzuri kwake na kwa wanadamu wenzetu,
kwa kumrudishia zaka na kutoa sadaka kwa ajili ya kutangaza injili Yake na kwa kulitegemeza na kulikuza kanisa lake.
Uwakili ni upendeleo uliotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika
upendo na ushindi dhidi ya choyo na tamaa. Wakili huifurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake.
22. Mwenendo wa Kikristo
Tumeitwa tuwe watu watawa wanaofikiri na kutenda kwa kufuatana na sheria za mbinguni. Ili Roho aumbe
upya tabia ya Bwana wetu ndani yetu tunajihusisha tu katika mambo ambayo yataleta katika maisha yetu utukufu, afya na
furaha inayofananana na ya Kristo.
Badala yake yatupasa tuyafuate yo yote yale yatakayotuletea mawazo na miili yetu iwe kamili, yenye furaha na wema
23. Ndoa na Familia
Ndoa ilianzishwa na Mungu katika Edeni na ikathibitishwa na Yesu kuwa muungano wa maisha yote kati mwanaume na mwanamke katika wenzi wa upendo.
Kwa Mkristo kifungo cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na wenzi wanaokishiriki sharti wawe wenye imani moja tu. Upendo wa hiari, heshima staha na wajibu
ndizo nyuzi za uhusiano huu, ambao utaakisi upendo, utakatifu, na uhusiano kati ya Kristo na Kanisa lake. Mungu hubariki familia na anakusudia kwamba jamaa katika familia watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu kamili.
24. Huduma ya Kristo katika Patakatifu pa Mbinguni
Kuna hekalu mbinguni, hekalu la kweli lililojengwa na Bwana na siyo mwanadamu. Ndani yake Kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha wamumini kufaidi manufaa ya
kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa Kuhani wetu Mkuu na akaanza huduma ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni.
Mwaka 1844, mwishoni mwa wakati wa unabii wa siku 2,300, aliingia katika awambu ya pili na ya mwisho ya huduma ya upatanisho upatanishi. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi ambayo
ni sehemu ya mwisho ya kukomesha dhambi yote, mfano wa kutakasa
patakatifu pa hekalu la Waeberania wa kale katika Siku ya Upatanisho.
25. Kuja kwa Yesu Mara ya Pili
Kuna hekalu mbinguni, hekalu la kweli lililojengwa na Bwana na siyo mwanadamu. Ndani yake Kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha wamumini kufaidi manufaa ya
kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa Kuhani wetu Mkuu na akaanza huduma ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni.
Mwaka 1844, mwishoni mwa wakati wa unabii wa siku 2,300, aliingia katika awambu ya pili na ya mwisho ya huduma ya upatanisho upatanishi. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi ambayo
ni sehemu ya mwisho ya kukomesha dhambi yote, mfano wa kutakasa
patakatifu pa hekalu la Waeberania wa kale katika Siku ya Upatanisho.
26. Mauti (Kifo) na Ufufuo
Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yake ana kutokufa, atawapa waliokombolewa wake uzima wa milele. Mpaka siku hiyo
mauti ni hali ya kutojifahamu kwa watu wote. Wakati Kristo, ambaye ni uzima wetu, atakapoonekana, wenye hai waliofufuliwa na wenye haki
walio hai watabadilishwa na kupewa miili ya utukufu na hivyo kunyakuliwa kwa pamoja na
kumlaki Bwana wao. Ufufuo wa pili, ambao ni ufufuo wa waovu, utatokea mika elfu moja baadaye.
27. Milenia na Mwisho wa Dhambi
Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati ya ufufuo wa kwanza na pili. Wakati huo waovu
waliokufa watahukumiwa, dunia itakuwa ukiwa na utupu, bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika zake.
Mwishowe kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni. Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na
shetani na malika zake watauzingira mji, Lakini moto kutoka mbinguni utawateketeza
ili kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele
28. Dunia Mpya
Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa, Mungu ataweka tayari makao ya milele waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele,
upendo, furaha na kujifunza mbele zake. Kwa hapa Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu na mauti vitakuwa vimepita.
Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakuwepo tena.
Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo, naye atatawala milele. Amina.