Tumeitwa tuwe watu watawa wanaofikiri na kujisikia, na kutenda kwa kufuatana na sheria za mbinguni. Ili Roho aumbe upya tabia ya Bwana wetu ndani yetu tunajihusisha tu katika mambo ambayo yataleta katika maisha yetu utukufu, afya na furaha inayofananana na ya Kristo. Maana yake ni kwamba furaha yetu na tafrija zetu zingefikia kanuni ya juu ya namna nzuri ya Kikristo. Wakati tukitambua kuwa tunazo tofauti mbalimbali za utamaduni, mavazi yetu yapaswa yawe ya kawaida, si ya anasa, ya kiasi, safi, yanayowastahili wale ambao uzuri wao wa kweli hauwi wa kujipamba kwa nje, bali kwa mapambo yasiyoharibika, yaani roho ya upole na utulivu. Pia ina maana ya kwamba kwa kuwa miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu, lazima tuitunze kwa busara. Pamoja na mazoezi ya kutosha na kupumzika yatupasa kuchagua vyakula vyenye afya kadiri inavyowezekana na kuepuka vyakula visivyo safi, vilivyo najisi, vilivyotajwa katika Maandiko Matakatifu. Kwa sababu vinywaji vya vileo, pombe, mvinyo, tembo, moshi, tumbako na matumizi mabaya ya madawa na madawa ya usingizi huleta madhara kwa miili yetu, yatupasa kuepukana nayo kabisa. Badala yake yatupasa tuyafuate yo yote yale yatkayotuletea mawazo na miile yetu iwe kamili, yenye furaha na wema.” (1Yoh.2; Efe.5:1-21; Rum.12:1, 2; 1Kor.6:19, 20; 10:31; 1Tim.2:9, 10; Law.11:1-47; 2Kor.6:4-7; 1Pet.3:1-4; 2Kor.4:8; Fil.4:8; 3Yoh.2)
Mwenendo wa Mkristo huja kama mwitikio kushukuru wokovu mkuu aliouleta Mungu kupitia Yesu Kristo. Paulo anawaomba waumini wote “Basi ndugu zangu, nawasihi kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza kwa ukamilifu. (Rum.12:1, 2).Kwa hiyo wakristo kwa makusudi, hulinda na kukuza uwezo wao wa kiakili, kimwili na wa kiroho ili wamheshimu na kumtukuza Mwumbaji na Mwokozi wao.
Kristo aliomba “siombi kwamba uwatoe katika uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.” (Yoh.17:15, 16). Ni muhimu kujua kwa jinsi gani wakristo wanaokaa duniani lakini wawe tofauti na ulimwengu. Kristo kielelezo chetu aliishi duniani humu akichanganyika na watu lakini hakutenda dhambi. Aliitwa mlafi na mlevi (Mt.11:19) lakini hakuna awezaye kuthibitisha kwamba alitenda dhambi (Yoh. 8:46).
Mwenendo na Wokovu
Katika kuchagua upi ni mwenendo unaofaa, twapaswa kuepuka kukithiri kwa aina mbili. Kwanza ni kuzipokea sheria na matumizi ya misingi ya afya kama njia ya wokovu. Kutaka kuhesabiwa haki kwa matendo ya mwili ni kujitenga na Kristo (Gal.5:4). Kinyume chake, kukithiri kwingine ni kutumia uhuru vibaya kwa kutenda dhambi. (Gal. 5:13). Ikiwa kila mtu atafuata aonavyo vema, hapatakuwa na kuonyana kama ilivyofundishwa na Yesu katika Mt.18 na Wagalatia 6:1, 2. Wakati mwenendo na hali ya kiroho vinahusiana sana, hatuwezi kuupata wokovu kwa mwenendo mwema. Wakati wokovu ni kwa njia ya Kristo peke yake, mwenendo mwema ni matokeo ya kile Yesu alichotimiza kutuokoa, pale Kalvari.
Mahekalu ya Roho Mtakatifu
Siyo Kanisa pekee bali hata mkristo mmoja mmoja hufanya hekalu la Roho Mtakatifu (1Kor.6:19). Kwa nafasi yetu kama Wakristo yatupasa kujali hali ya kiroho na kimwili ya wanadamu kama Yesu alivyojali. Twasoma kuwa aliponya “ugonjwa na udhaifu” wa kila namna (Mt.4:23). Sheria za Mungu ambazo hujumuisha sheria za afya, haziumizi bali zimewekwa na Muumbaji kutusaidia kuyafurahia maisha katika ujazo wake. (Angalia Yoh.10:10).
Baraka ya Mungu ya Afya Kamili
Kupata afya bora hutegemea kufuata kwa uaminifu kanuni zilizotolewa na Mungu. (Kut.15:26). Baadhi ya kanuni hizi ziko wazi na zinakubalika na watu wote. Kwa sababu wanadamu wana mazoea tofauti, kanuni zingine za afya huwakwaza, zikaonekana hazieleweki, zikahojiwa na hata kukataliwa.
A) Baraka ya mazoezi
Mazoezi ya kuzingatiwa daima ni kanuni ndogo iletayo nguvu, mwili imara, inaondoa msongo wa mawazo, ngozi yenye afya, kujiamini, kutawala uzito wa mwili, kusaidia uyeyushaji wa chakula mwilini na kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya shinikizo la damu na magonjwa ya moyo. Mazoezi siyo jambo la uchaguzi bali ni muhimu kwa afya bora. Kazi ya manufaa huleta ustawi na uvivu hufanya mtu awe omba omba (Angalia Mith.6:6-13; 14:23). Mungu aliwapa kazi wazazi wetu wa kwanza kutunza nyumba yao kwenye uwazi. (Mwa.2:5, 15; 3:19). Yesu alipokuwapo duniani aliweka kielelezo cha kufanya kazi, kwanza kwenye karakana ya seremala na pili akiwa katika huduma alitembea miji na vijiji.
B) Baraka ya mwanga wa jua
Mwanga ni muhimu kwa uhai. (Mwa.1:3). Nuru huwezesha michakato izalishayo lishe inayotupatia nguvu na kuachia hewa ya Oxgen tunayovuta. Mwanga hukuza hali ya afya na uponyaji.
C) Baraka ya maji
Asilimia sabini na tano (75%) ya miili yetu ni maji. Maji hupotea mwilini kwa njia ya kupumua, jasho na kuondosha uchafu. Ili tubaki na afya, ni muhimu kuyarejesha maji yanayopotea kwa kunywa glasi zisizopungua nane (8). Matumizi mengine ya maji ni kwa usafi na kuburudisha.
D) Baraka ya hewa saf
. Mazingira yasiyo na hewa safi husababisha damu kubeba hewa ya Oxygen kidogo kuliko inavyotakiwa. Hiyo humfanya mtu asiwe mwangalifu na mwenye kuitikia kwa uzito kutekeleza yanayohitajika. Hivyo ni muhimu kujipatia hewa safi ya kutosha kila siku.
E) Baraka ya kuishi kwa kiasi, bila madawa wala vichocheo
Madawa yamejaa kwenye jamii yetu kwa sababu huchangamsha mwili na kuondoa maumivu na msongo. Wakristo tumezungukwa na vishawishi kuvitumia madawa. Hata viburudisho vingine vinavyoonekana havina matatizo huwa vina madawa. Kahawa, chai na kola vina kafeini, na vinywaji baridi vyenye ladha ya matunda huwa na vilevi. Utafiti umethibitisha kwamba matumizi ya vinywaji vyenye vilevi kidogo huongoza kwenye vinywaji vyenye vilevi vinavyoathiri akili.
1. Tumbaku
Katika umbo lolote, tumbaku ni sumu inayoua polepole yenye kuathiri mwili, akili na uwezo wa kimaadili. Mara ya kwanza athari zake huwa hazionekani. Huchangamsha kisha huhafifisha mfumo wa fahamu, ikizorotesha na kuyumbisha uwezo wa ubongo. Wale wanaotumia tumbaku huwa wanajiua wenyewe polepole na kuvunja amri ya Mungu isemayo usiue. (Kut.20:13)
2. Vinywaji vya kulevya
Pombe (alcohol) hutumika sana duniani. Yapo mafungu ya Biblia yanashauri kutumia kidogo mvinyo. (Kumb.33:28), na la kushangaza, ilisemwa pia yaweza kutumika wakati wa sikukuu za ibada (Kumb.14:26). Kwenye Agano Jipya, Paulo anampa kilevi mchungaji kijana kama dawa (1Tim.5:23). Na kufundisha kuwa viongozi wa kanisa wasizoee ulevi (Tit. 1:7).
Izingatiwe kuwa pombe ineleta madhara makubwa kwenye ini na mfumo wa fahamu ikiwemo na ubongo. Kwa kuwa Mungu huwasiliana nasi kupitia ufahamu, kwa kutumia pombe, mfumo huathirika sana. Imethibitika kwamba kadiri kiwango cha pombe kinapoongeza, hali ya mtu hubadilika kutoka kukosa kuratibu mambo, kuchanganyikiwa, kutokuelewa, neva kushindwa kazi (kaput), kuzimia na hata kufa. Musa aliruhusu kutumia mvinyo, lakini kama Yesu alivyopata kuonya, mengine yaliruhusiwa kwa ugumu wa mioyo ya wanadamu tu. (Mt.19:8). Mwanzo Edeni, hatuna mahali paliporuhusiwa kutumia pombe. Kwa kuwa maarifa yaliyoko duniani yanasema kwamba ukianza kunywa kilevi, utazoelea na itakuwa vigumu kuiacha, ushauri mwema ni kwamba tuachilie mbali ulevi (1Sam. 1:14).
3. Madawa mengine na madawa ya kulevya
Yako madawa mengine hatari kwa matumizi ya mwanadamu pamoja na madawa ya kulevya ambayo Shetani hutumia kumharibu mwanadamu. Wakristo wa kweli watamtukuza Mungu kwa miili yao kwa kuwa na mali ya thamani ya Mungu ambayo imenunuliwa kwa bei kubwa. (1Kor.6:19,20).
F) Baraka ya Pumziko
Pumziko halisi ni muhimu kwa afya. Yesu anaendeleza agizo lake kwa wanafunzi waliochoka “njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo” (Mk.6:31). Nyakati za utulivu za mapumziko hutoa fursa kumtafakari Mungu “Acheni mjue ya kuwa Mimi ni Mungu” (Zab.46:10). Mungu alisisitiza hitaji la mwanadamu la pumziko kwa kuweka siku ya saba kama siku ya pumziko. (Kut.20:10). Mawazo yanayochoshwa kwa mahangaiko ya dunia, yapaswa kuelekezwa palipo na maburudiko yajengayo afya. Hivyo hatutaifuata dunia. (1Yoh.2:15, 16).
1. Sinema, televisheni, radio na video
Vifaa hivi vya mawasiliano vyaweza kuwa nyenzo za elimu. Vimegeuza ulimwengu na kufanya maisha, mawazo, matukio ya ulimwengu mzima kufikiwa kirahisi katika hali halisi. Mkristo apaswa kukumbuka kwamba vile tuonavyo, televisheni na video huathiri mtu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Athari zake ni kubwa sana nyumbani. Yesu alionya chochote kinachokosesha, chafaa kujitenga nacho. (Mt.5:29, 30). Paulo alisema tukitazama tunabadilishwa toka utukufu hadi utukufu. (2Kor.3:18). Katika kulinda moyo (Mith. 4:23) ni vema kutafakari yanayoleta maana katika maisha, yenye kupendeza, sifa nzuri, wema nk. (Filp. 4:8).
2. Kusoma na muziki
. Kanuni kama iliyotolewa kwa sinema, televisheni, radio na video itatumika kwenye muziki. Wafuasi wa Kristo hawatasoma mambo yenye mwelekeo wa uovu au kusikiliza muziki unaoshawishi kutenda dhambi. (Rum.13:11-14; 1Pet.2:11).
3. Matendo yasiyokubalika
Waadventista pia hufundisha kuwa kucheza kamari, karata, kwenda kwenye majumba ya kuigiza, na kusakata dansi vyafaa kuepukwa. (1Yoh.2:15-17). Huhoji matumizi ya wakati ambao hutumika michezo ya kuhatarisha. (Filp.4:8).
G) Baraka ya Chakula chenye Lishe
Kwa wanandoa wa awali, Mungu aliwapa chakula kinachotokana na mimea. (Mwa.1:29). Mara baada ya kuanguka dhambini, waliongezewa mboga za kondeni. (Mwa.3:18). Chakula bora ni kile kinachotokana na mimea.
1. Chakula cha asili
. Biblia haikatazi kutumia kama chakula nyama ya wanyama safi. Ni busara kutumia chakula kilichowekwa na Mungu tangu awali yaani kinachotokana na mimea; lakini ikiwa ni vigumu kukipata, twapaswa kutumia chakula bora kilichopo kwenye mazingira.
2. Wanyama safi na wasio saf
i. Ni baada ya gharika ndipo Mungu aliporuhusu Nuhu na familia yake kutumia nyama akionya wasitumie damu. (Mwa.9:3-5). Kwa kuruhusiwa kula nyama, Nuhu angechagua chakula chake kutoka kwa wanyama safi aliogizwa na Mungu waingie saba saba safinani. (Mwa.7:2, 3). Pamoja na kuwa wanyama safi walihitajika kwa chakula, bado walitumika pia kwa kutoa kafara. (Mwa.8:20). Maelezo ya kina ya wanyama safi na wasio safi hupatikana kwenye Walawi 11 na Kumbukumbu 14. Kwa kujitenga na vyakula najisi, watu wa Mungu walidhihirisha shukrani yao kukombolewa kutoka kwenye ulimwengu ulioharibika uliowazunguka. (Law.20:24-26; Kumb. 14:2). Agano jipya halikuondoa tofauti ya wanyama safi na wasio safi. Kuna mafungu yanayotumiwa vibaya kuelezea chakula (Rum.14:2, 14, 20, 23; Mdo.10:14, 15). Ieleweke kuwa Neno la Mungu hutakasa (Yoh. 17:17) na hivyo ruhusa ya Maandiko Matakatifu kwenye chakula ni muhimu (1Tim. 4:4, 5; Mk. 7:19).
3. Utaratibu, urahisi na uwiano
Matengenezo ya kufaa kwenye ulaji ni jambo la kuendelea na yapaswa kuingiwa kwa akili. Hatimaye twapaswa kutumia kidogo sana, vyakula vyenye sukari na mafuta. Zaidi, twapaswa kutayarisha chakula kwa njia rahisi na kwa asili inavyowezekana ili kupata mafao stahili. Chakula kitumiwe kwa utaratibu na kwa kujali wakati. Vyakula mchanganyiko na viungo husumbua uyeyushaji wake na mazoea ya kuvitumia hutumbukiza watu kwenye matatizo ya afya.
H) Baraka ya Mavazi ya Kikristo
Mungu alitengeneza mavazi ya kwanza kwa wazazi wetu (Mwa.2:25; 3:21) na hujua mahitaji yetu ya mavazi. (Mt.6:25-33). Twapaswa kuzingatia kanuni za urahisi, uadilifu, kufaa kwake, afya na uzuri wa asili tunapochagua mavazi.
1. Rahis
Kama ilivyo kwa mambo mengine yote, mavazi ya mkristo yapaswa kuwa rahisi, yenye kumtukuza Mungu. (1Kor.10:31)
2. Uadilifu
Wakristo hawatatia doa uzuri wa tabia zao kwa mitindo ya mavazi kwa ajili ya kuridhisha tamaa ya macho. (1Yoh.2:16)
3. Kufaa na gharama nafuu
Kwa sababu ni mawakili wa siri za Mungu (1Kor.4:1), wakristo watazingatia mavazi yawe ya kufaa na yenye gharama nafuu wakiepuka mapambo ya dhahabu, lulu au thamani kubwa. (1Tim.2:9). Mavazi ya Mkristo pia yatazingatia hali ya jinsia. (Kumb.22:5).
4. Afya
Siyo chakula tu chenye kuathiri afya. Hata mavazi yapaswa kutoa afya kwa kusitiri mwili, au kutokubana mishipa ya damu na kuathiri afya.
5. Jinsi yalivyo na uzuri wa asili
Wakristo wanaelewa onyo la kuepuka “kiburi cha uzima (1Yoh.2:16). Akirejea maua ya kondeni, Yesu alisema “hata Sulemani katika fahari yake yote, hakuvikwa kama mojawapo ya hayo.” (Mt.6:29). Hivyo alidhihirisha kwamba uzuri kwa mtazamo wa kimbingu, unatazamwa kwa neema, urahiri, usafi, na uzuri wa asili. Kujionyesha kwa namna ya kiulimwengu, kama inavyoonekana katika mitindo (fasheni) haina thamani mbele za Mungu. (1Tim. 2:9). Wakristo huongoa wasio amini siyo kwa kuigiza kile ulimwengu utendacho bali kwa kudhihirisha tofauti inayoburudisha na kuvutia. Petro alisema wenzi wa maisha wasioamini “waweza kuvutwa na mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi na wa hofu. Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. (1Pet.3:1-4)
a) Tabia huonesha uzuri wa kweli wa mtu
Wote Petro na Paulo wameweka kanuni ya kufuatwa na wanaume na wanawake wakristo kwenye eneo la mapambo. “Kujipamba kwenu kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;” (1Pet.3:3). “Vivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu” (1Tim.2:9, 10).
b) Urahisi unawiana na matengenezo na uamsho
Yakobo alipotoa wito kwenye familia yake kujitoa kwa Mungu, walimpa “miungu migeni yote iliyokuwa mikononi mwao, na pete zilizokuwa masikioni mwao, naye Yakobo akazificha chini ya mwaloni ulioko Shekemu” (Mwa.35:2, 4). Baada ya Waisraeli kwa ndama wa dhahabu, Mungu aliamuru “basi sasa vueni vyombo vyenu vya uzuri ili nipate kujua nitakalowatenda.” Kwa kutubu “wakavua vyombo vyao vyote vya uzuru, tangu mlima wa Horebu na mbele.”Paulo kwa uwazi anasema kuwa kumbukumbu hii iliwekwa ili kutuonya sisi tuliofikiwa na miisho ya zamani. (1Kor.10:11).
c) Uwakili mwema unahitaji maisha ya kujinyima
Wakati sehemu kubwa ya walimwengu hawana chakula, uyakinifu (materialism) unawatengea wakristo majaribu kuanzia kuwa na mavazi ya gharama, magari, mapambo na nyumba za fahari. Unyenyekevu katika maisha na mwonekano unawatenga wakristo kinyume na uchoyo, uyakinifu, majigambo ya kipagani, jamii ya karne ya 21, mahali ambako thamani huwekwa kwenye vitu badala ya kwa watu.
Biblia hukemea mapambo yasiyo ya asili na huyahusisha na upagani na uasi (2Waf. 9:30, Yer.4:30). Kuhusiana na mapambo, wakristo wapaswa kuwa na mwonekano wa asili. Ikiwa tutamwinua Mwokozi katika namna tunavyosema, tunavyotenda na tunavyovaa, tutakuwa sumaku tukiwavuta watu kwake. “Katika nchi nyingine desturi ya kuvaa pete ya ndoa huchukuliwa kuwa lazima, baada ya kuingia mawazoni mwa watu kuwa ni kipimo cha maadili mema, na hivyo haichukuliwi kuwa pambo. Katika hali ya namna hiyo Waadventista wa Sabato hawana nia ya kulaumu desturi hiyo.” (Angalia Mwongozo wa Kanisa).
Kanuni za Viwango vya Kikristo
Katika kujifunua kwake kote, mtindo wa maisha wa mkristo ni mwitikio wa wokovu unaopatikana kwa njia ya Kristo. Mkristo ananuia kumheshimu Mungu na kuishi kwa namna ambayo Yesu angeliishi.
Wakati wengine wanaweza kuwa na mtazamo kuwa kanuni za maisha ya kikristo zimejaa makatazo, twapaswa kuzitazama kanuni chanya katika katika mhimili wa wokovu. Roho Mtakatifu anapokuwa amefanya maskani kwenye moyo wa mtu, mabadiliko yanayotokea kumzunguka mtu huyo ni makubwa na yataonekana kwa wanaomzunguka. (Yoh. 3:8). Roho si kwamba hufanya mabadiliko katika moyo bali pia huendeleza kutenda kazi kwake kwa mkristo. Tunda la Roho ni upendo (Gal.5:22, 23). Hoja yenye nguvu ya ubora wa ukristo ni mkristo anayependa na kupendeka.
Kuishi na Nia ya Kristo
“Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yeu” (Filp.2:5). Katika mazingira yanayofaa au yasiyofaa, twapaswa kuelewa na kuishi sawa sawa na nia ya Kristo (1Kor.2:16). Utii wa kweli huanzia moyoni. Moyo ukipenda kufanya kazi na Yesu, na tukiridhia, Kristo atajitambulisha kwenye mawazo yetu na makusudi na hivyo kuunganisha nia zetu na nia yake. Kwa kuithamini tabia ya Kristo mioyoni mwetu na mawasiliano ya kudumu na Mungu, dhambi itakuwa kitu cha kuchukiza.
Kuishi Tukimsifu na Kumtukuza Mungu
Mungu ametutendea mengi sana. Njia mojawapo tunayoweza kuonyesha shukrani zetu kwake ni kwa kumsifu. Zaburi hukazia jambo hili la kiroho. “Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, nizione nguvu zako na utukufu wako, Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa Jina lako nitaiinua mikono yangu. Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha. (Zab.63:2-5).
Kwa mkristo mtazamo huo wa sifa utahifadhi mambo mengine ya kiroho katika mtazamo unaofaa. Kwa kumtazama Mwokozi aliyesulubiwa aliyetukomboa kutoka adhabu ya dhambi na mamlaka ya dhambi, tunavutwa kuzishika amri zake “na kuyatenda yapendezayo machoni pake.” (1Yoh.3:22 cf. Efe.5:10). Wakristo hawako “hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao” (1Kor.5:15). Kila aliye mkristo wa kweli atamweka Mungu kwanza katika yote atendayo, afikiriyo, asemayo na yote anayotamani. Hana Mungu mwingine mbele za Mkombozi. (1Kor.10:31).
Kuishi kuwa Mfano
Paulo alionya msikoseshe yeyote (1Kor.10:32). Alijizoeza asiwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele za watu siku zote. (Mdo.24:16). Tukikosesha tunakuwa kwazo kwa wale ambao Yesu aliwafia. (Luk.17:1, 2). Anayekaa ndani yake “imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda” (1Yoh.2:6).
Kuishi ili Kutumika
Sababu kubwa inayowafanya wakristo waishi kama waishivyo ni kuokoa wanaume na wanawake waliopotea. Paulo alisema anajitahidi kuwapendeza watu wote “nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.” (1Kor.10:33; cf. Mt.20:28).
Masharti na Mwongozo
Katika Kanuni za Kanisa, yamewekwa masharti juu ya kutotumia tumbaku, bangi, madawa na madawa ya kulevya, pombe, vyakula najisi. Haya ni mahitaji kidogo kwa mkristo anayekuwa. Hatupaswi kuhukumu wanaojaribiwa (Rum.14:1; 15:1). Kanuni njema ni kutenda yote kwa utukufu wa Mungu (1Kor.10:31)
1 Yohana 2X 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki, 2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote. 3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. 4 Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. 5 Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda. 7 Wapenzi, siwaandikii amri mpya, ila amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Na hiyo amri ya zamani ni neno lile mlilolisikia. 8 Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu; kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kung'aa. 9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa. 10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo. 11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho. 12 Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba. 14 Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 18 Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. 19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. 20 Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. 21 Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. 22 Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. 23 Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele. 26 Nimewaandikia haya katika habari za watu wale wanaotaka kuwapoteza. 27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake. 28 Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, mwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake. 29 Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
Waefeso 5:1-21X 1 Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; 2 mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato. 3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; 4 wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. 5 Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. 6 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. 7 Basi msishirikiane nao. 8 Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru, 9 kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; 10 mkihakiki ni nini impendezayo Bwana. 11 Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee; 12 kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena. 13 Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru. 14 Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza. 15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu. 17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana. 18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; 19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo; 21 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
Warumi 12:1, 2X 1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
1 Wakorintho 6:19, 20X 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
1 Wakorintho 10:31X 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1 Timotheo 2:9, 10X 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
M. Walawi 11:1-47X 1 Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. 4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. 8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. 9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao. 10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, 11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. 12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu. 13 Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake; 16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18 na mumbi, na mwari, na mderi; 19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo. 20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. 21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; 22 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. 23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu. 24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni; 25 na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni. 26 Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi. 27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni. 28 Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu 29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake, 30 na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi. 31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni. 32 Tena kitu cho chote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; kwamba ni chombo cha mti, au nguo, au ngozi, au gunia, chombo cho chote kitakachoangukiwa, ambacho ni chombo cha kufanyia kazi yo yote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hata jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. 33 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa. 34 Kila chakula kilichomo, ambacho ni kuliwa, hicho ambacho maji hutumiwa juu yake, kitakuwa ni najisi; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi. 35 Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu. 36 Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi. 37 Na kipande cho chote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa zitakazopandwa, zitakuwa safi. 38 Lakini kwamba hizo mbegu zilitiwa maji na cho chote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu. 39 Kama akifa mnyama awaye yote, ambaye mna ruhusa kumla, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hata jioni. 40 Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni. 41 Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. 42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo. 43 Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu cho chote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo. 44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. 45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. 46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi; 47 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.
2 Wakorintho 6:4-7X 4 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; 5 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; 6 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; 7 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto;
1 Petro 3:1-4X 1 Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. 2 Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.
2 Wakorintho 4:8X 8 Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa;
Wafilipi 4:8X 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
3 Yohana 1:2X 2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Warumi 12:1, 2X 1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Yohana 17:15, 16X 15 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. 16 Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Mathayo 11:19X 19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Yohana 8:46X 46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
Wagalatia 5:4X 4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
Wagalatia 5:13X 13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Mathayo 18X 1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema, 2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, 3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 4 Basi, ye yote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5 Na ye yote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi; 6 bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari. 7 Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha! 8 Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. 9 Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto. 10 Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. 11 Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea. 12 Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea? 13 Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisa na tisini wasiopotea. 14 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee. 15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni. 19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao. 21 Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? 22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. 23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake. 24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi. 25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni. 26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni. 28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia akamkamata,akamshika koo,akisema Nilipe uwiwacho. 29 Basi mjoli wake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia. 30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa kifungoni, hata atakapoilipa ile deni. 31 Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka. 32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nalikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi; 33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mjoli wako, kama mimi nilivyokurehemu wewe? 34 Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote. 35 Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.
Wagalatia 6:1, 2X 1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. 2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
1 Wakorintho 6:19X 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
Mathayo 4:23X 23 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.
Yohana 10:10X 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Kutoka 15:26X 26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
Mithali 6:6-13X 6 Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia zake ukapate hekima. 7 Kwa maana yeye hana akida, Wala msimamizi, wala mkuu, 8 Lakini hujiwekea akiba ya chakula wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno. 9 Ewe mvivu, utalala hata lini? Utaondoka lini katika usingizi wako? 10 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, Bado kukunja mikono upate usingizi! 11 Hivyo umaskini wako huja kama mnyang'anyi, Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. 12 Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; Huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. 13 Hukonyeza kwa macho, hunena kwa miguu, Huwaashiria watu kwa vidole vyake.
Mithali 14:23X 23 Chakula kingi chapatikana kwa ukulima wa maskini; Bali viko viharibiwavyo kwa sababu ya dhuluma.
Mwanzo 2:5, 15X 5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; 15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 3:19X 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 1:3X 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
K. Torati 33:28X 28 Na Israeli anakaa salama, Chemchemi ya Yakobo peke yake, Katika nchi ya ngano na divai; Naam, mbingu zake zadondoza umande.
K. Torati 14:26X 26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
1 Timotheo 5:23X 23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
Tito 1:7X 7 Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu.
Mathayo 19:8X 8 Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
1 Samweli 1:14X 14 Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hata lini? Achilia mbali divai yako.
1 Wakorintho 6:19,20X 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Marko 6:31X 31 Akawaambia, Njoni ninyi peke yenu kwa faragha, mahali pasipokuwa na watu, mkapumzike kidogo. Kwa sababu walikuwako watu wengi, wakija, wakienda, hata haikuwapo nafasi ya kula.
Zaburi 46:10X 10 Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
Kutoka 20:10X 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
1 Yohana 2:15, 16X 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Mathayo 5:29, 30X 29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.
2 Wakorintho 3:18X 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Mithali 4:23X 23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Wafilipi 4:8X 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Warumi 13:11-14X 11 Naam, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini 12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru. 13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu. 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
1 Petro 2:11X 11 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
1 Yohana 2:15-17X 15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. 17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.
Wafilipi 4:8X 8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
Mwanzo 1:29X 29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;
Mwanzo 3:18X 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;
Mwanzo 9:3-5X 3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote. 4 Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile. 5 Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
Mwanzo 7:2, 3X 2 Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili, mume na mke. 3 Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote.
Mwanzo 8:20X 20 Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
M. Walawi 11X 1 Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, 2 Neneni na wana wa Israeli, mkiwaambia, Wanyama hawa ndio wanyama wenye uhai mtakaowala, katika hayawani wote walio juu ya nchi. 3 Kila mnyama mwenye kwato katika miguu yake, mwenye miguu ya kupasuka kati, mwenye kucheua, katika hayawani, hao ndio mtakaowala. 4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 5 Na wibari, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6 Na sungura, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 7 Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. 8 Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. 9 Katika hao wote walio ndani ya maji mtakula hawa; kila aliye na mapezi na magamba, ndani ya hayo maji, na ndani ya bahari, na ndani ya mito, mtakula hao. 10 Na hao wote wasio na mapezi na magamba, ndani ya bahari, na ndani ya mito, katika hao waendao majini, na katika wote wenye uhai, waliomo majini, hao ni machukizo kwenu, 11 watakuwa machukizo kwenu; msiile nyama yao, na mizoga yao itakuwa machukizo kwenu. 12 Kila asiye na mapezi wala magamba aliye ndani ya maji ni machukizo kwenu. 13 Kisha katika ndege hawa watakuwa ni machukizo kwenu; hawataliwa, ndio machukizo; tai, na furukombe, na kipungu; 14 na mwewe, na kozi kwa aina zake, 15 na kila kunguru kwa aina zake; 16 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 17 na bundi, na mnandi, na bundi mkubwa; 18 na mumbi, na mwari, na mderi; 19 na korongo, na koikoi kwa aina zake, na hudihudi, na popo. 20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu. 21 Pamoja na hayo, hivi vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne ni halali kula, hao walio na miguu mirefu, ya kurukia juu ya nchi; 22 katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake. 23 Lakini vyote vitambaavyo vyenye mabawa, vilivyo na miguu minne, ni machukizo kwenu. 24 Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni; 25 na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni. 26 Kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, naye hana kwato mbili, wala hacheui, huyo ni najisi kwenu; kila agusaye wanyama hao atakuwa ni najisi. 27 Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni. 28 Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu 29 Tena katika vitu vile vitambaavyo, vitambaavyo juu ya nchi, hivi ni najisi kwenu; kicheche, na panya, na mjombakaka, kwa aina zake, 30 na guruguru na kenge, na mjusi na goromoe, na lumbwi. 31 Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; awaye yote atakayewagusa, wakiisha kufa, atakuwa ni najisi hata jioni. 32 Tena kitu cho chote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; kwamba ni chombo cha mti, au nguo, au ngozi, au gunia, chombo cho chote kitakachoangukiwa, ambacho ni chombo cha kufanyia kazi yo yote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hata jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi. 33 Na kila chombo cha udongo, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, kila kilichomo ndani yake kitakuwa ni najisi, na hicho chombo kitavunjwa. 34 Kila chakula kilichomo, ambacho ni kuliwa, hicho ambacho maji hutumiwa juu yake, kitakuwa ni najisi; na kila kinyweo ambacho ni cha kunywewa, kilichomo katika chombo kama hicho, kitakuwa ni najisi. 35 Na kila kitu kitakachoangukiwa na kipande cho chote cha mizoga yao kitakuwa najisi; kwamba ni tanuru, au meko ya vyungu, kitavunjwa vipande vipande; ni najisi vitu hivyo, navyo vitakuwa najisi kwenu. 36 Pamoja na hayo, chemchemi, au shimo, ambamo maji yakusanyika, vitakuwa ni safi; lakini hicho kitakachogusa mizoga yao kitakuwa ni najisi. 37 Na kipande cho chote cha mzoga kikiwa kimeangukia mbegu za kupandwa zitakazopandwa, zitakuwa safi. 38 Lakini kwamba hizo mbegu zilitiwa maji na cho chote cha mizoga yao kuziangukia, ni najisi kwenu. 39 Kama akifa mnyama awaye yote, ambaye mna ruhusa kumla, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hata jioni. 40 Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni. 41 Na kila kitu kitambaacho juu ya nchi ni machukizo; hakitaliwa. 42 Kila aendaye kwa tumbo lake, na kila aendaye kwa miguu minne, na kila aendaye kwa miguu mingi, maana, ni vyote vyenye kutambaa vitambaavyo juu ya nchi, hamtavila, kwa kuwa ni machukizo. 43 Msifanye nafsi zenu kuwa ni chukizo kwa kitu cho chote chenye kutambaa, kitambaacho, wala msifanye nafsi zenu kuwa ni najisi kwa vitu hivyo, mkajipatia uchafu kwa hivyo. 44 Kwa kuwa mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yo yote, kiendacho juu ya nchi. 45 Kwa kuwa mimi ni Bwana niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; basi mtakuwa watakatifu, kwa kuwa mimi ni Mtakatifu. 46 Hii ndiyo sheria katika hao wanyama, na ndege, na kila kiumbe kilicho hai, kiendacho ndani ya maji, na kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi; 47 ili kupambanua kati ya hao walio najisi na hao walio safi, na kati ya kiumbe kilicho hai ambacho chaliwa, na hicho kilicho hai ambacho hakiliwi.
K. Torati 14X 1 Ninyi mmekuwa wana wa Bwana, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa. 2 Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi. 3 Usile kitu cho chote kichukizacho. 4 Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, 5 kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; 6 na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla. 7 Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; 8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse. 9 Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula; 10 na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu. 11 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. 12 Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu; 13 na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake; 14 na kila kunguru kwa aina zake; 15 na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 16 na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa; 17 na mwari, na nderi, na mnandi; 18 na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo. 19 Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale. 20 Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi. 21 Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye. 22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako; 26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako; 27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe. 28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; 29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
M. Walawi 20:24-26X 24 Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni Bwana, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa. 25 Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye tohara na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu cho chote ambacho nchi imejaa nacho, niliowatenga nanyi kuwa ni najisi. 26 Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu mimi; kwa kuwa mimi Bwana ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba mwe wangu.
K. Torati 14:2X 2 Hii ndiyo sheria ya mwenye ukoma, katika siku ya kutakaswa kwake; ataletwa kwa kuhani,
Warumi 14:2, 14, 20, 23X 2 Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga. 14 Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. 20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza. 23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
Matendo 10:14, 15X 14 Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. 15 Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
Yohana 17:17X 17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
1 Timotheo 4:4, 5X 4 Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; 5 kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Marko 7:19X 19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
Mwanzo 2:25X 25 Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
Mwanzo 3:21X 21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Mathayo 6:25-33X 25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? 27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? 28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti 29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. 30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
1 Wakorintho 10:31X 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1 Yohana 2:16X 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
1 Wakorintho 4:1X 1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.
1 Timotheo 2:9X 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
K. Torati 22:5X 5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
1 Yohana 2:16X 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Mathayo 6:29X 29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
1 Timotheo 2:9X 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
1 Petro 3:1-4X 1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
1 Petro 3:3X 3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
1 Timotheo 2:9, 10X 9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Mwanzo 35:2, 4X 2 Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake, na wote waliokuwa pamoja naye, Ondoeni miungu migeni iliyoko kwenu, mjisafishe mkabadili nguo zenu.
1 Wakorintho 10:11X 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
2 Wafalme 9:30X 30 Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.
Yeremia 4:30X 30 Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta roho yako.
Yohana 3:8X 8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Wagalatia 5:22, 23X 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Wafilipi 2:5X 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
1 Wakorintho 2:16X 16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Zaburi 63:2-5X 2 Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, Nizione nguvu zako na utukufu wako. 3 Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai; Midomo yangu itakusifu. 4 Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai; Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu. 5 Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
1 Yohana 3:22X 22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
Waefeso 5:10X 10 mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
1 Wakorintho 5:15a href="#close" title="Close" class="close">X 11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
1 Wakorintho 10:31X 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
1 Wakorintho 10:32X 32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,
Matendo 24:16X 16 Nami ninajizoeza katika neno hili niwe na dhamiri isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu siku zote.
Luka 17:1, 2X 1 Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! 2 Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
1 Yohana 2:6X 6 Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.
1 Wakorintho 10:33X 33 vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
Mathayo 20:28X 28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Warumi 14:1X 1 Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake.
Warumi 15:1X 1 Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe.
1 Wakorintho 10:31X 31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.