Kuja Kwa Yesu Mara Ya Pili

Utangulizi


Kuja kwa kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la kanisa, hitimisho kuu la injili. Kuja kwa mwokozi kutakuwa halisi, binafsi, kutaonekana kwa dunia mzima. Atakaporudi wenye haki waliokufa watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu na kuchukuliwa kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa sehemu nyingi za unabii, pamoja na hakli ya sasa ya ulimwengu, huonyeshe kwamba kuja kwa kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote.” (Tit.2:13, Mt. 24; Mdo19:11, Mt.24:14; Ufu. 1:7, 14:14-20; Mt. 24:43-50, 1Kor.15:51-50, 1Thes.1:7, 4:13-18, 5:1-6, Luk 21:2; 2Tim 3:1-5).

Mama, mtoto moja alisema kabla ya kulala, akimwambia mama yake, natamani sana kuonana na rafiki yangu Yesu. Je, atakuja lini? Mtoto huyu mdogo alikuwa hajui kwamba tamanio lake la kurudi kwa Yesu ni tamanio la dahari (enzi). Maneno ya mwisho kwenye Biblia hutoa ahadi ya kuja kwa Yesu “Naam naja upesi” na mtume Yohana anaongeza “Amina, naam na uje Bwana Yesu.” Uf. 22:20. Kumwona Yesu!!! Kuungana milele na atupendaye kuliko tunavyoweza kufikiri! Kukomesha maumivu, vilio magonjwa na mauti, kufurahia umilele pamoja na watakatifu waliofufuliwa ambao kwa sasa wanapumzika makaburini! Ni tumaini lenye kuburudisha kwa kiasi gani!

Maelezo ya kuja kwa Yesu

Naam, siku moja Yesu atakuja. Kuja kwake litakuwa ni jambo la kushangaza kwa waliosubiri kwa muda mrefu hata wakalala usingizi (Mt. 25:5). Usiku wa manane, (Mt. 25:6) ikimaanisha wakati dunia ikiwa katika enzi za giza nene, Mungu atadhihirisha uwezo kuokoa watu wake. Maandiko hutoa maelezo ya kuja kwa YesuSauti kubwa itatoka kwenye Hekalu, kwenye kiti cha enzi ikisema Imekwisha kuwa (Ufu. 16:17), patakuwa na umeme, sauti ya radi, tetemeko kubwa juu ya nchi, (Uf. 16:18), milima itatetemeka, miamba itavunjika vunjika na kutawanyika kama mawimbi ya bahari, miji itaanguka, visiwa vitakimbia (Uf. 16:20). Mbingu zitakunjwa kama ukurasa, milima na visiwa vitaondolewa mahali pake (Uf. 6:14).

Pamoja na vurugu ya maumbile ya nchi, watu wa Mungu watakuwa na ujasiri kwa kuwa wataiona ishara ya kuja kwake Mwana wa Adam (Mt. 25:30). Atakapokuwa anashuka na mawingu (Mdo. 1:9-11), kila jicho litamwona (Uf. 1:7), akiwa Mfalme wa uzima na siyo mtu wa sikitiko, siyo aliyevaa taji ya miiba bali amevaa taji ya utukufu, (Uf. 19:12) na jina lililoandikwa kwenye vazi lake na paja lake MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA (Uf. 19:16).

Atakapokuwa anakuja, hofu itawakumba wote waliokataa neema yake pale alipowasihi “ghairini, muachane na njia yenu mbaya, mbona mnataka kufa?” (Ez. 33:11). Wafalme, wakuu, majemedari, matajiri, wenye nguvu, kila mtumwa na mwungana watajificha chini ya miamba na milima wakiiambia milima na miamba tuangukieni, tusitirini mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na hasira za Mwanakondoo (Uf. 6:15, 16). Kwa maana siku ya hasira yake imekuja naye ni nani awezaye kusimama? (Uf. 6:17). Furaha yao waliomtazamia kurudi itafunika hofu ya waovu. Kuja kwa mkombozi inahitimisha historia ya watu wa Mungu kwa utukufu. Kwa sauti yenye kupenya watasikika wakisema “Tazama huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja atusaidie. Huyu ndiye BWANA tuliyemngoja, na tushangilie na kuufurahia wokovu wake” (Isa. 25:9).

Atakapokaribia, atatuma sauti kubwa ya parapanda kuwakusanya wateule wake toka pande zote za dunia (Mt. 24:31). Ni kipindi cha kufurahisha kwa kuwa watakatifu walioko makaburini wataisikia sauti yake! (Yoh.5:28). Wale watakatifu watakaokutwa hai kufumba na kufumbua watabadilika (1Kor.15:52). Wakiwa wamevikwa utukufu na kutokufa, pamoja na watakatifu waliofufuliwa, watanyakuliwa kumlaki BWANA angani na kuwa naye milele (1Thes. 4:16, 17).

Mafundisho ya kuzingatia kuhusiana Yesu kuja mara ya pili

Uhakika wa Kuja kwake

Mitume na wakristo wa awali waliokuona kuja kwa Yesu kuwa tumaini lenye Baraka (Tit. 2:13 cf Ebr. 9:28). Walitumainia unabii na ahadi zote za Maandiko Matakatifu vitatimia wakati wa Yesu kuja mara ya pili. (2 Pet. 3:13 cf Isa. 65:17) kwa kuwa hilo ndilo lengo la safari ya kikristo. Wote wanaompenda Kristo wanatazamia fursa watakayomwona Yesu na kuwa na ushirika na Baba pamoja na Roho Mtakatifu.

Ushahidi wa Biblia kuwa Yesu anakuja tena

  1. Yoh. 14:3 Nami nikienda nitarudi tena niwakaribishe kwangu ili nilipo nanyi mwepo
  2. Henoko alitabiri juu ya kuja kwa Yesu akiwa na utukufu Yuda 14, 15.
  3. Miaka 1,000 kabla Yesu hajazaliwa, mtunga zaburi alitabiri atakuja na hatanyamaza... na kuwaita wale waliofanya naye agano kwa dhabihu (Zab. 50:3-5)
  4. Siku Yesu aliyopaa, malaika walitoa ahadi kwamba atarudi kama alivyoondoka Mdo.1:9–11
  5.  

Garantii (Amana) ya Yesu kuja mara ya pili ni kuja kwake mara ya Kwanza

Mara ya kwanza Yesu alikuja kuokoa, mara ya pili anakuja kukamilisha kile alichokiokoa kwa kukivika utukufu. Yesu alikuja akapata ushindi usiohojiwa (Wafil. 2:15) na hivyo ni muhimu akaja kukamilisha wokovu (Ebr. 9:26, 28).

Huduma ya Kristo inayoendelea Mbinguni

Ufunuo kwa Yohana unadhihirisha kwamba hekalu la mbinguni ni jambo la msingi kwa ajili ya mpango wa Mungu wa wokovu. (Uf. 1:12, 13, 3:12, 4:1-5, 5:8, 7:15, 8:3, 11:1, 19, 14:15, 17; 15:5, 6, 8; 16:1, 17). Unabii unaosema kwamba ameanza huduma ya mwisho kwa mwenye dhambi, huongeza kwamba atarudi kuwachukua watu wake. (Ebr. 9:26, 28 cf Uf.15:8, Uf. 16:15)

Namna atakavyokuja

Yesu alionya kwamba watatokea waongo ambao watapotosha juu ya ujio wake, wakisema ameonekana huku au kule na akaonya tusiwaamini (Mt. 24:23). Sasa anakuja vipi?

  1. Atakuja kama alivyoondoka, Mdo. 19:11, akiwa na mwili bila kuwa katika roho Luk. 24:36 – 43
  2. Kuja kwake kutaonekana. Kama umeme toka mashariki hadi magharibi (Mt. 24:27), Wanadamu watamwona (Uf. 17) na kutakuwa na nafasi ya kuomboleza (Mt. 24:30).
  3. Kuja kwake kutasikikaKutaambatana na mlio wa baragumu (1Thes. 4:13, Mt. 24:31)
  4. Atakuja na utukufu wa Baba yake (Mt. 16:27, Uf. 19:11-16)
  5. Kama siku za Babeli, ufalme wa Mungu hautasimama pamoja na falme zingineDan. 2:34, 44, 35)
  6.  

Kuja kwa Yesu na matokeo yake kwa wanadamu

Atawakusanya watakatifu (Mt. 24:31, Mt. 25:34, 35; Mk. 13:27), na kuwapa kuishi naye (Yoh. 14:3), Atawafufua watakatifu waliokufa Katika Kristo 1 Kor. 15:52, 53, 1 Thes. 4:16). Watakatifu wataizomea mauti (1Kor. 15:55), nao watavikwa utukufu wakiakisi utukufu wa Mungu katika miili, akili na roho (1Kor. 15:42-54), Waovu wataangamizwa (2 Thes. 2:9 -12, Uf. 6:16, 17) kwa upanga utokao kutoka kwake yeye aketiye juu ya farasi (Uf. 19:20, 21).

Dalili za Kuja kwa Yesu mara ya Pili

Biblia haifundishi tu jinsi Yesu atakavyokuja mara ya pili bali pia imesema dalili za kuja kwake. Hapa tunaziangalia kwa ujumla na kwa ufupi.

Dalili juu ya ulimwengu wa asili

Dalili juu ya jua kutiwa giza, mwezi kutokutoa nuru na nyota kuanguka (Luk. 21:25, Mk. 13:24-26). Yohana aliona tetemeko kubwa (Uf. 6:12). Hizi dalili zilionyesha kukoma kwa miaka 1260 za Uf. 12:6)

Dalili juu ya ulimwengu wa kidini

  1. Kuwepo uamsho mkubwa (Uf. 14:6,7).
  2. Kitabu cha Danieli kitafunguliwa (Dan. 12:4) na kuhubiriwa kwa ujumbe wa malaika watatu (Uf. 14:6-12)
  3. Kuhubiriwa injili Mt. 24:14, na watu wa Mungu kuitazamia siku ya kuja kwake (2 Pet. 3:12)Kupoa kwa hali ya kiroho Mt. 24:12, 2Tim. 31-5)
  4. Kuibuka Upapa (Uf. 13:3), nabii wa uwongo (Uf. 16:13, 14), Mnyama (Uf. 16:13, Uf. 3:13)
  5. Kupungua kwa uhuru wa kuabudu (Uf. 13:17, 15; Uf. 14:9-12)
  6. Taabu kwa watakatifu (Dan. 12:1)
  7. Kuongezeka Uovu. Kwa kuwa limezuka fundisho kwamba kutii amri za Mungu siyo jambo muhimu, dunia inaendelea kujaa maovu ya kila aina. Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, (Mt. 24:37-39), maovu ya zinaa (Mw. 6:2) dhuluma (Mw. 6:11, Yak. 5:1-6)
  8. Vita na Majanga. Taifa litaondoka kupigana na taifa, ufalme kupigana na ufalme
  9. Kutakuwa na njaa... (Mt.24:7; Mk. 13:7, 8; Mt. 24:7)
  10.  

Kuwa tayari wakati wote

Biblia hutufundisha kwamba Yesu anakuja lakini haijatuambia anakuja lini (Mt. 24:36). Matayarisho ya Mkristo yanapaswa kuwa ya siku zote ili tusije kukataliwa na Mungu (Mt. 7:21 -24. Mfano wa wanawali 10 huonyesha wako wakristo watakaokuja kukataliwa (Mt. 25:11, 12).

Kabla ya gharika Mungu alimtuma Nuhu (Mw. 6:13), kabla ya kuiharibu Sodoma alituma Malaika (Mw. 19) na kabla ya Yesu atatuma ujumbe “Heri aliyealikwa kwenye arusi ya mwana kondooo Uf. 19:9). Watakaosikia sauti ya Mungu ndio watakaoshangilia kuja kwake (Isa. 25:9)

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Mathayo 24X
1 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. 3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. 9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. 15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. 32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; 33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. 35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. 36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; 41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. 43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. 45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Matendo 19:11X
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
Mathayo 24:14X
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ufunuo 1:7X
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Ufunuo 14:14-20X
14 Kisha nikaona, na tazama, wingu jeupe, na juu ya wingu hilo ameketi mmoja, mfano wa Mwanadamu, mwenye taji ya dhahabu juu ya kichwa chake, na katika mkono wake mundu mkali. 15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. 16 Na yeye aliyeketi juu ya wingu akautupa mundu wake juu ya nchi, nchi ikavunwa. 17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali. 18 Na malaika mwingine akatoka katika ile madhabahu, yule mwenye mamlaka juu ya moto; naye akamlilia kwa sauti kuu yule mwenye mundu ule mkali, akisema, Tia mundu wako mkali, ukachume vichala vya mzabibu wa nchi, maana zabibu zake zimeiva sana. 19 Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu. 20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili.
Mathayo 24:43-50X
43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. 45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua,
1 Wakorintho 15:51-58X
51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. 55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
1 Wathesalonike 1:7X
7 Hata mkawa kielelezo kwa watu wote waaminio katika Makedonia, na katika Akaya.
1 Wathesalonike 4:13-18X
13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
1 Wathesalonike 5:1-6a href="#close" title="Close" class="close">X
1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. 3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. 5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. 6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.
Wafilipi 2:5-11X
5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Luka 21:2X
2 Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.
2 Timotheo 3:1-5X
1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. 2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, 3 wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema, 4 wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu; 5 wenye mfano wa utauwa, lakini wakikana nguvu zake; hao nao ujiepushe nao.
Ufunuo 22:20X
20 Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.
Mathayo 25:5X
5 Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi.
Mathayo 25:6X
6 Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki.
Ufunuo 16:17X
17 Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
Ufunuo 16:18X
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.
Ufunuo 16:20X
20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
Ufunuo 6:14X
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
Mathayo 25:30X
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Matendo 1:9-11X
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Ufunuo 1:7X
7 Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.
Ufunuo 19:12X
12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.
Ufunuo 19:16X
16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
Ezekieli 33:11X
11 Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Ufunuo 6:15, 16X
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima, 16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
Ufunuo 6:17X
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Isaya 25:9X
9 Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.
Mathayo 24:31X
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Yohana 5:28X
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
1 Wakorintho 15:52X
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
1 Wathesalonike 4:16, 17X
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Tito 2:13X
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Waebrania 9:28X
28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
2 Petro 3:13X
13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Isaya 65:17X
17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.
Yohana 14:3X
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Yuda 1:14, 15X
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, 15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.
Zaburi 50:3-5X
3 Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza, Moto utakula mbele zake, na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote. 4 Ataziita mbingu zilizo juu, Na nchi pia awahukumu watu wake. 5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Matendo 1:9–11X
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Wafilipi 2:15X
15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Waebrania 9:26, 28X
26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Ufunuo 1:12, 13X
12 Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; 13 na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.
Ufunuo 3:12X
12 Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.
Ufunuo 4:1-5X
1 Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo. 2 Na mara nalikuwa katika Roho; na tazama, kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu ya kile kiti; 3 na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe la yaspi na akiki, na upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya zumaridi. 4 Na viti ishirini na vinne vilikizunguka kile kiti cha enzi, na juu ya vile viti naliona wazee ishirini na wanne, wameketi, wamevikwa mavazi meupe; na juu ya vichwa vyao walikuwa na taji za dhahabu. 5 Na katika kile kiti cha enzi kunatoka umeme na sauti na ngurumo. Na taa saba za moto zilikiwaka mbele ya kile kiti cha enzi, ndizo Roho saba za Mungu.
Ufunuo 5:8X
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.
Ufunuo 7:15X
15 Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao.
Ufunuo 8:3X
3 Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Ufunuo 11:1, 19X
1 Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo. 19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
Ufunuo 14:15, 17X
15 Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa. 17 Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali.
Ufunuo 15:5, 6, 8X
Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa; 6 na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakatoka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, ya kung'aa, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu. 8 Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.
Ufunuo 16:1, 17X
1 Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Enendeni, mkavimimine vile vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi. 17 Na huyo wa saba akakimimina kitasa chake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.
Waebrania 9:26, 28X
26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Ufunuo 15:8X
8 Hekalu likajazwa moshi uliotoka kwenye utukufu wa Mungu na uweza wake. Wala hapakuwa na mtu aliyeweza kuingia ndani ya hekalu, hata yatimizwe mapigo saba ya wale malaika saba.
Ufunuo 16:15X
15 (Tazama, naja kama mwivi. Heri akeshaye, na kuyatunza mavazi yake, asiende uchi hata watu wakaione aibu yake.)
Mathayo 24:23X
23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki.
Matendo 19:11X
11 Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida;
Luka 24:36 – 43X
36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. 37 Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. 38 Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. 40 Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa? 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. 43 Akakitwaa, akala mbele yao.
Mathayo 24:27X
27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Ufunuo 17X
1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi; 2 ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. 3 Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi. 4 Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. 5 Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. 6 Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu. 7 Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi. 8 Yule mnyama uliyemwona alikuwako, naye hayuko, naye yu tayari kupanda kutoka kuzimu na kwenda kwenye uharibifu. Na hao wakaao juu ya nchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watastaajabu wamwonapo yule mnyama, ya kwamba alikuwako, naye hayuko, naye atakuwako. 9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. 10 Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. 11 Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu. 12 Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. 13 Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu. 15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. 16 Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. 17 Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe. 18 Na yule mwanamke uliyemwona, ni mji ule mkubwa, wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.
Mathayo 24:30X
30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.
1 Wathesalonike 4:13X
13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
Mathayo 24:31X
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Mathayo 16:27X
27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Ufunuo 19:11-16X
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana.
Danieli 2:34, 44, 35X
34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. 44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. 35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Mathayo 24:31X
31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Mathayo 25:34, 35X
34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. 35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Marko 13:27X
27 Ndipo atakapowatuma malaika na kuwakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande wa mwisho wa nchi hata upande wa mwisho wa mbingu.
Yohana 14:3X
3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
1 Wakorintho 15:52, 53X
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
1 Wathesalonike 4:16X
16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
1 Wakorintho 15:55X
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
1 Wakorintho 15:42-54X
42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
2 Wathesalonike 2:9-12X
9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu. 10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa; 11 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia; 12 ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.
Ufunuo 6:16, 17X
16 wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
Ufunuo 19:20, 21X
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Luka 21:25X
25 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;
Marko 13:24-26X
24 Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. 25 na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. 26 Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.
Ufunuo 6:12X
12 Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu,
Ufunuo 12:6X
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
Ufunuo 14:6,7X
6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
Danieli 12:4X
4 Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie muhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huko na huko, na maarifa yataongezeka.
Ufunuo 14:6-12X
6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. 8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Mathayo 24:14X
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
2 Petro 3:12X
12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka?
Mathayo 24:12X
12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa.
Ufunuo 13:3X
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
Ufunuo 16:13, 14X
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Ufunuo 16:13X
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Ufunuo 3:13X
13 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ufunuo 13:17, 15X
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. 15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
Ufunuo 14:9-12X
9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Danieli 12:1X
1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
Mathayo 24:37-39X
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Mwanzo 6:2X
2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.
Mwanzo 6:11X
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma.
Yakobo 5:1-6X
1 Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. 2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. 3 Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho. 4 Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. 5 Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo. 6 Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
Mathayo 24:7X
7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.
Marko 13:7, 8X
7 Nanyi mtakaposikia habari za vita na uvumi wa vita, msitishwe; hayo hayana budi kutukia, lakini ule mwisho bado. 8 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na matetemeko ya nchi mahali mahali; kutakuwako na njaa; hayo ndiyo mwanzo wa utungu.
Mathayo 24:7X
7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.
Mathayo 24:36X
36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.
Mathayo 7:21-24X
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
Mathayo 25:11, 12X
11 Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. 12 Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi.
Mwanzo 6:13X
13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Mwanzo 19X
1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi. 2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha. 3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala. 4 Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. 5 Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua. 6 Lutu akawatokea mlangoni, akafunga mlango nyuma yake. 7 Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi. 8 Tazama, ninao binti wawili ambao hawajajua mtu mume, nawasihi nitawatolea kwenu mkawafanyie vilivyo vyema machoni penu, ila watu hawa msiwatende neno, kwa kuwa wamekuja chini ya dari yangu. 9 Wakasema Ondoka hapa! Kisha wakanena, Mtu huyu mmoja amekuja kwetu kuketi hali ya ugeni; naye kumbe, anataka kuhukumu! Basi tutakutenda wewe vibaya kuliko hawa. Wakamsonga sana huyo mtu, huyo Lutu, wakakaribia wauvunje mlango. 10 Lakini wale watu wakanyosha mikono yao, wakamwingiza Lutu kwao nyumbani, wakaufunga mlango. 11 Kisha wakawapiga hao watu walioko mlangoni kwa upofu, wadogo kwa wakubwa, hata wakachoka kwa kuutafuta mlango. 12 Basi wale watu wakamwambia Lutu, Je! Unaye mtu hapa zaidi? Mkwe, wanao, na binti zako, na wo wote ulio nao katika mji, uwatoe katika mahali hapa; 13 maana tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu. 14 Lutu akatoka akasema na wakweze, waliowaposa binti zake, akasema, Ondokeni mtoke katika mahali hapa kwa sababu Bwana atauharibu mji huu. Lakini akawa kama achezaye machoni pa wakweze. 15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. 16 Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. 17 Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. 18 Lutu akawaambia, Sivyo, bwana wangu! 19 Tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. 20 Basi mji huu u karibu, niukimbilie, nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi. 21 Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji huo uliounena. 22 Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari. 23 Jua lilikuwa limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. 24 Ndipo Bwana akanyesha juu ya Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. 25 Akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. 26 Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi. 27 Ibrahimu akatoka asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana, 28 naye akatazama upande wa Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi ukapanda, kama moshi wa tanuru. 29 Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu. 30 Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili. 31 Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote. 32 Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. 33 Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. 34 Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye. 35 Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka. 36 Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao. 37 Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo. 38 Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.
Ufunuo 19:9X
9 Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Isaya 25:9X
9 Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.