Kwa ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu Kristo, na kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa uzima. Hivyo tunamtambua Kristo kama Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tupokelewa kama washiriki na kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa muungano wetu na Kristo msamaha wa dhambi zetu, na kumpokea kwetu Roho Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa majini na unategemea uthibitisho wa imani katika Yesu na ushuhuda wa toba ya dhambi. Unafuata mafundisho katika Maandiko Matakatifu na ukubali wa mafundisho yake. (Rum. 6:1-6; Kol. 2:12, 13; Mdo. 16:30-33; 22:16; 2:38; Mt.28:19, 20)
Nyangwira aliyeishi Afrika ya Kati, hakuona ubatizo kuwa ni jambo la ziada. Kwa zaidi ya mwaka moja alijifunza Biblia. Alitamani awe mkristo. Jioni moja alimwambia mume wake aliyojifunza. Akiwa amehamaki, mume wake alibwatuka, “sitaki dini ya namna hii nyumbani kwangu na ukiendelea kujifunza huko, nitakuua.” Pamoja na kuvunjwa moyo, Nyangwira aliendelea na mafundisho na akawa tayari kubatizwa. Kabla ya kuondoka kwenda kubatizwa, alimwambia mume wake kuwa anaenda kubatizwa. Mume wake alishika upanga, akamwambia, “nilikuambia sitaki ubatizwe, na siku utakayobatizwa, ntakuua.” Hata hivyo Nyangwira alidhamiria kumfuata Bwana na aliondoka kwenda kubatizwa mwangwi wa vitisho vya mume wake vikiwa masikioni mwake. Kabla ya kuingia majini, aliungama dhambi zake, akatoa maisha yake kwa Yesu, pasipo kujua kwamba huenda akawa anautoa na uhai wake pia kwa siku hiyo. Amani ilijaa moyoni mwake alipobatizwa. Aliporudi nyumbani, alichukua upanga wa mume wake akamwendea alipo. Mume wake alipomwona aliuliza kwa hasira, “Je, umebatizwa?” “Ndiyo” Nyangwira alijibu kirahisi akiendelea, “hapa kuna upanga”. Mume akahoji, “Je, uko tayari kuuawa? Mke akajibu“Ndiyo.” Akishangazwa na ujasiri, mume wake hakuwa na nia ya kumwua tena.
Ubatizo una umuhimu gani?
Je, ubatizo una umuhimu hata mtu akahatarisha maisha yake? Je, Mungu anaudai kwa lazima? Je, wokovu wetu unategemea kuwa tumebatizwa au la?
Kielelezo cha Yesu
Siku moja Yesu aliacha karakana ya seremala Nazareti, akaaga familia akaenda Yordani ambako binamu yake Yohana alikuwa akihubiri. Alipomkaribia Yohana, aliomba abatizwe. Kwa mshangao, Yohana aliuliza, mie nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? “Kubali hivi sasa” Yesu alijibu, “kwa kuwa ndivyo itupasayo kuitimiza haki yote.” (Mt.3:13-15). Ubatizo wa Yesu ulifanya desturi hii iwe ya kimbingu. (Mt. 3:17 cf. Mt.21:25). Ikiwa Yesu asiye na dhambi alibatizwa kutimiza haki, sisi wenye dhambi twapaswa nasi kubatizwa.
Amri ya Yesu
Mwishoni mwa huduma yake duniani, Yesu aliagiza “Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu na kuwafundisha yote niliyowaamuru ninyi (Mt.28:19, 20). Yesu alitaka wote wanaouingia ufalme wa neema, wote wanaoutamani ufalme wake wabatizwe na kusisitiza, na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari. (Mt.28:20). Baada ya kupaa, wanafunzi walihubiri umuhimu wa ubatizo (Mdo.2:38; 10:48; 22:16). Kuitikia wito huu, umati wa watu walibatizwa na kuunda kanisa la Agano Jipya, (Mdo.2:41, 47; 8:12) wakikubali mamlaka ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Ubatizo na Wokovu
Yesu alifundisha, aaminiye na kubatizwa ataokoka. (Mk.16:16). Katika kanisa la mitume, ubatizo ulifuata kumwamini Yesu, kuthibitisha imani ya muumini. (cf. Mdo.8:12; 16:30-32). Petro anasema kama Nuhu alivyookolewa kwa safina, sisi tunaokolewa kwa ubatizo (1Pet.3:20, 21). Siyo safina iliyomwokoa Nuhu bali ni Mungu, nasi si maji ya ubatizo yanayotuokoa, bali ni damu ya Yesu. Ila imani yetu inavyoonyeshwa kwa njia ya ubatizo, hutufanya kuupokea wokovu. Pamoja na ubatizo kuhusishwa na wokovu, hautoi uhakikisho wa kuokolewa. Mtume Paulo akitumia kielelezo cha taifa la Israeli, anasema wote walibatizwa katika wingu na katika bahari, wakala chakula na kunywa kinywaji cha roho lakini Mungu hakupendezwa na wengi wao. (1Kor.10:1-5). Ubatizo hautuhakikishii wokovu moja kwa moja na yule adhaniye amesimama, aangalie asianguke. (1Kor.10:11, 12)
Ubatizo Mmoja
Uendeshaji wa ubatizo katika ulimwengu wa kikristo unatofautiana. Baadhi huzamisha, wengine hunyunyizia maji, bado wengine humiminia maji. Tabia ya umoja ambayo Roho huleta kwenye kanisa ni namna moja ya kufanya ubatizo (Efe.4:5). Ni nini maana ya ubatizo na umuhimu wake wa kiroho?
Maana ya Neno Ubatizo
Neno batiza linatokana na neno la kiingereza babtize ambalo linatokana na kigiriki baptizein. Kitenzi chake ni neno bapto ambalo lina maana ya kuzamisha majini. Matumizi ya neno ubatizo katika Agano Jipya humaanisha (1) ubatizo wa maji (Mt.3:6; Mk.1:9; Mdo. 2:41), (2) mfano wa kuteseka na kufa kwa Kristo (Mt.20:22, 23; Mk.10:38, 39; Luk.12:50) (3) ujio wa Roho Mtakatifu (Mt.3:11; Mk.1:8; Luk.3:16; Yoh.1:33; Mdo.1:5; 11:16) na (4) kutawadha au kuosha mikono (Mk.7:3, 4; Luk.11:38). Hakuna ushahidi wa kimaandiko kuwa ubatizo wa kunyunyiza ulitumika wakati wa mitume.
Ubatizo katika Agano Jipya
Matukio ya ubatizo katika Agano Jipya yalihusisha kuzamisha majini. Tunasoma kuwa Yohana alibatiza mto Yordani. (Mt.3:6; cf. Mk.1:5) na Ainon karibu na Salim kwa sababu kulikuwa na maji tele. (Yoh.3:23). Ni ubatizo wa kuzamisha ndio unaohitaji maji mengi. Yohana alimbatiza Yesu, Yordani (ndani) na baada ya kubatizwa Yesu alipanda kutoka majini (Mk.1:9, 10; cf Mt.3:16).
Kanisa la Mitume pia lilibatiza kwa kuzamisha majini. Wakati Mwinjilisti Filipo alipombatiza towashi wa Kushi, wote wawili walitelemka ndani ya maji na wote wawili walipanda kutoka majini baada ya ubatizo (Mdo.8:38, 39).
Ubatizo katika Historia
Hili ni somo linalojitegemea nje ya Biblia. Kidokezo ni kuwa Wayahudi walikuwa na tabia ya kuzamisha wafuasi. Pia iko michoro ya Waesene kule Qumram inayoonyesha ubatizo wa kuzamisha.
Maana ya Ubatizo
Maana ya ubatizo inahusiana na jinsi unavyofanyika. Ni baada tu ya mtu kubatizwa kwa kuzamishwa ndipo maana yake inapoonekana.
Ishara ya Kifo cha Yesu na Kufufuka
Kule kufunikwa na maji kunaashiria kugubikwa na masumbufu na mateso, (Zab.42:7; 69:2; 124:4, 5), hivyo ubatizo wa maji wa Yesu aliwakilisha onyesho la unabii la kuteseka, kifo na kuzikwa (Mk.10:38; Luk.12:50) na kuinuka kwake kutoka kwenye maji kuliashiria kufufuka kwake kutoka wafu (Rum.6:3-5). Ubatizo ungekosa maana kitheolojia ikiwa Kanisa la Mitume lingetumia njia isiyo ya kuzamisha.
Ishara ya kuwa Mfu kwa dhambi na Kuwa Hai katika Kristo
Katika ubatizo, muumini huingia katika uzoefu wa kuteseka kwa Yesu. “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” (Rum.6:3, 4). Katika ubatizo, kifo cha Yesu kinakuwa kifo cha muumini na kufufuka kwa Yesu kunakuwa kufufuka kwa muumini.
1. Mfu kwa dhambi
Katika ubatizo waumini huwa “wameungana pamoja naye katika mfano wa mauti yake” (Kristo) (Rum.6:5) na kusulubiwa na Kristo (Gal.2:20). Hii inamaansiha utu wetu wa kale ulisu)lubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena. (Rum.6:6-8). Waumini wamekana mtindo wao wa zamani wa maisha, ya kale yanakuwa yamepita (2Kor.5:17), maisha yao yakiwa yamefichwa katika Kristo na katika Mungu. Ubatizo pia humaanisha kuzikwa na Kristo (Kol.2:12). Katika ubatizo, muumini huukana ulimwengu, kwa kutoka kati yake na kuishi maisha ya kutengwa na uchafu (2Kor.6:17). Kwenye Kanisa la Mitume, wito wa ubatizo pia uliita waumini kutubu. (Mdo.2:38). Hivyo, ubatizo ni utambulisho wa kutubu.
2. Kuwa Hai kwa Mungu
Uwezo ulio katika ufufuo wa Kristo hutenda kazi ndani yetu na kutufanya tutembee katika upya wa uzima. (Rum.6:4). Tunakuwa wafu kwa dhambi na tunakuwa hai kwa Mungu (Rum.6:11).
Ishara ya Uhusiano wa Kimaagano
Katika nyakati za Agano la Kale kutahiriwa kulikuwa ishara ya kimaagano baina ya Mungu na Ibrahimu. (Mwa.17:1-11). Agano la Ibrahimu lilibeba utambulisho wa kiroho na kitaifa pia. Kila mtoto aliyefikia umri wa siku nane na zaidi alipaswa kutahiriwa. (Mwa.17:10-14; 25-27). Mwanaume asiyetahiriwa alikatiliwa mbali (alitengwa) na watu wa Mungu kwa kuwa alikuwa amevunja agano. (Mwa.17:14). Desturi hii pia ilikuwa ishara ya kuhesabiwa haki kwa imani. (Rum.4:11). Peke yake haikutosha, bali kulidaiwa liwe jambo la moyoni. (Kumb.10:16; cf.30:6; Yer.4:4). Wasiotekeleza tohara ya moyoni wangeadhibiwa na mataifa. (Yer.9:25, 26).
Wayahudi walipomkataa Yesu kuwa Masihi, walivunja agano na Mungu, wakakoma kuwa wateule. (Dan.9:24-27, angalia somo la Mungu Mwana). Ijapokuwa agano la Mungu na ahadi zake zilibaki hizo hizo, alichagua watu wapya. Israeli wa kiroho walichukua nafasi ya Wayahudi. (Gal.3:27-29; 6:15, 16). Kifo cha Yesu kilihakikisha Agano Jipya, la kutahiriwa rohoni, kule kuitikia kwa imani kafara ya Kristo kwa njia ya kifo chake. (Gal.2:7). Agano Jipya linadai imani ya ndani siyo kitendo cha nje, kutahiriwa wala kutokutahiriwa siyo kitu, bali imani itendayo kazi kwa upendo (Gal.5:6; 6:15, 16).
Kifo cha Yesu kiliridhia Agano Jipya. Watu huingia kwenye Agano hili kupitia tohara ya kiroho, imani kwa kifo cha Yesu kinalipia dhambi. Wakristo wana injili ya wasiotahiriwa (Gal.2:7). Mtu huingia kwa imani, utu wa ndani siyo kwa onyesho la nje. Hivyo kutahiriwa au kutokutahiriwa, hakufaidii kitu ila imani itendayo kazi katika upendo. (Gal.5:6). Kinachozingatiwa ni tohara ya moyo, katika Roho (Rum.2:28, 29). Ubatizo ni ishara ya kuingia mahusiano yanayookoa na Yesu (Kol.2:11, 12). Mwili wa dhambi huondoshwa kupitia tohara ya kiroho na muumini humvaa Yesu na kuingia mahusiano ya kimaagano na Yesu.
Wakiwa wa Kristo, wanakuwa uzao wa Ibrahimu, warithi wa ile ahadi. (Gal.3:27-29). Wanaoingia mahusiano ya namna hii wanapata uthibitisho wa Mungu kuwa “nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu” (Yer.31:33).
Ishara ya Kujitoa kwa Utumishi wa Kristo
Katika ubatizo wake, Yesu alijazwa Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ishara ya kutiwa mafuta kufanya utume aliopewa na Baba yake. (Mt.3:13-17; Mdo.10:38). Kwenye Kanisa la Mitume, kujazwa Roho Mtakatifu kulifuatia ubatizo wa maji. Hivyo nasi tunapobatizwa tunaungana na uwezo wa kimbingu na kwa na kutangaza injili. Roho Mtakatifu hutuandaa kwa utume. Yohana alisema ajaye “atabatiza kwa moto” (Mt.3:11). Isaya, alisema Mungu atatakasa watu wake “kwa roho ya hukumu na roho ya kuteketeza” (Isa.4:4), kuteketeza kabisa bati lako (Isa.1:25). Mungu ni moto ulao dhambi (Ebr.12:29). Akiisha kuzichoma dhambi, Roho hutoa karama. Kwenye Kanisa la Mitume, walijazwa ujasiri wa kuhubiri Neno. (Mdo.1:5, 8). Kwa siku za mwisho, kujazwa Roho kutakamilisha utume. (Mt.24:14; Ufu.14:6)
Ishara ya kuingia Kanisani
Ikiwa ishara ya mtu kuzaliwa mara ya pili (Yoh.3:3, 5), ubatizo hutia alama ya mtu kuingia kwenye ufalme wa Mungu. Wanafunzi waliongezeka kwa ubatizo (Mdo.2:41, 47; 1Kor.12:13). Hivyo, hakuna aliyebatizwa, akaacha kujiunga na familia ya kanisa.
Masharti ya kupewa Ubatizo
1. Imani
Imani inayotakiwa ni kukiri kuwa mauti ya Kristo ilimkomboa mwanadamu. (Mk.16:16). Ni wale tu waliomwamini Yesu ndio waliobatizwa hapo kale (Mdo.8:12, 36, 37; 18:8). Chanzo cha imani ni kusikia (Rum.10:17). Hivyo, kupeleka injili kwa kila kiumbe ni wito wa kuwa mwanafunzi hufanya mafundisho kuwa muhimu (Mt.28:19, 20).
2. Kutubu
“Tubuni mbatizwe”, Petro alisema, (Mdo.2:38). Mafundisho ya Injili huleta pia toba na kuongoka.
3. Matunda ya toba
Wanaotaka ubatizo wapaswa kuonyesha matunda ya toba. (Mt.3:8). Matunda ya toba yatafanya wakae ndani ya Kristo na Kristo akae ndani yao. (Yoh.15:1-8).
4. Kupimwa
Kuwa mshiriki wa Kanisa ni huhusisha kuchukua hatua ya kiroho. Hivyo kupimwa ni muhimu ili kuwa na ushahidi wa kuonekana kuwa na imani, kutubu na kuwa na matunda ya toba kabla ya kukubaliwa kuingia kanisani.
===Mwisho wa Somo===
Je watoto wachanga nao wapaswa kubatizwa?
Ubatizo huhusisha kuwaingiza kwenye ushirika wa kanisa waumini kwa mtazamo wa “kuzaliwa mara ya pili”. Kuongoka kwao kunawastahilisha kubatizwa na kuwa washiriki wa Kanisa. Kufanywa washiriki wa kanisa hutokea kwenye kuzaliwa mara ya pili, siyo kwa kuzaliwa kimwili. Katika Agano Jipya wanaume na wanawake walibatizwa wakawa washiriki wa Kanisa. (Mdo.8:12, 13, 29-38; 9:17, 18; 1Kor.1:14). Hakuna popote katika Agano Jipya ambako ubatizo wa watoto wachanga unaruhusiwa au kuzuiwa. Kwa kuwa wachanga hawawezi kuongoka, hawana sifa ya kubatizwa. Yesu hakuwatenga watoto kwenye ufalme wake wa neema. “Waacheni watoto waje kwangu… walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao” (Mt.19:14, 15). Kitendo cha Yesu kuwabariki watoto kimeingiza utaratibu wa kuwaweka wakfu watoto.
Umri unaofaa kubatiza ni 1) Pale mtu anapokuwa anaweza kuelewa maana ya ubatizo 2) Wamejitoa kwa Yesu na kuongoka 3)Wanaelewa misingi ya ukristo 4) Wanafahamu umuhimu wa kuwa mshiriki wa kanisa. Mtu huhatarisha wokovu wake anapokuwa amefikia umri wa kuwajibika na kukataa mvuto wa Roho Mtakatifu. Wazazi wanaokubali watoto wao wabatizwe wakiwa wadogo, ni lazima wakubali jukumu la kuwalea wapate kukua kiroho na kukuza tabia njema. Kwa kuwa kukomaa hutofautiana, hakuna umri uliowekwa kwa ajili ya mtu kubatizwa. Matunda ya Ubatizo Tunda maarufu la ubatizo ni kumwishia Kristo. Malengo na matamanio humlenga Kristo siyo nafsi. “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko… Kwa maana mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. (Kol.3:1-3).
Ubatizo siyo upeo bali tunapompokea Yesu, tunaingia katika mpango wa Mungu wa kukua. “Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.” (2Pet.1:2).
Tunda la pili ni maisha ya kuishi kwa ajili ya Kanisa la Kristo. Hatuwi tena watu waliotengana bali tunakuwa mawe yanayojenga hekalu la Mungu (2Pet.2:2-5).Tunaingia kwenye mahusiano maalum ambayo hutufanya tupokee daima neema ya Mungu inayotuwezesha kukua katika upendo. (Efe.4:16). Tunachukua majukumu miongoni mwa wenye maagano na Mungu kulea waumini wapya (1Kor.12:12-26). Kwa ustawi wao na wa kanisa, waumini wapya wapaswa kujihusisha na maisha ya ibada na huduma ya upendo. (Efe.4:16).
Tunda la mwisho ni maisha ya kuishi kwa ajili ya ulimwengu. Ni kweli baada ya kubatizwa wenyeji wetu ni mbinguni (Wafilp 3:20). Hata hivyo tumeitwa tutoke ulimwengu na kufundishwa kushiriki huduma ya Yesu ya kuokoa. “Basi sasa unakawilia nini? Simama ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.” (Mdo.22:16).
Warumi 6:1-6X 1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
Wakolosai 2:12, 13X 12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. 13 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;
Matendo 16:30-33X 30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake. 33 Akawakaribisha saa ile ile ya usiku, akawaosha mapigo yao, kisha akabatizwa, yeye na watu wake wote wakati uo huo.
Matendo 22:16X 16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
Mathayo 28:19, 20a href="#close" title="Close" class="close">X 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 3:13-15X 13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali.
Mathayo 3:17X 17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Isaya 61:1, 2X 1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Mathayo 28:19, 20X 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28:20X 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Matendo 2:38X 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo 10:48X 48 Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.
Matendo 22:16X 16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
Matendo 2:41, 47X 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Matendo 8:12X 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Marko 16:16X 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Matendo 8:12X 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Matendo 16:30-32X 30 kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? 31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. 32 Wakamwambia neno la Bwana, yeye na watu wote waliomo nyumbani mwake.
1 Petro 3:20, 21X 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.
1 Wakorintho 10:1-5X 1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari; 2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari; 3 wote wakala chakula kile kile cha roho; 4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo. 5 Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
1 Wakorintho 10:11, 12X 11 Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani. 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
Waefeso 4:5X 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
Mathayo 3:6X 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.
Marko 1:9X 9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.
Matendo 2:41X 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Mathayo 20:22, 23X 22 Yesu akajibu akasema, Hamjui mnaloliomba. Je! Mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi? Wakamwambia, Twaweza. 23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kuume na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.
Marko 10:38, 39X 38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? 39 Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa;
Luka 12:50X 50 Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe!
Mathayo 3:11X 11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Marko 1:8X 8 Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Luka 3:16X 16 Yohana alijibu akawaambia wote, Kweli mimi nawabatiza kwa maji; lakini yuaja mtu mwenye nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto;
Yohana 1:33X 33 Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.
Matendo 1:5X 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.
Matendo 11:16X 16 Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohana alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.
Marko 7:3, 4X 3 Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; 4 tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba.
Luka 11:38X 38 Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.
Mathayo 3:6X 6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.
Marko 1:5X 5 Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao.
Yohana 3:23X 23 Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.
Marko 1:9, 10X 9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.
Mathayo 3:16X 16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
Matendo 8:38, 39X 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Zaburi 42:7X 7 Kilindi chapigia kelele kilindi kwa sauti ya maboromoko ya maji yako, Gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu.
Zaburi 69:2X 2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.
Zaburi 124:4, 5X 4 Papo hapo maji yangalitugharikisha, Mto ungalipita juu ya roho zetu; 5 Papo hapo yangalipita juu ya nafsi zetu Maji yafurikayo.
Marko 10:38X 38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?
Luka 12:50X 50 Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe!
Warumi 6:3-5X 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
Warumi 6:3, 4X 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Warumi 6:5X 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
Wagalatia 2:20X 20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Warumi 6:6-8X 6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 7 kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi. 8 Lakini tukiwa tulikufa pamoja na Kristo, twaamini ya kuwa tutaishi pamoja naye;
2 Wakorintho 5:17X 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Wakolosai 2:12X 12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
2 Wakorintho 6:17X 17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
Matendo 2:38X 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Warumi 6:4X 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Warumi 6:11X 11 Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.
Mwanzo 17:1-11X 1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. 9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. 10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi.
Mwanzo 17:10-14; 25-27X 10 Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. 11 Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. 12 Mtoto wa siku nane atatahiriwa kwenu, kila mwanamume katika vizazi vyenu, mzaliwa nyumbani, na mnunuliwa kwa fedha, kila mgeni asiyekuwa wa uzao wako. 13 Mzaliwa nyumbani mwako, na mnunuliwa kwa fedha yako, lazima atahiriwe; na agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele. 14 Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu. 25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa mtu wa miaka kumi na mitatu, alipotahiriwa nyama ya govi lake. 26 Siku ile ile akatahiriwa Ibrahimu na Ishmaeli mwanawe. 27 Na watu wote wa nyumba yake, wazaliwa nyumbani, na wanunuliwa kwa fedha katika mkono wa mgeni, wakatahiriwa pamoja naye.
Mwanzo 17:14X 14 Na mwanamume mwenye govi asiyetahiriwa nyama ya govi lake, mtu yule atatengwa na watu wake; amelivunja agano langu.
Warumi 4:11X 11 Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
K. Torati 10:16X 16 Basi, zitahirini govi za mioyo yenu, wala msiwe na shingo ngumu.
Yeremia 4:4X 4 Jitahirini kwa Bwana, mkaziondoe govi za mioyo yenu, enyi watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu; ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikawaka hata mtu asiweze kuizima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Yeremia 9:25, 26X 25 Tazama, siku zinakuja, asema Bwana, nitakapowaadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya kutokutahiriwa; 26 Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.
Danieli 9:24-27X 24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. 25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Wagalatia 3:27-29X 27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Wagalatia 2:7X 7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;
Wagalatia 5:6X 6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Wagalatia 2:7X 7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa;
Wagalatia 5:6X 6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Warumi 2:28, 29X 28 Maana yeye si Myahudi aliye Myahudi kwa nje tu, wala tohara siyo ile ya nje tu katika mwili; 29 bali yeye ni Myahudi aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko; ambaye sifa yake haitoki kwa wanadamu bali kwa Mungu.
Wakolosai 2:11, 12X 11 Katika yeye mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. 12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.
Wagalatia 3:27-29X 27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Yeremia 31:33X 33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Mathayo 3:13-17X 13 Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali. 16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake; 17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Matendo 10:38X 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Mathayo 3:11X 11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Isaya 4:4X 4 hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.
Waebrania 12:29X 29 maana Mungu wetu ni moto ulao.
Matendo 1:5, 8X 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Mathayo 24:14X 14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Ufunuo 14:6X 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Yohana 3:3, 5X 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Matendo 2:41, 47X 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
1 Wakorintho 12:13X 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
Marko 16:16X 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Matendo 8:12, 36, 37X 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.
Warumi 10:17X 17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Mathayo 28:19, 20X 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Matendo 2:38X 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Yohana 15:1-8X 1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Matendo 8:12, 13, 29-38X 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu. 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.
1 Wakorintho 1:14X 14 Nashukuru, kwa sababu sikumbatiza mtu kwenu, ila Krispo na Gayo;
Mathayo 19:14, 15X 14 Lakini Yesu akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu; wala msiwazuie; kwa maana walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao. 15 Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.
Wakolosai 3:1-3X 1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
2 Petro 1:2X 2 Neema na iwe kwenu na amani iongezwe katika kumjua Mungu na Yesu Bwana wetu.
2 Petro 2:2-5X 2 Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 3 Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala uvunjifu wao hausinzii. 4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu; 5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;
Waefeso 4:16X 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
1 Wakorintho 12:12-26X 12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi. 15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo? 16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo? 17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa? 18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka. 19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi? 20 Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja. 21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa; 25 ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 26 Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
Waefeso 4:16X 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Wafilipi 3:20X 20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Matendo 22:16X 16 Basi sasa, unakawilia nini? Simama, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.