Huduma ya Kristo katika Patakatifu pa Mbinguni

Utangulizi


Kuna hekalu mbinguni, hekalu la kweli lililojengwa na Bwana na siyo mwanadamu. Ndani yake Kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha wamumini kufaidi manufaa ya kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa Kuhani wetu Mkuu na akaanza huduma ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni. Mwaka 1844, mwishoni mwa wakati wa unabii wa siku 2,300, aliingia katika awambu ya pili na ya mwisho ya huduma ya upatanisho upatanishi. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi ambayo ni sehemu ya mwisho ya kukomesha dhambi yote, mfano wa kutakasa patakatifu pa hekalu la Waeberania wa kale katika Siku ya Upatanisho. Katika huduma hiyo ya mfano patakatifu palitakaswa kwa damu ya kafara ya wanyama, lakini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamilifu ya damu ya Yesu.

 

Hukumu ya Upelelezi hufunua kwa viumbe wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu wamelala mauti katika Kristo na hivyo, katika Yeye wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Pia inadhihirisha wazi nani miongoni mwa walio hai wanaishi katika Kristo, wakitunza amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu na katika Yeye, hivyo basi wako tayari kuhamishwa kwenda katika ufalme wake wa milele. Hukumu hii huthibitisha haki ya Mungu katika kuwaokoa wale wanaoamini katika Yesu. Hutangaza kwamba wale waliodumu kuwa watiifu kwa Mungu wataupokea ufalme. Hitimisho la huduma hii ya Kristo litakuwa ndiyo mwisha wa kufungwa mlango wa rehema kwa wanadamu kabla ya Marejeo ya Yesu.”

 

(Ebr. 8:1-5;

Waebrania 8:1-5 X
1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.

4:14-16;
Waebrania 4:14-16 X
14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
9:11-28
Waebrania 9:11-28 X
11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. 13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; 14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? 15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. 16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. 18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. 19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, 20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. 21 Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. 23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. 24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; 25 wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; 26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
10:19-22;
Waebrania 10:19-22 X
19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
1:3;
Waebrania 1:3 X
3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
2:16, 17;
Waebrania 2:16, 17 X
16 Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Dan: 7:9-27;
Danieli 7:9-27 X
9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. 11 Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. 12 Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. 13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. 15 Basi, mimi Danieli, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha. 16 Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo. 17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. 18 Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele. 19 Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; 20 na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. 21 Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; 22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme. 23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. 24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. 25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. 26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele. 27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
8:13, 14;
Danieli 8:13, 14 X
13 Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.
9:24-27;
Danieli 9:24-27 X
24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu. 25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu. 26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa. 27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Hes 14:34;
Hesabu 14:34 X
34 Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.
Eze. 4:6;
Ezekieli 4:6 X
6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.
Lawi: 16;
Mambo ya Walawi: 16 X
1 Bwana akasema na Musa, baada ya kufa kwa hao wana wawili wa Haruni, walipokaribia mbele za Bwana, wakafa; 2 Bwana akamwambia Musa, Sema na Haruni ndugu yako, kwamba asiingie wakati wo wote katika mahali patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kiti cha rehema, kilicho juu ya sanduku, asije akafa; maana, mimi nitaonekana katika lile wingu juu ya kiti cha rehema. 3 Haruni ataingia katika patakatifu na vitu hivi; ng'ombe mume mchanga kwa sadaka ya dhambi, na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. 4 Ataivaa ile kanzu takatifu ya kitani, atakuwa na zile suruali za kitani mwilini mwake, atafungwa ule mshipi wa kitani, naye atavaa ile kofia ya kitani; hayo ndiyo mavazi matakatifu, naye ataoga mwili wake majini, na kuyavaa. 5 Kisha atatwaa mikononi mwa mkutano wa Waisraeli mbuzi waume wawili, kwa sadaka ya dhambi; na kondoo mume kwa sadaka ya kuteketezwa. 6 Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake. 7 Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za Bwana mlangoni pa hema ya kukutania. 8 Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli. 9 Na Haruni atamleta yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Bwana, na kumtoa awe sadaka ya dhambi. 10 Bali yule mbuzi aliyeangukiwa na kura kwa ajili ya Azazeli atawekwa hai mbele za Bwana ili kumfanyia upatanisho, ili kumpeleka jangwani kwa ajili ya Azazeli. 11 Na Haruni atamsongeza ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake; naye atamchinja yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake. 12 Kisha atatwaa chetezo kilichojaa makaa ya moto yatokayo katika madhabahu iliyo mbele za Bwana, na konzi mbili za uvumba mzuri uliopondwa sana, mikononi mwake, naye atauleta ndani ya pazia. 13 Kisha atatia ule uvumba juu ya moto mbele za Bwana, ili moshi wa ule uvumba ukisitiri kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, asije akafa. 14 Kisha atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na kuinyunyiza kwa kidole chake juu ya kiti cha rehema upande wa mashariki; na mbele ya kiti cha rehema atainyunyiza ile damu kwa kidole chake mara saba. 15 Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya vile vile kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema, 16 naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao. 17 Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. 18 Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. 19 Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke. 20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai. 21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari. 22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani. 23 Na Haruni ataingia katika hema ya kukutania, naye atavua mavazi yake ya kitani, aliyoyavaa alipoingia katika patakatifu, atayaacha humo; 24 naye ataosha mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na kuvaa nguo zake, na kutoka, na kusongeza sadaka ya kuteketezwa yake mwenyewe, na sadaka ya kuteketezwa ya watu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake, na kwa ajili ya watu. 25 Na mafuta ya sadaka ya dhambi atayateketeza juu ya madhabahu. 26 Na mtu yule amwachaye mbuzi wa Azazeli aende zake, ataosha nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia katika marago. 27 Na yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, na yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, ambao damu yao ililetwa ndani ifanye ukumbusho katika patakatifu, watachukuliwa nje ya marago; nao watachoma moto ngozi zao, na nyama yao, na mavi yao. 28 Na yeye awachomaye moto atafua nguo zake, na kuosha mwili wake kwa maji, na baadaye ataingia maragoni. 29 Amri hii itakuwa amri ya milele kwenu; katika mwezi wa saba, siku ya kumi ya mwezi, mtajitaabisha roho zenu, msifanye kazi ya namna yo yote, mzalia na mgeni akaaye kati yenu. 30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana. 31 Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi
Ufu. 14: 6, 7;
Ufunuo 14: 6, 7 X
6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
20:12;
Ufunuo 20:12 X
12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.
14:12;
Ufunuo 14:12
12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
22:12)
Ufunuo 22:12; X
12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

Huduma ya Hekalu la Mbinguni

Huduma ya Patakatifu ni ujumbe wa wokovu na Mungu ameitumia kutangaza injili (Ebr. 4:2)Huduma za hekalu la kale zilikuwa kielelezo hadi kwa nyakati za sasa (Ebr. 9:9, 10) Kupitia vielelezo na desturi za hekalu Mungu alikusudia kuilekeza imani ya Israeli kwa Huduma ya Mwokozi wa ulimwengu, mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Gal. 3:23, Yoh. 1:29) Patakatifu palionyesha hatua tatu za huduma ya Yesu: (1) kafara mbadala ya upatanisho, (2) upatisho wa kikuhani na (3) hukumu ya mwisho.

Kafara mbadala ya upatanisho:

kila kafara iliyotolewa mahali patakatifu iliwakilisha Kristo aliyekufa ili mwanadamu asamehewe dhambi, akafunua ukweli kwamba pasipo kumwaga damu, hakuna ondoleo la dhambi (Ebr. 9:22).Kafara hizo zilionesha kweli zifuatazo: (1) Hukumu ya Mungu dhidi ya dhambi, kwamba mshahara wa dhambi ni mauti (Rum. 6:23). (2)Kifo cha Yesu ni badala ya kifo cha mwanadamu “ameweka juu yake maovu yetu yote (Isa.53:6; 1 Kor. 15:3) 3)Mungu ndiye mtoaji wa kafara ya upatanisho (Warumi 3:24, 25;) 2Kor. 5:21;). Na kwa kupigwa kwake tuliponywa (Isa. 53:5) . Tofauti na kafara za zamani, Kristo ametolewa mara moja tu (Ebr. 9:26-28; . 10: 10, 14). Haki ya Mungu ilitimizwa (Rum. 5:18).

Kuhani Mpatanishaji:

Ikiwa kafara ndiyo iliyoondoa dhambi, kwa nini uwepo wa Kuhani ulikuwa muhimu? Uwepo wake ulionyesha hitaji la kuwapo mpatanishi baina ya mdhambi na Mungu Mtakatifu. Mpatanishi ni mmoja tu, mwanadamu Kristo Yesu (1 Tim. 2:5).

1. Mpatanishinakipatanisho:

Kunyunyiza damu wakati wa huduma ya kuhani ilikuwa kuleta upatanisho (Law. 4:35). Ukuhani wa kale unadhihirisha kile Yesu akifanyacho kwenye hekalu la Mungu (Ebr. 8:1, 2). Yesu anaweza kuwaokoa kabisa wamjiao (Ebr. 7:25). Hivyo twahimizwa kumwendea kwa ujasiri (Ebr. 4:16).

2.Huduma katika Patakatifu:

Inaweza ikasemwa ilijumuisha kuingilia kati, msamaha, upatanisho na kurejesha. Mdhambi anaweza kuunganishwa na Mungu (Efe. 2:18;Ebr. 4: 14-16;7:25; 9:24; 10:19-22) . Damu ya matoleo ya dhambi ilitumika kwa mojawapo ya mawili (a) ilinyunyizwa kwenye pembe za madhabahu ya uvumba (Law. 4:6, 7, 17, 18) au (b) iliwekwa pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa (Law. 4:25, 30) na kuhani aliruhusiwa kula nyama (Law. 6:25, 26, 30) . Kwa yote, mdhambi aliyetubu alijua dhambi zake zimeondolewa kwake. Hivyo huduma za patakatifu zinahusiana na kuhani kumpatanisha mdhambi moja moja (Ebr. 7:25) . Mdhambi anasamehewa na kuhesabiwa haki (Efe. 4:32; 1 Yoh. 1:9; 2 Kor. 5:21; Rum. 3:24; Luk. 10:20) . Akidumisha imani kwa Yesu, mdhambi hubadilika na kuakisi tabia ya kimbingu (2Pet. 3:18; Gal. 5:22, 23). Hivyo huduma ya Patakatifu huleta kuhesabiwa haki na kutakaswa.

Hukumu ya Mwisho:

Matukio ya Siku ya Upatanisho yanaonyesha hatua tatu za hukumu ya mwisho ya Mungu: (1) hukumu kabla ya miaka 1000 au hukumu ya upelelezi ambayo pia hukumu kabla ya kurejea kwa Kristo (2) Hukumu wakati wa miaka 1000 na (3) hukumu ya utekelezaji haraka baada ya miaka 1000.

1. Huduma Patakatifu pa Patakatifu:

Huduma hii yahusu kutakasa hekalu na watu wa Mungu. Kwa ajili ya kutakasa hekalu, matoleo mawili yalihitajika, mbuzi kwa ajili ya Bwana na mbuzi kwa ajili ya Azazeli (Law:16:20; cf. 16:16-18. Damu ya mbuzi wa Bwana hupelekwa moja kwa moja kwenye uwepo wa Mungu yaani sanduku la agano, kwamba madai ya sheria ya Mungu yametimizwa. Mungu anayo hamu kubwa kupatanishwa na wanadamu ndiyo maana alitoa kafara ghali ya mwana wake (2Kor.5:19). Kuhani Mkuu akishafanya utakaso wa hekalu na wa watu, ndipo baadaye, akimwakilisha Kristo, huchukua dhambi zilizochafua hekalu na kuziweka kwa mbuzi anayepelekwa mbali na kambi ya watu wa Mungu. (Law. 16:16-20; 30-33).

2. Azazel:

Uchunguzi makini wa mbuzi wa Azazel huhitimisha kwamba hamwakilishi Yesu. (1) kwa sababu hakuchinjwa na pasipo hakuna ondoleo la dhambi (Ebr.9:22). (2) Hekalu lilitakaswa na mbuzi wa Bwana kabla mbuzi wa Azazeli hajaingizwa (Law.16:20); Azazeli yuko kinyume na anayempinga Bwana(Law.16:8) hivyo humwakilisha vema Shetani.

3. Hatua tofauti za hukumu:

  1. Kuondolewa dhambi Patakatifu huonyesha hukumu ya uchunguzi, kwa kuangalia majina yaliyoko kwenye kitabu cha uzima. (1Pet.4:17, 18)
  2. Kumwondosha mbuzi wa Azazeli huonyesha kifungo cha miaka 1,000 cha Shetani (Uf. 20:4; 1 Kor.6:1-3) na
  3. Kuwa na kambi safi, huwakilisha kutakaswa kwa dunia, moto utakapoharibu dhambi na wenye dhambi (Uf. 20:11-15; Mt. 25:31-46; 2 Pet.3:7-13)

Wakati wa Hukumu:

Wote Kristo na Baba wanaendesha hukumu ya uchunguzi. Kabla ya kuja duniani akiwa na utukufu, mwana wa Adamu alimjia Mzee wa Siku na kusimama mbele zake (Dan.7:13) . Tangu Yesu alipopaa (Mdo.1:9-11) , amekuwa Kuhani Mkuu akituombea (Ebr. 7:15). Lakini safari hii, anakuja kupokea ufalme (Dan.7:14).

1. Kuyoyoma kwa Huduma ya Yesu ya Kikuhani:

Danieli sura ya 8 hutuonyesha pambano baina ya wema na uovu, na hatimaye ushidi wa Mungu. Katika hii sura, huduma ya kikuhani inasimuliwa mwanzo wake hadi mwisho wake. Kondoo mume ni Ufalme wa Wamedi na Waajemi (Dan.8:3). Pembe zake mbili zaonyesha mamlaka mbili za Umedi na ile iliyoonekana zaidi, ni Uajemi (Dan.8:4) . Beberu anayeibukia magharibi ni Ufalme wa Ugiriki na pembe yake inamwakilisha mfalme wake wa kwanza, Alexander Mkuu (Dan. 8:21). Akitokea magharibi, Alexander Mkuu aliiteka Uajemi na baadaye ufalme wa Ugiriki uligawanywa kwa majemedari wake wane, Cassander, Lysimachus, Seleucus na Ptolemy (Dan.8:8, 22) . Mwisho wa Ugiriki iliyogawanyika, pembe ndogo ingekuja kuinuka (Dan.8:9). Baadhi ya wasomi wamedhani kwamba hii pembe ndogo ni Antiochus Epiphanes Mfalme wa Siria aliyetawala Palestina kwa kipindi kifupi kabla ya Yesu. Wengi, pamoja na Wanamatengenezo, wanaamini huu ni ufalme wa Rumi.

  1. Pembe ndogo ingekuwa na mamlaka tangu kuanguka ufalme wa Ugiriki hadi mwisho wa wakati, (Dan. 8:17). Ni Rumi pekee, ya kipagani na kipapa inayotimiza unabii huu.
  2. Danieli 2, 7 na 8 zinazungumzia mamlaka za dunia zinazofanana, hivyo, tafsiri ya chuma na mnyama wa kutisha bado ni Rumi ambayo kwenye sura ya 8, inaonekana kama pembe ndogo. (Dan. 8:25; cf. Dan.2:34)
  3. Umedi na Uajemi zilikuwa Kuu, lakini Rumi ilizidi (Dan. 8:4, 8, 9). Rumi pekee inatimiza unabii huu.
  4. Ni Rumi iliyopanua himaya yake hadi kusini yaani Misri (Dan.8:9)
  5. Rumi ilimpinga Mkuu wa Jeshi, ambaye ni Kristo (Dan. 8:11, 25). Rumi ya kipagani ilitaka kumwua wakati anazaliwa, na ilimsulubisha hata kuharibu hekalu lililokuwa Yerusalemu. Rumi ya Kipapa ilihafifisha huduma ya Yesu ya Ukuhani mbinguni (angalia Ebr.8:1, 2).
  6. Nguvu ingekuwa kubwa na kustawi (Dan.8:12)

2. Wakati wa Kurejeza, Kutakasa na Hukumu:

Mungu hakurusu kutoweka kwa ukweli wa huduma ya Kuhani Mkuu, Kristo Yesu. Katika kuelekea mwisho, huduma hii itainuliwa (Dan. 8:17) atakapoanza huduma ya upatanisho na hukumu ya upelelezi (Ebr. 7:25). Maono yanataja wazi wazi ni lini Kristo angeanza huduma hii. Hata nyakati za asubuhi elfu mbili na mia tatu ndipo Patakatifu patatakaswa (Dan. 8:14). Kwa kuwa inahusu nyakati za mwisho, haiwezekani, mambo ya hekalu yakahusu hekalu lililoko duniani kwa kuwa hilo liliharibiwa na Warumi mwaka 70BK. Sasa kuzielewa nyakati za asubuhi na jioni 2,300 ndiyo jukumu letu la sasa. Katika unabii, siku moja, huwakilisha mwaka moja (Eze. 4:6; Hes. 14:34). Hivyo siku 2,300 ni miaka halisi 2,300.

a) Danieli 9 inasaidia kuelewa Danieli 8:

Mungu alimwagiza malaika Gabrieli kumwelewesha Danieli (Dan.8:16) lakini ilimshtua sana Danieli kwa malaika kusitisha maelezo. “Nilifadhaishwa na maono, nami sikuweza kuyaelewa” (Dan.8:27). Kwa sababu ya kuingiliwa, Malaika Gabrieli alisubiri hadi hali iwe itengemae ndipo atoe ufafanuzi (Dan.9:23). Muda wa majuma 70 umeamriwa juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu. (Dan.9:24). Kuamriwa imetafsiriwa kutoka neno la kiebrania Chathak. Ni neno lililotumika mara moja tu katika maandiko matakatifu. Maana yake halisi ni ‘kukatwa’ au ‘kugawanywa’.

Kwa utangulizi huu sasa maelezo ya Malaika Gabrieli wazi. Kwamba miaka 490 ilikuwa ikatwe kutoka miaka 2,300. Mwaka wa kuanzia kuhesabu ni mwaka wa amri ya kujenga upya Yerusalemu. (Dan. 9:25) Amri ya mwisho kujenga ilitolewa na Artashasta - baada ya Koreshi na Dario mwaka 457KK (Dan.7:21 cf. 6:14). Miaka 490 ilikoma mwaka 34BK na hivyo miaka 2,300 kukoma 1844BK.

b) Kuelewa huduma ya Yesu ya Ukuhani Hekaluni Mbinguni:

Mwanzoni mwa karne ya 19, wakristo wengi wakiwamo Wabaptisti, Wapresbiterian, Wamethodist, Walutheri waanglikana na Waepiskopol wajifunza unabii wa Danieli sura ya 8. Wanafunzi hawa wa Biblia walitarajia tukio muhimu baada ya mwisho wa miaka 2,300. Walitabiri huenda kukawa na kutakaswa kanisa, ukombozi wa Palestina, kuanguka kwa Ufalme wa Kituruki, kukomeshwa kwa upapa na kuisafisha dunia kwa moto na kurejea kwa Kristo kwa mara ya pili. Utabiri wao haukutimia ila maumivu yaliwapata zaidi wale waliosubiri kuja kwa Yesu mara ya pili kuliko makundi mengine. Ndipo kujifunza upya juu ya hekalu kukaanza na hekalu la mbinguni kujulikana na huduma zake kueleweka.

Umuhimu katika Pambano Kuu

Kutukuzwa kwa tabia ya Mungu:

Kupitia kazi ya pembe ndogo, Shetani alithubutu kupinga mamlaka ya Mungu. Matendo ya mamlaka hiyo yamehafifisha na kukanyaga hekalu la mbinguni, ambako ndiko kiti cha enzi cha Mungu kilipo. Maono ya Danieli yanaonyesha hukumu ya upelelezi ambayo Mungu atajipatia haki na pembe ndogo kuhukumiwa, kwa nuru iliyoko msalabani. Hatimaye wote, watakubali kwamba Mungu yuko sahihi, na kwamba hawajibiki kwa kuwepo dhambi ulimwenguni. Tabia yake haitabishaniwa na utawala wake wa upendo utathibitika.

Kutukuzwa kwa watu wa Mungu:

Wakati hukumu inaipata mamlaka ya Pembe Ndogo, itawapa ijara njema watakatifu (Dan. 7:22). Hukumu hii haimpi Mungu utukufu peke yake ila na watu wake pia. Yeyote anayenikiri mbele za wanadamu, nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni (Mt. 10:32; Luk. 12:8, 9; Uf. 3:5)

Hukumu na Wokovu:

Je, hukumu ya upelelezi inahatarisha wokovu wetu? Jibu ni hapana. Tunamwamini Yesu kuwa ni mpatanishi (Rum. 8:34) na tunayo ahadi kwamba tunaye mwombezi kwa Baba. (1Yoh. 2:1). Hukumu ni muhimu kwa ajili ya ulimwengu, kwamba wataruhusiwa tu wale ambao wameongoka na ndiyo maana vitabu vinafunguliwa (Dan. 7:9, 10).

Wanadamu walio hai, wako katika makundi matatu (1) waovu, ambao wamekataa mamlaka ya Mungu (2) Waumini wa kweli wanaoamini katika kile alichowatendea Yesu na kutii amri zake na (3) Wale wanaoonekana kuwa ni waumini lakini kiukweli hawako hivyo.

Malaika ambao hawakuasi wanaweza kulitambua lile kundi la kwanza. Sasa yupi ni muumini halisi na wa uwongo? Majina ya halisi na wasio halisi yote katika kitabu cha uzima. (Luk.10:20; Wafil. 4:3; Dan. 12:1; Uf. 21:27).Kanisa lina ngano na magugu (Mt. 13:28-30). Viumbe wa Mungu hawana ujuzi wote, hawawezi kusoma mioyo. Hivyo vitabu vitashuhudia wale waliokiri imani, wakaishi sawa sawa na walivyoamini na hivyo kufungua vitabu ni muhimu. Yesu alikisema kipindi hiki kwa mfano wa mtu aliyekaguliwa akakosa vazi la arusi (Mt. 22:11). Vazi hili ni tabia safi isiyo na doa ambayo waumini watakuwa nayo (Uf. 19:8; Efe. 5:27). Wale wanaodai ni wafuasi wa Mungu lakini hawakuvikwa vazi la haki ya Kristo, watafutwa kwenye kitabu cha uzima (Angalia Kut. 32:33). Haki inayokubalika ni ile iliyo ya Kristo pekee (Wafi. 3:9) na kigezo cha miujiza auunabii hakitumiki hapa (Mt. 7:21-23). Badala ya kupora waumini uhakika wa wokovu, fundisho la hekalu, huimarisha uhakika wa wokovu kwa wote wanaoutafuta kwa makini.

Wakati wa Kuwa Tayari:

Mungu amekusudia kwamba hii habari ya wokovu kabla Yesu hajahitimisha huduma yake ya uombezi ienee duniani kote kabla Kristo hajerea. Ujumbe wa malaika wa kwanza unasema “mcheni Mungu na kumtukuza kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja (Uf. 14:7). Ujumbe huu huonya juu ya hukumu inayoendelea sasa. Kama Israeli ya zamani, tuko kwenye Siku ya Upatanisho na tunapaswa kuzitesa nafsi (Law. 23:27) . Hivyo Mungu anamwita kila mwanadamu atubu katika saa hii ya hukumu (Uf. 14:7). Huduma ya Kristo inaelekea kwenye ukomo. Haijulikani ni lini Mungu atasema inatosha: “Kesheni na kuomba kwa kuwa hamjui ni lini (Mk. 13:33). Hata kama tunaishi nyakati za kutisha, hatupaswi kutishika. “Basi iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.” (Ebr.4:14-16).

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Waebrania 4:2 X
2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.

Waebrania 9:9, 10 X
9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,

10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.

Wagalatia 3:23 X
23 Lakini kabla ya kuja ile imani tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ije ile imani itakayofunuliwa.
Yohana 1:29 X
29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
Waebrania 9:22X
22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Warumi 6:23X
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Isaya 53:6X
6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
1 Wakorintho 15:3X
3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
Warumi 3:24X
24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
2 Wakorintho 5:21X
21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Isaya 53:5X
5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Waebrania 9:26 – 28X
26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Waebrania 10:10, 14X
10 Katika mapenzi hayo mmepata utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu.14 Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.
Warumi 5:18X
18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima.
1 Timotheo 2:5X
5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
Mambo ya Walawi 4:35X
35 kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za Bwana zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.
Waebrania 8:1, 2X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Waebrania 7:25X
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 4:16X
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waefeso 2:18X
18 Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja.
Waebrania 4:14 - 16X
14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebrania 7:25X
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 9:24X
24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
Waebrania 10:19 - 22X
19 Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; 21 na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; 22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
Mambo ya Walawi 4:6, 7, 17, 18X
6 kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu na kuinyunyiza damu mbele ya Bwana mara saba, mbele ya pazia la mahali patakatifu. 7 Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya Bwana iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.17 kisha kuhani atatia kidole chake katika hiyo damu, na kuinyunyiza mbele za Bwana, mbele ya pazia mara saba. 18 Kisha nyingine katika hiyo damu ataitia katika pembe za madhabahu iliyo mbele za Bwana, iliyoko ndani ya hema ya kukutania, kisha damu yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mlangoni pa hema ya kukutania.
Mambo ya Walawi 4:25, 30X
25 Kisha kuhani atatwaa katika damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza. 30 Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu.
Mambo ya Walawi 6:25, 26, 30X
25 Nena na Haruni na wanawe, uwaambie, Amri ya hiyo sadaka ya dhambi ni hii; mahali hapo pachinjwapo sadaka ya kuteketezwa ndipo itakapochinjwa sadaka ya dhambi, mbele za Bwana; ni takatifu sana. 26 Huyo kuhani atakayeisongeza kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila; italiwa katika mahali patakatifu, katika ua wa hema ya kukutania.30 Wala haitaliwa sadaka ya dhambi yo yote, ambayo damu yake yo yote ililetwa ndani ya hema ya kukutania, ili kufanya upatanisho katika mahali patakatifu; itachomwa moto.
Waebrania 7:25X
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waefeso. 4:32X
32 tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
1 Yohana 1:9 X
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
2 Wakorintho 5:21X
21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Warumi 3:24X
24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
Luka 10:20X
20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
2 Petro 3:18X
18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
Wagalatia 5:22, 23X
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
2 Wakorintho 5:19X
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Mambo ya Walawi 16:16 - 20X
16 naye atafanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, kwa sababu ya mambo machafu ya wana wa Israeli, na kwa sababu ya makosa yao, naam, kwa ajili ya dhambi zao zote; naye atafanya vile vile kwa ajili ya hema ya kukutania, ikaayo pamoja nao katikati ya machafu yao. 17 Wala hapatakuwa na mtu katika hema ya kukutania, wakati aingiapo ili kufanya upatanisho katika patakatifu, hata atakapotoka nje, baada ya kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake, na kwa ajili ya mkutano wote wa Israeli. 18 Kisha atatoka na kuiendea madhabahu iliyo mbele za Bwana na kufanya upatanisho kwa ajili yake; atatwaa baadhi ya damu ya yule ng'ombe, na ya damu ya yule mbuzi, na kuitia juu ya pembe za madhabahu pande zote. 19 Tena atanyunyiza baadhi ya damu juu ya madhabahu kwa kidole chake mara saba, na kuitakasa, ili machafu yote ya wana wa Israeli yaitoke. 20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.
Mambo ya Walawi 16: 30 - 33X
30 Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana. 31 Ni Sabato ya raha ya makini kwenu nanyi mtajitaabisha roho zenu; ni amri ya milele. 32 Na kuhani atakayetiwa mafuta na kuwekwa wakfu badala ya baba yake, ataufanya huo upatanisho, naye atayavaa mavazi ya kitani, yaani, yale mavazi matakatifu. 33 Naye atafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya hema ya kukutania, na kwa ajili ya madhabahu; naye atafanya upatanisho kwa ajili ya makuhani, na kwa ajili ya watu wote wa kusanyiko.
Waebrania 9:22X
22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Mambo ya Walawi 16:20X
20 Naye akiisha kufanya upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu, na hema ya kukutania, na madhabahu, atamleta yule mbuzi aliye hai.
Mambo ya Walawi 16:8X
8 Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya Bwana; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.
1 Petro 4:17, 18X
17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? 18 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?
Ufunuo 20:4X
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
1 Wakorintho 6:1 - 3X
1 Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
Ufunuo 20:11 - 15X
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Mathayo 25:31 - 46X
31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; 33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. 34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. 41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; 42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; 43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama. 44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? 45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. 46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa
2 Petro 3:7-13X
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. 8 Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. 10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Danieli 7:13X
13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye.
Matendo 1:9 - 11X
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. 10 Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, 11 wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Waebrania 7:15X
15 Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;
Danieli 7:14X
14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Danieli 8:3X
3 Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho.
Danieli 8:4X
4 Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.
Danieli 8:21X
21 Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
s
Danieli 8:8, 22X
8 Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni. 22 Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.
Danieli 8:9X
9 Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.
Danieli 8:17X
17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.
Danieli 2X
1 Hata katika mwaka wa pili wa kumiliki kwake Nebukadreza, Nebukadreza aliota ndoto; na roho yake ikafadhaika, usingizi wake ukamwacha. 2 Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga, na wachawi, na wasihiri, na Wakaldayo, wapate kumweleza mfalme ndoto zake. Basi wakaingia, wakasimama mbele ya mfalme. 3 Mfalme akawaambia, Nimeota ndoto, na roho yangu imefadhaika hata niijue tafsiri yake. 4 Ndipo hao Wakaldayo wakamwambia mfalme, kwa lugha ya Kiaramu, Ee Mfalme, uishi milele; tuambie sisi watumishi wako ile ndoto, nasi tutakuonyesha tafsiri yake. 5 Mfalme akajibu, akawaambia Wakaldayo, Neno lenyewe limeniondoka; msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake, mtakatwa vipande vipande, na nyumba zenu zitafanywa jaa. 6 Bali kama mkinionyesha ile ndoto na tafsiri yake, nitawapa zawadi na thawabu na heshima nyingi; basi nionyesheni ile ndoto na tafsiri yake. 7 Wakajibu mara ya pili, wakasema, Mfalme na atuambie sisi watumishi wake ile ndoto, nasi tutamwonyesha tafsiri yake. 8 Mfalme akajibu, akasema, Najua hakika ya kuwa mnataka kupata nafasi, kwa sababu mmeona ya kuwa lile neno lenyewe limeniondoka. 9 Lakini msiponijulisha ile ndoto, iko amri moja tu iwapasayo; maana mmepatana kusema maneno ya uongo, na maneno maovu, mbele yangu, hata zamani zitakapobadilika; basi niambieni ile ndoto, nami nitajua ya kuwa mwaweza kunionyesha tafsiri yake. 10 Wakaldayo wakajibu mbele ya mfalme, wakasema, Hapana mtu duniani awezaye kulionyesha neno hili la mfalme; kwa maana hapana mfalme, wala bwana, wala liwali, aliyetaka neno kama hili kwa mganga, wala kwa mchawi, wala kwa Mkaldayo. 11 Ni neno la ajabu, hili analolitaka mfalme, wala hapana mwingine awezaye kumwonyesha mfalme neno hilo, ila miungu, wasio na kikao pamoja na wenye mwili. 12 Basi kwa hiyo mfalme akaghadhibika sana, akaona hasira nyingi, akatoa amri kuwaangamiza wenye hekima wote wa Babeli. 13 Basi ile amri ikatangazwa, na hao wenye hekima walikuwa karibu na kuuawa; watu wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauawe. 14 Ndipo Danieli kwa busara na hadhari akamjibu Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, aliyekuwa ametoka ili kuwaua wenye hekima wa Babeli; 15 alijibu, akamwambia Arioko, akida wa walinzi wa mfalme, Mbona amri hii ya mfalme ina ukali namna hii? Ndipo Arioko akamwarifu Danieli habari ile. 16 Basi Danieli akaingia, akamwomba mfalme ampe muda, kisha yeye atamwonyesha mfalme tafsiri ile. 17 Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake, akawapasha habari kina Hanania, na Mishaeli, na Azaria wenzake; 18 ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo, ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli. 19 Ndipo Danieli alipofunuliwa siri hiyo katika njozi ya usiku. Basi Danieli akamhimidi Mungu wa mbinguni. 20 Danieli akajibu, akasema, Na lihimidiwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na uweza ni wake. 21 Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa; 22 yeye hufunua mambo ya fumbo na ya siri; huyajua yaliyo gizani, na nuru hukaa kwake. 23 Nakushukuru, nakuhimidi, Ee Mungu wa baba zangu, uliyenipa hekima na uwezo, ukanijulisha hayo tuliyotaka kwako; maana umetujulisha neno lile la mfalme. 24 Basi Danieli akaenda kwa Arioko, aliyewekwa na mfalme kuwaangamiza wenye hekima wa Babeli; alikwenda akamwambia hivi, Usiwaangamize wenye hekima wa Babeli; niingize mimi mbele ya mfalme, nami nitamwonyesha mfalme ile tafsiri. 25 Ndipo Arioko akamwingiza Danieli mbele ya mfalme kwa haraka, akamwambia hivi, Nimemwona mtu wa hao wana wa Yuda waliohamishwa, atakayemjulisha mfalme ile tafsiri. 26 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, aliyekuwa akiitwa Belteshaza, Je! Waweza kunijulisha ile ndoto niliyoiona, na tafsiri yake. 27 Danieli akajibu mbele ya mfalme, akasema, Ile siri aliyoiuliza mfalme, wenye hekima hawawezi kumfunulia mfalme; wala wachawi, wala waganga, wala wanajimu; 28 lakini yuko Mungu mbinguni afunuaye siri, naye amemjulisha mfalme Nebukadreza mambo yatakayokuwa siku za mwisho. Ndoto yako, na njozi za kichwa chako ulizoziona kitandani pako, ni hizi; 29 Wewe, Ee mfalme, mawazo yako yaliingia moyoni mwako kitandani pako ya mambo yatakayokuwa halafu; na yeye afunuaye siri amekujulisha mambo yatakayokuwa. 30 Lakini mimi, sikufunuliwa siri hii kwa sababu ya hekima iwayo yote niliyo nayo zaidi ya watu wengine walio hai, bali kusudi mfalme afunuliwe ile tafsiri, nawe upate kujua mawazo ya moyo wako. 31 Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. 32 Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; 33 miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. 34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. 35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote. 36 Hii ndiyo ile ndoto, nasi tutaihubiri tafsiri yake mbele ya mfalme. 37 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; 38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu. 39 Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. 40 Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. 41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. 42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. 43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo. 44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. 45 Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti. 46 Ndipo Nebukadreza, mfalme, akaanguka kifudifudi, akamsujudia Danieli, akatoa amri wamtolee Danieli sadaka na uvumba. 47 Mfalme akajibu, akamwambia Danieli, Hakika Mungu wenu ndiye Mungu wa miungu, na Bwana wa wafalme, awezaye kufumbua siri, kwa kuwa wewe uliweza kuifumbua siri hii. 48 Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya uliwali wote wa Babeli, na kuwa liwali mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli. 49 Tena, Danieli akamwomba mfalme, naye akawaweka Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya uliwali wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi katika lango la mfalme.
Danieli 7X
1 Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza, mfalme wa Babeli, Danieli aliona ndoto, na maono ya kichwa chake, kitandani mwake; basi akaiandika ndoto, akatoa habari ya jumla ya mambo hayo. 2 Danieli akanena, akisema, Naliona katika maono yangu wakati wa usiku; na tazama, hizo pepo nne za mbinguni zilivuma kwa nguvu juu ya bahari kubwa. 3 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. 4 Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu. 5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele. 6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka. 7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi. 8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu. 9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. 11 Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. 12 Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; walakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira. 13 Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. 14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. 15 Basi, mimi Danieli, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha. 16 Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo. 17 Wanyama hao wakubwa walio wanne ni wafalme wanne watakaotokea duniani. 18 Lakini watakatifu wake Aliye juu wataupokea ufalme, na kuumiliki huo ufalme milele, naam hata milele na milele. 19 Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; 20 na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. 21 Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; 22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme. 23 Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. 24 Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. 25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati. 26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele. 27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. 28 Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.
Danieli 8X
1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya hayo yaliyonitokea hapo kwanza. 2 Nami naliona katika maono; ilitukia, nilipoona, nalikuwako huko Shushani ngomeni, katika wilaya ya Elamu; nikaona katika maono, nami nalikuwa karibu na mto Ulai. 3 Ndipo nikainua macho yangu nikaona, na tazama, mbele ya mto alisimama kondoo mume, mwenye pembe mbili; na pembe zile mbili zilikuwa ndefu; lakini moja ilikuwa ndefu kuliko ya pili, na ile iliyokuwa ndefu zaidi ilizuka mwisho. 4 Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake. 5 Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake. 6 Naye akamwendea huyo kondoo mume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake. 7 Nikamwona akimkaribia kondoo mume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo mume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo mume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyaga-kanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo mume katika mkono wake. 8 Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni. 9 Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri. 10 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga. 11 Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. 12 Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. 13 Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa. 15 Ikawa mimi, naam, mimi Danieli, nilipoyaona maono hayo, nalitafuta kuyafahamu, na tazama, alisimama mbele yangu mmoja mfano wa mwanadamu. 16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya. 17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho. 18 Basi alipokuwa akisema nami, nalishikwa na usingizi mzito na uso wangu uliielekea nchi; lakini alinigusa, akanisimamisha wima. 19 Akaniambia, Tazama, nitakujulisha yatakayokuwa wakati wa mwisho wa ghadhabu; maana, ni ya wakati wa mwisho ulioamriwa. 20 Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi. 21 Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. 22 Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake. 23 Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama. 24 Na nguvu zake zitakuwa nyingi mno, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe; naye ataharibu kiasi cha kustaajabisha watu, na kufanikiwa, na kutenda apendavyo; naye atawaangamiza hao walio hodari na watu watakatifu. 25 Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono. 26 Na maono ya hizo nyakati za jioni na asubuhi yaliyosemwa ni kweli; lakini wewe yafunike maono hayo; maana ni ya wakati ujao baada ya siku nyingi. 27 Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.
Danieli 8:25X
25 Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.
Danieli 2:34X
34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.
Danieli 8:4, 8, 9X
4 Nikamwona huyo kondoo mume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama ye yote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama ye yote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake. 8 Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni. 9 Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.
Danieli 8:9X
9 Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.
Danieli 8:11, 25X
11 Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini.25 Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.
Waebrania 8:1, 2X
1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu..
Danieli 8:12X
12 Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa.
Danieli 8:17X
17 Basi alipakaribia mahali niliposimama; nami naliogopa alipokaribia, nikaanguka kifudifudi; lakini aliniambia, Fahamu, Ee mwanadamu, kwa maana maono haya ni ya wakati wa mwisho.
Waebrania 7:25X
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Danieli 8:14X
14 Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.
Ezekieli 4:6X
6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.
Hesabu 14:34X
34 Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.
Danieli 8:16X
16 Nikasikia sauti ya mwanadamu katikati ya mto Ulai, iliyoita na kusema, Gabrieli, mfahamishe mtu huyu maono haya.
Danieli 8:27X
27 Na mimi, Danieli, nikazimia, nikaugua siku kadha wa kadha; kisha nikaondoka, nikatenda shughuli za mfalme; nami naliyastajabia yale maono, ila hakuna aliyeyafahamu.
Danieli 9:23X
23 Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari; maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii, na kuyafahamu maono haya.
Danieli 9:24X
24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Danieli 9:25X
25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Danieli 7:21X
21 Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;
Danieli 6:14X
14 Basi mfalme aliposikia maneno haya alikasirika sana, akakaza moyo wake ili kumponya Danieli; akajitaabisha kumwokoa hata jua likachwa.
Danieli 7:22X
22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
Mathayo 10:32X
32 Basi, kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni.
Luka 12:8, 9X
8 Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; 9 na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
Ufunuo 3:5X
5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.
Warumi 8:34X
34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
1 Yohana 2:1X
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Danieli 7:9, 10X
9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
Luka 10:20X
20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Wafilipi 4:3X
3 Naam, nataka na wewe pia, mjoli wa kweli, uwasaidie wanawake hao; kwa maana waliishindania Injili pamoja nami, na Klementi naye, na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.
Danieli 12:1X
1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
Ufunuo 21:27X
27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Mathayo 13:28-30X
28 Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye? 29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. 30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Mathayo 22:11X
11 Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.
Ufunuo 19:8X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Waefeso 5:27X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Kutoka 32:33X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Kutoka 32:33X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Mathayo 7:21 - 23X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Ufunuo 14:7X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Mambo ya Walawi 23:27X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Mambo ya Walawi 23:27X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Marko 13:33X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.
Waebraniam 4:14 - 16X
1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.