Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya nguvu za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, fyraha, na uhakika wa upendo wake.Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu. Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa ajili ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho.” (Zab.1:1, 2; 23:4; 77:11, 12; Kol.1:13, 14; 2:6, 14, 15; Luk.10:17-20; Efe. 5:19, 20; 6:12-18; 1Thes.5:23; 2Pet.2:9; 3:18; 2Kor.3:17, 18; Filp.3:7-14;
1Thes.5:16-18; Mt.20:25-28; Yoh.20:21; Gal.5:22-25; Rum.8:38, 39; 1Yoh. 4:4; Ebr.10:25)
Kuzaliwa huleta furaha. Mbegu ikiota humfurahisha mkulima, mtoto akizaliwa hufurahisha wazazi hata kumfanya mama asahau uchungu aliokuwa nao. Taifa likizaliwa, nako huleta furaha na watu waweza kuandamana wakipunga mikono, bendera au matawi kushangilia kuanza kwa taifa. Furaha zote zilizotajwa, zitayeyuka ikiwa mtoto hatakua, miche haitaendelea kukua au taifa kuvia. Kukua ni jambo muhimu kwa mambo ya kiroho pia.
Maisha Huanza na Kifo
Kanuni ya msingi kuhusiana na maisha ya kikristo ni kwamba maisha huanza na kifo, naam matukio mawili ya kifo. Kwanza, kifo cha Yesu msalabani kimewezesha maisha mapya kuanza (Kol. 1:13, 14), maisha huru kwa hukumu ya dhambi (Rum. 8:1) na huru kutokana na adhabu ya kifo (Rum. 6:23) na kuleta suluhisho na Mungu. Hivyo maisha mapya kuanza. Pili, kifo cha nafsi ambacho hutufanya tuweze kupokea maisha ya Kristo.
Kifo cha Yesu
Msalaba ndiyo nguzo ya mpango wa Mungu wa wokovu. Pasipo msalaba, Shetani asingeshindwa. Damu ya Yesu hutusafisha na udhalimu wote (1Yoh. 1:7). Vurugu zote alizotenda Shetani ilikuwa kumchokoza Yesu asitekeleze kile ambacho Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa. Kwa kukubali kufa, Yesu alimvua Shetani enzi na mamlaka (Wafil. 2:15). Yule ambaye alitaka kufanana naye aliye juu (Isa.14:14) sasa ameabika kwa wale ambao wamehama kwenye nguvu za giza na kuingia kwenye ufalme wa Mwana wa Mungu (Kol. 1:13). Hivyo msalaba wa Kristo: -
Ni njia ambayo msamaha wa dhambi unawezeshwa (Kol. 2:13). Ni uthibitisho kwamba ulimwengu umepatanishwa (2Kor. 2:18). Ni ushahidi wa kuwezekana maisha ya ushindi dhidi ya miili na nia zetu (Rum. 6:12) na kufanywa wana na binti za Mungu (Rum. 8:14). Ni uthibitisho kwamba dunia hii ya dhambi, siku moja itasafishwa (Uf. 21:1).
Katika kila hatua ya ngazi ya wokovu na ushindi, tunaona ushahidi wa kutimia unabii wa Yesu kwamba alimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama umeme (Luk. 10:18). Damu ya Yesu ilimwangika kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi (Mt. 26:28).
Gharama ya kuokoa kutoka dhambini ni kubwa mno yaani pasipo damu ya Yesu, hakuna ondoleo (1Pet. 1:19). Tulipokuwa hatuna nguvu, Yesu alikufa kwa ajili yetu (Rum. 5:6, 8). Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyotuondolea dhambi. (Zab. 103:12). Ni kifo cha Yesu, ndicho kinatupa kuonja uzuri wa maisha mapya (Efe. 2:14-16).
Kifo cha Nafsi
Jambo la pili muhimu katika upya wa maisha ya kikristo ni kuifia nafsi. Muumini huwa amesulubiwa pamoja na Kristo…si yeye aliye hai bali Kristo (Wagal. 2:20-21). Kanuni ya Yesu juu ya maisha mapya, ni kwamba chembe ya ngano lazima ife, ndipo izae (Yoh. 12:24). Lazima liwepo badiliko kamilifu (2Kor.5:17). Kielelezo cha ubatizo ni kwamba tunakufa, tunazikwa na kufufuka katika upya wa uzima (Rum.6:3,4). Kipo kitu kinachotokea mtu anapomkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi wake. Woga huondoka badala yake mtu anakuwa jasiri, kutokuamini kunapisha imani, wivu na kijicho hupisha upendo. Ubinafsi hutoweka na kupisha kujaliana. Dhambi hukosa nafasi kwenye maisha ya mtu. Utu wa kale huwa umevuliwa kabisa (Kol. 3:9,10). Yesu alisisitiza “mtu awaye yote atakaye kunifuata, na ajikane mwenyewe ajitwike msalaba wake anifutate(Mt. 16:24). Hivyo wito wetu ni kuufuata msalaba, ili hekima yetu isiwe ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu (1Kor. 2:5).
Kuishi Maisha Mapya
Jambo la tatu muhimu katika maisha ya kikristo ni kuishi maisha mapya. Kuko kutokuelewa kwa maisha ya kikristo kwamba wokovu umetolewa bure na wengine huishia hapo. Ni kweli tumekombolewa kwa damu kwa wingi wa rehema zake (Efe.1:7) na kwamba tumeokolewa kwa neema, mtu yeyote asije akajisifu (Efe. 2:8, 9). Ndiyo wokovu ni bure, lakini neema ya bure, haimaniishi neema isiyo na gharama. Neema isiyo na gharama ingelazimu kuhubiri msamaha pasipo kutubu, ubatizo pasipo nidhamu ya kanisa au kushiriki meza ya Bwana pasipo kuungama. Neema isiyo na gharama haina ufuasi/uanafunzi, haina msalaba, haina Yesu aishiye ndani yetu! Paulo anasema alikuwa alivyo kwa kuwa neema ilifanya kazi ndani yake (1Kor. 15:10). Hivyo anawasihi wakristo wasipokee neema bure (2Kor. 6:1).
Viashiria vya Kukua Katika Kristo
1. Maisha ya Kiroho
Yesu alimwambia Nikodemo, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho hatauona ufalme wa Mungu (Yoh. 3:5). Pasipo Roho, maisha ya kikristo hayawezekani. Ni Roho wa kweli (Yoh.14:17) atuongozaye katika kweli (Yoh.16:13), ahakikishiye dhambi, haki na hukumu (Yoh.16:7,8). Roho hutufanya sisi kuwa wana wa Mungu (Rum. 8:14) na kwa Roho Kristo hukaa nasi (1Yoh.3:24). Roho akikaa ndani yetu, twabadilika, tunakuwa viumbe vipya, vilivyopatanishwa na Mungu, tuliokombolewa na kuwekwa huru kwa kutengwa na dhambi ili tukue katika haki (Rum. 8:1-16). Tutaakisi taswira ya Yesu kutoka utukufu hadi utukufu (2Kor.3:17, 18). Roho anatufanya warithi pamoja na Kristo kwa mema hata kwa kuteswa pamoja naye (Rum.8:17). Tunalindwa kwenye dunia hii kwa ombi la Yesu kwamba pamoja na kwamba tuko ulimwenguni, sisi siyo wa ulimwengu (Wafil. 3:20). Maisha yenye nguvu ya roho yatakataa matendo ya mwili (Gal. 5:19-21) na kujawa na tunda la Roho (Gal. 5:22, 23)
2. Maisha ya upendo na umoja
Maisha ya kikristo hukomesha kutengwa na Mungu kulikoletwa na dhambi (Isa.59:1, 2). Mungu ametupatanisha kwa njia ya Kristo (2Kor. 5:18). Katika kukombolewa, huzaliwa jumuia ya waliokombolewa ambao Yesu aliomba wawe na umoja (Yoh. 17:20, 21). Mifarakano iliyoleta kubaguana yalifishwa kwa kupokea maisha mapya (Efe. 2:11-16). Amri ya kipekee katika Injili ya upendo, amri mpya (Yoh. 13:34) hutawala. Ni amri hiyo ambayo torati yote na manabii husimamia (Mt. 22:36-40). Tunapompenda Mungu, upendano wetu sisi kwa sisi huongezeka.
3. Maisha ya Kujifunza Biblia
Chakula ni muhimu kwa ajili ya kukua. Mwanadamu hataishi kwa mkate peke yake isipokuwa kwa neno la Mungu (Mt.4:4). Mtunga Zaburi alisema, moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi (Zab.119:12). Neno lina nguvu kutuwezesha kutambua mema na mabaya (Ebr. 4:12) na hivyo tutayatumia maneno yenye pumzi ya Mungu kuonyana na kutiana moyo (2Tim. 3:16, 17).
4. Maisha ya Maombi
Mungu huzungumza nasi kupitia nasi kwa njia ya neno lake. Sisi huwa tunamwendea kwa njia ya maombi. Tunahimizwa kuomba kwa ajili yetu na kwa ajili ya watakatifu (Efe. 6:18). Twaweza kukosea kwa kuonyesha kiburi cha sala kama Farisayo (Luk. 18:11) lakini sala ni jambo la unyenyekevu. Mifano ya maombi ni mingi katika Biblia. Yesu (Mk. 1:35) Daudi (Zab. 88:1,2) na Danieli (Dan. 6:10). Maombi huwa hayana kikomo (1Thes.5:17).
5. Maisha yenye Matunda
Kwa matunda yao, Yesu alisema, mtawatambua (Mt. 7:20). Ni kweli twaokolewa kwa neema wala siyo matashi yetu (Efe. 2:8-10, Yoh. 3:16). Lakini hatuokolewi ili tutende yanayotupendeza ila tutende yanayompendeza Mungu. Matendo mema ni matokeo ya imani itendayo kazi kwa kuwa yasipokuwapo, imani imekufa (Yak. 2:17). Yesu anapozungumzia mahusiano yake na Baba yake anasema amezitii amri za Baba yake (Yoh. 15:10, 12) na anatazamia nasi tutakaa ndani yake (Yoh. 15:4) na tutampenda, hata kumtii (Yoh.14:15).
6. Maisha ya Mapambano ya Kiroho
Maisha ya kikristo siyo rahisi wala mepesi. Tuko kwenye vita halisi ya hatari. Hatupambani juu ya mwili na nyama bali nguvu na mamlaka ya giza (Efe.6:12, 13). Kwenye vita hii, malaika wa giza hutunyemelea kutupinga kama vile malaika wa nuru wanavyotulinda (Zab. 34:7, (91:11, 12, Mdo. 5:19, 20, Ebr.1:14, 12:22). Biblia husema shetani na malaika zake wanakasirikia Kanisa (Uf. 12:17), na kama simba angurumaye, huzunguka akitafuta mtu ammeze (1Pet.5:8, 9). Maisha ya mkristo yamejaa mitego na ndiyo maana Paulo anatumia maneno magumu “simama” “vaeni silaha!”(Efe.6:12, 13). Mungu hajatuacha peke yetu kwa kuwa ametupatia ushindi katika Kristo (1Kor.15:57). Hivyo twapaswa kudumu katika vita tukiwa tumevaa silaha na kuomba (Efe. 6:13-18).
7. Maisha ya Kuabudu, Kushuhudia na Matumaini
Kukua kikristo hakutokei kwenye utupu, kwahitajika waumini wenye imani moja kuimarika na jamii isiyomwamini Yesu ili kuimarisha imani. Baada ya Yesu kupaa, kanisa la mitume lilishiriki pamoja ibada, ushirika, kushuhudia na kujifunza maandiko (Mdo. 2:42-47, (5:41, 42, (6:7). Hivyo mtume alishauri tuendelee kukusanyika kwa ibada (Ebr. 10:24, 25). Kukua kikristo kunahitajika katika huduma (Mt.20:25-28). Kama Baba alivyomtuma Yesu, nasi tumetumwa (Yoh.20:21). Maisha ya kukua ni yenye kushuhudia daima (Mdo. 1:8). Tunakaza mwendo kwa ili kufikia mede katika Kristo (Wafil. 3:12-14). Mungu hututakasa, hutuhifadhi bila lawama hata wakati wa kuja kwake Yesu. (1Thes. 5:23).
Zaburi 1:1, 2X 1 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
Zaburi 23:4X 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Zaburi 77:11, 12X 11 Nitayakumbuka matendo ya Bwana; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. 12 Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.
Wakolosai 1:13, 14X 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Wakolosai 2:6, 14, 15X 6 Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; 14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; 15 akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.
Luka 10:17-20X 17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. 18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. 19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. 20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.
Waefeso 5:19, 20X 19 mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu; 20 na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Waefeso 6:12-18X 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
1 Wathesalonike 5:23X 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Petro 2:9X 9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
2 Petro 3:18X 18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
2 Wakorintho 3:17, 18X 17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Wafilipi 3:7-14X 7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. 8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; 9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani; 10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu. 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
1 Wathesalonike 5:16-18X 16 Furahini siku zote; 17 ombeni bila kukoma; 18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
Mathayo 20:25-28X 25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; 28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Yohana 20:21X 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
Wagalatia 5:22-25X 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Warumi 8:38, 39X 38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Yohana 4:4X 4 Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.
Waebrania 10:25X 25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Wakolosai 1:13, 14X 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Warumi 8:1X 1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Warumi 6:23X 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Yohana 1:7X 7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Wafilipi 2:15X 15 mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Isaya 14:14X 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
Wakolosai 1:13X 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Wakolosai 2:13X 13 Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;
2 Wakorintho 2:18X 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Warumi 6:12X 12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
Warumi 8:14X 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Ufunuo 21:1X 1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Mathayo 26:28X 28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
1 Petro 1:19X 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Warumi 5:6, 8X 8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Zaburi 103:12X 12 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.
Waefeso 2:14-16X 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. 15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. 16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Wagalatia 2:20-21X 20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu. 21 Siibatili neema ya Mungu; maana, ikiwa haki hupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure.
Yohana 12:24X 24 Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.
2 Wakorintho 5:17X 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Warumi 6:3,4X 3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Wakolosai 3:9,10X 9 Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake; 10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba.
Mathayo 16:24X 24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.
Waefeso 1:7X 7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Waefeso 2:8, 9X 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
1 Wakorintho 15:10X 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami.
2 Wakorintho 6:1X 1 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure.
Yohana 3:5X 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
1
Yohana 14:17X 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 16:13X 13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 16:7,8X 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Warumi 8:14X 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
1 Yohana 3:24X 24 Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa.
Warumi 8:1-16X 1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. 5 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. 7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. 10 Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. 12 Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, 13 kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
2 Wakorintho 3:17, 18X 17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Warumi 8:17X 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Wafilipi 3:20X 20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Wagalatia 5:19-21X 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wagalatia 5:22, 23X 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Isaya 59:1, 2X 1 Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; 2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
2 Wakorintho 5:18X 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Yohana 17:20, 21X 20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Yohana 2:11-16X 11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. 12 Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi. 13 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu. 14 Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng'ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi. 15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng'ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
Yohana 13:34X 34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Mathayo 22:36-40X 36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Mathayo 4:4X 4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Zaburi 119:12X 12 Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako.
Waebrania 4:12X 12 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
2 Timotheo 3:16, 17X 16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Waefeso 6:18X 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Luka 18:1X 1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
Marko 1:35X 35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Zaburi 88:1,2X 1 Ee Bwana, Mungu wa wokovu wangu Mchana na usiku nimelia mbele zako. 2 Maombi yangu yafike mbele zako, Uutegee ukelele wangu sikio lako.
Daniel 6:10X 10 Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu;) akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Mathayo 7:20X 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Waefeso 2:8-10X 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Yohana 3:16X 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yakobo 2:17X 17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
Yohana 15:10, 12X 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Yohana 15:4X 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Waefeso 6:12, 13X 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Zaburi 34:7X 7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
Zaburi 91:11, 12X 11 Kwa kuwa atakuagizia malaika zake Wakulinde katika njia zako zote. 12 Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
Matendo 5:19, 20X 19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema, 20 Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya Uzima huu.
Waebrania 1:14X 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Waebrania 12:22X 22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
Ufunuo 12:17X 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
1 Petro 5:8,9X 8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 9 Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.
Waefeso 6:12, 13X 12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
1 Wakorintho 15:57X 57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Waefeso 6:13-18X 13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. 14 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, 15 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; 16 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. 17 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; 18 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Matendo 2:42-47X 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Matendo 5:41, 42X 41 Nao wakatoka katika ile baraza, wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuaibishwa kwa ajili ya Jina hilo. 42 Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo.
Matendo 6:7X 7 Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Waebrania 10:24, 25X 24 tukaangaliane sisi kwa sisi na kuhimizana katika upendo na kazi nzuri; 25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Mathayo 20:25-28X 25 Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. 26 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; 27 na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; 28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Yohana 20:21X 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi.
Matendo 1:8X 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Wafilipi 3:12-14X 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
1 Wathesalonike 5:23X 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.