Milenia Na Mwisho Wa Dhambi

Utangulizi


Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati ya ufufuo wa kwanza na pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa, dunia itakuwa ukiwa na utupu, bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika zake. Mwishowe kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni. Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na shetani na malika zake watauzingira mji, Lakini moto kutoka mbinguni utawateketeza ili kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele.” (Ufu. 20; 1Kor. 6:2-3, Yer. 4:23-26, Ufu.21:1-5; Mal 4:1; Eze.28:18-19)

Katika historia yote, wamekuwako watu wanaodai kwamba kuzimu kunatisha, wakiwajengea watu hofu ili kwa hofu hiyo watu wamwabudu Mungu. Je, ni Mungu wa namna gani wanayemtangaza? Hivi, hatimaye Mungu ataikomeshaje dhambi. Nini kitamtokea Shetani. Nini kitaifanya dhambi isijiinue tena? Hivi, inakuwaje Mungu mwenye haki awe pia Mungu mwenye upendo?

Matukio Kabla ya Miaka 1,000

Kipindi cha miaka 1,000 ambacho Ufunuo sura ya 20 huzungumzia, ushawishi wa Shetani katika dunia utazuiliwa na Kristo atatawala na watakatifu wake. (Ufu.20:1-4)

Kuja kwa Yesu Mara ya Pili

Ufunuo 19 na 20 hufuatana, hakuna palipoachana. Huelezea kuja kwa Yesu mara ya pili (Uf.19:11 – 21) na papo kwa hapo huingiza miaka 1,000, ikimaanisha miaka 1,000 huanza Yesu akirudi mara ya pili. Kabla Yesu hajarudi, mamlaka tatu zitapinga kazi ya Kristo ambazo ni joka, mnyama na nabii wa uwongo (Uf. 16:13). Kuja kwa Yesu kutaangamiza washirika wawili (Uf.19:19, 20). Mshirika mwingine atashughulikiwa kwenye miaka 1,000. Ufalme wa Yesu hautakuwa wa ubia (Dan.2:44).

Ufufuo wa Kwanza

Ufu. 20:6 “Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri aliye na sehemu katika ufufuo huu.

Watakatifu watanyakuliwa kwenda mbinguni

Baada ya ufufuo wa wenye haki: watakatifu waliofufuliwa na watakaokutwa hai watanyakuliwa kumlaki BWANA hewani (1 Thes. 4:17) Pia, watakaribishwa mbinguni (Yoh.14:2, 3)

Maadui wa Kristo watakufa

Uf.19:21 Watauawa kwa upanga utokao kwa yule aketiye juu ya kiti kile cha enzi. Litakuwa ni jambo la ghafla kwao - kama ilivyokuwa siku za Nuhu, na siku za Sodoma (Mt.24:37-39, Luk. 17:29). BWANA anakuja kutoka mahali pake.. ili kuwaadhibu wakaao duniani… (Isa.26:21).

Nchi itakuwa ukiwa

Kwa kuwa watakatifu watakuwa wamenyakuliwa na waovu kuangamizwa, dunia itabaki kwa kipindi haina wanadamu walio wakazi ndani yake. Yer.4:23-25. Yeremia anatumia neno linalopatikana kwenye Mwa.1:2 dunia ilikuwa utupu.

Shetani atafungwa

Kama mbuzi wa Azazeli alivyowekewa dhambi za Waisraeli, (Law. 16:21), alipelekwa porini (Law. 16:22). Shetani atafungwa kuzimu (Uf. 20:2, 3) yaani kwenye dunia iliyoharibiwa kwa kupondwa kwa mapigo saba (Uf.16:18 – 21).

Matukio Katika Miaka 1,000

Kristo mbinguni pamoja na Watakatifu

Watakatifu watakuwa na Kristo mbinguni. Kama Musa na Waisraeli wa zamani, watamshukuru Mungu kwa ukombozi nao wataimba wimbo wa Musa na Mwanakondoo Uf.15:2, 3.

Watakatifu watatawala pamoja na Kristo

Watakatifu watakuwa mbinguni wakitawala na kupewa hukumu (Uf. 20:4). Ashindaye… atapewa mamlaka juu ya mataifa. (Uf.2:26). Watakatifu watakuwa na ufalme, ukuu, mamlaka chini ya mbingu zote (Dan. 7:27).

Hukumu ya Waovu

Ufu. 20:4 Watakatifu juu ya viti vya enzi wakihukumu. Shetani na malaika zake watahukumiwa (2 Pet. 2:4, Yuda 6). Watakatifu watahukumu malaika kitatimia (1 Kor. 6: 1 – 3). Hukumu wanayofanya watakatifu siyo kuamua nani ataokolewa au kupotea. Hiyo itakuwa imefanywa na Mungu. Wao wataangalia kwa nini wanadamu wengine walinyimwa uzima na hilo litajenga imani kwa mamlaka ya Mungu katika mioyo yao.

Shetani atapata fursa kutafakari

Akiwa hana wa kudanganya, Shetani atanyong’onyea. Atatafakari chanzo cha dhambi na matokeo yake na sehemu aliyofanya kwenye shindano la wema na uovu. Atatafakari kwa hofu adhabu inayomstahili. Siku za mwisho Miaka 1, 000 Umilele Kristo anarejea Ufufuo wa Kwanza Ufufuo wa Pili Watakatifu wanyakuliwa Waovu waangamizwa (wabaki makaburini) Shetani afungwa Dunia inabaki ukiwa (mapigo saba, tetemeko la Yesu kurudi mara ya pili) Watakatifu watawala na Kristo miaka elfu Wanachofanya ni kupitia hukumu Dunia inabaki ukiwa miaka elfu Yesu , watakatifu pamoja na mji washuka Waovu waliokufa wanafufuliwa Shetani anafunguliwa apanga kushambulia mji mtakatifu Hukumu ya waovu yatekelezwa (Shetani, waovu, matokeo ya dhambi vyaangamizwa Dunia yafanywa upya kama maskani ya milele ya Watakatifu

Matukio Baada ya Miaka 1,000

Baada ya miaka 1,000, waovu watafufuliwa na Shetani atafunguliwa kutoka kwenye kifungo chake (Uf.20:5, 7). Atawadanganya kwamba waweza kuiteka kambi ya watakatifu ambayo itakuwa imeshuka pamoja na Yesu wakati huu (Uf.20:9).

Kristo, watakatifu pamoja na mji mtakatifu washuka

Mji wa Yerusalemu mpya utashuka (Uf. 21:2). Yesu atatengeneza bonde, ambako mji huo utashukia (Zek. 14:4). Atakuwa mfalme wa dunia yote (Zek. 14:9)

Ufufuo wa waovu

Walioko makaburini wataisikia sauti (Yoh. 5:28) na kwa kuwa watakatifu walikwisha fufuliwa ufufuo wa kwanza wa uzima, safari hii ni ufufuo wa hukumu (Yoh.5:29). Ufufuo wa wafu waliosalia (Uf.20:5).

Kifungo cha Shetani kinakoma

Ufufuo wa waovu mwisho wa miaka 1,000 utamfungulia Shetani. (Uf.20:3). Atathubutu kudanganya mataifa kwenye pembe nne za nchi (Uf.20:8).

Jiji litazingirwa

Katika uwongo wake wa mwisho, Shetani atawatia moyo waovu kwamba wanaweza kuuteka ufalme wa Mungu kwa nguvu. (Uf.20:8, 9). Kutaka kumpindua Mungu, kutafanya tabia ya Shetani kudhihirika kwa wote.

Kiti kikubwa cheupe cha enzi

Yohana anasema aliona kiti kikubwa cheupe cha enzi ambako Mungu atahukumu (Uf.20:11-15). Hapa ndipo Yesu aliposema watashangaa kumwona Ibrahimu, Isaka, Yakobo na manabii katika ufalme lakini wenyewe wametupwa nje (Luk. 13:28). Tutasimama wote mbele ya kiti cha hukumu (Rum. 14:10). Wema kwa waovu tutamsujudia Mungu (Wafil.2:10, 11, Isa.45:22, 23)

Shetani na waovu wataangamizwa

Baada ya kusomewa hukumu, Shetani, malaika zake na waovu watapata ijara yao. (Uf.20:9, 12-15). Nje ya mji kunayeyuka na kuonekana ziwa la moto (2 Pet.3:7), siku ya kisasi cha Mungu (Isa.34:8) atakayofanya kitendo cha ajabu (Isa.28:21). Kila asiyeonekana katika kitabu cha uzima alitupwa kwenye ziwa la moto (Uf.20:15). Shetani naye atatupwa kwenye ziwa la moto (Uf.20:10).

===Mwisho wa Somo===

Adhabu Ya Waovu

Mafungu kadha wa kadha ya Biblia yanaweza kumsumbua msomaji wa kawaida akadhani kwamba adhabu ya waovu yawezekana kuungua moto milele pasipo kufa. Mafungu machache ni kama yafuatayo: -

Ondokeni kwangu mliolaaniwa mwende kwenye moto wa milele.... (Mt. 25:41). Na hao watakwenda zao kuingia kwenye adhabu ya milele... (Mt.25:46). Watakapoangamizwa kwa maangamizi ya milele (2 Thes.1:9). Ziwa liwakalo moto na kiberiti (Uf.21:8). ...yeye naye atateswa kwa moto na kiberiti...na moshi wa maumivu yao hupanda juu milele hata milele. (Uf. 14:9 – 11).

Hivyo yafaa kusoma somo hili, la hukumu ya waovu ili kuondoa dhana potofu inayoweza kutokeza

Hukumu / Adhabu ya waovu inasemwaje na Biblia?

Chanzo chema kwa ajili ya kuondoa shaka juu ya wazo linaloweza kuzuka, ni Maandiko matakatifu.

Hukumu ya waovu itatekelezwa wakati ujao, siyo sasa

Wako wanaoamini kwamba mtu akifa akiwa mwovu, hutupwa jehanamu. Wengine husema kwamba waovu hupata ijara yao hapahapa wakiwa hai. Inawezekana waovu wakaadhibiwa kwa kusutwa na jamii au hata kufungwa na Serikali au mamlaka. Lakini huo siyo adhabu kwa ajili ya dhambi. Ni adhabu kwa makosa yao ya jinai tu. Dhambi ni uhalifu dhidi ya sheria ya Mungu, hivyo itapatilizwa na Mungu mwenyewe, siyo mamlaka ya kidunia.

Hata malaika waliokosea hawajapata ijara yao. Yesu alipokuwapo duniani, mapepo yalipata kuuliza, je umekuja kutuhukumu kabla ya muhula wetu? (Mt.8:29). Malaika waovu wanalindwa hata ije hukumu (2Pet. 2:4) au siku ya hukumu kuu (Yuda 9). Waovu watahukumiwa katika siku ya hukumu (2Pet.2:9).

Kinachofanya hukumu / adhabu ya waovu

  1. Waovu watakufa. Roho itendayo dhambi itakufa (Ez.18:4). Mshahara wa dhambi ni mauti (Rum.6:23). Inasisitizwa kwamba adhabu wa waovu ni mauti. Waovu wanatajwa kuwa wanastahili mauti (Rum.1:31). Mwisho wa dhambi unatajwa ni mauti (Rum. 6:21) na dhambi ikishakukomaa huzaa mauti (Yak. 1:15).
  2. Waovu wataharibiwa. Zab: 37:9, 34. Katika Ezekieli 28:16, neno kali zaidi limetumiwa, ‘kerubi ameangamizwa’.
  3. Waovu watapotea. Watapotea (Zab.37:20), watatoweka. Hawatakuwapo. (Zab.37:10 ) Watapotea usoni pa Mungu (Zab.68:2). Katika agano jipya, Yoh.3:16, inaunga mkono kuwa wasio mwamini Yesu watapotea.
  4. Waovu watachomwa moto. Msemo mkali wa kuchoma moto umejirudia rudia pia. Angalia siku inawaka kama tanuru, haitaacha shina wala tawi (Mal. 4:1). Watafungwa matita matita na kuchomwa (Mt. 13:30), magugu yatachomwa (Mt. 13:40). Petro naye anasema dunia na kazi zake zitachomwa (2 Pet.3:10). Kikomo cha mwisho cha waovu ni ziwa la moto (Uf.20:15). Hiyo ndiyo mauti ya pili (Uf.21:8).
  5. Waovu wataangamizwa. Waovu wote wataangamizwa (Zab. 145:20), Mapepo yalipata kuuliza, je umekuja kutuangamiza? (Mk. 1:24). Tena waovu wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele (2Thes.1:9). Hata Ibilisi naye ataharibiwa (Ebr.2:14)

Maelezo ya waandishi waliovuviwa kwingine walitumia misemo mikali. Kwamba siyo tu waovu watachomwa, (Uf.19:20, 21) bali pia watateketezwa (2Pet.3:10). Siyo tu wataangamizwa (Mt. 21:41, Mk. 1:24) bali pia wataangamizwa na kutengwa (Mdo. 3:23), Siyo tu watatoweshwa (Zab.104:35, Zab.37:20), bali pia watatoweshwa kwa utisho (Zab.73:19). Hivyo ndivyo Biblia isemavyo juu ya adhabu ya waovu.

Vielelezo hufafanua mwisho wa Waovu

Lugha inayoelezea hatma ya waovu iko wazi. Waovu wanafananishwa na vinavyowaka yaani makapi (Zab.1:4) mabua (Isa.40:24) na makapi yatakayoteketezwa (Mal.4:1)

Kama ilivyoangamizwa Sodoma na Gomora ndivyo itakavyokuwa kwa waovu. Miji ilipinduliwa (Kumb.29:23, Isa.13:19). Na kwamba iliangamizwa (Mw.19:29). Maangamizi yalikuwa makamilifu kwa kuwa tunasoma waliangamia wote (Luk.17:29)

Maangamizi ya Sodoma hayakuwa ya muda mrefu kwa kuwa Biblia inasema yalikuwa kama ya dakika moja (Maombolezo 4:6). Zaidi, yaliangamizwa yakabaki majivu (2Pet. 2:6). Yuda, anasema adhabu ilikuwa ya moto wa milele (Yuda 7). Hii haiwezi kumaanisha moto ambao unaowaka milele bila kwisha, kwa kuwa ile miji haiendelei kuwaka moto leo. Hivyo, moto unaosemwa hapa ni wa milele kwa matokeo yake; yaani matokeo ya maangamizi yalikuwa ya kudumu.

Je, ‘daima’ au ‘milele’ Yaweza Kumaanisha Isiyo ya Kudumu?

Matumizi ya neno daima au milele laweza kuwa na kikomo. Tutazame mafungu machache: -

Pasaka ilipaswa kuadhimishwa milele (Kut.12:17). Mtumwa aliyekubali alipaswa kumtumikia bwana wake milele (Kut. 21: 6), Mtoto Samweli alipaswa kuhudumu hekaluni milele (1Sam.1:22), Yona alikaa kwenye tumbo la samaki milele (Yon. 2:6) na ukoma ulipaswa kutomwacha Gehazi na uzao wake milele (2 Waf.5:27). Filemoni naye katika agano jipya aliombwa kukaa na Onesmo milele. (Filem. 15). Kwa hiyo ukombozi wa milele (Ebr. 9:12) na hukumu ya milele (Ebr. 6:2) ni maelezo yanayoelezea ukamilifu wa ukombozi na ukamilifu wa hukumu katika matokeo; siyo katika mchakato. (Angalia pia Uf.19:3, Uf.20:10, Uf. 14:11, Zab. 92:7). Misemo hii mikali yaweza tu kueleweka kwa mtazamo wa Isaya 34:8 – 10) “Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni. Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itakuwa lami iwakayo. Haitazimwa mchana wala usiku, moshi wake utapaa milele; tangu kizazi hata kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele”

Sababu za kukataa mateso ya milele

  1. Kwa sababu uzima wa milele ni karama kutoka kwa Mungu (Rum. 6:23). Waovu hawataona uzima (Yoh. 3:36). Hakuna muuaji aliye na uzima wa milele (1Yoh.3:15).
  2. Kwa sababu mateso ya milele yatadumisha matokeo ya dhambi, vilio, machozi na masikitiko ambavyo ni kinyume na Uf.21:4 inayosema havitakuwako.
  3. Kwa sababu kuwa na kisehemu chenye watu wanaoteseka milele kutatia doa kwenye ulimwengu wa Mungu na itaonekana Mungu hawezi kuondosha doa hilo.
  4. Kwa sababu mawazo ya watakatifu yataondoshwa kwenye tabia ya Mungu ya upendo na badala yake yataelekezwa kwenye ghadhabu ya Mungu isiyoweza kutulizwa.
  5. Kwa sababu Maandiko Matakatifu hufundisha kwamba kazi ya kafara ya Kristo ni kufutilia mbali dhambi (Ebr.9:26) kwanza katika wanadamu na baadaye katika ulimwengu. Ukamilifu wa kile ambacho kafara ya Yesu imefanya kitaonekana siyo tu kwa wanadamu waliokombolewa, bali pia katika ulimwengu ulioumbwa upya (Ef.1:14)

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Ufunuo 20X
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. 11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
1 Wakorintho 6:2-3X
2 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?
Yeremia 4:23-26X
23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. 24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. 25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. 26 Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka mbele za Bwana, na mbele za hasira yake kali.
Ufunuo 21:1-5X
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
Malaki 4:1X
1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Ezekieli 28:18-19X
18 Kwa wingi wa maovu yako, katika uovu wa uchuuzi wako, umepatia unajisi patakatifu pako; basi nimetokeza moto kutoka ndani yako, nao umekuteketeza, nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. 19 Wote wakujuao kati ya kabila za watu watakustaajabia; umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.
Ufunuo 20:1-4X
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
Ufunuo 19:11 – 21X
11 Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. 12 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. 13 Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. 14 Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. 15 Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. 16 Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA Bwana WA MABwana. 17 Kisha nikaona malaika mmoja amesimama katika jua; akalia kwa sauti kuu, akiwaambia ndege wote warukao katikati ya mbingu, Njoni mkutane kwa karamu ya Mungu iliyo kuu; 18 mpate kula nyama ya wafalme, na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari, na nyama ya farasi na ya watu wawapandao, na nyama ya watu wote, waungwana kwa watumwa, wadogo kwa wakubwa. 19 Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake. 20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa
Ufunuo 16:13X
13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo.
Ufunuo 19:19, 20X
19 Wakatupa mavumbi juu ya vichwa vyao, wakalia, wakitokwa na machozi na kuomboleza, wakisema, Ole, ole, mji ule ulio mkuu! Ambao ndani yake wote wenye merikebu baharini walipata mali kwa utajiri wake; kwa kuwa katika saa moja umekuwa ukiwa. 20 Furahini juu yake, enyi mbingu, nanyi watakatifu na mitume na manabii; kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.
Danieli 2:44X
44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
1 Wathesalonike 4:17X
17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Yohana 14:2, 3X
2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Ufunuo 19:21X
21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
Mathayo 24:37-39X
37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.
Luka 17:29X
29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
Isaya 26:21X
21 Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.
Yeremia 4:23-25X
23 Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. 24 Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. 25 Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao.
Mwanzo 1:2X
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
M. Walawi 16:21X
21 Na Haruni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha yule mbuzi aliye hai, na kuungama juu yake uovu wote wa wana wa Israeli, na makosa yao, naam, dhambi zao zote; naye ataziweka juu ya kichwa chake yule mbuzi, kisha atampeleka aende jangwani kwa mkono wa mtu aliye tayari.
M. Walawi 16:22X
22 Na yule mbuzi atachukua juu yake uovu wao wote, mpaka nchi isiyo watu; naye atamwacha mbuzi jangwani.
Ufunuo 20:2, 3X
2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Ufunuo 16:18–21X
18 Pakawa na umeme na sauti na radi; na palikuwa na tetemeko la nchi kubwa, ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo. 19 Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake. 20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena. 21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno.
Ufunuo 15:2, 3X
2 Tena nikaona kitu kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, na wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kando-kando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. 3 Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa mataifa.
Ufunuo 20:4X
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
Ufunuo 2:26X
26 Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,
Danieli 7:27X
27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Ufunuo 20:4X
4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
2 Petro 2:4X
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Yuda 1:6X
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Ufunuo 20:5, 7X
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
Ufunuo 20:9X
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
Ufunuo 21:2X
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Zekaria 14:4X
4 Na siku hiyo miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, unaoelekea Yerusalemu upande wa mashariki, nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake, upande wa mashariki na upande wa magharibi; litakuwako huko bonde kubwa sana; na nusu ya mlima ule utaondoka kwenda upande wa kaskazini, na nusu yake itaondoka kwenda upande wa kusini.
Zekaria 14:9X
9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Yohana 5:28X
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
Yohana 5:29X
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Ufunuo 20:5X
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
Ufunuo 20:3X
3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Ufunuo 20:8X
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
Ufunuo 20:8, 9X
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
Ufunuo 20:11-15X
11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Luka 13:28X
28 Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje.
Warumi 14:10X
10 Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
Wafilipi 2:10, 11X
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Isaya 45:22, 23X
22 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine. 23 Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Ufunuo 20:9, 12-15X
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
2 Petro 3:7X
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
Isaya 34:8X
8 Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.
Isaya 28:21X
21 Maana Bwana ataondoka kama vile katika mlima Perasimu, ataghadhibika kama vile katika bonde la Gibeoni; apate kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu; na kulitimiza tendo lake, tendo lake la ajabu.
Ufunuo 20:15X
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 20:10X
10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Mathayo 25:41X
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Mathayo 25:46X
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.
Ufunuo 21:8X
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo 14:9 – 11X
9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Mathayo 8:29X
29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
2 Petro 2:4X
4 Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
Yuda 1:9X
9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.
2 Petro 2:9X
9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
Ezekieli 18:4X
4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.
Warumi 6:23X
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 1:31X
ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.
Warumi 6:21X
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti.
Yakobo 1:15X
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.
Zaburi 37:9, 34X
9 Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi. 34 Wewe umngoje Bwana, Uishike njia yake, Naye atakutukuza uirithi nchi, Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.
Ezekieli 28:16X
16 Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.
Zaburi 37:20X
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Zaburi 37:10 X
10 Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
Zaburi 68:2X
2 Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
Yohana 3:16X
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Malaki 4:1X
1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Mathayo 13:30X
30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Mathayo 13:40X
40 Basi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia.
2 Petro 3:10X
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Ufunuo 20:15X
15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 21:8X
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Zaburi 145:20X
20 Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.
Marko 1:24X
24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
2 Wathesalonike 1:9X
9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
Waebrania 2:14X
14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Ufunuo 19:20, 21X
20 Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; 21 na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote wakashiba kwa nyama zao.
2 Petro 3:10X
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.
Mathayo 21:41X
41 Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
Marko 1:24X
24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
Matendo 3:23X
23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
Zaburi 104:35X
35 Wenye dhambi waangamizwe katika nchi, Watendao ubaya wasiwepo tena. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Zaburi 37:20X
20 Bali wasio haki watapotea, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.
Zaburi 73:19X
19 Namna gani wamekuwa ukiwa mara! Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho.
Zaburi 1:4X
4 Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.
Isaya 40:24X
24 Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
Malaki 4:1X
1 Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
K. Torati 29:23X
23 ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake;
Isaya 13:19X
19 Na Babeli, huo utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo, utakuwa kama Sodoma na Gomora hapo Mungu alipoiangamiza.
Mwanzo 19:29X
29 Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Luka 17:29X
29 lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
Maombolezo 4:6X
6 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake.
2 Petro 2:6X
6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;
Yuda 7X
7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
Kutoka 12:17X
17 Nanyi mtaitunza ile sikukuu ya mikate isiyochachwa; kwa kuwa katika siku iyo hiyo mimi nimeyatoa majeshi yenu katika nchi ya Misri; kwa hiyo mtaitunza siku hiyo katika vizazi vyenu vyote, kwa amri ya milele.
1 Samweli 1:22X
22 Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za Bwana, akae huko daima.
Yona 2:6X
6 Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu,
2 Wafalme 5:27X
27 Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.
Filemoni 15X
15 Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele;
Waebrania 9:12X
12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
Waebrania 6:2X
2 na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele.
Ufunuo 19:3X
3 Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele.
Ufunuo 20:10X
10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
Ufunuo 14:11X
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake.
Zaburi 92:7X
7 Wasio haki wakichipuka kama majani Na wote watendao maovu wakistawi. Ni kwa kusudi waangamizwe milele;
Isaya 34:8 – 10X
8 Maana ni siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni. 9 Na vijito vyake vitageuzwa kuwa lami, na mavumbi yake yatageuzwa kuwa kiberiti, na ardhi yake itakuwa lami iwakayo. 10 Haitazimwa mchana wala usiku, moshi wake utapaa milele; tangu kizazi hata kizazi itakuwa ukiwa; hapana mtu atakayepita kati yake milele na milele.
Warumi 6:23X
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Yohana 3:36X
36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
1 Yohana 3:15X
15 Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.
Ufunuo 21:4X
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Waebrania 9:26X
26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake.
Waefeso 1:14X
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.