Kwa upendo usio na kifani na rehema, Mungu alimfanya Kristo asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, kusudi katika Yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu, tunatambua hitaji letu, na kukiri hali yetu ya dhambi, tunatubia uasi wetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo, kuwa mbadala na Kielelezo chetu. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia uwezo wa kimbingu kwa Neno na ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia Kristo tunahesabiwa haki, kufanywa wana na binti wa Mungu, na kuokolewa kutoka katika mamlaka ya dhambi. Kupitia Roho Mtakatifu tunazaliwa upya na kutakaswa; Roho hufanya upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ndani ya mioyo yetu, na tunapewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani Yake tunakuwa washirika wa hali ya asili ya uungu na kuwa na hakika ya wokovu sasa na katika siku ya hukumu. (2Kor.5:17-21; Yoh.3:16; Gal.1:4; 4:4-7; Tit.3:3-7; Yoh. 16:8; Gal.3:13, 14; 1Pet.2:21, 22; Rum.10:17; Luk.17:5; Mk. 9:23, 24; Efe.2:5-10; Rum.3:21-26; Kol.1:13, 14; Rum.8:14-17; Gal.3:26; Yoh.3:3-8; 1Pet.1:23; Rum.12:2; Ebr.8:7-12; Eze.36:25-27; 2Pet.1:3, 4; Rum.8:1-4; 5:6-10).
Maisha ya Mkristo ambaye Roho wa Mungu anakaa ndani yake (Rum. 8:9) hayawezi yakabaki yaleyale. Kristo alilipenda Kanisa hata akajitoa kwa ajili yake ili alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apatae kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa (Efe. 5:25-27). Utakaso wa jinsi hiyo ndilo lengo la Kanisa. Washiriki wa Kanisa wanaweza wakakiri kwamba “ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya kila siku (2 Kor. 4:16). Kwa hiyo tunaakisi utukufu wa Bwana, tukibadilishwa tufanane nao, toka utukufu hadi utukufu (2 Kor. 3:18).
Kwenye maandiko, uzoefu wa muumini wa wokovu yaani kuhesabiwa haki, kutakaswa, kusafishwa, na kukombolewa kunaelezewa kuwa (1) kumekamilika (2) kunaendelea kukamilishwa (3) kutakamilishwa wakati ujao. Kuelewa mitazamo hii kutaondosha misuguano inayotokana na kutokuelewa.
Uzoefu wa Wokovu na Wakati Uliopita
Kujua kuhusu Mungu na pendo lake hakutoshi. Jitihada isiyomhusisha Yesu kamwe haitaleta matunda ya wokovu. Yesu alisema, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu (Yoh. 3:3). Wokovu hupatikana kwa Yesu peke yake (Mdo. 4:12). Yesu ndiye njia na kweli na uzima (Yoh. 14:6). Uzoefu wa wokovu hujumuisha kutubu, kuungama, msamaha, kuhesabiwa haki na kutakaswa.
1. Kutubu (toba)
Roho alipogusa mioyo watu waliokuja kuhiji siku ya Pentekoste, Petro aliawaambia tubuni (Mdo. 2:37, 38Mdo. 3:19).
Maana ya kutubu:
Neno kutubu / toba, hutokana na neno la Kiebrania nachum lenye maana ya kuhuzunika, kusikitika. Neno la Kigiriki lenye maana sawa na hilo ni metanoeo, lenye maaana ya kubadilisha mawazo/nia. Utambuzi wa afichaye dhambi zake hatafanikiwa (Mith. 28:13), huongoza mtu kuungama maovu yake maalum. Toba hufikia kilele kwa kuongoka (Mdo. 15:3).
Mfano wa toba inayoongoza kwenye ushindi wa dhambi ni toba ya Daudi. Aliomba asamehewe na kuumbiwa moyo mpya (Zab. 51:3, 1, 10). Uzoefu wa baadaye wa Daudi unadhihirisha kwamba msamaha wa Mungu siyo kwamba husamehe dhambi, bali pia huokoa kutoka dhambini.
Japokuwa toba inatangulia msamaha, mwenye dhambi hawezi kujipatia baraka ya Mungu yeye mwenyewe. Toba ni karama inayotolewa na Mungu (Mdo. 5:31Rum. 2:4)
Msukumo wa kutubu: Yesu alikufa tulipokuwa tungali wenye dhambi (Rum. 5:6-10). Hakuna kinachogusa moyo kama upendo wa Yesu unaosamehe (Yoh. 12:32). Huo ndio wema unaotuvuta kutubu (Rum. 2:4).
2. Kuhesabiwa Haki
Kwa upendo na rehema visivyo kifani, Mungu alimfanya mwana wake dhambi ili sisi tuwe haki ya Mungu (2 Kor.5:21). Kwa njia ya imani, moyo hujazwa na Roho Mtakatifu. Na kwa imani hiyo hiyo ambayo ni kipaji kutoka kwa Mungu cha neema (Rum. 12:3; Efe. 2: 8), mwenye dhambi atubuye huhesabiwa haki (Rum. 3:28).
Neno kuhesabiwa haki hutumika kuwasilisha kitendo cha Mungu cha kumtangaza mwenye dhambi kuwa ana haki. Ni kinyume cha kuhukumiwa (Rum. 5:16). Kuhesabiwa haki siyo kwa sababu ya matendo yetu. Ni kwa sababu mtu mmoja alitii, nasi tunahesabiwa haki (Rum.5:18, 19). Utii wa Yesu unafanywa kuwa utii wa mdhambi bure (Rum. 3:24), siyo kwa sababu ya utii wetu bali kwa neema yake (Tito 3:5).
Kuhesabiwa haki na matendo
Wengi wetu huamini uwongo kwamba kusimama kwetu mbele za Mungu kunategemea matendo yetu yawe mema au mabaya. Paulo alifundisha kwa msisitizo wokovu uliotolewa bure na Mungu. Tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa kwa imani iliyo katika Kristo (Wafil. 3:8, 9). Ibrahimu alihesabiwa haki kwa imani (Rum. 4:3, (Mwa. 15:6). Alihesabiwa haki kabla ya kutahiriwa na siyo kwa sababu ya kutahiriwa (Rum. 4:9,10). Ni imani gani Ibrahimu alikuwa nayo?
Kwa imani Ibrahimu alipoitwa, alitii “aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa kuwa urithi…” (Ebr. 11:8-10, (Mwa. 12:4, (Mwa. 13:18). Kwamba alikuwa na imani ya kweli, kulidhihirishwa na matendo yake. Mtume Yakobo alionya juu ya uwongo mwingine wa imani isiyo na matendo. Kwa Ibrahimu, imani yake ilidhihirishwa na matendo kwa kumtoa Isaka (Yak. 2:21). Hivyo imani hukamilishwa na matendo (Yak. 2:22). Kama imani haina matendo imekufa (Yak. 2:17). Hivyo imani inayohesabiwa haki ni imani iliyo hai, yenye kufuatiwa na matendo (Yak.2:24).
Uzoefu wa Kuhesabiwa Haki
Tunapohesabiwa haki, Yesu ambaye hakuijua dhambi alifanywa dhambi ili sisi tupate haki yake ya kuwa wana wa Mungu (2Kor. 5:21). Kama wadhambi wenye kutubu, tunapokea kwa kipimo tele, msamaha mkamilifu. Mungu husema kama ilivyokuwa kwa Joshua, hiki si kinga kilichotoka motoni? (Zek. 3:2). Ndipo hutamka “tazama nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi (Zek. 3:4). Dhambi zilizoungamwa huwekwa kwa Yesu na Mdhambi aliyetubu hupokea haki ya Yesu.
Matokeo ya Kuhesabiwa Haki
Kutakaswa. Neno kutakaswa humaanisha kufanywa mtakatifu.Toba ya kweli na kuhesabiwa haki huongoza kwenye kutakaswa. Utakaso nayo ni kazi ya neema ya Mungu. Hatua tatu za kutakaswa zinazofundishwa na Biblia ni (1) ni jambo lililokwisha kutimizwa (2) ni jambo linaloendelea kutimizwa sasa katika maisha ya mkristo (3) ni jambo litakalokamilishwa Yesu akirudi. Kwa wakati uliopita, wakati mtu anapohesabiwa haki, pia huwa amepokea utakaso kwa jina la Bwana Yesu (1Kor. 6:11 cf. Yoh. 15:3). Kama matokeo ya kuitwa na Mungu (Rum. 1:7) waumini huitwa watakatifu kwa kuwa wako katika Kristo (Wafil. 1:1, Yoh. 15:1-7).
Kufanywa watoto wa Mungu. Wakati huo huo tunapokea Roho ya kufanywa wana na warithi pamoja na Yesu (Rum. 8:15-17). Ni fursa bora kiasi gani, raha iliyoje?
Kuthibitishiwa wokovu. Kuhesabiwa haki kunatuthibitishia kuwa ukombozi wetu ni hakika (Efe. 1:7)
Mwanzo wa maisha mapya ya ushindi. Kutambua kwamba dhambi zetu zilizopita zimefunikwa, huleta uponyaji katika maisha yetu. Imani yetu kwake ikiongezeka, uponyaji wetu na kubalishwa nako kutaongezeka. Kuushinda kwake ulimwengu hutupatia garantii kwa wokovu wetu juu ya dhambi (Yoh. 16:33)
Zawadi ya Uzima wa Milele. Mahusiano yetu mapya na Yesu hutupatia zawadi ya uzima wa milele. Aliye na mwana ana uzima wa milele, asiye na mwana hana uzima (1Yoh. 5:12)
Uzoefu wa Wokovu na Wakati wa Sasa
Kwa damu ya Yesu kutupatia kuhesabiwa haki, kutakaswa, kusafishwa, muumini anakuwa kiumbe kipya na ya kale hupita (2Kor. 5:17)
Wito wa kuishi maisha matakatifu.
Wokovu hujumuisha kuishi maisha matakatifu kwa msingi wa kile Yesu alichotufanyia msalabani. Paulo alitoa wito kwa waumini kuishi maisha ya maadili (1Thes. 4:7). Ili waweze kuishi maisha matakatifu, Mungu huwezesha kwa kutoa Roho (Rum. 1:4), kwa kadiri ya utajiri wa neema yake (Efe. 3:16, 17). Kwa kuwa ni viumbe vipya, waumini wanayo majukumu mapya (Rum. 6:12-14, 19). Sasa wataishi kwa kuongezwa na Roho (Gal. 5:25).
Waumini waliojawa na Roho hawatembei kwa jinsi ya mwili bali kwa roho. (Rum. 8:1 cf 8:4). Wanabadilishwa kwamba kuishi kimwili ni mauti (Rum. 8:6) na kwa kuwa wana Roho, basi hawako kimwili bali kiroho (Rum. 8:9). Lengo lao kuu ni kumtukuza Mungu (1Thes. 4:1), wakiepuka zinaa na kudhulumu ndugu (1Thes. 4:3, 6, 7).
Mabadiliko ya Ndani
Siku Yesu atakapokuja mara ya pili tutabadilishwa mwili wa kufa uvae kutokufa, wenye kuharibika, uvae kutokuharibika (1Kor. 15:51-54). Hata hivyo, mabadiliko ya tabia yanapaswa kuendelea kwa ajili ya kumlaki Yesu ajapo mara ya pili. Mabadiliko ya ndani huhusisha utu wa ndani na hufanyika kila siku (2 Kor. 4:16, Rum. 12:2).
1. Kumhusisha Yesu na Roho Mtakatifu.
Ni mwumbaji tu ndiye awezaye kukamilisha kazi ya uumbaji kutubadilisha maisha yetu (1Thes. 5:23). Hata hivyo hatafanya hivyo pasipo kutushirikisha. Ni Roho ndiye atendaye kazi ya kumfunua Kristo na kurejesha ndani yetu taswira ya Mungu iliyopotea (Rum. 8:1-10).
Ahadi kubwa mno ya Yesu ni kutupatia uwezo kukamilisha mabadiliko ndani yetu (2Pet. 1:4). Kuufikia uwezo wa kimbingu hutusaidia kutoka imani hadi wema, maarifa, kiasi, saburi, utauwa, upendano wa ndugu hadi upendo (2Pet. 1:5-7). Kuwa na karama hizo hutuepusha na uvivu na kukosa matunda, kwani akosaye hayo ni kipofu (2Pet. 1:8, 9)
a) Kupitia Kristo Pekee
Kinachobadilisha wanadamu hadi kufikia kushiriki asili ya uungu ni kumvaa Kristo (Rum. 13:14, Ebr. 3:14) na kufanyanywa upya na Roho Mtakatifu (Tit. 3:5). Ni kukamilisha upendo wa Mungu ndani yetu (1Yoh. 4:12).
b) Ni mchakato Unaoendelea
Kutakaswa ni zoezi la kuendelea. Kwa maombi na kujifunza Maandiko (kumla Yesu) Matakatifu tunaendelea kushirikiana na Mungu. (Yoh. 6:53-56). Maneno nisemayo ni roho na ndiyo uzima (Yoh. 6:63, pia Mt. 4:4).
Mabadiliko ya Kiaina
Mungu anatumaini kuwabadili wanadamu walioanguka nia, mawazo, matamanio na tabia hata wajae matunda ya Roho (Efe. 5:27, Gal. 5:22,23)
Mungu hutulinda tusianguke (Yud. 24). Maisha ya kiroho ni ya mabadiliko ya daima. Hakuna nafasi ya katikati linapokuja ufalme wa Mungu na wa Shetani (Rum. 6:17, 18). Yule atawalaye mawazo yetu, ndiye atutawalaye sisi. Ikiwa tunamchagua Kristo atutawale fikra (2Kor. 10:5) yeye ndiye anayekuwa mtawala wetu.
Ukamilifu wa Kristo
Ukamilifu wa Biblia ni nini, unapatikanaje?
Ukamilifu wa Biblia
Neno la kiebrania linalowakilisha ukamilifu ni tam au tamim lenye maana ya kutimia, vema, kamili, isiyo na doa. Kwa kigiriki, neno teleios humaanisha kukamilika, kukomaa. Kwenye Agano la Kale limetumika kuelezea maana iliyopungua. Nuhu, Ibrahimu na Ayubu wanaelezewa kuwa walikuwa wakamilifu (Mwa. 6:9; (17:1, (22:18Ayu. 1:1, 8) lakini nao walikuwa na mapungufu yao (Mwa. 9:20, 21 na Ayu. 40:2-5) Katika Agano Jipya, ukamilifu huelezea mkristo aliyeishi kwa uaminifu kadiri ya nuru aliyonayo (cf. 1Kor.14:20; Wafil. 3:15; Ebr. 5:14). Tumeitwa kuwa wakamilifu (Mt. 5:48) na kwa neema ya Mungu twaweza kushangilia ushindi (cf. Kol. 4:12, Yak. 3:2).
Ukamilifu katika Kristo. Roho Mtakatifu hutuletea ukamilifu wa Kristo. Kwa imani, ukamilifu wa Kristo unakuwa wetu. Bila Kristo haiwezekani (Yoh. 15:5). Kristo ndiye hekima ya Mungu, utakatifu na ukombozi (1Kor. 1:30). Tunatimilika utimilifu wa Mungu (Efe. 3:19)
Kukaza mwendo kufikia ukamilifu. Kupitia Kristo akaaye ndani yetu twaweza kufikia utimilifu wa Kristo (Efe.4:13), na kuondokana na uchanga wa imani (Efe. 4:14), na kuweza kula chakula kigumu yaani kupambanua mema na mabaya (Ebr.5:14). Kwa nafasi yetu ya kuwa Wakristo, tunaitwa kukaza mwendo kufikia utimilifu (Ebr. 6:1) uliojaa matunda (Wafil. 1:9-11).
Maisha matakatifu siyo maisha yasiyo ya matatizo. Tumeitwa kutimiza wokovu kwa kuogopa na kutetemeka (Wafil. 2:12, 13). Tuonyane…kushikamana na mwanzo wa uthabiti kwa nguvu hadi mwisho (Ebr. 3:13, 14, cf. Mt. 24:13). Maandiko huonya, tukitenda dhambi kusudi, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi (Ebr. 10:26). Hivyo, maombi yasiyokoma ni muhimu kwa maisha ya utakaso na ukamilifu (Kol. 1:9, 10)
Kuhesabiwa haki kila siku
Kuna wakati hatuwezi kuyatambua makosa yetu (Zab.19:12) kwa kuwa moyo hudanganya (Yer. 17:9). Kwa hali hiyo, tunaambiwa tusitende dhambi, ila kama mtu ametenda dhambi, tunaye mwombezi kwa Baba (1Yoh. 2:1). Tukiungama, tunasamehewa (1Yoh. 1:9)
Uzoefu wa Wokovu na Wakati Ujao
Wokovu wetu hatimaye hukamilika tunapokuwa tumefufuliwa na kuvikwa kutokufa au kunyakuliwa mbinguni. Hilo ndilo tumaini la utukufu wa Mungu (Rum. 5:2). Ujio wa Yesu mara ya pili pia unaleta wokovu (Ebr. 9:28).
Kuvikwa Utukufu na Kutakaswa
Kuwa na Yesu moyoni ni sharti la kuokoleaw siku za usoni kwa kuvikwa utukufu (Kol. 1:27). Kwa Roho anayekaa ndani yetu, miili yetu itahuishwa (Rum.8:11). Ni jambo la kushukuru kwamba tangu mwanzo tulichaguliwa kupata wokovu, tunatakaswa na tutavikwa utukufu (2Thes. 2:13, 14). Katika Kristo, tayari tuko kwenye kiti cha enzi cha Mungu mbinguni (Kol. 3:1-4). Tayari tumeonja enzi ijayo (Ebr. 6:4, 5).
Wako wanaoamini kwa uwongo kwamba ukamilifu utakaoletwa na utukufu wa Mungu tayari upo kwa wanadamu. Paulo alikataa jambo hilo kabla ya kufa kwake, aliposema siyo kwamba nimekwisha kufika, nakaza mwendo, niifikile mede ya dhahabu (Wafil. 3:12-14). Aliyesimama na aangalie asianguke (1Kor. 10:12). Historia ya Daudi, Sulemani na Petro ipo kutufundisha juu ya hayo.
Msingi wa Kukubaliwa kwetu na Mungu
Siyo kule kuwa na tabia ya Yesu au kutokuwa na doa kunakomfanya Mungu atukubali.Haki inayookoa inatoka kwa mwenye haki mmoja, Yesu Kristo na huwasilishwa kwetu na Roho Mtakatifu. Hakuna aliye na haki isipokuwa Kristo (Rum. 3:10), mwanadamu alivyo ni mavazi yaliyotiwa unajisi (Isa. 64:6, pia Dan. 9:7, 9, 11, 20 na 1Kor. 1:30). Kristo ndiye haki yetu nasi tunatakaswa ndani yake. (1Kor. 1:30).
2 Wakorintho 5:17-21X 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 20 Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Yohana 3:16X 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Wagalatia 1:4X 4 ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu.
Wagalatia 4:4-7X 4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. 6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. 7 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Tito 3:3-7X 3 Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, tulikuwa waasi, tumedanganywa, huku tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukiishi katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana. 4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa; 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu; 7 ili tukihesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.
Yohana 16:8X 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
1 Petro 2:21, 22X 21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
Warumi 10:17X 17 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
Luka 17:5X 5 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
Marko 9:23, 24X 23 Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. 24 Mara babaye yule kijana akapaza sauti, akasema, Naamini, nisaidie kutokuamini kwangu.
Waefeso 2:5-10X 5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. 6 Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; 7 ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Wafilipi 2:6, 7X 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Wakolosai 1:13, 14X 13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Waumi 8:14-17X 14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Wagalatia 3:26X 26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.
Yohana 3:3-8X 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
1 Petro 1:23X 23 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
Warumi 12:2X 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Waebrania 8:7-12X 7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. 8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; 9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. 12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena.
Ezekieli 36:25-27X 25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. 26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
2 Petro 1:3, 4X 3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Warumi 8:1-4X 1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Warumi 5:6-10X 6 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 7 Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. 8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. 10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Warumi 8:9X 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Waefeso 5:25-27X 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
2 Wakorintho 4:16X 16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
2 Wakorintho 3:18X 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Yohana 3:3X 3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Matendo 4:12X 12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Yohana 14:6X 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Matendo 2:37, 38X 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo 3:19X 19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
Mithali 28:13X 13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Matendo 15:3X 3 Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Zaburi 51:3, 1, 10X 3 Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. 1 Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. 10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
Matendo 5:31X 31 Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.
Warumi 2:4X 2 Nasi twajua ya kuwa hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao hayo.
Warumi 5:6-10X 6 Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. 7 Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. 8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. 9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. 10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.
Warumi 2:4X 4 Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
2 Wakorintho 5:21X 21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Warumi 12:3X 3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
Waefeso 2:8X 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
Warumi 3:28X 8 Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki.
Warumi 5:16X 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki.
Warumi 5:18, 19X 18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
Warumi 3:24X 5 Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)
Tito 3:5X 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Wafilipi 3:8, 9X 8 Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo; 9 tena nionekane katika yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani;
Warumi 4:3X 3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
Mwanzo 15:6X 6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Warumi 4:9, 10X 9 Basi je! Uheri huo ni kwa hao waliotahiriwa, au kwa hao pia wasiotahiriwa? Kwa kuwa twanena ya kwamba kwake Ibrahimu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki. 10 Alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa.
Waebrania 11:8-10X 8 Kwa imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako. 9 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. 10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Mwanzo 12:4X 4 Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani.
Mwanzo 13:18X 18 Basi Abramu akajongeza hema yake, akaja akakaa kwenye mialoni ya Mamre, nayo ni miti iliyoko Hebroni, akamjengea Bwana madhabahu huko.
Yakobo 2:21X 21 Je! Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
Yakobo 2:22X 22 Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
Yakobo 2:17X 17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
Yakobo 2:24X 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
2 Wakorintho 5:21X 21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Zekaria 3:2X 2 Bwana akamwambia Shetani, Bwana na akukemee Ewe Shetani; naam, Bwana, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je! Hiki si kinga kilichotolewa motoni?
Zekaria 3:4X 4 Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.
1 Wakorintho 6:11X 11 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.
Yohana 15:3X 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia.
Warumi 1:7X 7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Wafilipi 1:1X 1 Paulo na Timotheo, watumwa wa Kristo Yesu, kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu, walioko Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi.
Yohana 15:1-7X 1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.
Warumi 8:15-17X 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Waefeso 1:7X 7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Yohana 16:33X 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
1 Yohana 5:1X 1 Kila mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na kila mtu ampendaye mwenye kuzaa, ampenda hata yeye aliyezaliwa na yeye.
2 Wakorintho 5:17X 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
1 Wathesalonike 4:7X 7 Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.
Waebrania 1:4X 4 amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.
Waefeso 3:16, 17X 16 awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. 17 Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo;
Warumi 6:12-14, 19X 12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; 13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. 14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
Wagalatia 5:25X 25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
Warumi 8:1X 1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Warumi 8:4X 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Warumi 8:6X 6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
Warumi 8:9X 9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
1 Wathesalonike 4:1X 1 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
1 Wathesalonike 4:3, 6, 7X 3 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 6 Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. 8 Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
1 Wakorintho 15:51-54X 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
2 Wakorintho 4:16X 16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Warumi 12:2X 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
1 Wathesalonike 5:23X 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Warumi 8:1-10X 1 Paulo, mtumwa wa Kristo Yesu, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri Injili ya Mungu; 2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu; 3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu; 5 ambaye katika yeye tulipokea neema na utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake; 6 ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa Yesu Kristo; 7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. 8 Kwanza namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima. 9 Kwa maana Mungu, nimwabuduye kwa roho yangu katika Injili ya Mwana wake, ni shahidi wangu jinsi niwatajavyo pasipo kukoma, 10 siku zote katika sala zangu, nikiomba nije kwenu hivi karibu, Mungu akipenda kuifanikisha safari yangu.
2 Wakorintho 6:16X 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Yohana 3:24X 24 Maana Yohana alikuwa hajatiwa gerezani.
Yohana 4:12X 12 Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake?
Wagalatia 2:20X 20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
Yohana 14:23X 23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
2 Wakorintho 4:16X 16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.
Warumi 12:2X 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Wafilipi 2:5X 5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
2 Petro 1:4X 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
2 Peteo 1:5-7X 5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, 6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, 7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
2 Petro 1:8, 9X 8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Maana yeye asiyekuwa na hayo ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.
Warumi 13:14X 14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
Waebrania 3:14X 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
1
Tito 3:5X 5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
1 Yohana 4:12X 12 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
Yohana 6:53-56X 53 Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. 54 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake.
Yohana 6:63X 63 Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Mathayo 4:4X 4 Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Waefeso 5:27X 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Wagalatia 5:22,23X 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Yuda 1:24X 24 Yeye awezaye kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu;
Warumi 6:17, 18X 17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; 18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
2 Wakorintho 10:5X 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
Mwanzo 6:9X 9 Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu. Nuhu alikuwa mtu wa haki, mkamilifu katika vizazi vyake; Nuhu alikwenda pamoja na Mungu.
Mwanzo 17:1X 1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Mwanzo 22:18X 18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Ayubu 1:1, 8X 1 Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. 8 Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
Mwanzo 9:20, 21X 20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu; 21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
Ayubu 40:2-5X 2 Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi? Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye. 3 Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema, 4 Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini? Naweka mkono wangu kinywani pangu. 5 Nimenena mara moja, nami sitajibu; Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
1 Wakorintho 14:20X 20 Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu; lakini katika uovu mgeuzwe watoto wachanga, bali katika akili zenu mkawe watu wazima.
Wafilipi 3:15X 15 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.
Waebrania 5:14X 14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.
Mathayo 5:48X 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Wakolosai 4:12X 12 Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili kwamba msimame wakamilifu na kuthibitika sana katika mapenzi yote ya Mungu.
Yakobo 3:2X 2 Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.
Yohana 15:5X 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
1 Wakorintho 1:30X 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Waefeso 3:19X 19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
Waefeso 4:13X 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Waefeso 4:14X 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Waebrania 5:14X 14 Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.
Waebrania 6:1X 1 Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu,
Wafilipi 1:9-11X 9 Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; 10 mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; 11 hali mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.
Wafilipi 2:12, 13X 12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
Waebrania 3:13, 14X 13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
Mathayo 24:13X 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Waebrania 10:26X 26 Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Wakolosai 1:9, 10X 9 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; 10 mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu;
Zaburi 19:12X 12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.
Yeremia 17:9X 9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
1 Yohana 2:1X 1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
1 Yohana 1:9X 9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Warumi 5:2X 2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Waebrania 9:28X 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
Wakolosai 1:27X 27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu
Warumi 8:11X 11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
2 Wathesalonike 2:13, 14X 13 Lakini imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; 14 aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Wakolosai 3:1-4X 1 Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. 2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. 3 Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
Waebrania 6:4, 5X 4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo,
2 Wakorintho 3:18X 18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Warumi 8:19, 23X 19 Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu. 23 Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Waefeso 4:30X 30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Matendo 3:21X 21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
Mathayo 19:28X 28 Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Wafilipi 3:12-14X 12 Si kwamba nimekwisha kufika, au nimekwisha kuwa mkamilifu; la! Bali nakaza mwendo ili nipate kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu. 13 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; 14 nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
1 Wakorintho 10:12X 12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
Warumi 3:10X 10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
Isaya 64:6X 6 Kwa maana sisi sote tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi; sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo.
Danieli 9:7, 9, 11, 20X 7 Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa. 9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; 11 Naam, Israeli wote wameihalifu sheria yako, kwa kugeuka upande, wasiisikilize sauti yako; basi kwa hiyo laana imemwagwa juu yetu, na uapo ule ulioandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu; kwa sababu tumemtenda dhambi. 20 Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu;
1 Wakorintho 1:30X 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
1 Wakorintho 1:30X 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;