Utangulizi
Sisi tu wmawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa na Yeye wakati, fursa, uwezo, na mali na mibaraka ya dunia na rasilmali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake mazuri. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa kutoa utumishi mzuri kwake na kwa wanadamu wenzetu, kwa kumrudishia zaka na kutoa sadaka kwa ajili ya kutangaza injili Yake na kwa kulitegemeza na kulikuza kanisa lake. Uwakili ni upendeleo uliotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika upendo na ushindi dhidi ya choyo na tamaa. Wakili huifurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake. (Mwa.1:26-28; 2:15; 1Nyak.29:14; Hagai 1:3-11;
3 Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?
5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.
7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.
9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.
11 Nami nikaita wakati wa joto uje juu ya nchi, na juu ya milima, na juu ya nafaka, na juu ya divai mpya, na juu ya mafuta, na juu ya kila kitu itoacho nchi, na juu ya wanadamu, na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono.
Mal. 3:8-12;
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
1Kor.9:9—14;
9 Kwa maana katika torati ya Musa imeandikwa, Usimfunge kinywa ng'ombe apurapo nafaka. Je! Hapo Mungu aangalia mambo ya ng'ombe?
10 Au yamkini anena hayo kwa ajili yetu? Naam, yaliandikwa kwa ajili yetu; kwa kuwa alimaye nafaka ni haki yake kulima kwa matumaini, naye apuraye nafaka ni haki yake kutumaini kupata sehemu yake.
11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?
12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo.
13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?
14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.
Mt. 23:23;
23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
2Kor.8:1-15;
1 Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia;
2 maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao.
3 Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;
4 wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu.
5 Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.
6 Hata tukamwonya Tito kuwatimilizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha.
7 Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia.
8 Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu.
9 Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.
10 Nami katika neno hili natoa shauri langu; maana neno hili lawafaa ninyi mliotangulia, yapata mwaka, licha ya kutenda hata na kutaka pia.
11 Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
12 Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.
13 Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
14 bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
15 Kama ilivyoandikwa, Aliyekusanya vingi, hakuzidi, wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa.
Rum.15:26, 27
26 maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini. 27 Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili.
Hakuna kinachoweza kuelezea vema maisha kikristo zaidi ya kujisalimisha – kujitoa kwetu na kumkubali Yesu. Pale tunapomwona Yesu akitoa vyote kwa ajili yetu, huwa tunalia, nimrudishie nini BWANA, kwa ukarimu wote alionitendea? (Zab. 116:12).
12 Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Tunapotoa vyote kwa Mungu na kwa kweli vitu vyote kwa uhalisi ni vyake (1 Kor.3:21 – 4:2),
1 Wakorintho 3:21 - 23
21 Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu; 22 kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; 23 nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
1 Wakorintho 4:1-2
1 Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. 2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Mungu huvikubali lakini anatupatia tena ili tuwe mawakili na watunzaji wa vyote tulivyonavyo. Pale tunapomwona Mwokozi akiwa uchi, alivyofungwa, na mgeni, na lile agizo lake la “Basi enendeni mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi, (Mt. 28:19),
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
kwa ajili yake tutatafuta kuwa mawakili waaminifu.
Uwakili ni nini?
Kamusi ya Webster inatafsiri wakili ni mtu aliyekabidhiwa nyumba au miliki aitunze. Kanuni ya kutunza hutokana na maelekezo ya mmiliki. Kwa kamusi hiyo hiyo, Uwakili ni kazi au ofisi ya wakili. Umiliki wa Mungu wa vitu vyote ni ukweli wa msingi kwa madai ya kimbingu na ahadi zake, na wa majukumu yote ya mwanadamu. Umiliki ndio hutupatia picha ya uhalisi hata katika mpango wa Mungu kwa kazi yake.
Mungu ni mmiliki:
Ushahidi gani wa Bibilia hudhihirisha kuwa Mungu ndiye mmiliki wa vyote? Mungu anamiliki dunia( Zab. 24:1;
1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake.
Mungu anamiliki bahari (Zab. 95: 5).
5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu.
Mungu anamiliki ng’ombe, hayawani na ndege wa angani (Zab. 50: 9 – 12).
9 Sitatwaa ng'ombe katika nyumba yako, Wala beberu katika mazizi yako. 10 Maana kila hayawani ni wangu, Na makundi juu ya milima elfu. 11 Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu 12 Kama ningekuwa na njaa singekuambia, Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo.
Mungu anamiliki fedha na dhahabu (Hagai 2:8);
8 Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi.
Mungu anamiliki miili yetu (1Kor. 6:19, 20)
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Hivyo, twaweza kudai twamiliki mali kadha wa kadha, hata hivyo, kwa ajili ya kazi ya Mungu, hatimaye itakubalika kuwa Mungu hujipatia rasilimali kwa kazi yake kutokana na vile vilivyo vyake. Hatukuja na kitu duniani na hatutaondoka na kitu (1Tim. 6: 7).
7 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
Vyote vyatoka kwa Mungu na kutokana na vyake, sisi tunamtolea Yeye.(1 Nyak. 29: 14)
14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
Kutambua kwamba Mungu ni mmiliki ni muhimu katika kuleta mapinduzi katika maisha ya kiroho na kutufanya kuelewa uwakili wa mwanadamu.
Mwanadamu ni Wakili
Mt. 14 – 14-30
14 Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.
15 Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.
16 Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi vyakula.
17 Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
18 Akasema, Nileteeni hapa.
19 Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano.
20 Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.
21 Nao waliokula walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
22 Mara akawalazimisha wanafunzi wake wapande chomboni na kutangulia mbele yake kwenda ng'ambo, wakati yeye alipokuwa akiwaaga mkutano.
23 Naye alipokwisha kuwaaga makutano, alipanda mlimani faraghani, kwenda kuomba. Na kulipokuwa jioni, alikuwako huko peke yake.
24 Na kile chombo kimekwisha kufika katikati ya bahari, kinataabika sana na mawimbi; maana upepo ulikuwa wa mbisho.
25 Hata wakati wa zamu ya nne ya usiku Yesu akawaendea, akienda kwa miguu juu ya bahari.
26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.
27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.
28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.
29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.
30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.
Mfano wa talanta - wote ni mawakili wa Mungu tuliogawiwa kadiri ya uwezo kwa kila mmoja wetu kulingana na uwezo wetu.1Kor. 4:2
2 Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.
Wakili anapaswa kuwa mwaminifuLuk. 12:42
42 Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake?
Wakili anatazamiwa kuwa na busara na bidiiMt. 25: 27
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
Wakili anatarajiwa kuwekeza rasilimali za BWANA wakeMt. 21: 34
34 Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake.
Wakili anatazamiwa kurejesha mafao kwa BWANA wakeLuk. 16:2
2 Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena.
Wakili anawajibika kutoa hesabu ya shughuli za uwakili wakeMwa. 2: 16, 17
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Wakili anawajibika kuheshimu vile alivyozuilia Bwana wake
Njia za kukiri kuwa Mungu ndiye mmiliki
Maisha yaweza kugawanywa katika makundi ya msingi manne, kila moja ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mungu. Mungu ndiye aliyetupatia miili, uwezo, wakati na mali zinazowezekana kumilikika. Hivyo, katika maeneo hayo, kila kundi twaweza kabisa kuonyesha kuwa Mungu ndiye mmiliki.
Uwakili wa miili
Miili tuliyo nayo ni mali ya Mungu. (1 Kor. 6:19 – 20)
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
tumeitwa kula, kunywa au tutende yoyote kwa utukufu wa Mungu. (1 Kor. 10: 31)
31 Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Watu wa Mungu ni mawakili wao wenyewe pale inapoamriwa: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili yako yote (Luk. 10:27)
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Kuzitii amri za Mungu, kunachangia afya ya mwili na akili. (Kut. 15:26,
26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
Kut. 20: 8-20)
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 13 Usiue. 14 Usizini. 15 Usiibe. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. 18 Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. 19 Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. 20 Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi.
Uwakili wa Uwezo (talanta)
Mt. 25: 14 -16
14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. 16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
Kila mwanadamu ana uwezo maalumu kiakili na kimwili. Moja aweza kuwa na ujuzi wa uimbaji (muziki) mwingine kuweza biashara na wengine waweza kuwa mafundi wa kushona kwa cherehani au ufundi makenika. Wengine hufanya marafiki haraka, wengine hujichanganya na watu upesi. Kila mtu aweza kuiimarisha talanta alioyonayo kwa utukufu wa Mungu.
Zab. 90:12
12 Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima.
Basi utujulishe kuzihesabu siku zetu, tujipatie moyo wa hekima Ef. 5: 15, 16
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; 16 mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
Kuutambua wakati huleta hekima. Kama Yesu, twapaswa kuwa kwenye kazi ya Baba yetu (Luk. 2:49).
49 Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?
“Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo. (Kol.3:23, 24).
23 Lo lote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu, 24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.
Katika amri 10 za Mungu, amri ya Sabato huhusu utunzaji wa wakati, kwamba siku sita watu wafanye kazi na siku ya saba wapumzike(Kut.20:8-11).
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Mungu ametoa wakati kwa wanadamu wote kwa usawa.
Uwakili wa vile tunavyoweza kuvimiliki
Mungu alipomwumba mwanadamu alimmilikisha vitu. (Mw. 1: 28, 2:15).
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. 15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Alichozuilia, ni kwamba aliweka mti wa ujuzi wa mema na mabaya akaagiza wasile matunda yake. (Mw.2:16, 17).
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Baada ya dhambi, wanadamu walipaswa kukumbushwa kwamba Mungu ndiye chanzo cha mema Yakobo 1:17
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
na kwamba hutupatia nguvu za kupata utajiri (Kumb. 8:18).
18 Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.
Kuukumbusha ukweli huu daima, Mungu alianzisha mfumo wa zaka na sadaka.
Swali:
Maisha toa mwili, wakati, talanta, mali sawa sawa na nini? Hivyo kuwa wakili ni kutimiza amri ya Mungu ya upendo kwake na kwa wanadamu wenzetu. (Luk. 10:27).
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Zaka
Ni sehemu ya saba ya wakati (Kut. 20:9,10)
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
na vitu tunavyopata (Law. 27:30, 32).
30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. 32 Tena zaka yote ya ng'ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana.
Mungu anapoagiza tupeleke zaka ghalani (Mal. 3:10)
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
huwa hatuiti tumfanyie upendeleo kwa kuwa zaka ni mali yake.
Iko mifano ya Zaka- Ibrahimu (Mw. 14:20),
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Yakobo (Mw. 28:20 -20).
20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;
Waisraeli waliifanya zaka kuwa sehemu ya sheria ya taifa (Law.27: 30-32,
30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. 31 Na kama mtu akitaka kukomboa cho chote cha zaka yake, ataongeza sehemu yake ya tano juu yake. 32 Tena zaka yote ya ng'ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa Bwana.
Hes.18: 24, 26, 28
24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote. 26 Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka. 28 Hivyo ninyi nanyi mtasongeza sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana katika zaka zenu zote, mpokeazo mikononi mwa wana wa Israeli; kwa hiyo mtampa Haruni kuhani hiyo sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana.
Kumb. 12:6, 11, 17.)
6 pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng'ombe na ya kondoo; 11 wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana. 17 Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
Yesu hakuzuia zaka (Mt. 23: 23).
23 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache.
Waisraeli wa kiroho hutoa zaka zao kwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki (Hes. 5:9, 10, 7: 1 – 25).
Hesabu 5:9, 10
9 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyosongeza kwa kuhani, itakuwa ni yake. 10 Tena vitu vilivyowekwa wakfu na mtu awaye yote, vitakuwa ni vya kuhani; kitu cho chote mtu atakachompa kuhani, kitakuwa chake.
Hesabu 7:1 – 25
1 Ilikuwa siku hiyo Musa alipokwisha kuisimamisha maskani, na kuitia mafuta, na kuitakasa, na vyombo vyake vyote, na hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na kuvitia mafuta, na kuvitakasa; 2 ndipo wakuu wa Israeli, vichwa vya nyumba za baba zao, wakatoa matoleo; hao ndio wakuu wa kabila, hao ndio waliokuwa juu yao waliohesabiwa; 3 nao wakamletea Bwana matoleo yao, magari sita yenye mafuniko juu, na ng'ombe kumi na wawili; gari moja kwa wakuu wawili wawili, na ng'ombe mmoja kwa kila mkuu; nao wakayasongeza hapo mbele ya maskani. 4 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, 5 Pokea mikononi mwao, ili kwamba viwe vya kutumiwa katika utumishi wa hema ya kukutania; nawe utawapa Walawi vitu hivyo, kila mtu utampa kama utumishi wake ulivyo. 6 Basi Musa akapokea hayo magari, na ng'ombe, akawapa Walawi. 7 Wana wa Gershoni akawapa magari mawili na ng'ombe wanne, kama utumishi wao ulivyokuwa; 8 na wana wa Merari akawapa magari manne na ng'ombe wanane kama utumishi wao ulivyokuwa, chini ya mkono wa Ithamari, mwana wa Haruni kuhani. 9 Lakini hakuwapa wana wa Kohathi; maana, utumishi wa vile vitu vitakatifu ulikuwa ni wao; nao wakavichukua mabegani mwao. 10 Kisha wale wakuu wakatoa matoleo kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu, katika siku hiyo iliyotiwa mafuta, wakuu wakayatoa matoleo yao mbele ya madhabahu. 11 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Watasongeza matoleo yao, kila mkuu kwa siku yake, kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu. 12 Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda; 13 na matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha uzani wake ni shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga; 14 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kimejaa uvumba; 15 ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mmoja mume, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 16 mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; 17 na kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe waume wawili, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nashoni mwana wa Aminadabu. 18 Siku ya pili Nethaneli mwana wa Suari, mkuu wa Isakari, alitoa; 19 yeye akasongeza matoleo yake, sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa ni sadaka ya unga; 20 na kijiko kimoja cha dhahabu, uzani wake shekeli kumi, kilikuwa kimejaa uvumba; 21 na ng'ombe mmoja mume mchanga, na kondoo mume mmoja, na mwana-kondoo mume mmoja wa mwaka wa kwanza, kuwa sadaka ya kuteketezwa; 22 na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi; 23 na kwa dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe wawili waume, na kondoo waume watano, na mbuzi waume watano, na wana-kondoo watano waume wa mwaka wa kwanza; hayo ndiyo matoleo ya Nethaneli mwana wa Suari. 24 Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, mkuu wa wana wa Zabuloni; 25 matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;
Matumizi ya zaka: Law. 27:30,)
30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.
ni takatifu kwa Bwana. Ni ya kutumika kwenye nyumba ya Bwana (Mal. 3:10.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
1Kor. 9:11 – 14).
11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.
Bwana ameagiza wafanyao kazi ya injili wapate riziki yao kupitia injili. (1Kor.9:11-14).
11 Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? 12 Ikiwa wengine wanashiriki uwezo huu juu yenu, sisi si zaidi? Lakini hatukuutumia uwezo huo; bali twayavumilia mambo yote tusije tukaizuia Habari Njema ya Kristo. 13 Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? 14 Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili.
Washiriki wa Kanisa, kwa hiari yao huleta zaka ghalani, ili kiwemo chakula kwenye nyumba ya Mungu (Mal.3:10).
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Kwa maneno mengine, kwamba ziwepo fedha za kutosha kwenye Kanisa la Mungu kuliwezesha kutoa huduma yake na kupeleka injili kwa kile kiumbe.
Sadaka
Wakristo wakarimu hawatajizuilia michango yao kwa kanisa kwa zaka peke yake. Katika Israeli ya kale, ujenzi wa mahali pa ibada ilipatikana kwa michango ya ukarimu. (Kut. 36:2-7, cf.
2 Basi Musa akawaita Bezaleli na Oholiabu, na kila mtu aliyekuwa na moyo wa akili, ambaye Bwana alimtia moyoni mwake hekima, kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza ili aende kuifanya kazi hiyo; 3 nao wakapokea mkononi mwa Musa matoleo yote, ambayo hao wana wa Israeli walikuwa wameyaleta kwa ajili ya huo utumishi wa mahali patakatifu, ili wapafanye. Kisha wakamletea matoleo kila siku asubuhi kwa moyo wa kupenda. 4 Na hao watu wote wenye hekima, waliotumika katika kazi yote ya mahali patakatifu, wakaenda kila mtu kutoka katika kazi yake aliyokuwa akiifanya; 5 nao wakasema na Musa, na kumwambia, Watu waleta vitu vingi sana zaidi ya hivyo vitoshavyo kwa ajili ya utumishi wa hiyo kazi, ambayo Bwana aliagiza ifanywe. 6 Basi Musa akatoa amri, nao wakatangaza mbiu katika marago yote, wakisema, Wasifanye kazi tena, mtu mume wala mwanamke, kwa ajili ya matoleo kwa mahali patakatifu. Basi watu wakazuiwa wasilete tena. 7 Kwani vile vitu walivyokuwa navyo vilikuwa vyatosha kwa kuifanya kazi hiyo yote, kisha vilizidi.
, cf. 1Nya. 29:14.)
14 Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuweze kutoa kwa hiari hivi? Kwani vitu vyote vyatoka kwako na katika vitu vyako mwenyewe tumekutolea.
Sadaka za ukarimu ziliendesha ibada (Kut. 30:12-16,
12 Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapompa Bwana kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu. 13 Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini;) nusu shekeli kwa sadaka ya Bwana. 14 Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka ya Bwana. 15 Matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua, katika hiyo nusu shekeli, watakapotoa hiyo sadaka ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu. 16 Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania; ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele ya Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.
2Falm. 12:4, 5.
4 Yoashi akawaambia makuhani, Fedha yote ya vitu vitakatifu iliyoletwa nyumbani mwa Bwana, fedha ya matumizi, fedha ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na fedha yote iliyoletwa kama mtu ye yote aonavyo moyoni mwake kuileta nyumbani mwa Bwana, 5 makuhani na waitwae, kila mtu kwa hao awajuao; nao watatengeneza palipobomoka nyumbani, kila mahali palipoonekana pamebomoka.
2 Nyak. 24:4 – 13,
4 Ikawa baada ya haya, Yoashi alikuwa na nia ya kuitengeneza nyumba ya Mungu. 5 Akawakusanya makuhani na Walawi, akawaambia, Nendeni mijini mwa Yuda, mkakusanye katika Israeli wote fedha, ili kuitengeneza nyumba ya Mungu wenu mwaka kwa mwaka, mkafanye bidii kuliharakisha neno hili. Walakini Walawi hawakuliharakisha. 6 Mfalme akamwita Yehoyada mkuu wao, akamwambia, Mbona hukuwataka Walawi waitoze Yuda na Yerusalemu kodi ya Musa mtumishi wa Bwana, na ya kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya hema ya ushuhuda? 7 Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya Bwana wamewapatia mabaali. 8 Basi mfalme akaamuru, nao wakafanyiza kasha, wakaliweka nje langoni pa nyumba ya Bwana. 9 Wakapiga mbiu katika Yuda na Yerusalemu, kumletea Bwana kodi aliyoiweka Musa mtumishi wa Mungu, juu ya Israeli jangwani. 10 Wakafurahi maakida wote na watu wote, wakaleta na kutia ndani ya kasha, hata wakaisha. 11 Ikawa wakati walipoletewa kasha wasimamizi wa mfalme kwa mkono wa Walawi, nao wakaona ya kwamba kuna fedha nyingi, huja karani wa mfalme, na msimamizi wake kuhani mkuu, wakatoa yaliyomo kashani, kisha hulichukua kasha, na kulirudisha mahali pake. Ndivyo walivyofanya siku kwa siku, wakakusanya fedha tele. 12 Na mfalme na Yehoyada waliwapa hao waliofanya kazi ya utumishi wa nyumba ya Bwana; nao wakawaajiri waashi na maseremala ili kuitengeza nyumba ya Bwana, na hao pia wafuao chuma na shaba ili kuitengeza nyumba ya Bwana. 13 Hivyo mafundi wakafanya kazi yao, nao wakaimaliza, wakaisimamisha nyumba ya Mungu kama ilivyopasa, wakaifanya imara.
Neh. 10:32, 33).
32 Tena tukajifanyia maagizo, kujitoza mwaka kwa mwaka theluthi ya shekeli kwa huduma ya nyumba ya Mungu wetu; 33 kwa mikate ya wonyesho, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.
Wale waliopewa vingi, vitadaiwa kwao pia vingi (Luk. 12:48.)
48 Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Ukipokea bure, toa bure (Mt. 10: 8.)
8 Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.
Hakuna katika agano jipya kunakohafifisha utaratibu wa sadaka.
Ni yakini Waisraeli walimtolea Mungu viwango vinapofikia robo hata theluthi ya mapato yao. Je, kwa kutoa kwao hivyo waliingia kwenye ufukara? Hapana. Badala yake Mungu aliahidi kuwabariki kwa uaminifu wao. (Mal.3:10-12).
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la. 11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi. 12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
Tumeitwa kumrudia Mungu atupaye upendeleo (Mal. 3: 7)
7 Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
Tunapoacha, tunaitwa wezi na kulaaniwa (Mal. 3: 8, 9.)
8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
Kinachosalia Baada ya Zaka na Sadaka
Mali yaweza kuwa nguvu ya mema. Mema tunayotendea watu wahitaji, huwa tunamtenda Kristo (Mt. 25: 34 – 40).
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; 35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; 36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia. 37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? 38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? 39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia? 40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Dini iliyo safi inajumuisha kanuni ya kuwajali wahitaji katika jamii kwa nafasi zao kama wajane, yatima na kujilinda na dunia pasipo mawaa. ( Yak. 1:27).
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Amhurumiaye maskini, humkopesha BWANA (Mith. 19:17).
17 Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.
Kutunza familia ni wajibu na wanaoudharau, hawafai kuliko wasio waamini. (1Tim. 5: 8).
8 Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.
Manufaa ya Uwakili:
Kwa Mtu binafsi
Kwamba tumeonywa kujilinda na choyo kwani uzima wa mtu haupo kwenye vitu alivyo navyo.(Luk. 12:15).
15 Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Uwakili huongoza kuisulubisha mwili na tamaa zake. (Gal.5:24).
24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.
Siku moja Yesu atasema “kadiri mlivyowatendea hao, mlinitendea mimi” (Mt.25:40).
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
Kwa wengine
“Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo, huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.” 1Tim.6:18, 19,).
18 Watende mema, wawe matajiri kwa kutenda mema, wawe tayari kutoa mali zao, washirikiane na wengine kwa moyo; 19 huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Kwa kanisa
Kupokea mpango wa Biblia wa uwakili ni muhimu kwa uhai wa Kanisa. Kwa kutoa kwao hulifanya kanisa liwe imara katika kutimiza utume wake na kupeleka injili kwa wote, ili Yesu arudi (Mt. 24:14).
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.