Umoja Katika Mwili wa Kristo

Utangulizi


Kanisa ni mwili moja wenye viungo vingi, vilivyoitwa kutoka katika kila taifa, kabila, lugha na jamaa. Katika Kristo tu uumbaji mpya; tofauti za rangi, utamaduni, elimu na utaifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu na ya chini, tajiri na maskini, mwanamume na mwanamke miongoni mwetu visitugawanye. Sisi sote ni sawa katika Kristo, ambaye kwa Roho mmoja, ametungamanisha katika ushirika mmoja pamoja Naye na sisi kwa sisi; yatupasa tutumike na kutumikiwa bila upendeleo au usetiri. Kupitia ufunuo wa Yesu Kristo katika Maandiko Matakatifu tunashiriki imani ile ile, na tumaini, na kuwafikia wote kwa ushuhuda mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu mwenye nafsi tatu, ambaye ametufanya kuwa watoto wake. (Rum.12:4, 5; 1Kor.12:12-14; Mt. 28:19, 20; Zab.133:1; 2Kor.5:16, 17; Mdo.17:26, 27; Gal. 3:27, 29; Kol.3:10-15; Efe.4:14-16; 4:1-6; Yoh.17:20-23)

Yesu baada ya kukamilisha jukumu lake duniani (Yoh.17:4) aliendelea kunyong’onyea kwa hali ya wanafunzi wake hata katika jioni ile kabla ya kusulubishwa. Wivu ulikuwa umetawala juu ya nani atakuwa na nafasi kubwa katika ufalme wa Kristo. Maelezo ya Yesu kwamba unyenyekevu ndio tunu kwenye ufalme wake yalionekana kuyafikia masikio yaliyoziba. (Luk.17:10). Hata kielelezo cha kuinama na kuosha miguu, hakikutosha kufikisha ujumbe. (Yoh.13:12-15). Yesu ni pendo na ndio maana alifuatwa na umati wa watu. Wanafunzi hawakuelewa jambo hilo na ndiyo maana waliwabagua wanawake, wasio Wayahudi, wenye dhambi na maskini. Ni upendo ndio unaomtambulisha Kristo na kututofautisha na ulimwengu (cf. Yoh.13:34, 35). Hata Getsemane, jambo kubwa lililomwelemea Yesu lilikuwa umoja wa Kanisa. (Yoh.17:21). Umoja ni zana isiyoshindwa ya kumshuhudia Yesu. (Yoh.17:23)

Umoja Kimaandiko na Kanisa

Hivi Kristo aliopoombea umoja, alikuwa na nia gani kwa ajili ya Kanisa linaloonekana leo? Huo upendo na umoja unawezekanaje? Misingi yake ni nini?

Umoja wa Roho

Roho Mtakatifu ndiye uwezo unaoshikilia umoja wa Kanisa. Kupitia kwake waumini wanavutwa kuingia Kanisani kwa kuwa wamebatizwa katika mwili moja. (1Kor.12:13). Waliobatizwa wapaswa kuwa na kile Paulo anachokiita umoja wa Roho. (Efe.4:3). Umoja huu ni wa mwili moja na Roho Moja kutokana na kumwamini Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja aliye Baba wa wote. (Efe.4:4-6).

Akiwaita watoke kwenye kila taifa na rangi, Roho Mtakatifu huwabatiza watu waingie katika mwili mmoja ambalo ndilo Kanisa.(cf.1Pet.2:5). Kila kanisa liko sawa, hata kama kuna makanisa yanayopokea misaada ya kiutume kutoka makanisa mengine.

Kanisa lenye umoja lina tumaini moja, “tumaini lenye baraka” ambalo litatimia katika “mafunuo ya utukufu wa Kristo, Mungu mkuu na Mwokozi wetu.” (Tit.2:13). Tumaini hili ni chanzo cha amani na furaha na hututia nguvu kuhubiri (Mt.24:14). Hutuongoza kubadilika kuwa watakatifu ili kufanana naye (1Yoh.3:3).

Kutokana na imani moja, imani ya mtu binafsi katika kifo cha Yesu kinalipia deni la dhambi, wote tunakuwa sehemu ya mwili moja. Ubatizo ambao huelezea kifo cha Yesu (Rum.6:3-6), huelezea vema ushuhuda wa umoja huu. Hatimaye Maandiko hufundisha kwamba yuko Roho mmoja, Bwana mmoja na Mungu mmoja ambaye ni Baba.

Mambo yote ya umoja hupatana katika Umoja katika Utatu Mtakatifu. Kwamba ziko karama tofauti, huduma tofauti, lakini ni kwa ajili ya Bwana yuleyule. Iko tofauti katika utendaji lakini ni Mungu azitendaye kazi zote katika wote. (1Kor.12:4-6).

Umoja hadi kufikia hatua gani?

Waumini hupitia uzoefu wa umoja wa kunia na kufanya maamuzi. Wanapaswa “kunia mamoja…na shauri moja” (Rum.15:5, 6; 1Kor.1:10). “Mkae kwa amani na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. (2Kor.13:11).

Umoja katika kutofautiana

Umoja wa kibiblia haumaanishi kufanana. Kwa kutumia mfano wa mwili wa mtu, ina maana umoja huwepo kwa kutofautiana. Mwili una viungo vingi lakini hufanya kazi tofauti, na hivyo, hakuna kiungo kisicho na kazi. Kanuni hiyo hutumika kanisani, Mungu anapogawa karama kadiri apendavyo. (1Kor.12:11). Ili kukamilisha utume, Kanisa lahitaji viungo vyake vyote. Yesu alitumia mfano wa mzabibu, kwamba Yeye ni mzabibu na wafuasi wake ni matawi. (Yoh.15:1-6). Kila tawi laweza ni mwendelezo wa mzabibu wa kweli, yaani Kristo. Zipo karama nyingi lakini Roho ni mmoja. Vile vile utendaji ni tofauti lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote katika wote. (1Kor.12:6)

Umoja katika Imani

Kuwepo tofauti katika karama, haina maana kwamba kutakuwapo tofauti katika imani. Katika siku za mwisho, watakatifu wote watajulikana kwa kuwa washirika wa injili ya milele (Uf.12:6) wenye kuzishika amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu. (Uf.14:12).

Umoja unao umuhimu gani?

Pasipo umoja, kanisa halitaweza kuutimiza utume wake. Umoja hufanya Juhudi ya Kanisa ifanikiwe. Katika ulimwengu uliovunjika kwa kutoridhika na migogoro, upendo na umoja wa washiriki wa kanisa wa aina tofauti, tabia tofauti na nafasi tofauti kwa vyeo, elimu na mali, hushuhudia ujumbe wa kanisa kuliko kitu chochote. Hili huonyesha muungano wao na mbinguni na kuthibitisha kwamba ni wanafunzi wa Kristo. (Yoh.13:35). Migogoro ya kikristo imefanya wasioamini watilie shaka ujumbe wa kikristo, na imekuwa kikwazo kikubwa kwa wao kuipokea injili. Umoja huvunja mtazamo huo. (Yoh.17:23)

Umoja hufunua Uhalisi wa ufalme wa Mungu

Kanisa lililoungana duniani huonyesha umakini wa wakristo katika matazamio yao ya kwenda kuishi pamoja mbinguni. Ufalme wa milele wa Mungu unafunuliwa na hutimiza maneno ya “Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza, ndugu wakae pamoja na kwa umoja.” (Zab.133:1)

Umoja huonesha nguvu ya Kanisa. Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kanisa huwa na ustawi na kuwa imara wakati washiriki wake wameungana na Kristo na wao kwa wao. Ndipo wanapokuwa watenda kazi pamoja na Mungu (1Kor.3:9).

Kuufikia Umoja

Chanzo cha umoja

Maandiko Matakatifu huonyesha kuwa umoja una chanzo katika (1) uwezo wa Baba Mungu, (Yoh.17:11); (2) Utukufu wa Baba ambao Yesu aliwapa wafuasi wake (Yoh.17:22); Kristo kukaa ndani ya waumini (Yoh.17:23). Roho Mtakatifu, Roho wa Kristo, ndiyo uwezo na kinachofanyisha kila kiungo kushikamana kwa umoja.

Roho Mtakatifu mwunganishi

Lengo ni umoja

Roho anapoingia kwa waumini, hufanya wapande juu dhidi ya mitazamo hasi ya tofauti za tamaduni, rangi, jinsia, utaifa na hadhi. (Gal.3:26-28).

Jukumu la karama za Roho kukamilisha umoja.

Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii, na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikilia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo na kimo cha utimilifu wa Kristo” (Efe.4:11-13). Tofauti ya karama zitakuza umoja wa Roho kuwa umoja wa imani (Efe.4:3, 13). Waumini wataimarika hata hawatadanganyika (Efe.4:14). Kupitia karama za Roho, waumini huusema ukweli kwa upendo na kukua katika Kristo, aliye kiongozi wa Kanisa. (Efe.4:16)

Msingi wa umoja

Ni kama Roho wa kweli (Yoh.15:26) Roho Mtakatifu atendaye kazi kutimiza ahadi ya Kristo. Jukumu lake ni kuongoza waumini katika kweli yote (Yoh.16:13). Kwa uwazi kinachofuatia ni kuwa, ukweli uliojengwa kwa Kristo ndio msingi wa umoja. Ni kweli kuwa ushirika, karama za roho, na upendo ni muhimu, lakini utimilifu wake huja kwa yule aliye kweli, na njia na uzima. (Yoh.14:6). Yesu aliomba uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli (Yoh.17:17). Kupata uzoefu wa umoja, waumini wapaswa kupokea nuru itokayo kwenye Neno. Ukweli huu ukikaa ndani, utawatakasa, kuwainua na kusafisha maisha, ukiondoa chuki na misuguano.

Amri Mpya ya Yesu

Kama mwanadamu, Kanisa limeumbwa kwa mfano wa na sura ya Mungu. Kristo aliagiza waumini wadhihirishe upendo wao kwa Mungu kwa kupendana wao kwa wao. (Mt.22:39). Kristo mwenyewe aliitii amri ya upendo kwa kipeo cha juu hadi Kalvari. Kabla ya kufa kwake aliagiza waumini wapendane, kama Yeye alivyotupenda. (Yoh.15:12 cf. Yoh.13:34).

Alikuwa kama anasema, “nawaagiza msisimamie haki zenu, kuona kwamba mnapokea mnachostahili, eti ikishindikana, mshitaki. Nawaagiza ninyi kuachia migongo wazi ili ichapwe, kugeuza shavu lenu mpigwe, kushtakiwa uwongo, kudhihakiwa, kukejeliwa, kuchubuliwa, kuvunjwavunjwa, kupigiliwa misumari kufa na kuzikwa, ikiwa kutenda hivyo, kutakuwa kuonyesha upendo wenu kwa wengine kama mimi nilivyofanya.

Kusikowezekana kunakowezekana

Je, twawezaje kupenda kama Kristo alivyopenda? Hili ni jambo lisilowezekana. Yesu anadai kisichowezekana. Hata hivyo ameahidi, Nami nikiinuliwa juu ya nchi nitawavuta wote kwangu (Yoh.12:32) Umoja katika mwili wa Kristo ni jambo lililotamkwa liwezekane. Una mizizi kwenye msalaba na kuchipua mioyoni mwa waumini.

Umoja katika msalaba

Tunapotambua kuwa pasipo Yeye hatuwezi kufanya lolote (Yoh.15:5), ndipo tunauona upendo wa Yesu kwa kuwa alikufa kwa ajili ya kila mtu pamoja na tofauti tulizonazo. Anatupenda sawa, yaani watu wa kila taifa, rangi, jamii na matabaka. Kalvari inamaanisha kuchukuliana mizigo (Gal.6:2). Alibeba mzigo wote wa mwanadamu uliovunja maisha Yake ili atupatie sisi uhai na kutuweka huru tupate kusaidiana.

Hatua za kufikia umoja.

Umoja hauji moja moja. Yapaswa kupitia hatua kuufikia.

1. Umoja nyumbani.

Eneo muhimu kwa ajili ya kufundisha umoja ni kwenye familia. (Zab.133:1)

2. Kukusudia kuwa na umoja

Hatutafikia umoja tusipoufanyia kazi kwa njia ya kuondoa tofauti kwa mazungumzo na kuuombea.

3. Kufanya kazi pamoja kufikia lengo la pamoja

Kanisa halitafikia umoja hadi, likifanya kazi kama kikosi kimoja, kutangaza habari njema ya ufalme.(Mt.28:19). Twapaswa kuunganisha huduma ya kuponya na kuhubiri, kama Yesu alivyofanya. (Luk.9:2; 10:9).

4. Kuwa na mtazamo wa kiulimwengu

Enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Pasipo kutazama kanisa kiulimwengu, haiwezekani kufikia umoja.

5. Kuondoa mitazamo inayoleta mgawanyo

Mitazamo ya kiubinafsi, kiburi, kujiamini, kujiona, chuki, kukosoa, kukemea and kutafutana makosa huchangia kudorora umoja wa kanisa. Mtazamo mpya wa Kalvari kutachipusha upendo wetu sisi kwa sisi (1Yoh.4:9-11). Paulo alitoa ushauri wa kutembea kwa roho (Gal.5:16) na kutembea huko huleta matunda ya roho ambayo ni dawa ya kufarakana. (Gal.5:22, 23). Yakobo alishauri kuepuka kupendeleana. (Yak. 2:9) hii ni kwa sababu Mungu hana upendeleo. (Mdo.10:34). Ni sawa kuheshimiana lakini kamwe tusione watu wengine kuwa wanapendwa zaidi na Mungu kuliko wenzao. (Mt.25:40). Kama Yesu kwa kuwa mwana wa Adamu alivyokuwa kaka kwa kila mtu, ndivyo alivyotutuma kwenda kuhubiri injili ya milele kwa kila taifa, lugha na jamaa.

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Warumi 12:4, 5X
4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
1 Wakorintho 12:12-14X
12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
Zaburi 133:1X
1 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
2 Wakorintho 5:16, 17X
16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. 17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Matendo 17:26, 27X
Matendo 3:27, 29X
27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. 29 Basi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wanadamu.
Wakolosai 3:10-15X
10 mkivaa utu mpya, unaofanywa upya upate ufahamu sawasawa na mfano wake yeye aliyeuumba. 11 Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, mgeni wala mshenzi, mtumwa wala mwungwana, bali Kristo ni yote, na katika yote. 12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, 13 mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. 15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
Waefeso 4:14-16X
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Waefeso 4:1-6X
1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; 2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
Yohana 17:20-23X
20 Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. 21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. 22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. 23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Yohana 17:4X
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
Luka 17:10X
10 Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Yohana 13:12-15X
12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo.
Yohana 13:34, 35X
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. 35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Yohana 17:21X
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Yohana 17:23X
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
1 Wakorintho 12:13X
13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
Waefeso 4:3X
3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
Waefeso 4:4-6X
4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
1 Petro 2:5X
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
Tito 2:13X
13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Mathayo 24:14X
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
1 Yohana 3:3X
3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
Warumi 6:3-6X
3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena;
1 Wakorintho 12:4-6X
4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Warumi 15:5, 6X
5 Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; 6 ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Wakorintho 1:10X
10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
2 Wakorintho 13:11X
11 Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
1 Wakorintho 12:11X
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Yohana 15:1-6X
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.
1 Wakorintho 12:6X
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Ufunuo 12:6X
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
Ufunuo 14:12X
12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Yohana 13:35X
35 Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Yohana 17:23X
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Zaburi 133:1X
1 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
1 Wakorintho 3:9X
9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Yohana 17:11X
11 Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.
Yohana 17:22X
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
Yohana 17:23X
23 Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
Wagalatia 3:26-28X
26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
Waefeso 4:11-13X
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Waefeso 4:3, 13X
3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Waefeso 4:14X
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.
Waefeso 4:16X
16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Yohana 15:26X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Yohana 16:13X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 14:6X
6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yohana 17:17X
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
Mathayo 22:39X
39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
Yohana 15:12 X
12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
Yohana 13:34X
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Yohana 12:32X
32 Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.
Yohana 15:5X
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Wagalatia 6:2X
2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.
Zaburi 133:1X
1 Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja.
Mathayo 28:19X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Luka 9:2X
2 Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.
Luka 10:9X
9 waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
1 Yohana 4:9-11X
9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. 10 Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 11 Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.
Wagalatia 5:16X
16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.
Wagalatia 5:22, 23X
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Yakobo 2:9X
9 Bali mkiwapendelea watu, mwafanya dhambi na kuhukumiwa na sheria kuwa wakosaji.
Matendo 10:34X
34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo;
Mathayo 25:40X
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
1 Wakorintho 1:10X
10 Basi ndugu, nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.