Mungu Mwana wa milele alifanyika mwili katika Yesu Kristo. Katika Yeye vitu vyote viliumbwa, tabia ya Mungu imefunuliwa katika Yeye, wokovu wa jamii yote ya mwanadamu unakamilishwa na ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu aliye Kristo. Alizaliwa na bikira Mariamu kutokana na mimba iliyotungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu alioneysha mfano wa haki na upendo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha uwezo wa Mungu na alithibitishwa kuwa Masihi aliyeahidiwa. Aliteswa na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, alifufuliwa kutoka katika wafu, na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa ajili yetu. Atakuja tena kwa utukufu mwingi kwa ukombozi wa mwisho wa watu wake na kurejeshwa kwa vitu vyote.” (Yoh.1:1-3, 14; Kol.1:15-19; Yoh.10:30; 14:9; 2Kor.5:17-19; Yoh.5:22, 23; Luk.1:35; Filp. 2:5-11; 1Kor.15:3, 4; Ebr.2:9-18; 4:15; 7:25; 8:1, 2;Yoh.14:1-3)
Jangwa liligeuka janga la majoka. Nyoka walilala karibu na vyungu vya kupikia, walijiviringa kwenye mambo za kujengea mahema, walisubiri kwenye mahali pa kulala. Kuuma kwao kulizama ndani, wakitema sumu za kufisha. Jangwa ambalo lilikuwa kimbilio la Waisraeli, sasa liligeuka mahali pa kuzikia. Watu kwa mamia walilala wakifa. Wakitambua kero yao, watu waliharakisha kumwendea Musa. Musa akaombea watu (Hes.21:7). Jibu la Mungu la maombi? Tengeneza nyoka wa shaba na mwinue na yeyote atakayemwangalia ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi (Hes.21:9). Nyoka daima amekuwa kielelezo cha Shetani (Mwa.3, Ufu. 12) akiwakilisha dhambi. Kambi ilikuwa imetumbukia kwenye mikono ya Shetani. Dawa aliyotoa Mungu haikuwa kuangalia mwana kondoo kwenye madhabahu patakatifu bali kuangalia nyoka wa shaba.
Ilikuwa kielelezo cha kushangaza kwa Kristo. Kama nyoka aumaye alivyoinuliwa juu ya nguzo, Yesu naye aliinuliwa kwenye nguzo. Yesu alitumwa kwa mwili wa dhambi (Rum.8:3), alipaswa kuinuliwa juu ya msalaba wa aibu (Yoh.3:14, 15). Alikuwa dhambi, akichukua dhambi za kila mmoja aliyepata au atakayepata kuishi. “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yeetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. (2Kor.5:21)
Kufanyika Mwili – Utabiri na Utimilifu wake
Mpango wa Mungu kuokoa wale waliotanga mbali na hekima yake (Yoh.3:16; 1Yoh.4:9) kwa ushawishi mkubwa, inafunua upendo wake. Katika mpango huo, Mwana wake “aliyejulikana zamani kabla haijawekwa misingi ya dunia” alikuwa kafara kwa ajili ya dhambi, tumaini la mwanadamu (1Pet. 1:19, 20). Angeturejeza kwa Mungu kwa kuzivunja kazi za Ibilisi (1Pet.3:18; Mt.1:21; 1Yoh. 3:8).
Dhambi ilimkatilia mbali Adam na Hawa kutoka kwenye chanzo cha uzima na ingesababisha mauti ya mara moja. Lakini kutokana na mpango uliowekwa kabla ya misingi ya dunia (1Pet.1:20, 21), shauri la amani (Zek.6:13, Mungu Mwana aliingilia kati yao na hukumu ya Mungu, akaweka daraja kwa utengano na kuzuilia kifo. Hata kabla ya msalaba, neema yake iliwaweka hai wenye dhambi na kuwahakikishia wokovu. Lakini kuturejeza kikamilifu kama wana na binti wa Mungu, alilazimika kuja kama mwanadamu.
Mara baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi, Mungu aliwapa tumaini kwa kuingiza uadui baina ya nyoka na mwanamke, baina ya uzao wa nyoka na uzao wa mwanamke. Katika tamko la Mwanzo 3:15, nyoka na uzao wake unawakilisha Shetani na wafuasi wake, na mwanamke na uzao wake unamwakilisha watu wa Mungu na Mwokozi wa ulimwengu. Hakuna ambaye angebaki pasipo kujeruhiwa. Kutoka wakati huo, wanadamu wamemtafuta aliyeahidiwa. Agano la Kale, hufunua kutafuta huko. Unabii unasema kwamba Aliyeahidiwa akija, ulimwengu utakuwa na ushahidi wa kumtambua.
Onyesho la Kiunabii la Wokovu
Baada ya dhambi kuingia, Mungu alianzisha utaratibu wa kafara za wanyama kama kielelezo cha utume wa mwokozi ajaye. Utaratibu huu wa kielelezo, ulionyesha jinsi Mungu Mwana angeondosha dhambi.
Kwa sababu ya dhambi – uasi wa sheria ya Mungu – wanadamu walikabiliwa na kifo. (Mwa.2:17; 3:19; 1Yoh.3:4; Rum.6:23). Sheria ya Mungu ilihitaji kifo cha mdhambi. Lakini kwa upendo wake usio na kipimo, Mungu alimtoa Mwana wake “ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele (Yoh.3:16). Kitendo cha kujinyenyekeza kwa hali ya juu namna gani! Mungu, Mwana wa milele analipia adhabu ya dhambi, ili atupatie msamaha na upatanisho na Mungu.
Baada ya Waisraeli kutoka Misri, matoleo ya kafara yalifanyikia kwenye hema ya kukutania kama sehemu ya mahusiano ya maagano baina ya Mungu na watu wake. Likijengwa na Musa kufuatana na hekalu la mbinguni, hema takatifu na huduma zake lilianzishwa kuelezea mpango wa wokovu (Kut.25:8; 9, 40;Ebr.8:1-5).
Kupata msamaha, mdhambi aliyetubu alileta mnyama wa kafara asiye na ila, akimwakilisha Mwokozi asiye na dhambi. Ndipo mwenye dhambi aliweka mikono yake juu ya mnyama asiye na kosa na kuungama dhambi zake (Law.1:3, 4). Kitendo hicho kiliwakilisha kuhamisha dhambi kutoka kwa mdhambi hadi kwa mhanga asiye na kosa, ikitoa picha ya hali ya kubadilishana ya kafara.
Kwa kuwa pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi (Ebr.9:22), ndipo mdhambi alipomwua mnyama, akifanya hali ya kuleta kifo ya dhambi ilivyo wazi. Ni njia ya maumivu ya kuelezea tumaini, lakini ndiyo njia pekee ya mdhambi ya kuonyesha imani. Baada ya huduma ya Kuhani (Law. 4-7), mwenye dhambi alipokea msamaha wa dhambi zake kwa imani yake katika kifo mbadala cha Mkombazi ajaye; ambacho kafara ilidhihirisha. (Law.4:26, 31, 35). Agano Jipya linamtambua Yesu kuwa ni Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu (Yoh.1:29). Kupitia damu yake ya thamani “kama mwanakondoo asiye na ila wala waa” (1Pet.1:19) alipata ukombozi wa mwanadamu kutoka kwenye hatma ya adhabu ya dhambi.
Utabiri Juu ya Mwokozi
Mungu aliahidi kwamba Mwokozi – Mesiya- Mtiwa mafuta atatokea kupitia uzao wa Ibrahimu; “katika uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa” (Mwa.22:18; cf. 12:3) Isaya alitabiri kuwa Mwokozi atakuja kama mtoto wa kiume, atazaliwa akiwa Mungu na Mwanadamu “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani” (Isa. 9:6). Mkombozi huyu, angekalia kiti cha enzi cha Daudi na kuanzisha ufalme wa miele wa amani (Isa. 9:7). Bethlehemu ndiko ambako angezaliwa (Mik.5:2).
Kuzaliwa kwake Mungu mwanadamu huyu kutakuwa siyo kwa kawaida. Ikinukuu Isaya 7:14, Agano Jipya linasema: “Tazama bikira atachukua mimba, na kuzaa Mwana, nao watamwita jina lake Imanueli, maana yake, Mungu pamoja nasi” (Mt.1:23).
Utume wa Mwokozi unaelezewa kwa maneno haya: “Roho ya Bwana Mungu I juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwanganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao (Isa.61:1, 2 cf. Luk. 4:18, 19).
Cha kushangaza, Masihi angekataliwa. Atahesabika kuwa “mzizi kwenye nchi kavu. Yeye hana umbo wala uzuri; na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani… alidharauliwa na kukataliwa na watu, mtu wa huzuni nyingi ajuaye sikitiko, na kama mtu ambaye humficha nyuso zao, …hatukumhesabu kuwa ni kitu” (Isa.53:2-4).
Rafiki wa karibu atamsaliti (Zab.41:9) kwa vipande thelathini vya pesa (Zek.11:12). Wakati wa mashtaka yake, angetemewa mate na kupigwa (Zab.50:6). Wale watakaomwua watapigia kura mavazi yake aliyovaa (Zab.22:18). Hakuna mfupa wake utakaovunjika (Zab.34:20). Hata hivyo ubavu wake moja utachomwa (Zek.12:10). Katika masumbufu hatapinga lakini, “kama kondoo akatwavyo manyoya yake, atanyamaza kimya” (Isa.53:7).
Mwokozi asiye na hatia ataumia sana kwa wenye dhambi. “Hakika ameyachukua masikitiko yetu…Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake tumepona. Na BWANA ameweka juu yake, maovu yetu yote…Maana alikatiliwa mbali nan chi ya walio hai, alipigwa kwa makosa ya watu wangu” (Isa.53:4-8).
Mwokozi Atambulishwa
Ni Yesu Kristo tu ndiye aliyetimiza unabii huu. Maandiko yanaonyesha uzao wake kupitia Ibrahimu, Ikimwita Mwana wa Ibrahimu (Mt.1:1), na Paulo anathibitisha kwamba ahadi kwa Ibrahimu na uzao wake ilitimizwa katika Kristo. (Gal.3:16). Cheo cha Masihi Mwana wa Daudi kilitumika (Mt.21:9). Alitambulika kuwa Masihi aliyeahidiwa ambaye angekalia kiti cha enzi cha Daudi (Mdo.2:29, 30).
Kuzaliwa Yesu kulikuwa kwa miujiza. Bikira Mariam alionekana ana ujauzito wa Roho Mtakatifu. (Mt. 1:18-23). Amri ya kirumi ilimleta hadi Bethlehemu, mahali ilipotabiriwa atazaliwa (Luk.2:4-7). Mojawapo ya majina ya Yesu ni Imanueli, au Mungu pamoja nasi ambayo inaakisi hali ya Uungu na uanadamu na hutambulisha wa Mungu pamoja na wanadamu (Mt.1:23). Jina Yesu lililenga kuonyesha huduma yake kumwokoa mwanadamu. “Nawe utamwita jina lake Yesu kwani ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mt.1:21). Yesu alitambulisha huduma yake na Masihi aliyetabiriwa katika Isaya 61:1, 2: “Leo Maandiko haya yametimia masikioni mwenu” (Luk. 4:17-21). Ijapokuwa alileta mguso mkubwa kwa watu, kwa ujumla, ujumbe wake ulikataliwa (Yoh.1:11; Luk.23:18). Isipokuwa kwa watu wachache, hakutambulikana kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Badala ya kukubaliwa, alikabiliwa na vitisho vya kifo (Yoh.5:16; 7:19; 11:53).
Kuelekea mwisho wa miaka mitatu na nusu ya huduma, Yuda Iskariote, mwanafunzi, alimsaliti (Yoh.13:18; 18:2) kwa vipande thelathini vya fedha (Mt.26:14, 15). Badala ya kupambana, aliwakemea kwa kujaribu kumlinda (Yoh.18:4-11). Ijapokuwa hakuwa na hatia ya kosa lolote la jinai, chini ya saa ishirini na nne tangu kutiwa kwake mbaroni, alikuwa ametemewa mate, amepigwa, ameshtakiwa, amehukumiwa kifo na kusulubishwa (Mt.26:67; Yoh.19:1-16; Luk.23:14, 15). Askari waligombea mavazi yake na kupigia kura (Yoh.19:23, 24). Wakati wa kusulubiwa kwake, hakuna mfupa wake uliovunjika (Yoh.19:32, 33, 36), na baada ya kufa, askari walimchoma ubavuni kwa mkuki (Yoh.19:34, 37).
Wafuasi wa Kristo walitambua kifo chake kuwa kafara pekee itoshayo kwa wenye dhambi. “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu siis, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa wenye dhambi” (Rum.5:8). Mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yenu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.” (Efe.5:2).
Wakati wa Huduma yake na Kifo
Biblia hufunua kwamba Mungu alimtuma Mwana wake duniani katika “utimilifu wa wakati| (Gal.4:4). Yesu alipoanza huduma yake, alitangaza, “Wakati umetimia” (Mk.1:15). Marejeo haya kwa wakati hudokeza kwamba utume wa Mwokozi ulitekelezwa kwa kuzingatia ratiba makini ya kiunabii. Zaidi ya karne tano awali, kupitia Danieli, Mungu alitabiri wakati halisi wa Kristo kuanza huduma na wakati wa kufa kwake. Kuelekea mwisho wa miaka sabini ya utumwa wa Israeli Babeli, Mungu alimwambia Danieli kwamba alitenga wakati wa rehema kwa Wayahudi na jiji la Yerusalemu kuwa majuma sabini. Katika kipindi hicho, kwa kutubu na kujiandaa wenyewe kwa ujio wa Masihi, taifa la Uyahudi lilipaswa kutimiza makusudi ya Mungu kwa ajili yao.
Danieli pia aliandika juu ya “upatanisho kwa ajili ya uovu” na “kuleta haki ya milele” kuwa alama za kutambua wakati husika. Hivi vitendo vya Masihi huonyesha kuwa Mwokozi alipaswa kuja katika kipindi hicho. (Dan.9:24). Unabii wa Danieli ulitaja wakati halisi wa kuja Masihi kuwa ni” majuma saba na majuma sitini na mawili” yaani jumla ya majuma sitini na tisa, baada ya amri ya kuijenga upya Yerusalemu. (Dan.9:25). Baada ya juma la sitini na tisa, Masihi “atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu (yaani siyo kwa mambo yanayomhusu mwenyewe) (Dan.9:26) ikimaanisha kifo chake kwa ajili ya wanadamu. Alikuwa afe katikati ya juma la sabini, “kuikomesha sadaka na dhabihu” (Dan.9:27).
Ufunguo wa kuelewa unabii wa wakati imejengwa juu ya kanuni kwamba, siku katika wakati wa unabii, huhesabika kuwa ni mwaka moja wa kawaida (Hes.14:34; Eze. 4:6). Kufuatana na kanuni hii ya siku sawa na mwaka, majuma sabini yaani siku 490 zinamaanisha miaka 490. Danieli anasema kwamba kipindi hiki kingeanza kwa “kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu. (Dan.9:25). Amri hii ya kuwapa Wayahudi uhuru wa kujiendeshea mambo wenyewe, ilitolewa mwaka wa saba wa Mfalme wa Kiajemi Atashasta na ikatekelezwa wakati wa kiangazi mwaka 457 KK. (Ezr.7:8, 12-26; 9:9). Kufuatana na unabii, miaka 483 (majuma 69 ya kiunabii), baada ya amri, Masihi, Mkuu atatokea. Miaka mia nne na themanini na tatu baada ya mwaka 457KK inatuleta mwaka 27BK, wakati Yesu alipobatizwa na kuanza huduma yake. Kwa kukubali tarehe za mwaka 457KK na 27BK, inasemwa kuwa ni unabii wa kale uliotimizwa kwa usahihi kweli kweli. Ni Mungu ndiye ambaye angeweza kutabiri ujio wa Mwana wake duniani kwa usahihi mkuu kiasi hicho.
Katika ubatizo wake Yordani, Yesu alitiwa mafuta na Roho Mtakatifu na kutambuliwa na Mungu kuwa Masihi (Kiebrania) au Kristo (Kigiriki) yote yakiwa na maana ya Mtiwa mafuta. (Luk3:21; Mdo.10:38; Yoh.1:41). Tamko la Yesu “Wakati umetimia” (Mk.1:15) ilirejea kutimizwa kwa unabii huu wa wakati. Katikati ya juma la sabini, masika ya mwaka 31BK, miaka mitatu na nusu halisi baada ya Yesu kubatizwa, Masihi alikomesha mfumo wa kafara kwa kutoa uhai wake. Wakati wa kifo chake, pazia la hekalu lilipasuka kutoka juu hadi chini (Mt.27:51) ikimaanisha kuondoshwa kwa huduma za hekalu.
Matoleo na kafara zote zilisonda kwa kafara itoshayo ya Masihi. Wakati Kristo, Mwanakondoo halisi wa Mungu alipochinjwa Kalvari kama fidia kwa dhambi zetu (1Pet.1:19), mfano ulikutana na kivuli vilikutana na halisi. Huduma za hekalu la dunia hazikuwa muhimu tena. Kwa wakati ule uliotabiriwa wakati wa Sikukuu ya Pasaka, alikufa. “Kwa maana”, Paulo anasema “Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristo” (1Kor.5:7). Usahihi wa kushangaza wa unabii huu unatoa mojawapo ya ushahidi usio shaka wa msingi wa ukweli wa kihistoria kwamba Yeus Kristo ndiye Masihi aliyetabiriwa tangu kale.
Kufufuka kwa Mwokozi
Biblia haikutabiri tu kifo cha Mwokozi bali pia kufufuka kwake. Daudi alitabiri “kwamba roho yake haikuachwa kuona kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu” (Mdo.2:31; cf. Zab.16:10). Ijapokuwa Kristo alikuwa amefufua wengine kutoka wafu (Mk.5:33-42; Luk.7:11-17; Yoh.11), ufufuo wake mwenyewe ilidhihirisha nguvu ya madai yake kwamba “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima, Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.” (Yoh.11:25, 26) Baada ya kufufuka alitangaza, “Usiogope, mimi ni wa kwanza na wa mwisho, na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hai hata milele na milele” (Uf.1:17,18).
Asili mbili za Yesu Kristo
Kwa kutamka “Naye Neno akafanyika mwili na kuishi pamoja nasi (Yoh.1:14), Yohana anasema ukweli mkuu. Kufanyika mwili kwa Yesu Kristo ni siri. Biblia huitaja kuwa Mungu kudhihirishwa katika mwili ni “siri ya utauwa’ (1Tim.3:16).
Muumbaji wa ulimwengu, Yeye ambaye utimilifu wa Uungu ulikuwa ndani yake alifanyika mtoto mchanga asiyeweza chochote katika hori ya kulia ng’ombe. Mwenye hadhi kubwa kupita malaika, mwenye hadhi sawa na Baba na utukufu, alijishusha chini kuvaa uanadamu! Ni vigumu kuelewa vema maana ya siri hii takatifu, isipokwa kwa kumwalika tu Roho Mtakatifu asaidie kuangaza mawazo. Katika kutaka Yesu kufanyika mwili ni vema kukumbuka kwamba “mambo ya siri ni ya BWANA, na yaliyofunuliwa kwetu ni ya kwetu hata milele” (Kumb.29:29)
Yesu Kristo ni Mungu Kikamilifu
Ni ushahidi gani tulionao kwamba Yesu Kristo ni Mungu? Alijihesabu vipi, je kuna watu waliomtambua kama Mungu?
1. Sifa zake za Uungu
Kristo alikuwa na sifa za Uungu. Alisema Baba amempa mamlaka yote, mbinguni na duniani (Mt.28:18; Yoh.17:2). Anajua vyote. Ndani yake, Paulo anasema “hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika” (Kol. 2:3). Yesu alisisitiza kuwepo kwake kwa milele aliposema “Na tazama niko nanyi hadi utimilifu wa dahari.” (Mt.28:20). Na “wakutanapo wawili au watatu kwa Jina langu, nami nipo pamoja nao (Mt.18:20). Pamoja na kwamba Uungu wake anaweza kupatikana mahali pote, wakati wote, Yesu aliyefanyika mwili alijizuilia jambo hilo. Amechagua kuwapo mahali pote wakati wote kupitia huduma ya Roho Mtakatifu (Yoh.14:16-18). Waebrania ikizungumzia kutokubadilika kwake, inasema “Yesu Kristo ni yeye Yule, jana, leo na hata milele.” (Ebr.13:8).
Kuwepo kwake mwenyewe pasipo kuumbwa kulionekana alipodai uzima ndani yake (Yoh.5:26), na Yohana anashuhudia, ndani yake kulikuwapo uzima na uzima ulikuwa nuru kwa watu (Yoh.1:4). Tamko la Yesu kwamba “Mimi ndimi ufufuo na uzima (Yoh.11:25), ilisisitiza kwamba ndani yake kuna uzima, wa asili, usioazimwa wala kutengenezwa.
Utakatifu ni sehemu ya asili yake. Awali Malaika alimwambia Mariamu “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” (Luk.1:35). Kwa kumwona Yesu, mapepo yalilia “Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti?” (Mk.1:24). Yu pendo. “Katika hili tunalifahamu pendo, kwa Yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu (1Yoh.3:16).
Yeye ni wa milele. Isaya alimwita “Baba wa milele” (Isa.9:6). Mika anamwita “matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele” (Mik.5:2).Paulo aliweka tarehe ya kuwepo kwake “kabla ya vitu vyote.” (Kol.1:17) na Yohana anakubaliana naye anaposema “tangu mwanzo alikuwako na Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo, wala pasipo Yeye, hakuna kilichofanyika. (Yoh.1:2, 3).
Majina yake yanaonyesha kuwa Yesu ni Mungu. Imanueli maana yake ni “Mungu pamoja nasi” (Mt.1:21). Waumini na mapepo walimtambua na kumwita Mwana wa Mungu (Mk.1:1; Mt.8:29; cf. Mk.5:7). Jina la Yehova lililoko kwenye Agano la Kale limetumiwa kwa Yesu. Mathayo anatumia maneno ya Isaya 40:3 “Itengenezeni njia ya Bwana” kuandaa utume wa Yesu (Mt.3:3)
4. Uungu wake Umetambuliwa
Yohana ana picha ya Yesu kuwa ni Neno la Mungu ambalo lilifanyika mwili (Yoh. 1:1, 14). Tomaso alimkiri Yesu aliyefufuka kuwa ni “Bwana wangu na Mungu wangu” (Yoh. 20:28). Paulo anamrejea Yesu kuwa ni “Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu mwenye kuhimidiwa milele” (Rum.9:5). Na Waebrania wanamzungumza kuwa ni Mungu na Bwana wa uumbaji (Ebr.1:8, 10)
5. Ushuhuda wake Binafsi
Yesu mwenyewe alidai yuko sawa na Mungu Baba. Alijitambulisha kuwa MIMI NIKO (Yoh. 8:58) – Mungu wa Agano la Kale. Alimwita Mungu “Baba Yangu” badala ya Baba yetu (Yoh.20:17). Na kauli yake “Mimi na Baba tu mmoja” (Yoh. 10:30) inaweka hoja kuwa alikuwa na asili moja na Baba, akiwa na sifa na mamlaka sawa.
6. Alihesabika kuwa Sawa na Mungu
Kuwa sawa na Mungu kunahesabika katika kanuni ya kubatiza “Kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu” (Mt.28:19). Maneno ya kubariki ya kimitume (2Kor.13:14), ushauri wake wakati anaondoka (Yoh.14-16), na Paulo akiweka wazi karama za Roho (1Kor.12:4-6). Maandiko yanamwelezea Yesu kuwa mng’ao wa utukufu wa Mungu na “chapa ya nafsi yake” (Ebr.1:3). Na alipoulizwa aonyeshe watu Baba, alisema aliyemwona Yeye, amekwisha mwona Baba (Yoh.14:9)
7. Anaabudiwa kama Mungu
Watu walimwabudu (Mt.28:17; cf. Luk.14:33). Malaika wote wa Mungu wanamsujudu (Ebr.1:6). Paulo aliandika kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRITO NI BWANA kwa utukufu wa Mungu Baba (Fil.2:10, 11). Baadhi ya maneno ya kuagana humpa Yesu “utukufu milele na milele” (2Tim.4:18; Ebr.13:21; cf. 2Pet.3:18)
8. Kuwa na Uungu ni muhimu
Kristo alipatanisha mwanadamu na Mungu. Watu walihitaji ufunuo wa tabia ya Mungu ili kuwa na mahusiano naye. Kristo alitimiza hitaji hili kwa kufunua utukufu wa Mungu. (Yoh.1:14). Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba huyo ndiye aliyemfunua (Yoh.1:18; cf. 17:6). Yesu alishuhudia kuwa aliyemwona Yeye, amemwona Baba (Yoh.14:9).
Akimtegemea Baba kikamilifu (Yoh.5:30), Kristo alitumia uwezo wa kimungu kufunua upendo wa Mungu. Akiwa na uwezo wa kimungu, alijifunua mwenyewe kuwa ni Mwokozi anayependa, aliyetumwa na Baba kuponya, kurejesha, na kusamehe dhambi. (Luk.6:19; Yoh.2:11; 6:1-15, 36; 11:41-45; 14:11; 8:3-11). Kamwe, hakutenda muujiza ili kujinusuru mwenyewe na ugumu wa maisha au maumivu ambayo watu wengine hukutana nayo. Yesu Kristo ana asili, tabia na makusudi sawasawa na Mungu Baba. Kwa kweli ni Mungu.
Yesu Kristo ni Mwanadamu kweli kweli.
Biblia hushuhudia kwamba pamoja na kuwa na asili ya kiungu, Kristo alikuwa na asili ya mwanadamu. Kukubaliana na fundisho hili ni jambo muhimu. Kila mtu “akiriye kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, ni wa Mungu” (1Yoh.4:2, 3). Kuzaliwa kwa Yesu kama binadamu, kukua, tabia na ushuhuda wake hutoa ushahidi wa uanadamu wake.
1. Kuzaliwa kwake kibinadamu
“Naye Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu” (Yoh.1:14). Hapa mwili ina maana ya “uanadamu”- asili iliyo dhaifu kuliko ya mbinguni. Kwa lugha ya wazi, Paulo kwa lugha iliyo wazi anasema “Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke” (Gal.4:4 cf. Mwa.3:15). Kristo alifanywa “kwa mfano wa wanadamu” na “umbo kama mwanadamu” (Fil.2:7, 8). Huku kudhihirishwa kwa Mungu katika umbo la kibinadamu, ni siri ya utauwa (1Tim.3:16). Ukoo wa Kristo unamweka kuwa “Mwana wa Daudi”, “ Mwana wa Ibrahimu” (Mt.1:1). Kwa asili yake kibinadamu, alizaliwa kwa “ukoo wa Daudi (Rum.1:3; 9:5) alikuwa “mwana wa Mariam” (Mk.6:3). Ijapokuwa alizaliwa na mwanamke kama watoto wengine wanavyozaliwa, kulikuwa na tofauti kubwa, upekee wa aina yake. Mariam alikuwa bikira, na mimba ilipatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Mt.1:20-23; Luk.1:31-37). Angeweza kudai ni mwanadamu kupitia mama yake.
2. Kukua kwake kama mwanadamu
Yesu alitawaliwa na kanuni ya kukua ya kibinadamu; “alikua, akaongezeka nguvu, akazidi kuendelea katika hekima na kimo” (Luk.2:40, 52). Katika utoto wake, alikuwa chini ya uongozi wa wazazi wake (Luk.2:51).
Njia ya msalaba ilikuwa daima yenye kukua daima na mateso, ambayo yalichangia katika kukua kwake. “alijifunza kutii kwa mateso hayo na alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii” (Ebr.5:8, 9; 2:10, 18). Katika kukua kwake, hakutenda dhambi.
3. Aliitwa mtu
Yohana Mbatizaji na Petro wanamwita Mtu (Yoh.1:30; Mdo. 2:22). Paulo naye anazungumzia “neema ya mwanadamu mmoja Yesu Kristo (Rum.5:15). Yeye ni ‘Mtu” aliyeleta “kiyama ya wafu”. (1Kor.15:21); “mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu&rdquo (1Tim.2:5). Alipoongea na adui zake, Yesu alijisema kuwa ni mtu.”mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli” (Yoh.8:40) .
Yesu alipenda kujihesabu kwa cheo alichokitumia mara sabini na saba cha “Mwana wa Adamu” (cf. Mt.8:20; 26:2). Cheo cha Mwana wa Mungu kinalenga kuonyesha uhusiano wake na Uungu. Mwana wa Adamu ni cheo kinachoonyesha kuungana kwake na wanadamu kupitia kufanyika mwili.
4. Tabia zake za kibinadamu
Mungu aliwaumba mwanadamu “mdogo punde kuliko Malaika” (Zab.8:5). Kadhalika, Maandiko yanamwakilisha Kristo aliyefanywa punde kuliko malaika (Ebr.2:9). Asili yake ya kibinadamu ilikuwa imeumbwa na haikuwa na nguvu zisizo za kawaida. Kristo alikuwa awe mwanadamu kiukweli; hiyo ilikuwa sehemu ya utume wake. Kuhitajika kwake kuwa na asili ya mwanadamu: alikuwa “nyama na damu” (Ebr.2:14). “Katika mambo yote” Kristo alifanyika sawa na wanadamu (Ebr.2:17). Asili yake ya kibinadamu ilimfanya ajisikie uhitaji kama wanadamu, njaa, kiu, kuchoka na kuwa na huzuni (Mt.4:2; Yoh.19:28; 4:6; cf. Mt. 26:21, 8:24). Katika huduma yake kwa watu wengine alionyesha huruma, hasira ya haki na sikitiko (Mt.9:36; Mk.3:5). Kuna nyakati alionekana kukosa raha, kuhuzunika na hata kulia machozi (Mt.26:38; Yoh. 12:27; 11:33, 35; Luk.19:41). Aliomba akilia na machozi, mara moja alifikia kutiririka jasho la damu (Ebr.5:7; Luk. 22:44). Maisha yake ya kuomba yalionyesha alivyomtegemea kikamilifu Mungu (Mt.26:39-44; Mk.1:35; 6:46; Luk.5:16; 6:12) Yesu alipata kufa (Yoh.19:30, 34). Alifufuka siyo akiwa roho, bali akiwa na mwili (Luk.24:36-43).
Kiwango cha kujitambulisha kwake na asili ya Mwanadamu
Biblia hufunua kuwa Kristo ni Adamu wa pili; aliishi “kwa mfano wa mwili ulio wa dhambi” (Rum.8:3). Ni kwa kiasi gani alijitambulisha au alifanana na mwanadamu aliyeanguka? Usahihi wa tamko “mfano wa mwili ulio wa dhambi” or “mwanadamu mdhambi” ni muhimu. Maoni yasiyo sahihi juu ya jambo hili yamefarakanisha wakristo katika historia ya kanisa la kikristo.
Alikuwa kwa mfano wa mwili ulio wa dhambi
Nyoka aliyeinuliwa jangwani hutoa uelewa wa asili ya kibinadamu ya Yesu Kristo. Kama sanamu ya shaba ilivyofanywa kwa mfano wa nyoka wenye sumu ilivyoinuliwa, kwa uponyaji wa watu, ndivyo Mwana wa Mungu aliyekuwa kwa mfano wa mwili wenye dhambi angekuwa Mwokozi wa ulimwengu.
Alikuwa Adamu wa Pili
Biblia humfananisha Adamu na Kristo ikimwita Adamu “mtu wa kwanza” na Kristo “Adamu wa mwisho” or “mtu wa pili&rdquo (1Kor.15:45, 47). Tofauti na damu, alichukua uanadamu miaka 4,000 baadaye wakati miili iliishadhoofika na akili kuwa hafifu zaidi, hata hivyo aliishi bila kutenda dhambi.
Alipochukua uanadamu, Yesu alibeba athari za dhambi, na kuwa na udhaifu ambao wote huupata. Asili yake ya uanadamu ilikabiliwa na udhaifu (Ebr.5:2, Mt.8:17; Isa.53:4). “Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea Yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu” (Ebr.5:7). Kwa hiyo Yesu hakuchukua uanadamu wa Adamu kabla ya anguko dhambini, bali uanadamu halisi kama miaka 4000 baada ya kufanya dhambi.
5. Uzoefu wake na majaribu
Majaribu yalimwathirije Yesu? Je, ilikuwa rahisi au vigumu kwake kukabiliana nayo?
i) alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote
Alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote (Ebr.4:15). Siyo kwamba alijaribiwa sawa sawa nasi katika kuangalia programu ya kuhafifisha katika televisheni au kuendesha gari kwa kuvuka spidi iliyowekwa. Jambo la msingi katika majaribu ni swali ni kuacha moyo utawaliwe na Mungu au vinginevyo. Kwa kumtegemea Mungu, alishinda majaribu makali kabisa, hata kama alikuwa mwanadamu. Ushindi wa Yesu katika majaribu ulimfanya aweze kuwahurumia wanadamu. Ushindi wetu kwa majaribu upo katika kumtegemea. “Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea.” (1Kor. 10:13)
ii) Majaribu yalimtesa:
Mwenyewe aliteswa alipojaribiwa (Ebr.2:18). Alikamilishwa kwa kupitia mateso (Ebr.2:10). Uzoefu wake nyikani, Gesthemane, na Golgotha unadhihirisha alishindana na majaribu kwa kiwango cha kumwaga dhambi (cf. Ebr.12:4). Pamoja na hayo, Yesu pia alijaribiwa jaribu ambalo wanadamu hawawezi kulipata, la kujaribiwa kutumia Uungu wake kujihudumia. Na alijaribiwa pasipo kufanya dhambi (Ebr.4:15).
Je Kristo angeweza kufanya dhambi?
“Ikiwa Kristo angewezeshwa kutoka mwanzo kutokutenda dhambi, basi asingekuwa mwanadamu halisi wala asingekuwa mfano kwetu wa kumcha Mungu na mateso yake yangekuwa onyesho lisilo halisi.” “Historia ya majaribu isingekuwa na umuhimu wowote na maelezo ya Waraka kwa Waebrania kuwa alijaribiwa sawasawa na sisi pasipo kutenda dhambi yangekosa maana.”
6. Hali ya kutokuwa dhambi ya Unadamu wa Yesu
Ni dhahiri asili ya Uungu ya Yesu haikuwa na dhambi. Vipi, kuhusu asili yake ya uanadamu wake? Biblia inaonyesha uanadamu wa Yesu haukuwa na dhambi. Alizaliwa kwa hali inayopita kawaida, mimba yake ilipatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Mt.1:20). Alipokuwa mtoto, aliitwa Mtakatifu (Luk.1:35). Alichukua uanadamu ulioanguka dhambini, akabeba athari za dhambi, pasipo kuchukua hali yake ya dhambi.
Yesu “Alijaribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi “ “aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, “ (Ebr.4:15; 7:26). Paulo aliandika “yeye asiyejua dhambi” (2Kor.5:21). Petro anashuhudia kuwa “Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake” (1Pet.2:22) na kumfananisha na “mwanakondoo asiye na ila wala waa” (1Pet.1:19; Ebr.9:24). “Ndani yake,” Yohana anasema “ hakuna dhambi” “Yuna haki” (1Yoh.3:5-7).
Yesu alichukua asili yetu pamoja na mizigo yake yote bila tendo la dhambi. Aliwapa changamoto waliompinga “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye kuwa nina dhambi?” (Yoh.8:46). Alipokabiliwa na jaribu lake kubwa, alitamka “yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.” (Yoh.14:30). Yesu hakupata kuungama au kutoa kafara. Aliomba “Baba uwasamehe” (Luk. 23:34) siyo Baba unisamehe. Daima alipenda kufanya mapenzi ya Baba yake (cf. Yoh.5:30).
7. Umuhimu wa Kristo kuchukua asili ya kibinadamu
Biblia hutoa sababu mbali mbali kwa nini Kristo alipaswa kuchukua asili ya kibinadamu.
a) kuwa Kuhani Mkuu wa Wanadamu.
Kama Masihi, Yesu alipaswa kuwa Kuhani Mkuu au mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu (Zek.6:13; Ebr.4:14-16). Jukumu hilo lilihitaji kuwa na hali ya uanadamu. (i) angeweza “kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na wenye kupotea kwa sababu mwenyewe yu katika hali ya udhaifu” (Ebr.5:2). (ii) Ni “mwenye rehema na mwaminifu kwa sababu ilimpasa kufananishwa na ndugu zake (Ebr.2:17). (iii) Aweza kuwasaidia wanaojaribiwa kwa sababu aliteswa na majaribu (Ebr.2:18). (iv) anawaonea huruma wanaojaribiwa kwa sababu mwenyewe alijaribiwa sawasawa na sisi (Ebr.4:15)
b) Kuokoa hata aliyepotea katika hali duni kabisa. Kuwafikia watu walipo na kuwaokoa wasio na tumaini, alishuka akawa na hadhi ya mtumwa (Fil.2:7)
c) Kutoa uhai wake uwe fidia kwa dhambi. Hali ya Mungu haifi. Ili afe, ilimpasa kuchukua asili ya mwanadamu. Alichukua uanadamu na kulipa adhabu ya dhambi ambayo ni kifo (Rum.6:23; 1Kor.15:3). Akiwa mwanadamu alionja mauti kwa ajili ya kila mtu. (Ebr.2:9).
d) Kuwa kielelezo kwetu. Kuweka kielelezo jinsi mwanadamu anavyopaswa kuishi, Kristo lazima awe na maisha yasiyo na dhambi. Alidhihirisha kuwa mwanadamu aweza kutii mapenzi ya Mungu. Katika nguvu zake, ushindi wake waweza ukawa wetu (Yoh.16:33). Kwa kumwangalia, watu wanabadilishwa wafanane na mfano uo huo, toka utukufu hadi utukufu. (2Kor.3:18). Hebu tumtazame Yesu, mwenye kuanzisha na kuikamilisha imani yetu…tumtafakari sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu… tusije kuchoka tukizimia nafsini mwetu (Ebr.12:2, 3). Kwa kweli Kristo aliumia kwa ajili yetu akituachia kielelezo kwamba tufuate nyayo zake (1Pet.2:21; cf. Yoh.3:15).
Muungano wa Asili Mbili
Nafsi ya Kristo ilikuwa na asili mbili. Ya Mungu na mwanadamu. Siyo kwamba uanadamu ulivikwa uungu, bali Uungu ulivikwa uanadamu. Katika Kristo asili hizi ziliunganishwa katika nafsi moja.
Kristo ni Muungano wa Asili mbili
Uwingi unaoambatana na Utatu Mtakatifu haupo katika Kristo Yesu. Biblia humsimulia Yesu kuwa Nafsi moja siyo mbili. Mafungu mengi huzungumzia kuwa Kristo kuwa na asili ya Uungu na Uanadamu lakini hayasemi kuwa ni nafsi mbili bali ni moja. Paulo alimwelezea nafsi ya Yesu Kristo kuwa ni Mwana wa Mungu aliyezaliwa na mwanamke (Gal. 4:4). Kwa hiyo Yesu Kristo ambaye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, hakuona kule kufanana na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya hana utukufu akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu (Fil.2:6, 7).
Yesu siyo nguvu ya Kimungu iliyonyofolewa kutoka Uungu ikaunganishwa na uanadamu. Biblia inatuambia, Neno alifanyika Mwili na kukaa kwetu, nasi tukaona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. (Yoh.1:14). Paulo anaandika, Mungu alimtuma mwanaye kwa mfano wa mwili wenye dhambi (Rum.8:3). Mungu alifunuliwa katika mwili (1Tim.3:16; 1Yoh.4:2).
Kuunganisha Asili Mbili
Mara kadhaa Biblia inamwelezea Mwana wa Mungu katika asili yake ya kibinadamu. Mungu alinunua Kanisa lake kwa damu yake (Mdo.20:28; cf. Kol.1:13, 14). Nyakati fulani, inampa tabia za kiuungu Mwana wa Adamu (cf. Yoh.3:13).
Wakati Kristo alipokuja duniani, “mwili” ulikuwa umewekwa tayari (Ebr.10:5). Alipochukua uanadamu, Uungu wake ulifichwa na uanadamu. Hili halikufanyika kwa kubadilisha Uungu kuwa uanadamu au uanadamu kuwa Uungu. Hakuchukua asili nyingine bali alichukua uanadamu ukawa wake. Kwa hiyo Uungu na uanadamu viliungana.
Alipokuwa amefanyika mwanadamu, Kristo hakukoma kuwa Mungu, wala Uungu wake haukupunguzwa uwe uanadamu. Kila asili ilidumu kuwako. “Katika Yeye”, Paulo anasema, “unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.” (Kol.2:9). Aliposulubiliwa, uanadamu wake ulikufa, siyo Uungu wake kwa kuwa hilo lisingewezekana.
Umuhimu wa Kuunganisha Uungu na Uanadamu
Kuelewa asili mbili za Kristo zinatupatia picha ya utume wake na wokovu wetu.
Kumwunganisha Mwanadamu na Mungu
Ni mwokozi mwenye Uungu na uanadamu pekee ndiye angeweza kuokoa. Alipofanyika mwili, Kristo, ili awapatie wanadamu asili ya Uungu, alijiletea uanadamu kwake mwenyewe. Kupitia damu ya damu ya Mungu- mwanadamu, waumini wanaweza washirika wa tabia ya Uungu (2Pet.1:4).
Ngazi katika ndoto ya Yakobo, ikiwa kielelezo cha Kristo, hutufikia pale tulipo. Alichukua uanadamu na akashinda, ili kwamba kwa kutwaa asili yake, tupate kushinda. Mkono wake wa Uungu unaungana na kiti cha enzi cha Mungu, na uanadamu wake unakumbatia jamii yote ya mwanadamu, ukituunganisha na Mungu, nchi na mbingu.
Asili ya Mungu – mwanadamu iliyounganishwa inawezesha kafara ya iliyotolewa kutosheleza. Maisha yasiyo ya dhambi ya mwanadamu au hata malaika yasingeweza kulipia dhambi za wanadamu. Ni mkombozi Mungu mwanadamu Mwumbaji ndiye angekomboa mwanadamu.
Kufunika Uungu na uanadamu
Kristo alifunika Uungu wake na uanadamu, akiacha utukufu wake wa mbinguni ili wenye dhambi waweze kuishi mb)ele zake pasipo kuangamizwa. Ijapokuwa alikuwa Mungu, hakuonekana kama Mungu. (Fil.2:6-8).
Kuishi maisha ya ushindi
Uanadamu wa Kristo pekee usingeweza kuhimili uwongo wa Shetani. Bali ndani yake ulikuwepo utimilifu wa Uungu (Kol.2:9). Aliweza kushinda dhambi kwa sababu alimtegemea kikamilifu Mungu Baba (Yoh.5:19, 30;8:28). Na uwezo wa kimungu uliounganishwa na uanadamu ukampatia mwanadamu ushindi usio kikomo.
Uzoefu wa Kristo katika maisha ya ushindi siyo fursa yake peke yake. Hakutumia uwezo ambao wanadamu hawawezi kutumia. Nasi pia twaweza “kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.” (Efe. 3:19). Kupitia kwa uwezo wa Kiuungu wa Kristo, twaweza kufikia “vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa&rdquo. Ufunguo kwa uzoefu huu ni imani katika “ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo tupate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, tukiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa” (2Pet.1:3, 4). Hutoa uwezo ule ambao aliweza kushinda dhambi ili wote watii na kupata maisha ya ushindi.
Ahadi ya Yesu ni ya ushindi: “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja name katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.” (Ufu.3:21).
Vyeo vya Yesu Kristo
Vyeo vya Nabii, Kuhani na Mfalme yalikuwa tofauti na vilihitajika kuwekwa wakfu kwa kumiminiwa mafuta. (1Fal.19:16; Kut.30:30; 2Sam.5:3). Ujio wa Masihi, aliye Mtiwa mafuta, unabii ulionyesha atakuwa na majukumu yote matatu.
Kristo Nabii
Mungu alikifunua cheo cha Kristo cha nabii kwa Musa. “Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.” (Kumb.18:18). Walioishi na Kristo, walitambua kutimizwa kwa unabii huu. (Yoh.6:14; 7:40; Mdo.3:22, 23). Yesu alijisema kuwa ni nabii (Luk. 13:33). Alifundisha kwa mamlaka ya nabii (Mt.7:29), mafundisho ya misingi ya ufalme wa Mungu. (Mt.5-7; 22:36-40) na kufunua mambo yajayo (Mt.24:1-51; Luk.19:41-44).
Kabla ya kufanyika mwili, Kristo aliwajaza waandishi wa Biblia kwa Roho wake na akawapa unabii kuhusu kuteswa kwake na utukufu utakaofuatia baada ya hayo (1Pet.1:11). Alipopaa aliendelea kujifunua kwa watu. Biblia inasema hutoa ushuhuda, roho ya unabii kwa waliosalia (Uf.12:17; 19:10)
Kristo Kuhani
Kiapo cha Mungu kwa msisitizo, kilianzisha ukuhani wa Masihi. “BWANA ameapa wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, kwa mfano wa Melkizedeki” (Zab.110:4). Yesu hakuwa mzao wa Haruni, hivyo wito wake kuwa kuhani ulifanywa na Mungu (Ebr.5:6, 10). Utumishi wake wa ukuhani ulikuwa na hatua ya duniani na mbinguni.
1. Ukuhani wa Kristo Duniani
Jukumu la kuhani mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa inawakilisha huduma ya Kristo duniani. Alikuwa mwanadamu aliyeitwa na Mungu na kutenda yamhusuyo Mungu na kushughulikia sadaka na kafara kwa ajili ya dhambi (Ebr.5:1, 4, 10). Kuhani aliwapatanisha wanaoabudu na Mungu kupitia huduma ya kafara (Law.1:4; 4:29, 31, 35; 5:10; 16:6; 17:11). Kafara hazikuwa kamilifu. Zisingemtakasa mtoaji wala kumkamilisha (Ebr.10:1-4; 9:9). Vilikuwa vivuli tu ya mazuri yajayo (Ebr.10:1; cf. 9:9, 23, 24). Agano la kale lasema Masihi atatwaa nafasi ya wanyama wa kafara (Zab.40:6-8; Ebr.10:5-9). Kafara hizi zilielekeza kwa kafara ya Kristo msalabani. Damu yake yatusafisha na udhalimu wote (2Kor.5:21; Gal.3:13; 1Yoh.1:7; cf. 1Kor.15:3). Hivyo duniani, Kristo alikuwa Kuhani na wakati huo huo kafara.
2. Ukuhani wa Kristo Mbinguni
Huduma ya ukuhani ya Yesu mbinguni ilianzia duniani na kukamilishwa mbinguni. Kunyenyekea kwake duniani, kulimfanya astahili kuwa Kuhani Mkuu mbinguni (Ebr.2:17, 18; 4:15; 5:2). Unabii unasema Masihi angekuwa kuhani kwenye kiti cha enzi cha Mungu (Zek.6:13). Baada ya ufufuo, kudhalilishwa kumekoma na Kuhani Mkuu yuko akihudumu mbinguni. (Ebr.8:1; cf. 1:3; 9:24). Huduma yake inatia moyo waumini (Ebr.7:25). Kwa sababu ya huduma ya maombezi ya Kristo, madai ya Shetani yamekosa uhalali (1Yoh. 2:1; cf. Zek.3:1). Hakuna wa kutuhukumu kwa sababu Kristo anatuombea (Rum.8:34). Akithibitisha jukumu lake la kututetea, alisema tukiomba chochote katika Jina lake, atatupatia (Yoh.16:23)
3. Kristo Mfalme
Mungu “ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unavitawala vitu vyote.” (Zab.103:19). Kristo akiwa sehemu ya Utatu Mtakatifu anachangia kutawala. Kristo aliye Mungu-mwanadamu atakuwa na ufalme kwa wale waliomkubali kuwa BWANA na mwokozi wao. (Zab.45:6; Ebr.1:8, 9). Ufalme wa Kristo haukuanzishwa pasipo mashindano (Zab. 2:2). Wanaompinga watashindwa. (Zab.2:6, 7; Ebr.1:5). Jina la Mfalme atakayekalia kiti cha enzi cha Daudi ni BWANA HAKI YETU (Yer.23:5, 6). Ufalme wake ni tofauti kwa kuwa atatumika akiwa Kuhani na Mfalme (Zek.6:13). Ulipotangazwa, ufalme wake haukuwekewa kikomo. (Luk.1:33). Ufalme wake una viti vya enzi viwili ambavyo ni kiti cha enzi cha neema (Ebr.4:16) ikimaanisha ufalme wa neema na ufalme wa utukufu (Mt.25:31) ikiwa inamaanisha ufalme wa utukufu.
1. Ufalme wa Neema
Ufalme wa neema ulianza mara baada ya dhambi kuingia. Alipopaza sauti “Imekwisha”, agano jipya lilianzishwa, ambako wanadamu watakuwa warithi. (cf. Ebr.9:15-18). Hubiri la Yesu, “Ufalme wa Mungu umekaribia (Mk.1:15) ilimaanisha ufalme ambao ungeanzishwa kwa kifo chake. Umejengwa juu ya kazi ya ukombozi. Hakuna atakayeuingia ufalme wa Mungu pasipo kuzaliwa mara kwa maji na kwa Roho. (Yoh.3:5 cf. 3:3). Anaufananisha na punje ya haradali iotayo na kuwa mti mkubwa au chachu ambayo huchachusha donge zima (Mk. 4:22-31; Mt.13:33).
Ufalme hauonekani, lakini unaathiri mioyo ya wanadamu. (Luk.17:20, 21). Siyo ufalme wa dunia hii. (Yoh.18:37). Ufalme wa Kristo ni wa haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu (Rum.14:17; Kol.1:13). Uanzishwaji wa ufalme huu ulikuwa unasisitiza hautaingiwa pasipo msalaba. Alipokuja Yerusalemu amepanda punda (Zek. 9:9, Mt.21:8, 9), akajitambulisha kuwa Masihi na Mfalme. Hata hivyo alipingwa. Aliposhitakiwa, alikiri mbele ya watu kuwa ni Mwana wa Mungu na Mfalme (Luk.23:3; Yoh.18:33-37). Kuitikia tamko lake, alidhihakiwa kwa kuvikwa vazi la kifalme na taji ya miiba. (Yoh.19:2). Akasalimiwa kwa kebehi (Yoh.19:3). Gavana wa Kirumi alipowaambia angalieni mfalme wenu, walimkataa wakapaza sauti zao wakisema asulubishwe (Yoh.19:14, 15). Kwa kudhalilishwa na kifo cha msalaba, Kristo alianzisha ufalme wa neema. Baada ya kupaa, aliingia kiti cha enzi mbinguni akiwa Kuhani na Mfalme akishiriki kukalia kiti cha enzi cha Baba yake. (Zab.2:7, 8; cf. Ebr.1:3-5; Filp. 2:9-11, Efe.1:20-23). Si kwamba hakuwa na madaraka hayo kabla, ila aliingia kwa nafasi hiyo kwa mara ya kwanza akiwa Mungu – mwanadamu.
2. Ufalme wa Utukufu
Alipobadilika mlimani, uso wake ukang’aa kwa mwanga wa jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga, akitokewa na Musa na Eliya, Yesu alionyesha ufalme wake wa utukufu. (Mt.17:2). Ufalme wa utukufu utaanzishwa kwa matukio ya kutisha ya mwisho wa dunia na kuja kwa Yesu mara ya pili. (Mt.24:27, 30, 31;25:31, 32). Hii itatokana na hukumu ya Mzee wa siku itakayompa Yesu ufalme wa utukufu (Dan.7:9, 10, 14). na watakatifu (Dan. 7:27). Ufalme wa utukufu utakamilishwa baada ya miaka 1,000, wakati Yerusalemu utakaposhuka kutoka mbinguni (Ufu. 20, 21). Kwa kumkubali Kristo sasa, twaweza kuwa raia wa ufalme wa neema sasa na raia wa ufalme wa utukufu Kristo atakapokuja. Ufalme wa kuishi kama Kristo, matunda ya Roho ya upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. (Gal.5:22, 23)
Yohana 1:1-3, 14X1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Wakolosai 1:15-19X15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 19 Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae;
Yohana 14:9X9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
2 Wakorintho 5:17-19X17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Yohana 5:22, 23X22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote; 23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
Luka 1:35X35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Wafilipi 2:5-11X5 Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
1 Wakorintho 15:3, 4X3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
Waebrania 2:9-18X9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. 10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. 11 Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; 12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. 13 Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. 14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, 15 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. 16 Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. 17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. 18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Waebrania 7:25X25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Waebrania 8:1, 2X1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
Yohana 14:1-3X1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Hesabu 21:7X7 Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Hesabu 21:9X9 Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
Mwanzo 3X1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. 9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. 13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala. 14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. 16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. 20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai. 21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; 23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. 24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Ufunuo 12X1 Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili. 2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa. 3 Ikaonekana ishara nyingine mbinguni; na tazama, joka kubwa jekundu, alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na juu ya vichwa vyake vilemba saba. 4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 5 Naye akazaa mtoto mwanamume, yeye atakayewachunga mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Na mtoto wake akanyakuliwa hata kwa Mungu, na kwa kiti chake cha enzi. 6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini. 7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; 8 nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. 13 Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo. 15 Nyoka akatoa katika kinywa chake, nyuma ya huyo mwanamke, maji kama mto, amfanye kuchukuliwa na mto ule. 16 Nchi ikamsaidia mwanamke; nchi ikafunua kinywa chake, ikaumeza mto ule alioutoa yule joka katika kinywa chake. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Warumi 8:3X3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
Yohana 3:14, 15X14 Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; 15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
2 Wakorintho 5:21X21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Yohana 3:16X16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
1 Yohana 4:9X9 Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.
1 Petro 1:19, 20X19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. 20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;
1 Petro 3:18X18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,
Mathayo 1:21X21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
1 Yohana 3:8X8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Petro 1:20, 21X20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.
Zekaria 6:13X13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Mwanzo 3:15X15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Mwanzo 2:17X17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 3:19X19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
1 Yohana 3:4X4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Warumi 6:23X23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Yohana 3:16X16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kutoka 25:8, 9, 40X8 Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.9 Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.40 Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, ulioonyeshwa mlimani.
Waebrania 8:1-5X1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
M. Walawi 1:3, 4X3 Matoleo yake kwamba ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe mume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya Bwana. 4 Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
Waebrania 9:22X22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
M. Walawi 4:7X7 Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya Bwana iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.
M. Walawi 4:26, 31, 35X26 Na mafuta yake yote atayateketeza juu ya madhabahu, kama alivyoyateketeza mafuta ya hizo sadaka za amani; naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake, naye atasamehewa.31 Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.35 kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za Bwana zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.
Yohana 1:29X29 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
1 Petro 1:19X19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Mwanzo 22:18X18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Mwanzo 12:3X3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Isaya 9:6X6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Isaya 9:7X7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
Mika 5:2X2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Isaya 7:14X14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Mathayo 1:23X23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Isaya 61:1, 2X1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Luka 4:18, 19X18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
Isaya 53:2-4X2 Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani. 3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. 4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Zaburi 41:9X9 Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
Zekaria 11:12X12 Nikawaambia, Mkiona vema, nipeni ujira wangu; kama sivyo, msinipe. Basi wakanipimia vipande thelathini vya fedha, kuwa ndio ujira wangu.
Zaburi 50:6X6 Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
Zaburi 22:18X18 Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura.
Zaburi 34:20X20 Huihifadhi mifupa yake yote, Haukuvunjika hata mmoja.
Zekaria 12:10X10 Nami nitawamwagia watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, roho ya neema na kuomba; nao watamtazama yeye ambaye walimchoma; nao watamwombolezea, kama vile mtu amwombolezeavyo mwanawe wa pekee; nao wataona uchungu kwa ajili yake, kama vile mtu aonavyo uchungu kwa ajili ya mzaliwa wake wa kwanza.
Isaya 53:7X7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake.
Isaya 53:4-8X4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. 5 Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. 6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote. 7 Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. 8 Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani atakayeisimulia? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Mathayo 1:1X1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Wagalatia 3:16X16 Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi, Kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa mzao wako, yaani, Kristo.
Mathayo 21:9X9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Matendo 2:29, 30X29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. 30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;
Mathayo 1:18-23X18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. 22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, 23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Luka 2:4-7X4 Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; 5 ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. 6 Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, 7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
Mathayo 1:23X23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Mathayo 1:21X21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Isaya 61:1, 2X1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Luka 4:17-21X17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, 18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. 20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. 21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.
Yohana 1:11X11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
Luka 23:18X18 Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba.
Yohana 5:16X16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
Yohana 7:19X19 Je! Musa hakuwapa torati? Wala hakuna mmoja wenu aitendaye torati. Mbona mnatafuta kuniua?
Yohana 11:53X53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.
Yohana 13:18X18 Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake.
Yohana 18:2X2 Naye Yuda, yule aliyetaka kumsaliti, alipajua mahali pale; kwa sababu Yesu alikuwa akienda huko mara nyingi pamoja na wanafunzi wake.
Mathayo 26:14, 15X14 Wakati huo mmoja wa wale Thenashara, jina lake Yuda Iskariote, aliwaendea wakuu wa makuhani, 15 akasema, Ni nini mtakachonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vipande thelathini vya fedha.
Yohana 18:4-11X4 Basi Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Ni nani mnayemtafuta? 5 Wao wakamjibu, Ni Yesu Mnazareti. Yesu akawaambia, Ni mimi. Yuda naye aliyemsaliti alikuwa amesimama pamoja nao. 6 Basi alipowaambia, Ni mimi, walirudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Basi akawauliza tena, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti. 8 Yesu akajibu, Nimekwisha kuwaambieni ya kwamba ni mimi; basi ikiwa mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao. 9 Ili litimizwe lile neno alilolisema, Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja wao. 10 Basi Simoni Petro alikuwa na upanga, akaufuta, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. Na yule mtumwa jina lake ni Malko. 11 Basi Yesu akamwambia Petro, Rudisha upanga alani mwake; je! Kikombe alichonipa Baba, mimi nisikinywee?
Mathayo 26:67X67 Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi,
Yohana 19:1-16X1 Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. 2 Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. 3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi. 4 Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake. 5 Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu! 6 Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake. 7 Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu. 8 Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa. 9 Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. 10 Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? 11 Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. 12 Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari. 13 Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. 14 Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari. 16 Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu.
Luka 23:14, 15X14 akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki; 15 wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa.
Yohana 19:23, 24X23 Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. 24 Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari.
Yohana 19:32, 33X32 Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. 33 Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu;
Yohana 19:34, 37X34 lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.37 Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.
Warumi 5:8X8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Waefeso 5:2X2 ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii ambayo mnasimama ndani yake; na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu.
Wagalatia 4:4X4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,
Marko 1:15X15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Danieli 9:24X24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
Danieli 9:25X25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Danieli 9:26X26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
Danieli 9:27X27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Hesabu 14:34X34 Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu.
Ezekieli 4:6X6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.
Danieli 9:25X25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
Ezra 7:8X8 Naye Ezra akafika Yerusalemu mwezi wa tano katika mwaka wa saba wa huyo mfalme.
Ezra 7:12-26X12 Artashasta, mfalme wa wafalme, kwa Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, salamu kamili; wakadhalika. 13 Natoa amri ya kwamba wote walio wa watu wa Israeli, na makuhani wao, na Walawi, katika ufalme wangu, wenye nia ya kwenda Yerusalemu kwa hiari yao wenyewe, waende pamoja nawe. 14 Kwa kuwa umetumwa na mfalme, na washauri wake saba, ili kuuliza habari za Yuda na Yerusalemu, kwa sheria ya Mungu wako iliyo mkononi mwako; 15 na kuichukua fedha na dhahabu, ambayo mfalme, na washauri wake, kwa hiari yao, wamemtolea Mungu wa Israeli, akaaye Yerusalemu; 16 na fedha yote na dhahabu utakayoona katika wilaya ya Babeli, pamoja na vitu watakavyotoa watu kwa hiari yao, na vitu vya makuhani walivyotoa kwa hiari yao, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wao iliyoko Yerusalemu. 17 Kwa sababu hiyo ujitahidi kununua kwa fedha hiyo mafahali, kondoo waume, wana-kondoo, pamoja na sadaka zao za unga, na sadaka zao za kinywaji; nawe utazitoa juu ya madhabahu ya nyumba ya Mungu wenu, iliyoko Yerusalemu. 18 Na neno lo lote mtakaloona vema kulitenda, wewe na ndugu zako, kwa ile fedha na dhahabu itakayobaki, hilo litendeni, kama apendavyo Mungu wenu. 19 Na vile vyombo upewavyo kwa huduma ya nyumba ya Mungu wako, virejeze mbele za Mungu wa Yerusalemu. 20 Na cho chote kitakachohitajiwa zaidi, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wako, kitakachokupasa kukitoa, kitoe katika nyumba ya hazina ya mfalme. 21 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina, walio ng'ambo ya Mto, ya kwamba, kila neno ambalo Ezra, kuhani, mwandishi wa torati ya Mungu wa mbinguni, atalitaka kwenu, na litendeke kwa bidii nyingi, 22 hata kiasi cha talanta mia za fedha, na vipimo mia vya ngano, na bathi mia za divai, na bathi mia za mafuta, na chumvi bila kuuliza kiasi chake. 23 Kila neno litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya nyumba ya Mungu wa mbinguni. Kwa nini itokee ghadhabu juu ya ufalme wa mfalme na wanawe? 24 Tena twawaarifuni ya kuwa katika habari ya makuhani, na Walawi, na waimbaji, na mabawabu na Wanethini, au watumishi wa nyumba hii ya Mungu, si halali kuwatoza kodi, wala ada, wala ushuru. 25 Na wewe, Ezra, kwa kadiri ya hekima ya Mungu wako iliyo mkononi mwako, waweke waamuzi na makadhi, watakaowahukumu watu wote walio ng'ambo ya Mto, yaani, wote wenye kuzijua amri za Mungu wako; ukamfundishe yeye asiyezijua. 26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kwa bidii, kwamba ni kuuawa, au kwamba ni kuhamishwa, au kuondolewa mali yake, au kufungwa.
Ezra 9:9X9 Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, kuisimamisha nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu.
Luka 3:21X21 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka;
Matendo 10:38X38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Yohana 1:41X41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
Marko 1:15X15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Mathayo 27:51X51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
1 Petro 1:19X19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
1 Wakorintho 5:7X7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
Matendo 2:31X31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Marko 5:33-42X33 Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. 34 Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. 35 Hata alipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? 36 Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. 37 Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye Yakobo. 38 Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. 39 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. 40 Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamaye, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana.
Luka 7:11-17X11 Baadaye kidogo alikwenda mpaka mji mmoja uitwao Naini, na wanafunzi wake walifuatana naye pamoja na mkutano mkubwa. 12 Na alipolikaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, ni mwana pekee wa mamaye ambaye ni mjane, na watu wa mjini wengi walikuwa pamoja naye. 13 Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie. 14 Akakaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Inuka. 15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. 16 Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. 17 Habari hii yake ikaenea katika Uyahudi wote, na katika nchi zote za kando kando.
Yohana 11X1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. 2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. 3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. 4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. 5 Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro. 6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. 7 Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. 8 Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? 9 Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. 10 Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. 15 Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwako huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. 16 Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi, ili tufe pamoja naye. 17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. 18 Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu, kadiri ya maili mbili hivi; 19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. 20 Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. 21 Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 22 Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. 23 Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. 24 Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. 25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? 27 Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni. 28 Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. 29 Naye aliposikia, aliondoka upesi, akamwendea. 30 Na Yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo pale pale alipomlaki Martha. 31 Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. 32 Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. 33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, 34 akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. 35 Yesu akalia machozi. 36 Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. 37 Bali wengine wao wakasema, Je! Huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? 38 Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. 39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake. 45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. 46 Lakini wengine wakaenda zao kwa Mafarisayo, wakawaambia aliyoyafanya Yesu. 47 Basi wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakakusanya baraza, wakasema, Tunafanya nini? Maana mtu huyu afanya ishara nyingi. 48 Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu. 49 Mtu mmoja miongoni mwao, Kayafa, aliyekuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, akawaambia, Ninyi hamjui neno lo lote; 50 wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima. 51 Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa Kuhani Mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo. 52 Wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wamoja. 53 Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua. 54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake. 55 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; na wengi wakakwea toka mashambani kwenda Yerusalemu kabla ya Pasaka, ili wajitakase. 56 Basi wao wakamtafuta Yesu, wakasemezana hali wamesimama hekaluni, Mwaonaje? Haji kabisa sikukuu hii? 57 Na wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri ya kwamba mtu akimjua alipo, alete habari, ili wapate kumkamata.
Yohana 11:25, 26X25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; 26 naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo?
Ufunuo 1:17, 18X17 Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, 18 na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.
Yohana 1:14X14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
1 Timotheo 3:16X16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Mathayo 28:18X18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Yohana 17:2X2 kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.
Wakolosai 2:3X3 ambaye ndani yake yeye hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.
Mathayo 28:20X20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 18:20X20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Yohana 14:16-18X16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
Waebrania 13:8X8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.
Yohana 5:26X26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
Yohana 1:4X4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 11:25X25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
Luka 1:35X35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Marko 1:24X24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
1 Yohana 3:16X16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Isaya 9:6X6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
Mika 5:2X2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.
Wakolosai 1:17X17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Yohana 1:2, 3X2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1:3X3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Wakolosai 1:16X16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
Wakolosai 1:7X7 kama mlivyofundishwa na Epafra, mjoli wetu mpenzi, aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu;
Waebrania 1:3X3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Yohana 5:28X28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
Mathayo 25:31, 32X31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
Mathayo 9:6X6 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (amwambia yule mwenye kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, uende nyumbani kwako.
Marko 2:5, 9X5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?
Mathayo 1:21X21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Marko 1:1X1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
Mathayo 8:29X29 Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
Marko 5:7X7 akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese.
Isaya 40:3X3 Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya Bwana; Nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu.
Mathayo 3:3X3 Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
Yohana 1:1, 14X1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 20:18X18 Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo.
Warumi 9:5X5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Waebrania 1:8, 10X8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.10 Na tena, Wewe,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, Na mbingu ni kazi za mikono yako;
Yohana 8:58X58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Yohana 20:17X17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia. 5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. 7 Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. 8 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. 9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? 10 Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake. 11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe. 12 Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. 13 Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14 Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya. 15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu. 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. 19 Bado kitambo kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona. Na kwa sababu mimi ni hai, ninyi nanyi mtakuwa hai. 20 Siku ile ninyi mtatambua ya kuwa mimi ni ndani ya Baba yangu, nanyi ndani yangu, nami ndani yenu. 21 Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 22 Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? 23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. 24 Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. 25 Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia. 27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. 28 Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. 29 Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. 30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. 31 Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Yohana 15
1 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3 Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6 Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. 16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 17 Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana. 18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20 Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. 21 Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka. 22 Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao. 23 Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. 24 Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. 25 Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure. 26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27 Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.
Yohana 16
1 Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. 2 Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. 3 Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. 4 Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi. 5 Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi? 6 Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. 7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. 13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. 16 Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. 17 Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? 18 Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo. 19 Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? 20 Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. 21 Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. 22 Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. 23 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. 24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. 25 Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. 26 Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; 27 kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. 28 Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. 29 Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. 30 Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu. 31 Yesu akawajibu, Je! Mnasadiki sasa? 32 Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. 33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
1 Wakorintho 12:4-6X4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Waebrania 1:3X3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Yohana 14:9X9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Mathayo 28:17X17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
Luka 14:33X33 Basi, kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.
Waebrania 1:6X6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.
Wafilipi 2:10, 11X10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi;
2 Timotheo 4:18X18 Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
Waebrania 13:21X21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
2 Petro 3:18X18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
Yohana 1:14X14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Yohana 1:18X18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Yohana 17:6X6 Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika.
Yohana 14:9X9 Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba?
Yohana 5:30X30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Luka 6:19X19 Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.
Yohana 2:11X11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Yohana 6:1-15, 36X1 Baada ya hayo Yesu alikwenda zake ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, nayo ndiyo ya Tiberia. 2 Na mkutano mkuu wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa. 3 Naye Yesu akakwea mlimani, akaketi huko pamoja na wanafunzi wake. 4 Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi, ilikuwa karibu. 5 Basi Yesu alipoinua macho yake akaona mkutano mkuu wanakuja kwake, alimwambia Filipo, Tununue wapi mikate, ili hawa wapate kula? 6 Na hilo alilinena ili kumjaribu; kwa maana alijua mwenyewe atakalotenda. 7 Filipo akamjibu, Mikate ya dinari mia mbili haiwatoshi, kila mmoja apate kidogo tu. 8 Wanafunzi wake mmojawapo, Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia, 9 Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa? 10 Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao. 11 Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka. 12 Nao waliposhiba, aliwaambia wanafunzi wake, Kusanyeni vipande vilivyobaki, kisipotee cho chote. 13 Basi wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri vilivyowabakia wale waliokula. 14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. 15 Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake.36 Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini.
Yohana 11:41-45X41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia. 42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. 43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. 44 Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake. 45 Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini.
Yohana 14:11X11 Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.
Yohana 8:3-11X3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. 6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. 7 Usistaajabu kwa kuwa nilikuambia, Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. 8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho. 9 Nikodemo akajibu, akamwambia, Yawezaje kuwa mambo haya? 10 Yesu akajibu, akamwambia, Je! Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu? 11 Amin, amin, nakuambia kwamba, Lile tulijualo twalinena, na lile tuliloliona twalishuhudia; wala ushuhuda wetu hamwukubali.
1 Yohana 4:2, 3X2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
Yohana 1:14X14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Wagalatia 4:4X4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,
Mwanzo 3:15X15 Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.
Wafilipi 2:7, 8X7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
1 Timotheo 3:16X16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Mathayo 1:1X1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.
Warumi 1:3X3 yaani, habari za Mwanawe, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili,
Warumi 9:5X5 ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Marko 6:3X3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na maumbu yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
Mathayo 1:20-23X20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao. 22 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, 23 Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Luka 1:31-37X31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Luka 2:40, 52X40 Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.52 Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Luka 2:51X51 Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake.
Waebrania 5:8, 9X8 na, ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; 9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Waebrania 2:10, 18X10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Yohana 1:30X30 Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.
Matendo 2:22X22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;
Warumi 5:15X15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
1 Wakorintho 15:21X21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.
1 Timotheo 2:5X5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
Yohana 8:40X40 Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivyo.
Mathayo 8:20X20 Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Mathayo 26:2X2 Mnajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa Pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa asulibiwe.
Zaburi 8:5X5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
Waebrania 2:9X9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Waebrania 2:14X14 Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi,
Waebrania 2:17X17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Mathayo 4:2X2 Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.
Yohana 19:28X28 Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Yohana 4:6X6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita.
Mathayo 8:24X24 Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
Mathayo 9:36X36 Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.
Marko 3:5X 5 Akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
Mathayo 26:38X38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.
Yohana 12:27X27 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Yohana 11:33, 35X33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,35 Yesu akalia machozi.
Luka 19:41X41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,
Waebrania 5:7X7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
Luka 22:44X44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.
Mathayo 26:39-44X39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. 42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe. 43 Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito. 44 Akawaacha tena, akaenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yale yale.
Marko 1:35X35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
Marko 6:46X46 Hata alipokwisha kuagana nao akaenda zake mlimani kuomba.
Luka 5:16X16 Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.
Luka 6:12X12 Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.
Yohana 19:30, 34X30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.34 lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.
Luka 24:36X36 Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Warumi 8:3X3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
1 Wakorintho 15:45, 47X45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.
Waebrania 5:2X2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;
Mathayo 8:17X17 ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu, Na kuyachukua magonjwa yetu.
Iasya 53:4X4 Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Waebrania 5:7X7 Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
1 Wakorintho 10:13X13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
Waebrania 2:18X18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Waebrania 2:10X10 Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso.
Waebrania 12:4X4 Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Mathayo 1:20X20 Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba neno.
Luka 1:35X35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Waebrania 7:26X26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
2 Wakorintho 5:21X21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
1 Petro 2:22X22 Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.
1 Petro 1:19X19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
Waebrania 9:24X24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
1 Yohana 3:5-7X5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. 6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 7 Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;
Yohana 8:46X46 Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi? Nami nikisema kweli, mbona ninyi hamnisadiki?
Yohana 14:30X30 Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.
Luka 23:34X34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura.
Yohana 5:30X30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
1
Zekaria 6:13X13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Waebrania 4:14-16X14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Waebrania 5:2X2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;
Waebrania 2:17X17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.
Waebrania 2:18X18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Wafilipi 2:7X7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Warumi 6:23X23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Wakorintho 15:3X3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
Waebrania 2:9X9 ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.
Yohana 16:33X33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
2 Wakorintho 3:18X18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Waebrania 12:2, 3X2 tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 Maana mtafakarini sana yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu.
1 Ptero 2:21X21 Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
Yohana 3:15X15 ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.
Wagalatia 4:4X4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria,
Wafilipi 2:6, 7X6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu;
Yohana 1:14X14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Warumi 8:3X3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili;
1 Timotheo 3:16X16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
1 Yohana 4:2X2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Matendo 20:28X28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Wakolosai 1:13, 14X13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;
Yohana 3:13X13 Wala hakuna mtu aliyepaa mbinguni, ila yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.
Waebrania 10:5X5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari;
Wakolosai 2:9X9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
2 Petro 1:14X14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionyesha.
Wafilipi 2:6-8X6 ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 7 bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 8 tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Wakolosai 2:9X9 Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili.
Yohana 5:19, 30X19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Yohana 8:28X28 Basi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye; na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo.
Waefeso 3:19X19 na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.
2 Petro 1:3, 4X3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. 4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Ufunuo 3:21X21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
1 Wafalme 19:16X16 Na Yehu mwana wa Nimshi mtie mafuta awe mfalme wa Israeli; na Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola mtie mafuta awe nabii mahali pako.
Kutoka 30:30X30 Nawe utawatia mafuta Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
2 Samweli 5:3X3 Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za Bwana; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.
Kumbukumbu 18:18X18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
Yohana 6:14X14 Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
Yohana 7:40X40 Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.
Matendo 3:22, 23X22 Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. 23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
Luka 13:33X33 Pamoja na hayo imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa; kwa kuwa haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemu.
Mathayo 7:29X29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.
1 Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia; 2 akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema, 3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. 5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. 7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. 9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. 12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu. 13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. 17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. 21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. 23 Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. 25 Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. 26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho. 27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 30 Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. 31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; 32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini. 33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako; 34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. 38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; 39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 40 Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. 41 Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. 42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. 43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; 44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, 45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? 47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? 48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Mathayo 6
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. 2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, 10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupe leo riziki yetu. 12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. 13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina. 14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. 16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 19 Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. 22 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo! 24 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. 25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? 27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? 28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti 29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. 30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Mathayo 7
1 Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. 2 Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. 3 Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? 4 Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? 5 Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. 6 Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. 7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; 8 kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. 9 Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10 Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? 12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. 13 Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. 14 Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache. 15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; 25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. 26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; 27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa. 28 Ikawa, Yesu alipoyamaliza maneno hayo, makutano walishangaa mno kwa mafundisho yake; 29 kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye amri, wala si kama waandishi wao.
Mathayo 22:36-40X36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Mathayo 24:1-51X1 Yesu akaenda zake, akatoka hekaluni; wanafunzi wake wakamwendea ili kumwonyesha majengo ya hekalu. 2 Naye akajibu akawaambia, Hamyaoni haya yote? Amin, nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa. 3 Hata alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakisema, Tuambie, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia? 4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 Nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali. 8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa utungu. 9 Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. 10 Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana. 11 Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. 12 Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. 13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. 14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. 15 Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), 16 ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani; 17 naye aliye juu ya dari asishuke kuvichukua vitu vilivyomo nyumbani mwake; 18 wala aliye shambani asirudi nyuma kuichukua nguo yake. 19 Ole wao wenye mimba na wanyonyeshao siku hizo! 20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato. 21 Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. 22 Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo. 23 Wakati huo mtu akiwaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko kule msisadiki. 24 Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. 25 Tazama, nimekwisha kuwaonya mbele. 26 Basi wakiwaambia, Yuko jangwani, msitoke; yumo nyumbani, msisadiki. 27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 28 Kwa kuwa po pote ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai. 29 Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika; 30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi. 31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu. 32 Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu; 33 nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni. 34 Amin, nawaambia, Kizazi hiki hakitapita, hata hayo yote yatakapotimia. 35 Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe. 36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa; 41 wanawake wawili watakuwa wakisaga; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa. 42 Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. 43 Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. 44 Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. 45 Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? 46 Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. 47 Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. 48 Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; 49 akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; 50 bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, 51 atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Luka 19:41-44X41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia, 42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako. 43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; 44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.
1 Petro 1:11X11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Ufunuo 12:17X17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ufunuo 19:10X10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
Zaburi 110:4X4 Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrani 5:6, 10X6 kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 5:1, 4, 10X1 Maana kila kuhani mkuu aliyetwaliwa katika wanadamu amewekwa kwa ajili ya wanadamu katika mambo yamhusuyo Mungu, ili atoe matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi;4 Na hapana mtu ajitwaliaye mwenyewe heshima hii, ila yeye aitwaye na Mungu, kama vile Haruni.10 kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
M. Walawi 1:4X4 Kisha ataweka mkono wake juu ya kichwa cha hiyo sadaka ya kuteketezwa; nayo itakubaliwa kwa ajili yake, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
M. Walawi 4:29, 31, 35X29 Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa.31 Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa Bwana; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.35 kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za Bwana zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.
M. Walawi 5:10X10 Kisha huyo ndege wa pili atamsongeza kuwa sadaka ya kuteketezwa, sawasawa na sheria; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.
M. Walawi 16:6X6 Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake.
M. Walawi 17:11X11 Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.
Waebrania 10:1-4X1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. 2 Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? 3 Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. 4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.
Waebrania 9:9X9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,
Waebrania 10:1X1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
Waebrania 9:9, 23, 24X9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye,23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. 24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
Zaburi 40:6-8X6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. 7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) 8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Waebrania 10:5-9X5 Kwa hiyo ajapo ulimwenguni, asema, Dhabihu na toleo hukutaka, Lakini mwili uliniwekea tayari; 6 Sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukupendezwa nazo; 7 Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja (katika gombo la chuo nimeandikiwa) Niyafanye mapenzi yako, Mungu. 8 Hapo juu asemapo, Dhabihu na matoleo na sadaka za kuteketezwa na hizo za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo (zitolewazo kama ilivyoamuru torati), 9 ndipo aliposema, Tazama, nimekuja niyafanye mapenzi yako. Aondoa la kwanza, ili kusudi alisimamishe la pili.
2 Wakorintho 5:21X21 Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.
Wagalatia 3:13X13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
1 Yohana 1:7X7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Wakorintho 15:3X3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko;
Waebrania 2:17, 18X17 Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. 18 Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa.
Waebrania 4:15X15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Waebrania 5:2X2 awezaye kuwachukulia kwa upole wao wasiojua na wenye kupotea, kwa kuwa yeye mwenyewe yu katika hali ya udhaifu;
Zekaria 6:13X13 Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,
Waebrania 8:1X1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
Waebrania 1:3X3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Waebrania 9:24X24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;
Waebrania 7:25X25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
1 Yohana 2:1X1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Zekaria 3:1X1 Kisha akanionyesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kushindana naye.
Warumi 8:34X34 Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Yohana 16:23X23 Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu.
Zaburi 103:19X19 Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.
Zaburi 45:6X6 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Waebrania 1:8, 9X8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
Zaburi 2:2X2 Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake.
Zaburi 2:6, 7X6 Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu. 7 Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
Waebrania 1:5X5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
Yeremi 23:5, 6X5 Tazama siku zinakuja, asema Bwana, nitakapomchipushia Daudi Chipukizi la haki; naye atamiliki mfalme, atatenda kwa hekima, naye atafanya hukumu na haki katika nchi.6 Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli atakaa salama, na jina lake atakaloitwa ni hili, Bwana ni haki yetu.
Zekaria 6:13X13 Naam, yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
Luka 1:33X33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
Waebrania 4:16X16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Mathayo 25:31X31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
Waebrania 9:15-18X15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. 16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. 18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu.
Marko 1:15X15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Yohana 3:5X5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Yohana 3:3X3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Marko 4:22-31X22 Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi. 23 Mtu akiwa na masikio ya kusikilia, na asikie. 24 Akawaambia, Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena mtazidishiwa. 25 Kwa maana mwenye kitu atapewa, naye asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. 26 Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi; 27 akawa akilala na kuondoka, usiku na mchana, nayo mbegu ikamea na kukua, asivyojua yeye. 28 Maana nchi huzaa yenyewe; kwanza jani, tena suke, kisha ngano pevu katika suke. 29 Hata matunda yakiiva, mara atapeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika. 30 Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? 31 Ni kama punje ya haradali, ambayo ipandwapo katika nchi, ingawa ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika nchi,
Mathayo 13:33X33 Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyoitwaa mwanamke, akaisitiri ndani ya pishi tatu za unga, hata ukachachwa wote pia.
Luka 17:20, 21X20 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; 21 wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
Yohana 18:37X37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Warumi 14:17X17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Wakolosai 1:13X13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
1
Zekaria 9:9X9 Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda.
Mathayo 21:8, 9X8 Watu wengi katika ule mkutano wakatandaza nguo zao njiani; na wengine wakakata matawi ya miti, wakayatandaza njiani. 9 Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Luka 23:3X3 Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu akamwambia, Wewe wasema.
Yohana 18:33-37X33 Basi Pilato akaingia tena ndani ya Praitorio, akamwita Yesu, akamwambia, Je! Wewe ni Mfalme wa Wayahudi? 34 Yesu akamjibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, au watu wengine walikuambia habari zangu? 35 Pilato akajibu, Ama! Ni Myahudi mimi! Taifa lako na wakuu wa makuhani ndio waliokuleta kwangu. Umefanya nini? 36 Yesu akajibu, Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania, nisije nikatiwa mikononi mwa Wayahudi. Lakini ufalme wangu sio wa hapa. 37 Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Yohana 19:2X2 Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.
Yohana 19:3X3 Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi.
Yohana 14:6X6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Zaburi 2:7, 8X7 Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. 8 Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako, Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
Waebrania 1:3-5X3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba. 4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu. 5 Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
Wafilipi 2:9-11X9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Waefeso 1:20-23X20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Mathayo 17:2X2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Mathayo 24:27, 30, 31X27 Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.30 ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni; ndipo mataifa yote ya ulimwengu watakapoomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbinguni pamoja na nguvu na utukufu mwingi.31 Naye atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya parapanda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka mwisho huu wa mbingu mpaka mwisho huu.
Mathayo 25:31, 32X31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; 32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
Danieli 7:9, 10, 14X9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.14 Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.
Danieli 7:27X27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. 11 Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. 12 Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao. 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 21
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. 9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; 11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; 12 ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. 13 Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. 14 Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo. 15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa. 17 Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika. 18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto. 21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu. 22 Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake. 23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. 24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake. 25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku. 26 Nao wataleta utukufu na heshima ya mataifa ndani yake. 27 Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.
Wagalatia 5:22, 23X22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.