Utangulizi
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii. Karama hii ni alama inayolitambulisha masalio na ilidhihirika katika huduma ya Ellen G. White. Kama mjumbe wa Bwana, maandishi yake yanaendelea kuwa chanzo madhubuti cha ukweli yanayotoa kwa kanisa faraja, uongozi, mafundisho, na maonyo. Pia yanaweka wazi kwamba Biblia ndiyo kanuni ambayo kwayo mafundisho yote na uzoefu lazima vipimwe.” (Yoe. 2:28, 29;Mdo. 2: 14-21Yoeli 2:28,29;X 28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; 29 tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.Ebr. 1: 1-3;Matendo 2:14-21X 14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake. 15 Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), akasema, 16 Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu; 17 kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. 18 (Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka. 19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.) 20 Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; 21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu,Ufu. 12:17;Waebrania 1:1-3;X 1 Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu. 3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;Uf. 19:10)Ufunuo 12:17X 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.Ufunuo 19:10X 10 Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.
Manabii walitekeleza jukumu muhimu kwenye nyakati za Agano la Kale na Agano Jipya. Je, unabii utakoma baada ya Biblia kuandikwa? Ili kupata jibu, ni vema tukapitia historia ya manabii.
Karama ya Unabii nyakati za Biblia
Ijapokuwa dhambi ilikomesha mawasiliano ya moja kwa moja baina ya Mungu na wanadamu (Isa. 59:1,2;
Majukumu ya Manabii katika Agano Jipya
- Kusaidia Kuanzisha Kanisa:Kanisa limejengwa kwa msingi wa mitume na manabii, Yesu Kristo akiwa jiwe kuu la pembeni (Efe.2:20,21).
Waefeso 2:20,21X 20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; - Walianzisha Utume wa Kanisa: Ni kwa njia ya manabii, Roho Mtakatifu aliwachagua Paulo na Barnaba kwa safari yao ya kwanza ya kiutume (Mdo. 13:1, 2)
na akaelekeza ni wapi waende kufanya kazi (Mdo.16:6-10)
Matendo 13:1,2X 1 Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.Matendo 16:6-10X 6 Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. 7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, 8 wakapita Misia wakatelemkia Troa. 9 Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. 10 Basi alipokwisha kuyaona yale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema. - Walijenga kanisa kiroho: Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji (1Kor.14:3)
. Pamoja na karama zingine za roho, unabii umetolewa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa ajili ya kazi za huduma, ili kwamba mwili wa Kristo upate kujengwa.(Efe.4:12)
1 Wakorintho 14:3X 3 Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.Waefeso 4:12X 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; - Waliunganisha na kulilinda kanisa: Manabii walisaidia umoja wa imani na kulilinda na mafundisho ya uwongo mpaka sote tutakapoufikia umoja katika imani na katika kumjua sana Mwana wa Mungu na kuwa watu wazima kwa kufikia kipimo cha ukamilifu wa Kristo. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwatupwa huku na huku na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho kwa hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu.(Efe.4:13,14)
Waefeso 4:13,14X 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. - Walionya juu ya hatari zijazo: Nabii moja katika Agano Jipya alionya juu ya njaa itakayokumba watu karibuni (Mdo.11:27-30)
na wengine walionya kwamba Paulo atakamatwa na kufungwa Yerusalemu (Mdo. 20:23, 21:4, 10-14)
Matendo 11:27-30X 27 Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia. 28 Na tulipokusanyika akasimama mmoja wao, jina lake Agabo, akaonyesha kwa uweza wa Roho Mtakatifu kwamba njaa kubwa itakuja karibu katika dunia nzima, nayo ikatukia katika siku za Klaudio. 29 Na wale wanafunzi, kila mtu kwa kadiri ya alivyofanikiwa, wakaazimu kupeleka msaada kwa ndugu zao waliokaa Uyahudi. 30 Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.Matendo 20:23,21:4,20-14X 23 isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. 4 Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu. 14 Alipotufikia huko Aso, tukampakia, kisha tukafika Mitilene. - Walithibitisha imani wakati wa ushindani: Baada ya baraza la kanisa kuamua juu ya hoja za wokovu wa mataifa mengine, manabi walitumwa kwenda kuimarisha waumini. “Yuda na Sila, ambao wenyewe walikuwa manabii wakanena maneno mengi ya kuwatia moyo na kuwajenga katika imani wale ndugu walioamini.” (Mdo. 15:32)
Matendo 15:32X 32 Tena Yuda na Sila, kwa kuwa wao wenyewe ni manabii, wakawausia ndugu kwa maneno mengi, wakawathibitisha.
Karama ya Unabii katika Siku za Mwisho
Wengi huamini kwamba karama ya unabii ilikoma wakati wa mitume kwenye Agano Jipya. Hata hivyo Biblia huthibitisha kuwepo kwa karama hii wakati wa taabu, siku za mwisho.
Kuendelea kwa karama ya unabii
Hakuna ushahidi kwamba Mungu ataondosha karama ya unabii iliyotolewa kujenga kanisa (Efe.4:13)
Karama ya Unabii karibu na Kuja kwa Yesu mara ya Pili
Kama alivyotoa karama ya unabii kwa Yohana Mbatizaji amtambulishe Yesu kwa wanadamu, Mungu atatoa karama ya unabii ili kuja kwa Yesu mara ya pili kutangazwe kwa nguvu. Ni ukweli kwamba Yesu alitabiri ujio wa manabii wa uongo kabla ya ujio wake (Mt. 24:11, 24)
Karama ya Unabii katika Kanisa la Masalio
Ufunuo 12 kinaonyesha vipindi viwili vya mateso kwa watu wa Mungu. Kipindi cha kwanza ni kile cha miaka 1260 ya mtu wa kuasi (Uf.12:6, 14).
Kupima Karama ya Unabii
Kwa kuwa watakuja manabii wa uwongo na wito wa Paulo kwamba “msitweze unabii, pimeni mambo yote, chagueni lililo jema (1Thes.5: 20-22 cf.
- Je ujumbe unakubaliana na Biblia? “Na waende kwa sheria na ushuhuda, kama hawasemi sawasawa na neno hili ni kwa sababu hao hakuna asubuhi”(Isa.8:20 cf.Kumb.13:1-4)
Isaya 8:20 20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.Roho za manabii hutii manabii (1Kor. 14:32)K. Torati 13:1-4X 1 Kukizuka katikati yako nabii, au mwotaji wa ndoto, akikutolea ishara au ajabu, 2 ikatukia hiyo ishara au hiyo ajabu aliyokuambia akisema, Na tuifuate miungu mingine usiyoijua, tuitumikie hiyo; 3 wewe usiyasikize maneno ya nabii yule, au yule mwotaji wa ndoto, kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, yuawajaribu, apate kujua kwamba mwampenda Bwana, Mungu wenu, kwa mioyo yenu yote na roho zenu zote. 4 Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.na pia kwa Mungu hakuna kugeuka geuka (Yak.1:17).1 Wakorintho 14:32X 32 Na roho za manabii huwatii manabii.Yakobo 1:17X 17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka. - Je atabiricho kinatimia? Tutajuache kwamba huyu ametumwa na Bwana, ni kwamba anachosema ni lazima kitimie (Kumb.18:21, 22 cf.
Jer. 28: 9).
K. Torati 18:21,22X 21 Nawe ukisema moyoni mwako, Tutajuaje neno asilolinena Bwana? 22 Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope.Hata hivyo ni vema kuzingatia unabii wenye masharti (Jer. 18:7-9).Jeremia 28:9X 9 Nabii atabiriye habari za amani, neno la nabii yule litakapotokea, ndipo nabii yule atakapojulikana, kuwa Bwana amemtuma kweli kweli.Jeremia 18:7-9X 7 Wakati wo wote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuung'oa, na kuuvunja, na kuuangamiza; 8 ikiwa taifa lile nililolitaja litageuka, na kuacha maovu yake nitaghairi, nisitende mabaya yale niliyoazimia kuwatenda. 9 Na wakati wo wote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda, - Je, kufanyika mwili kwa Kristo kunaheshimiwa? Akikiri Yesu amekuja katika mwili atakubalika, akikataa basi hakubaliki (1Yoh. 4:1-3).
1 Yohana 4:1-3X 1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. 2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. 3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani. - Je, nabii ana matunda mema au mabaya? Kwa kuwa unabii unatoka kwa Mungu (2Pet 1:21)
lazima matunda yake yawe mema. “Mtawatambua kwa matunda yao” (Mt. 7:16, 18-20).
2 Petro 1:21X 21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.Eliya alikuwa na hali ya kibiunadamu (Yak.5:17)Mathayo 7:16, 18-20X 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.hata hivyo, maisha yake hayakuwa ya kimwili bali yalijawa na tunda la roho (Gal. 5:19-22).Yakobo 5:17X 17 Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.Pili, matokeo yake kazi ya nabii daima ni kulisaidia kanisa (Efe.4:12-16)(Wagalatia 5:19-22X 19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,Waefeso 4:12-16 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Roho ya Unabii katika Kanisa la Waadventista Wasabato
Karama ya unabii ilijidhihirisha katika huduma ya Mama Ellen G. White, mojawapo ya waanzilishi wa Kanisa.Tangu mwaka 1844 alipokuwa na miaka 17 hadi mwaka aliofikwa na mauti 1915, alipata maono zaidi ya 2,000. Alifanya kazi Marekani, Ulaya na Australia akishauri, akifungua kazi, akihubiri na kuandika. Kwa kumpima kwa vigezo tulivyobainisha, anatosheleza kabisa.
- Kukubaliana na Biblia: Kazi yake ya uandishi imenukuu aya maelfu za Biblia, mara nyingi yakifafanuliwa. Uchunguzi makini umedhihirisha kwamba maandiko yake yanalingana, ni sahihi na yanapatana kabisa na Biblia.
- Usahihi wa Utabiri: Ellen alitabiri mengi na mengine yanasubiri kutimizwa. Hata hivyo, yaliyotimia ni (1) Kuinuka kwa umizimu – mwaka 1850 wakati umizimu unaanza alionya kwamba ni udanganyifu utakaoendelea hadi siku za mwisho. (2) Ushirikiano wa karibu baina ya Ukatoliki na Uprotestanti (3) Kazi ya kuchapa vitabu, kwamba mwanzo wake ni mdogo lakini hatimaye utafaulu.
- Kumkiri Yesu katika mwili: Katika kitabu chake cha Tumaini la Vizazi Vyote (Desire of Ages) Mama White amekiri kwamba Yesu amekuja katika mwili. Pia kwenye kitabu cha Njia Salama (Steps to Christ) anamkiri Yesu.
- Mvuto wa Kazi yake: Zaidi ya karne na nusu imepita tangu afariki, lakini maoni haya yanawakilisha vema mguso wake: Ingawa hakuwa ofisa wa kanisa wala hakupokea mshahara hadi mume wake alipofariki, kando ya Biblia, huduma yake ndiyo imeunda sura ya Kanisa la Waadventista wa Sabato.” Richard Hammill, Karama za Roho katika Kanisa Leo, Ministry Julai 1982.
Roho ya Unabii na Biblia
Maandiko ya Ellen White siyo badala ya Maandiko Matakatifu. Haiwezekani kuwekwa kwenye ngazi sawa. Maandiko Matakatifu husimama peke yake, kiwango pekee cha kupima mafundisho yote pamoja na maandishi ya Ellen White.
- Biblia kipimo pekee: Waadventista Wasabato huamini katika kanuni ya Sola Scriptura kwamba Biblia na Biblia peke yake ndiyo mtafsiri wake, na msingi wa mafundisho yote. Kanisa halikupokea mafundisho yake kutoka kwa Ellen White ila kutoka kwenye Biblia. Huduma yake ilisaidia kuelewa Biblia na kuthibitisha hitimisho lililofikiwa kwa kusoma Biblia.
- Kuongoza Kwenye Biblia: Yeye mwenyewe aliona kazi yake kuwa ni kuongoza watu kurudi kwenye Biblia, kwa kuwa watu walikuwa wameacha kuifuata.
- Kuongoza kuelewa Biblia: Ellen White aliona kuwa mafundisho yake yanasaidia mtu kuelewa vema Biblia. Shuhuda zilizotolewa siyo nuru mpya, bali hukazia nuru iliyokwisha kutolewa yaani Biblia.
- Kuongoza kutumia Kanuni za Biblia: Unabii wa Ufunuo utadhihirika pale ambako kila moja atapima na kuchukua kilicho chema. Twaweza kupata au kupoteza kulingana na jinsi tunavyochunguza Maandiko.
Maisha na Huduma ya Ellen White
(Dondoo kutoka Church Heritage)- Alizaliwa Novemba 26, 1827 shambani Gorham, Maine, kama maili 12 kutoka Portland. Akiwa na pacha mwenzake, alikuwa mdogo kuliko wote katika familia yenye watoto wanane. Alikuwa mtoto mwenye furaha akipenda sana mambo ya imani.
- Maisha yake yalibadilika siku moja wakati akiwa anavuka Park alipopigwa jiwe na msichana mwingine. Pua yake ilivunjika na uso wake uliharibika kwa muda. Alizimia wiki tatu na mshtuko ulimfanya asiweze kufanya chochote kwa wakati mrefu. Kusoma kwake kulikoma kwa kuwa afya yake haikuruhusu.
- Mwaka 1840 hadi mwaka 1844 Ellen na familia yao walisikiliza mahubiri ya William Miller, juu ya ujio wa Yesu ulivyo karibu. Walikubaliana na mahubiri na hawakuhama kutoka kwenye kanisa lao la Methodist. Hata hivyo haikuwa rahisi. Katika mkutano wa kambi mojawapo, alijitoa na ndipo roho yake ilipotulia. Tangu wakati huo alianza mahusiano mapya na Bwana wake.
- Familia yake ilikubali Kilio cha Usiku wa Manane na kuacha makanisa yaliyoasi – yaani yaliyokataa ujumbe wa Yesu kurejea mara ya pili. Pamoja na kwamba Yesu hakurudi kama walivyotarajia, hawakukata tamaa kuacha imani yao.
- Maono yake ya kwanza yalikuja muda mfupi baada ya mategemeo yao ya Yesu kurejea kutokutimizwa. Akiwa na umri mdogo (miaka 17), uwezo wake mdogo kuongea, afya yake iliyozorota, na kipindi kigumu alichokabiliana nacho, alimwomba Mungu amwepushe na jukumu la kuwa mjumbe wake. Hata hivyo wito wake haukubadilishwa, na hivyo alikubali kufanya kile ambacho Mungu alimwamuru.
- Apili Mwaka 1847 alipewa njozi ya Sabato. Aliona Hekalu mbinguni Yesu akifungua pazia. Kwenye Patakatifu pa Patakatifu, aliona Amri Kumi za Mungu na mng’ao wa mwanga ukimulika amri ya nne, ambayo ni Sabato. Akajulishwa kwamba kama Sabato ingeendelea kutunzwa kwa uaminifu na wanadamu, asingekuwako asiyeamini Mungu, wenye mashaka na ulimwengu usingeingia kwenye ibada ya sanamu. Njozi hii, ilifungua mlango wa kuhubiri ujumbe wa Malaika wa Tatu kwa nguvu. Waumini walioona umuhimu wa Patakatifu, Sabato na Ujio wa Yesu mara ya pili, walikuja kuwa waanzilishi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. (Life Sketches pp. 95)
- Kwa miaka 70 iliyofuata, jukumu lake lilikuwa kupokea mashauri kutoka kwa Mungu naye aliyatoa kwa watu wake. Alizungumza katika mikutano mingi na aliandika vitabu vipatavyo 40 ambavyo vilikuja kujulikana kama Roho ya Unabii, akachangia pia kuchapisha makala nyingi katika machapisho ya kanisa la Waadventista wa Sabato. Kitabu kinachopendwa zaidi ni habari za maisha ya Yesu – Tumaini la Vizazi Vyote. Alisafiri kuzunguka sehemu nyingi za Amerika Kaskazini, Ulaya, Australia na New Zealand, akifungua kazi katika maeneo mapya. Alikuwa muhimu katika kufungua chuo cha Avondale kilichoko Australia.
- Ellen White alipokea ujumbe kwa njia ya maono. Katika maono, uko ushahidi kwamba aliongozwa na Mungu. Aliangalia vitu vilivyo mbali, kuhema kwake kulikoma lakini hakubadilika rangi wala moyo wake haukukoma kudunda. Shuhuda za waliomwona, pamoja na madaktari, walishuhudia kwamba utaratibu wote haukuwa wa kidunia. Kuna wakati alibeba Biblia kubwa ya paundi 18 kwa nusu saa pasipo kuyumba wala kuidondosha.
- Baadhi ya vitabu alivyoandika ni Shuhuda kwa Kanisa (1855-4909), Early Writings (1882), The Great Controversy (1888), Patriarchs and Prophets (1890), Gospel Workers (1892), Steps to Christ (1892), Thoughts from the Mount of Blessings (1896), Christ’s Object Lessons (1900), Education (1903), The Ministry of Healing (1905), The Acts of Apostles (1911), Counsels to Parents, Teachers and Students (1913), Prophets and Kings (1916).
- 10. Ellen White alilala usingizi wa mauti nyumbani kwake Elmshaven Julai 16, 1915 akazikwa alikozikwa mume wake na watoto wake Battle Creek.


