Dunia Mpya

Utangulizi


Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa, Mungu ataweka tayari makao ya milele waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na kujifunza mbele zake. Kwa hapa Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakuwepo tena. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo, naye atatawala milele. Amina. (2Pet. 3:13; Isa. 35, 65:17-25; Mt. 5:5; Ufu 21:1-7, 22:1-5, 11:5).

Wengi wa wanadamu hudhani kwamba mbinguni ni bora kuliko kule kwingine. Hata hivyo kutokana na nuru ya Maandiko Matakatifu, nchi mpya ni ya kutamanika kuliko maisha tuliyonayo kwa sasa.

Maelezo ya Nchi Mpya

Nchi mpya ni kitu halisi

Sura mbili za kwanza za Biblia husimulia uumbaji wa Mungu wa maskani ya wanadamu iliyokuwa kamili. Sura mbili za mwisho za Biblia pia husimulia uumbaji mwingine mkamilifu wa maskani ya wanadamu, bali sasa utakuwa uumbaji mpya, baada ya ule wa awali kuharibiwa na dhambi. Mara zote, Biblia hutuambia kuwa maskani ya milele ya watakatifu ni mahali halisi, mahali ambako watu wakiwa na miili yao wataona, watasikia, watagusa, wataonja, watanusa, watapima, watapata picha, na kuifurahia. Waraka wa pili wa Petro sura ya tatu, unatoa muhtasari wa dunia tatu, ya kwanza ni ile kabla ya gharika, ya pili ni hii tuliyonayo itakayotakaswa kwa moto na ile ya tatu ni ile ambayo haki inatawala (2 Pet. 3: 6, 7, 13).

Kuendelea na kutofautiana

Nchi mpya huleta wazo kwamba dunia inaendelea kuwapo lakini inatofautiana na ile ya kwanza. Petro na Yohana waliona dunia ya awali ikitakaswa kwa moto, ikafanywa upya (2Pet.3:10-13, Uf. 21:1). Ijapokuwa itafanywa mpya, itaendelea kujulikana – kwamba ni nyumbani. Pia itakuwa mpya kwa kuwa Mungu atakuwa ameondosha kila doa la dhambi.

Yerusalemu mpya

Yerusalemu mpya ni mji mkuu wa hii Nchi Mpya. Yerusalemu maana yake ni jiji la amani. Jina hilo limekosa maana kwenye dunia tuliyonayo leo. Katika nchi mpya, litaonyesha uhalisi wa amani.

Kiunganishi

Jiji hili litaunganisha mbingu mpya na nchi mpya. Kimsingi, mbingu humaanisha anga (Mwa. 1:20), anga la mbingu (Mwa.1:14-17), mbingu ya tatu ambako ndiko Paradiso (2 Kor. 12:2-4). Mungu atajibu lile ombi kwenye sala ya BWANA, kwamba ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama mbinguni. Kwa kuiweka Yerusalemu Mpya kwenye Nchi Mpya, (Uf. 21: 1, 2) hatakuwa tu ameongezea nchi mpya umaridadi, bali pia atakuwa ameiinua Nchi Mpya ng’ambo ya ilivyokuwa, kabla ya kuanguka na kuifanya maskani Yake kutawala ulimwengu mzima. (Uf. 21:3)

Maelezo jinsi Yerusalemu mpya ilivyo

Yohana anasema Yerusalemu mpya itakuwa sawa na bibi arusi aliyepambwa kwa mumewe(Uf. 21: 2)
  1. Nuru yake. Kitu cha kwanza alichoona Yohana ni nuru ya mji wa Yerusalemu. Mwana kondoo, mume wa bibi arusi aliyepambwa, ndiye nuru yake (Uf. 21:9, 11). Utukufu wa Mungu utaangazia mji kiasi cha kufanya mianga mingine kufifia (Uf. 21:23, 24). Hakuna vichochoro vya giza (Uf. 21:25). Hapatahitajika, taa wala nuru ya jua, kwa Mungu mwenyewe atatoa nuru (Uf. 22:5)
  2. Ujenzi wake Mungu anatumia vito (madini) ya thamani nyingi kuujenga mji huu yaspi, kama bilauri (Uf. 21:11, 18).Msingi wake umetegemezwa kwa vito aina 12, yaspi, yakuti samawi, kalkedoni, zumaridi, sardoniki, akiki, kriolitho, zabarajadi, yakuti ya manjano, krisopraso, hiakinto na amethisto. (Uf. 21:19 -20). Hata hivyo, vito hivyo sivyo vyenye thamani kubwa. Mji umejengwa kwa dhahabu safi (Uf. 21:18, 21). Malango 12 yataufanya mji kuingilika. Vipimo vya mji marefu, mapana na kwenda juu kwake ni sawasawa, kama maili 1,500. (Uf. 21: 15, 16)
  3. Vyakula vyake na maji yake. Mto unatitirisha maji kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu, mto wa maji ya uzima ( Uf. 22:1). Mti moja wa uzima kando ya kila upande wa mto, hutoa aina 12 tofauti za matunda ambazo zitawafanya wasizeeke wala kuchoka (Uf. 22:2, Mwa. 3:22). Walao matunda ya mti huu hawahitaji usiku kupumzika (Uf. 21:25), kwa kuwa katika nchi mpya hawatachoka.
  4.  

Maskani yetu ya Milele

Biblia huweka wazi urithi wa watakatifu kuwa ni nchi. (Mt. 5:5, Zab. 37:9, 29, 115:16). Yesu alikwenda kutuandalia mahali (Yoh. 14:1–3), na kama tulivyoona, Maandiko Matakatifu huyaweka Maskani ya Mungu duniani (Uf. 21:2, 3, 5).

1. Maskani ndani ya Jiji.

Jiji la Yerusalemu ndilo ambalo Ibrahimu alilitamani (Ebr. 11:10). Humo humo kuna makao mengi (Yoh. 14:2).

2. Maskani kwenye nchi isiyo Jiji

Watakatifu hawatazuiliwa ndani ya Jiji la Yerusalemu tu, kwa kuwa watairithi nchi. Kutoka ndani ya jiji watakwenda kubuni na kujenga nyumba zao (Isa. 65:21).

3. Nyumbani pamoja na Mungu na Kristo

Ahadi ya Yesu ya nilipo mimi nanyi mwepo itatimia (Yoh. 14:3). Makusudi ya Mungu kufanyika mwili (Yoh. 1:14) yatatimia. Maskani ya Mungu na wanadamu, Mungu akiwa Mungu wao, na watu wakiwa watu wake (Uf. 21:3).

Maisha katika Nchi Mpya

1. Kutawala pamoja na Mungu na Kristo (Uf. 22:3-5, cf. 5:10)

2. Shughuli za vitendo katika nchi mpya. Tumekwisha kuona kuwa watakatifu watajenga (Isa. 65:21) ikiwa ni maana ya kubuni, kujenga, kuweka samani, kubadilisha muundo wa ujenzi na kadhalika. Mpango wa Mungu wa awali utarejeshwa. Huko mwanzo, Adamu alipewa kulima na kutunza bustani (Mwa. 2:15). Ukamilifu mtupu (Mw.1:31)

Maisha ya Kijamii kwenye Nchi mpya

1. Marafiki na familia.

Kutakuwa na kufahamiana. Ibrahimu, Isaka na Yakobo wataendelea kuwa na majina yao (Mt. 8:11). Bila shaka tutaendelea kusalimiana na wenzetu ambao kwa sasa tunashirikiana pamoja nao.

2. Je, kutakuwako Ndoa?

Jibu la Yesu kwa swali la Masadukayo linasema hakutakuwa na ndoa kwenye nchi mpya. (Mt. 22:29, 30). Mungu hatanyima watu wake kilicho chema (Zab. 84:11). Kwa kuwa Mungu ni pendo, upendo wake utafurika nasi tutaufurahia (1 Yoh. 4:8, Zab. 16:11).

Maisha ya Kiakili kwenye Nchi Mpya

1. Je, kutakuwako na magonjwa huko?

Majani ya mti yataponya mataifa (Uf.22:2). Kuponywa kunakosemwa hapa ni kurejesha hali ya mwanadamu kurejea kutokana na kuharibiwa na dhambi. Hivyo uponyaji unamaana ya kuponya na akili pia kwa kuwa hapatakuwa na kuugua. (Isa. 33:24, 20).

2. Hapatakuwa na kikomo cha kuongeza maarifa.

Mambo makuu ya ajabu yatafikiwa na hali ya juu ya mawazo na vifiko vyote vitafikiwa. Hata hivyo kutakuwa na mambo mengi ya ajabu ya kupekua. Kwa milele na milele kutakuwa na mafunzo yasiyo na mwisho wala hakuna kuchoka. Hazina zote za Mungu zitafunguliwa kwa wana wa Mungu waliokombolewa. Watatembea dunia nyingine bila kuwa na safari za kuchosha. Wana wa nchi hii wataingia katia ulimwengu wa wasiokuwa na dhambi na kushiriki maajabu ya elimu yao isiyokuwa na kasoro, ambayo wao wamekuwa nayo vizazi kwa vizazi”. Ellen G. White Great Controversy 677

3. Maisha ya Kiroho kwenye Nchi Mpya.

Kama Yesu alivyokuja kutumika (Mt. 20:28), watakatifu watamtumikia Yesu (Ufu. 22:3). Sabato hata sabato watapata fursa ya kumwabudu Mungu. (Isa. 66:23).

Ambavyo Havitakuwako tena Kwenye Nchi Mpya

1. Maovu yote yataondoshwa Uf. 21:4.

Garantii kwamba dunia itabaki bila uovu ni kwa kuwa waovu hawataruhusiwa kuwemo (Uf. 21:8, Uf. 22:15). Alama itakayobaki ni makovu ya Yesu yanayotokana na kusulubiwa kwake. (Ellen G. White Great Controversy 677)

2. Yaliyopita hayatakumbukwa (Isa. 65:17).

Uko ushahidi kwamba taabu ya maisha ya dunia hazitakumbukwa (Isa. 65:16). Mateso hayatainuka tena (Hab. 1:9)

Thamani ya Imani katika Uumbaji Mpya

Imani katika uumbaji mpya huleta faida kwa mkristo: -
  1. Inampa ujasiri wa kuvumilia (Ebr.12:2, 2 Kor. 4:16, 17).
  2. Huleta furaha na uhakika wa ijara (Mt. 5: 12, 1 Kor. 3:14).
  3. Huimarisha kwa kutoa nguvu kuyapinga majaribu (Ebr. 11:26)
  4. Inampa kuonja raha ya mbinguni kabla hajafika huko (2 Kor. 1:22, 2 Kor.5:5, Efe. 1:14, Uf. 3:20).
  5. Huongoza kwenye utendaji wa juhudi
  6. Hudhihirisha tabia ya Mungu.
  7. Hutuvuta kwa Mungu.
  8.  

Daima Mpya

Ufalme utakuwa wa Mungu na Kristo wake. (Uf. 11:15). Hakuna yeyote atakayeruhusiwa kuupindua au kuwa mshirika kwenye utawala huo. (Dan. 2:44, Dan. 7:27). Kila kiumbe kitaungana kuimba na kumtukuza Mungu (Uf. 5:13). “Mapambano makuu yamekoma. Dhambi na wenye dhambi hakuna tena. Ulimwengu mzima sasa umeshafika. Umoja na ushirikiano ulio kamili kabisa umeenea ulimwenguni. Kutoka kwa Muumbaji hufurika uzima, nuru na furaha na kuenea mahali pote. Tangu kwa kitu kidogo mno mpaka kwa kikubwa kilinganacho na ulimwengu mzima, vitu vyote, vilivyo hai na visivyo hai, katika hali yote, hutangaza kuwa Mungu ni pendo.” (Ellen G. White Great Controversy 678).

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
2 Petro 3:13X
13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Isaya 35X
1 Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. 2 Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Bwana, ukuu wa Mungu wetu. 3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea. 4 Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. 5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 6 Ndipo mtu aliye kilema ataruka-ruka kama kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. 7 Na mchanga ung'aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi. 8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo. 9 Hapo hapatakuwa na simba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake; hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo. 10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
Isaya 65:17-25X
17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni. 18 Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha. 19 Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya kuomboleza. 20 Hatakuwapo tena mtoto wa siku chache, wala mzee asiyetimia siku zake; kwa maana mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia; bali mtenda dhambi mwenye umri wa miaka mia atalaaniwa. 21 Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake. 22 Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi. 23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao. 24 Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia. 25 Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema Bwana.
Mathayo 5:5X
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Ufunuo 21:1-7X
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. 6 Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye mwenye kiu, ya chemchemi ya maji ya uzima, bure. 7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
Ufunuo 22:1-5X
1 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, 2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. 3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Ufunuo 11:5X
5 Na mtu akitaka kuwadhuru, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao. Na mtu akitaka kuwadhuru, hivyo ndivyo impasavyo kuuawa.
2 Petro 3: 6, 7, 13X
6 kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia. 7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu. 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
2 Petro 3:10-13X
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 11 Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, 12 mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu, na kuihimiza; ambayo katika hiyo mbingu zitafumuliwa zikiungua, na viumbe vya asili vitateketea na kuyeyuka? 13 Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.
Ufunuo 21:1X
10 Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
Mwanzo 1:20X
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.
Mwanzo 1:14-17X
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; 15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. 16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi
2 Wakorintho 12:2-4X
2 Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. 3 Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua); 4 ya kuwa alinyakuliwa mpaka Peponi, akasikia maneno yasiyotamkika, ambayo haijuzu mwanadamu ayanene.
Ufunuo 21:1, 2X
1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. 2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Ufunuo 21:3X
3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Ufunuo 21:9, 11X
9 Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. 11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri;
Ufunuo 21:23, 24X
23 Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-Kondoo. 24 Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.
Ufunuo 22:5X
5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Ufunuo 21:11, 18X
11 wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; 18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi.
Ufunuo 21:19 -20X
19 Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; 20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
Ufunuo 21:18, 21X
18 Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya yaspi, na mji ule ulikuwa wa dhahabu safi, mfano wa kioo safi. 21 Na ile milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
Ufunuo 21: 15, 16X
15 Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake. 16 Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Ufunuo 22:1X
1 Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo,
Ufunuo 22:2X
2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Mwanzo 3:22X
22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Ufunuo 21:25X
25 Na milango yake haitafungwa kamwe mchana; kwa maana humo hamna usiku.
Mathayo 5:5X
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Zaburi 37:9, 29X
9 Maana watenda mabaya wataharibiwa, Bali wamngojao Bwana ndio watakaoirithi nchi. 29 Wenye haki watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
Zaburi 115:16X
16 Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.
Yohana 14:1–3X
1 Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. 4 Nami niendako mwaijua njia.
Ufunuo 21:2, 3, 5X
2 Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. 3 Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. 5 Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
Waebrania 11:10X
10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.
Isaya 65:21X
21 Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.
Yohana 1:14X
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Ufunuo 21:3X
3 Simoni Petro aliwaambia, Naenda kuvua samaki. Nao wakamwambia, Sisi nasi tutakwenda nawe. Basi wakaondoka, wakapanda chomboni; ila usiku ule hawakupata kitu.
Ufunuo 22:3-5X
3 Wala hapatakuwa na laana yo yote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake watamtumikia; 4 nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. 5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Ufunuo 5:10X
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.
Isaya 65:21X
21 Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.
Mwanzo 2:15X
15 Bwana Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.
Mwanzo 1:31X
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Mathayo 8:11X
11 Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
Mathayo 22:29, 30X
39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Zaburi 84:11X
11 Kwa kuwa Bwana, Mungu, ni jua na ngao, Bwana atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema Hao waendao kwa ukamilifu.
1 Yohana 4:8X
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Zaburi 16:11X
11 Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
Ufunuo 22:2X
2 katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.
Isaya 33:24, 20X
24 Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao. 20 Angalia Sayuni, mji wa sikukuu zetu; macho yako yatauona Yerusalemu umekuwa kao la raha; hema isiyotanga-tanga; vigingi vyake havitang'olewa, wala kamba zake hazitakatika.
Mathayo 20:28X
28 kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Isaya 66:23X
23 Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.
Ufunuo 21:4X
4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:8X
8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo 22:15X
15 Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Isaya 65:17X
17 Maana, tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya, na mambo ya kwanza hayatakumbukwa, wala hayataingia moyoni.
Isaya 65:16X
16 Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.
Habakuki 1:9X
9 Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.
Waebrania 12:2X
2 Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
2 Wakorintho 4:16, 17X
16 Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. 17 Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;
Mathayo 5:12X
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.
1 Wakorintho 3:14X
14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu.
Waebrania 11: 26X
26 akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri; kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo.
2 Wakorinrho 1:22X
22 naye ndiye aliyetutia muhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.
2 Wakorintho 5:5X
5 Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.
Waefeso 1:14X
14 Ndiye aliye arabuni ya urithi wetu, ili kuleta ukombozi wa milki yake, kuwa sifa ya utukufu wake.
Ufunuo 3:20X
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.
Ufunuo 11:15X
15 Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.
Danieli 2:44X
44 Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Danieli 7:27X
27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Ufunuo 5:13X
13 Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.