Utatu Mtakatifu

Utangulizi

Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, umoja wa Nafsi tatu za milele. Mungu asiyeweza kufikwa na mauti, mwenye enzi zote, mwenye uwezo wote, mwenye kujua yote, juu ya yote, na aliyepo daima. Hana kikomo na anapita ufahamu wa kibinadamu, walakini akijulikana kupitia ufunuo wake mwenyewe. Yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa na kutumikiwa na viumbe vyote milele zote.” (Kumb. 6:4; Mt. 28:19; 2Kor.13:14; Efe. 4:4-6; 1Pet. 1:2; 1Tim. 1:17; Uf. 14:7) .
Pale Kalvari, karibu kila mtu alimkataa Yesu. Wachache tu walitambua Yesu alikuwa nani kiuhalisi. Mwizi aliyekuwa anakufa aliyemwita Bwana (Luk. 23:42) na askari wa Kirumi aliyesema hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu (Mk. 15:39) . Yohana alipoandika alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea (Yoh.1:11), hakumaanisha ule umati uliokuwa Kalvari au taifa la Israeli peke yake walioshindwa kumtambua Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao. Hili ni tatizo la wanadamu wote kwa kuwa uelewa wao wa Mungu umepungua sana.


Ufahamu wa Mungu

Nadharia nyingi zajaribu kumwelezea mungu na hoja nyingi zikitetea na kupinga kuwepo kwake huonesha kwamba hekima ya mwanadamu haiwezi kupenya Uungu. Kutegemea hekima ya mwanadamu peke yake kumjifunza Mungu ni kama mtu anayetumia lensi kujifunza anga za juu. Hivyo kwa wengi hekima ya Mungu ni hekima iliyofichwa (1Kor.2:7). Kwao Mungu ni siri. Watawala wa dunia hii hawaijui na kama wangeijua wasingemsulubisha Bwana wa utukufu (1Kor.2:8). Mojawapo ya amri za msingi ni kumpenda Mungu kwa moyo wote, roho yote na akili yote (Mt. 22:37 cf Kumb. 6:5). Hatuwezi kumpenda tusiyejua chochote juu yake wala hatuwezi kutafiti kuujua ukuu wa Mungu (Ay.11:7). Je twawezaje kumjua na kumpenda Mwumbaji?


Mungu Aweza Kujulikana

Kwa kuelewa upungufu wa kibinadamu, Mungu katika upendo na huruma yake, alitufikia kupitia Biblia. Hudhihirisha kuwa ukristo siyo kumbukumbu ya mwanadamu kumtafuta Mungu bal ni kile Mungu alivyojifunua na makusudi yake kwa mwanadamu. Mwana wa Mungu alikuja ili tumjue aliye kweli (1Yoh. 5:20). Na uzima ndio huu, wakujue Mungu wa pekee na kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. (Yoh. 17:3). Hii ni habari njema. Pamoja na kwamba haiwezekani kumjua Mungu kikamilifu, upo uwezekano wa kumjua na kuingia mahusiano naye yanayotuwezesha kuokolewa.


Kupata Ufahamu wa Mungu

Elimu ya Mungu ni tofauti na elimu nyingine. Ni suala la kufungua moyo na utayari wa kufanya mapenzi yake na akili. (Yoh. 7:17 cf. Mt. 11:27). Heri walio na moyo safi kwa kuwa watamwona Mungu (Mt.5:8). Wasioamini hawawezi kumjua Mungu. Yuko wapi mwenye hekima … mleta hoja? Mungu alichagua kuwaokoa wanadamu kwa upuuzi wa neno linalohubiriwa (1Kor.1:20, 21). Waliokataa kujiweka chini ya roho walitafsiri vibaya ujumbe wa Mungu kwa upotevu wao.


Kuwako kwa Mungu

Kuna vyanzo viwili vya ushahidi vya kuwako kwa Mungu. Cha kwanza ni kitabu cha maumbile asili na cha pili Maandiko Matakatifu.

Ushahidi wa Uumbaji

Kila moja aweza kujifunza kupitia maumbile asili na uzoefu wa kibinadamu. “Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu na anga latangaza kazi ya mikono yake (Zab.19:1). Ufunuo wa Mungu kupitia maumbile ya asili hutia nuru kila mtu (Yoh. 1:9). Mambo yasiyoonekana yanaonekana kupitia na kufahamika kwa kazi zake (Rum. 1:20). Tabia ya binadamu pia hutoa ushahidi kuwapo kwa Mungu. Paulo asema alihubiri Wagiriki habari za Mungu ambaye wanamwabudu pasipo kumjua (Mdo. 17:23). Tabia ya mwanadamu pia yaonyesha torati iliyoko ndani ya mioyo yao. (Rum.2:14, 15).


Ushahidi wa Maandiko Matakatifu

Biblia haithibitishi kuwako kwa Mungu. Inachukulia kuwa inajulikana. Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi (Mwa. 1:1). Biblia humweleza Mungu kuwa Muumbaji, Mtunzaji na Mtawala wa uumbaji wote. Ufunuo kutokana na uumbaji ni dhahiri sana kiasi kwamba hakuna sababu yoyote kutetea ukafiri (Zab.14:1, Rum. 1:18-22, 28). Upo ushahidi wa kutosha kumshawishi yeyote kujua ukweli kumhusu Mungu. Hata hivyo, imani ni jambo la msingi katika kumjua Mungu maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza (Ebr. 11:1, 6)

Mungu wa Maandiko Matakatifu

Biblia humfunua sifa muhimu za Mungu kupitia majina yake, matendo yake na tabia zake.

Majina ya Mungu

Wakati Maandiko Matakatifu yanaandikwa, majina yalikuwa muhimu kama yalivyo muhimu hata sasa kwa watu wa Mashariki ya Kati na maeneo yanayozunguka. Huko, jina huhesabika kubeba tabia ya aliyepewa hilo jina na utambulisho wake. Umuhimu wa majina ya Mungu, hufunua asili yake, tabia yake, sifa zake na hudhihirishwa na ile amri isemayo: usilijataje bure jina la Bwana Mungu wako… (Kut. 20:7).

Daudi aliimba: Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu (Zab. 7:17), Jina lake ni takatifu na la kuogopwa (Zab. 119:9); Na walisifu Jina la Bwana, Maana jina lake peke yake limetukuka (Zab. 148:13). Majina ya Kiebrania El na Elohim (Mungu) hufunua uwezo wa kiuungu. Hutoa picha ya Mungu kuwa mwenye nguvu, mwenye uwezo mkuu, Mungu wa uumbaji (Mwa. 1:1;Kut. 20: 2; Dan. 9:4). Elyon (Aliye juu) hulenga sifa ya kuinuliwa (Mwa. 14: 18-20; Isa. 14:14). Adonai (Bwana) hutoa picha ya Mungu kuwa ni mtawala (Isa. 6:1;Zab. 35: 23). Majina haya hukazia tabia ya Mungu ya utukufu usiolinganishwa.

Majina mengine huonesha uhiari wa Mungu kuingia kwenye mahusiano na watu. Shaddai (Mwenye enzi) na El Shaddai (Mungu Mwenye enzi) huonesha Mungu aliye chanzo cha baraka na faraja (Kut. 6:3;Zab. 91:1). Jina Yahweh lililotafsiriwa Yehova au BWANA, hukazia agano la Mungu la uaminifu na rehema (Kut. 15:2, 3;Hos. 12:5, 6). Katika (Kutoka 3:14).


Yahweh anajieleza kuwa Niko ambaye Niko au Nitakuwa jinsi nilivyo akimaanisha uhusiano wake usiobadilika kwa watu wake. Mara nyingine Mungu amejifunua kwa karibu sana kama Baba (Kumb. 32:6; Isa. 63:16; Yer. 31:9;Mal.2:10) akimwita Israeli “Mwanangu” na “Mzaliwa wangu wa Kwanza” (Kut. 4:22 cf. Kumb. 32:19).


Isipokuwa kwa Baba, majina ya Agano Jipya yana maana ile ile ya Agano la Kale. Katika Agano Jipya, Yesu alitumia Baba kutuletea sisi uhusiano wa karibu na Mungu (Mt. 6:9;Mk.6:36; cf. Rum. 8:15; Gal.4:6).

Matendo ya Mungu

Waandishi wa Biblia wanatumia wakati mwingi kuandika matendo ya Mungu kuliko Alivyo. Anatambulishwa kama mwumbaji (Mwa. 1:1;Zab. 24:1, 2), anayeushikilia ulimwengu (Ebr.1:3) na Mkombozi na Mwokozi (Kumb.5:6;2Kor.5:19), akihimili hatma ya mwanadamu. Mungu huweka mipango (Isa.46:11; hutabiri (Isa.46:10), na huahidi (Kumb. 15:6; 2Pet.3:9). Husamehe dhambi (Kut.34:7) and ndiye anayestahili ibada yetu (Uf.14:6, 7). Katika ujumla wake, Maandiko Matakatifu humdhihirisha Mungu kama mtawala (1Tim. 1:17) . Matendo yake yamthibitisha ni Mungu mwenye nafsi.

Tabia ya Mungu

Waandishi wa Biblia hutoa habari za ziada juu ya vile Mungu alivyo kwa kutoa shuhuda za tabia ya kiungu.

Tabia za Mungu ambazo hazihamishiki (zisizowasilishwa)

Hizi ni tabia au sifa za Uungu ambazo haiwezekani viumbe walioumbwa kupewa tabia hizo. Tabia hizo ni kama ifuatavyo:

Mungu yupo pasipo kuumbwa, anao uzima ndani yake (Yoh. 5:26). Yu huru kuradhi chochote kwa mapenzi yake (Efe. 1:5). Katika uwezo (Zab.115:3). Mungu ajua vyote (Ayu.37:16; Zab.139:1-18; 147:5; 1Yoh.3:20) kwa sababu akiwa Alfa na Omega (Uf.1:8) anaujua mwisho tangu mwanzo (Isa.46:9-11). Mungu hupatikana wakati wote na mahali pote (Zab.139:7-12; Ebr.4:13), akipita anga za juu, wakati huo huo akiwa ndani ya kila kitu kwenye anga. Mungu ni wa milele (Zab.90:2; Uf.1:8), akivuka vikomo vya wakati, na wakati huo huo akiwamo katika kila kipengele cha wakati. Mungu anao uwezo wote. Yaani, hakuna kinachoshindikana kwake hututhibitishia kuwa chochote anachokikusudia, hukifanya (Dan. 4:17; 25, 35;Mt. 19:26; Uf.19:6). Mungu habadiliki kwa sababu ni mkamilifu (Mal. 3:6; Angalia Zab. 33:11; Yak. 1:17).


    Kwa kuwa tabia hizi humtambulisha Mungu pekee asiyelinganishwa na yeyote waa chochote, huwa tabia hizi au sifa hizi hazihamishiki.

    Ziko tabia zinazohamishika za Mungu,

    Tabia hizi anaouwezo wa kuzitoa kwa viumbe wake aliowaumba, na wakawanazo. Hujumuisha


    Uenyezi wa Mungu

    Maandiko Matakatifu hufundisha kwa uwazi uenyezi wa Mungu. “…naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?” (Dan. 4:35). “…kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo vikaumbwa.” (Ufu. 4:11). “Bwana amefanya kila lililompendeza, katika mbingu na katika nchi.” (Zab. 135:6). Hivyo Sulemani husema “Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa BWANA; kama mifereji ya maji huugeuza popote apendapo.” (Mith. 21:1). Paulo, akiutambua uenyezi wa Mungu aliandika: “Nitarejea tena kwenu, Mungu akinijalia. (Mdo. 18:21; Angalia Rum. 15:32), wakati Yakobo anaonya: “Badala ya kusema Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi” (Yak. 4:15).

    Uteule wa Asili na Uhuru wa Mwanadamu

    Biblia hufunua utawala thabiti wa Mungu kwa ulimwengu. Aliwateua tangu asili wanadamu wafananishwe na mfano wa Mwana wake (Rum. 8:29, 30), tufanywe wanawe na kupata urithi (Efe. 1:4, 5, 11). Je, uenyezi wake unamaanisha nini kwa uhuru wa mwanadamu?

    Neno kuteuliwa tangu asili maana yake kuamuliwa tangu awali. Wengine wametafsiri kuwa kuna watu ambao Mungu amechagua waokolewe tangu asili, na wengine wameachwa kupotea tangu asili. Paulo, hafundishi mwanadamu yeyote kuachwa na Mungu. Badala yake Mungu hutaka watu wote waokolewe na kujua kweli (1Tim. 2:4). Hapendi yeyote apotee bali walifikie toba (2Pet. 3:9). Hakuna ushahidi wa Mungu kutaka watu wapotee. Hiyo itakuwa kuikataa Kalvari ambako Yesu alikufa kwa ajili ya kila mtu. Ile kila mtu iliyomo katika fungu la “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” (Yoh.3:16) ina maana yeyote anaweza kuokolewa. Ule uhuru wa mwanadamu ndicho kinachofanya mtu aokolewe au apotee na hii inasisitizwa kwa matokeo ya kutii au kutotii na humhimiza mwanadamu achague utii na uzima (Kumb.30:19;Josh.24:15; Isa.1:16, 20;Ufu. 22:17) na kwa ukweli kuwa inawezekana kwa muumini aliyepata kupokea neema kuanguka na kupotea (1Kor.9:27, Gal. 5:4;Ebr.6:4-6;10:29).


    Mungu aweza kuona kabla mtu hajachagua, kile atakachochagua na matokeo yake, lakini kujua kabla, hakufanyi Mungu kuhusika na uchaguzi huo. Uteule wa Mungu ni kule kutimiza makusudi ya Mungu kuwa yeyote atakayechagua kumwamini Kristo ataokolewa (Yoh.1:12;Efe. 1:4-10).


    Sasa Maandiko yanamaanisha nini yanaposema Mungu alimpenda Yakobo akamchukia Esau? (Rum.9:13) na aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu?( fungu la 17, 18, cf. 15, 16;Kut.9:16;4:21). Muktadha wa mafungu hayo huonyesha kuwa anachojadili Paulo ni utume siyo wokovu. Wokovu ulikuwapo kwa Yakobo vile vile kwa Esau, ila Mungu alimchagua Yakobo uwe uzao wa kupeleka habari ya wokovu kwa watu wengine. Mungu hutumia uenyezi katika utume wake. Maandiko yanaposema kuwa aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu inampa Mungu utukufu kwa uhuru alioruhusu wanadamu kuwa nao na siyo kwa sababu aliusimika ugumu katika moyo wa Farao.

    Ufahamu wa kabla na Uhuru wa Mwanadamu

    Ufahamu wa Mungu wa kile mtu anataka kufanya hakuingilii uchaguzi wa wanadamu wa kile wafanyacho, kama vile wanahistoria wanavyojua kilichotokea wakati uliopita hakuingilii kile walichofanya. Kama kamera inavyochukua picha ya tukio pasipo kuingilia kulibadili tukio, ufahamu wa kabla utaliona tukio husika pasipo kulibadili. Ufahamu wa kabla wa Mungu hakuingilii uhuru wa mwanadamu.

    Utendaji katika Utatu Mtakatifu

    Je, kuna Mungu moja? Vipi kuhusu Kristo na Roho Mtakatifu?


    Kuwa Mungu ni moja tu

    Kutofautiana na mataifa na mataifa yaliyowazunguka, Israeli waliamini yuko Mungu moja tu
    (Kumb.4:35;6:4;Isa.45:5;Zek. 14:9). Agano Jipya linakazia kuwa Mungu ni moja tu. (Mk. 12:29-32;Yoh. 17:3;1Kor.8:4-6;Efe. 4:4-6;1Tim. 2:5). Kuwako Mungu moja tu, hakupingi Utatu Mtakatifu wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu badala yake kunaondoa wazo tete la kuwako miungu watatu.

    Wingi katika Utatu Mtakatifu

    Ingawa Agano la Kale halifundishi Utatu Mtakatifu, linaweka uwingi katika Uungu. “Na tufanye mtu kwa mfano wetu” (Mwa.1:26). “ Huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu” (Mwa. 3:22). “Haya na tushuke huko, tukawachafulie usemi” (Mwa.11:7). Wakati mwingine Malaika wa Bwana anajitambulisha kama Mungu. Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo” (Kut. 3:2, 6). Rejea mbalimbali humtofautisha Roho wa Mungu na Mungu. Katika kisa cha uumbaji, Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji (Mwa.1:2). Mafungu mengine hutambulisha nafsi tatu katika kazi ya ukombozi. “Bwana Mungu amenituma na roho yake” (Isa.48:16). “Tazama mtumishi wangu, nimetegemezaye; mteule wangu…nimetia roho yangu juu yake…” (Isa.42:1).


    Mahusiano katika Utatu Mtakatifu

    Kuja kwa Yesu mara ya kwanza inatupatia mwanga kuhusu Utatu Mtakatifu. Injili ya Yohana inatuambia kuwa Utatu Mtakatifu unaye Baba, Mwana na Roho Mtakatifu wenye mahusiano ya kipekee na usiri.

    1. Mahusiano ya Upendano

    Yesu alipolia Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha? (Mk. 15:34), alikuwa akisononekea kutengwa na Baba yake kulikotokana na dhambi. Dhambi ilivunja uhusiano uliokuwapo baina ya Mungu na mwanadamu (Mwa. 3:6-10;Isa.59:2). Katika saa zake za mwisho Yesu asiyejua dhambi alifanyika dhambi kwa ajili yetu, akaonja kutengwa na Baba yake ambalo lilikuwa fungu letu na akafa ikiwa ni matokeo ya kutengwa huko.
    Wenye dhambi hawatakaa watambue kifo cha Yesu kilimaanisha nini katika Utatu Mtakatifu. Tangu milele, Yesu alikuwa pamoja na Baba pamoja na Roho Mtakatifu. Waliishi pamoja katika umilele, wakijitolea. Mungu ni pendo (1Yoh. 4:8), inamaanisha kila moja aliishi kwa ajili ya mwenzake na hilo liliwajaza kuridhika na furaha.


    Upendo umetafsiriwa katika 1Wakorintho 13. Wengine watashangaa kwa nini uvumilivu na subira vitajwe katika Utatu Mtakatifu. Subira ilihitajika wakati wa kushughulika na malaika walioasi na baadaye wanadamu waliotanga mbali. Hakuna umbali kwa washirika wa Utatu Mtakatifu. Wote ni Mungu, na wanashirikiana mamlaka na sifa. Kwa wanadamu, mamlaka kuu hushikwa na Mwenyekiti au Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni (President), lakini katika Utatu, mamlaka ya mwisho iko kwa washirika wote wa Utatu.


    Wakati Mungu siyo nafsi moja, Mungu ni moja katika makusudi, akili na tabia. Umoja hauharibu nafsi nafsi tofauti wala kutofautiana kwa nafsi hakuharibu ukweli kwamba Mungu ni mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.


    2. Mahusiano ya kutenda kazi


    Katika utatu, utaratibu wa kufanya kazi kwa mgawanyo upo. Mungu halazimiki kufanya kazi mara mbilimbili. Utaratibu ni kanuni inayotawala mbinguni na Mungu hutenda kazi kwa utaratibu. Kuwepo utaratibu kunadumisha umoja katika Utatu Mtakatifu. Baba aonekana kama chanzo, Mwana kama mpatanishi, na Roho kama mwezeshaji au mwenye kufanya kitumike. Yesu kufanyika mwili ni kielelezo bora kuelezea utendaji wa Mungu. Baba alimtoa mwanawe, Yesu akajitoa mwenyewe na Roho akafanya Yesu azaliwe (Yoh.3:16;Mt. 1:18, 20). Ushuhuda wa malaika kwa Mariamu huonyesha matendo ya Utatu: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nguvu zake Aliye juu zitakufunika… hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu (Luk. 1:35).

    Kila mshirika kwenye Utatu Mtakatifu alikuwako wakati wa ubatizo wa Kristo. Baba akitia moyo (Mt. 3:17), Yesu akijitoa mwenyewe kubatizwa ili kuwa kielelezo (Mt. 3:13-15) na Roho akijitoa kumwezesha Yesu (Luk. 3:21, 22). Karibu na mwisho wa maisha yake duniani, Yesu aliahidi kumtuma Roho Mtakatifu kuwa msaidizi na mshauri (Yoh. 14:16). Saa chache baadaye alilia Mungu wangu Mungu wangu, mbona umeniacha? (Mt. 27:46). Katika saa hizo za historia ya wokovu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu walihusika.

    Sasa hivi Baba na Mwana wanatufikia kupitia Roho Mtakatifu (Yoh. 15:26). Mzigo mkubwa wa Utatu ni kumtuma Roho amfunue Baba kwa kila mtu (Yoh.17:3), na kumfanya Yesu awepo kwa uhalisi (Mt. 28:20 cf. Ebr.13:5). Waumini wanateuliwa kwa wokovu kwa ufahamu wa asili wa Baba, wanatakaswa na Roho na kunyunyizwa damu ya Yesu (1Pet.1:2).


    Baraka ya Mitume inajumuisha Nafsi zote tatu: “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na Pendo la Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote” (2Kor.13:14). Kristo anaongoza orodha. Mguso wa Mungu kwa mwanadamu umekuwa na utadumu kupitia kwa Yesu Kristo. Ijapokuwa Nafsi zote zatenda kazi kuokoa, ni Yesu pekee aliyekuwa Mwanadamu, akaishi na kufa kama mwanadamu kutuokoa. (Yoh. 6:47;Mt.1:21;Mdo. 4:12). Yesu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake (1Kor.5:19), hivyo naye aweza kuitwa mwokozi cf. (Tit. 3:14), kwa kuwa alituokoa kwa Kristo Mwokozi (Efe.5:23;Filp 3:20 cf. Tit. 3:6).


    Mgawanyo wa kazi hufanya Nafsi tatu kutenda majukumu tofauti katika kumwokoa Mwanadamu. Jukumu la Roho Mtakatifu haliongezi chochote katika kutosha kwa kafara ya Kristo aliyoitoa msalabani. Kupitia Roho Mtakatifu, kafara ya msalabani inatumiwa na Yesu Mpatanishi anapoingia ndani ya muumini. Hivyo Paulo asema Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu (Kol. 1:27)


    Lengo ni Wokovu

    Kanisa la awali lilibatiza kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Kwa kuwa ni kupitia Yesu kwamba upendo wa Mungu na madhumuni yalifunuliwa, Biblia humlenga Yeye. Yesu ndiye kweli na njia na uzima (Yoh.14:6). Msalabani, Yesu alifanyika haki yetu, na utakaso na ukombozi (1Kor.1:30). Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu (Filp.4:7).

    ×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
    Kumbukumbu la Torati 6:4X
    4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
    Mathayo 28:19X
    19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
    2 Wakorintho 13:14X
    14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
    Waefeso 4:4-6X
    4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
    1 Petro 1:2X
    2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
    1 Timotheo 1:17X
    17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
    Ufunuo 14:7X
    7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
    Luka 23:42X
    42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
    Marko 15:39X
    39 Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
    Yohana 1:11X
    11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
    1 Wakorintho 2:7X
    7 bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu;
    1 Wakorintho 2:8X
    8 ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
    Mathayo 22:37X
    37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.
    Kumbukumbu 6:5X
    5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
    Ayubu 11:7X
    7 Je! Wewe waweza kuuvumbua ukuu wa Mungu? Waweza kuufikilia upeo wa huyo Mwenyezi?
    1 Yohana 5:20X
    20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
    Yohana 17:3X
    3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
    Yohana 7:17X
    17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
    Mathayo 11:27X
    27 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
    Mathayo 5:8X
    7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
    1 Wakorintho 1:20, 21X
    20 Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
    Zaburi 19:1X
    1 Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
    Yohana 1:9X
    9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
    Warumi 1:20X
    20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru;
    Matendo 17:23X
    23 Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya ibada yenu, naliona madhabahu iliyoandikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYEJULIKANA. Basi mimi nawahubirini habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua.
    Warumi 2:14, 15X
    14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;
    Mwanzo 1:1X
    1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
    Zaburi 14:1X
    1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
    Warumi 1:18-22, 28X
    18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
    Waebrania 11:1, 6X
    1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 16 Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
    Kutoka 20:7X
    7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
    Zaburi 7:17X
    17 Nitamshukuru Bwana kwa kadiri ya haki yake; Nitaliimbia jina la Bwana aliye juu.
    Zaburi 119:9X
    9 Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.
    Zaburi 148:13X
    13 Na walisifu jina la Bwana, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
    Mwanzo 1:1X
    1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
    Kutoka 20:2X
    2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
    Danieli 9:4X
    4 Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;
    Mwanzo 14:18-20X
    18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
    Isaya 14:14X
    14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
    Isaya 6:1X
    1 Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
    Zaburi 35:23X
    23 Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu.
    Kutoka 6:3X
    3 nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
    Zaburi 91:1X
    1 Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
    Kutoka 15:2, 3X
    2 Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. 3 Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.
    Hosea 12:5, 6X
    5 Naam, Bwana, Mungu wa majeshi; Bwana ndilo kumbukumbu lake. 6 Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.
    Kutoka 3:14X
    14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO;akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu.
    Kumbukumbu 32:6X
    6 Je! Mnamlipa Bwana hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
    Isaya 63:16X
    16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
    Yeremia 31:9X
    9 Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawaendesha penye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.
    Malaki 2:10X
    10 Je! Sisi sote hatuna Baba mmoja? Mungu aliyetuumba siye mmoja tu? Basi, mbona kila mmoja wetu anamtenda ndugu yake mambo ya hiana, tukilinajisi agano la baba zetu?
    Kutoka 4:22X
    22 Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;
    Kumbukumbu la Torati 32:19X
    19 Bwana akaona, akawachukia, Kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake.
    Mathayo 6:9X
    9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
    Marko 6:36X
    36 uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula.
    Warumi 8:15X
    15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
    Wagalatia 4:6X
    6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
    Mwanzo 1:1X
    1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.
    Zaburi 24:1, 2X
    1 Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. 2 Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
    Waebrania 1:3X
    3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
    Kumbukumbu 5:6X
    6 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
    2 Wakorintho 5:19X
    19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
    Isaya 46:11X
    11 Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.
    Isaya 46:10X
    10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
    Kumbukumbu 15:6X
    6 Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
    2 Petro 3:9X
    9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
    Kutoka 34:7X
    7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.
    Ufunuo 14:6, 7X
    6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
    1 Timotho 1:17X
    17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
    Yohana 5:26X
    26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
    Waefeso 1:5X
    5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
    Zaburi 115:3X
    3 Lakini Mungu wetu yuko mbinguni, Alitakalo lote amelitenda.
    Ayubu 37:16X
    16 Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa, Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
    Zaburi 139:1-18X
    1 Ee Bwana, umenichunguza na kunijua. 2 Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; Umelifahamu wazo langu tokea mbali. 3 Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote. 4 Maana hamna neno ulimini mwangu Usilolijua kabisa, Bwana. 5 Umenizingira nyuma na mbele, Ukaniwekea mkono wako. 6 Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, Hayadirikiki, siwezi kuyafikia. 7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; 10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. 11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa. 13 Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu, Uliniunga tumboni mwa mama yangu. 14 Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, 15 Mifupa yangu haikusitirika kwako, Nilipoumbwa kwa siri, Nilipoungwa kwa ustadi pande za chini za nchi; 16 Macho yako yaliniona kabla sijakamilika; Chuoni mwako ziliandikwa zote pia, Siku zilizoamriwa kabla hazijawa bado. 17 Mungu, fikira zako zina thamani nyingi kwangu; Jinsi ilivyo kubwa jumla yake! 18 Kama ningezihesabu ni nyingi kuliko mchanga; Niamkapo nikali pamoja nawe.
    Zaburi 147:5X
    5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
    1 Yohana 3:20X
    20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.
    Ufunuo 1:8X
    8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
    Isaya 46:9-11X
    9 kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi; 10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote. 11 Nikiita ndege mkali kutoka mashariki, mtu wa shauri langu toka nchi iliyo mbali; naam, nimenena, nami nitatekeleza; nimekusudia, nami nitafanya.
    Zaburi 139:7-12X
    7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; 10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika. 11 Kama nikisema, Hakika giza litanifunika, Na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; 12 Giza nalo halikufichi kitu, Bali usiku huangaza kama mchana; Giza na mwanga kwako ni sawasawa.
    Waebrania 4:13X
    13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.
    Zaburi 90:2X
    2 Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
    Ufunuo 1:8X
    8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.
    Danieli 4:17; 25, 35X
    17 Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge. 25 ya kuwa utafukuzwa mbali na wanadamu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa kondeni, nawe utalazimishwa kula majani kama ng'ombe, nawe utatiwa maji kwa umande wa mbinguni, na nyakati saba zitapita juu yako; hata utakapojua ya kuwa Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote. 35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?
    Mathayo 19:26X
    26 Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
    Ufunuo 19:6X
    6 Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki.
    Malaki 3:6X
    6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
    Zaburi 33:11X
    11 Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
    Yakobo 1:17X
    17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.
    Warumi 5:8X
    8 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.
    Warumi 3:24X
    24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
    Zaburi 145:9X
    9 Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
    2 Petro 3:15X
    15 Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;
    Zaburi 99:9X
    9 Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
    Ezra 9:15X
    15 Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ndiwe mwenye haki, maana sisi tumesalia, mabaki yaliyookoka, kama hivi leo; tazama, sisi tupo hapa wenye hatia mbele zako; maana hapana mtu awezaye kusimama mbele zako kwa sababu ya jambo hili.
    Yohana 17:25X
    25 Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma.
    Ufunuo 22:12X
    12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
    1 Yohana 5:20X
    20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
    Danieli 4:35X
    35 na watu wote wanaokaa duniani wamehesabiwa kuwa si kitu, naye hufanya kama atakavyo, katika jeshi la mbinguni, na katika hao wanaokaa duniani; wala hapana awezaye kuuzuia mkono wake, wala kumwuliza, Unafanya nini wewe?
    Zaburi 135:6X
    6 Bwana amefanya kila lililompendeza, Katika mbingu na katika nchi, Katika bahari na katika vilindi vyote.
    Mithali 21:1X
    1 Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo.
    Matendo 18:21X
    21 bali aliagana nao, akisema, Nitarejea kwenu tena, Mungu akinijalia. Akatweka, akatoka Efeso,
    Warumi 15:32X
    32 nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi.
    Yakobo 4:15X
    15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
    Warumi 8:29, 30X
    29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. 30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.
    Waefeso 1:4, 5, 11X
    4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 11 na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.
    1 Timotheo 2:4X
    4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
    2 Petro 3:9X
    9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.
    Yohana 3:16X
    16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
    Kumbukumbu la torati 30:19X
    19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako;
    Luka 10:7X
    7 Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
    Yoshua 24:15X
    15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
    Isaya 1:16, 20X
    16 Jiosheni, jitakaseni; ondoeni uovu wa matendo yenu usiwe mbele za macho yangu; acheni kutenda mabaya;
    Ufunuo 22:17X
    17 Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.
    1 Wakorintho 9:27X
    27 bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.
    Wagalatia 5:4X
    4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu;
    Waebrania 6:4-6X
    4 Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, 6 wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
    Waebrania 10:29X
    29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
    Yohana 1:12X
    12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
    Waefeso 1:4-10X
    4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. 7 Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. 8 Naye alituzidishia hiyo katika hekima yote na ujuzi; 9 akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake, sawasawa na uradhi wake, alioukusudia katika yeye huyo. 10 Yaani, kuleta madaraka ya wakati mkamilifu atavijumlisha vitu vyote katika Kristo, vitu vya mbinguni na vitu vya duniani pia. Naam, katika yeye huyo;
    Warumi 9:13X
    13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
    Warumi 9:17, 18X
    17 Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
    Warumi 9:15, 16X
    15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
    Kutoka 9:16X
    16 lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu hii hii, ili nikuonyeshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.
    Kutoka 4:21X
    21 Bwana akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.
    Kumbukumbu la Torati 4:35X
    35 Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye.
    Kumbukumbu la Torati 6:4X
    4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.
    Isaya 45:5X
    5 Mimi ni Bwana, wala hapana mwingine; zaidi yangu mimi hapana Mungu; nitakufunga mshipi ijapokuwa hukunijua;
    Zakaria 14:9X
    9 Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.
    Marko 12:29-32X
    29 Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; 30 nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote. 31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi. 32 Yule mwandishi akamwambia, Hakika, Mwalimu, umesema vema ya kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye;
    Yohana 17:3X
    3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
    1 Wakorintho 8:4-6X
    4 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu. 5 Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; 6 lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.
    Waefeso 4:4-6X
    4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
    1 Timotheo 2:5X
    5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
    Mwanzo 1:26X
    26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
    Mwanzo 3:22X
    22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
    Mwanzo 11:7X
    7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.
    Kutoka 3:2, 6X
    2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
    Mwanzo 1:2X
    2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
    Isaya 48:16X
    16 Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.
    Isaya 42:1X
    1 Tazama mtumishi wangu nimtegemezaye; mteule wangu, ambaye nafsi yangu imependezwa naye; nimetia roho yangu juu yake; naye atawatolea mataifa hukumu.
    Marko 15:34X
    34 Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
    Mwanzo 3:6-10X
    6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. 9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
    Isaya 59:2X
    2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.
    1 Yohana 4:8X
    8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
    1 Wakorintho 13X
    1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. 2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu. 4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; 5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; 6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; 7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. 8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika. 9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu; 10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika. 11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto. 12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana. 13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
    Yohana 3:16X
    16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
    Mathayo 1:18, 20X
    18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
    Luka 1:35X
    35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
    Mathayo 3:17X
    17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
    Mathayo 3:13-15X
    13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa. 14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema, Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa; Kutazama mtatazama, wala hamtaona. 15 Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.
    Luka 3:21, 22X
    21 Ikawa, watu wote walipokwisha kubatizwa, na Yesu naye amebatizwa, naye anaomba, mbingu zilifunuka; 22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili, kama hua; sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
    Yohana 14:16X
    16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
    Mathayo 27:46X
    46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
    Yohana 15:26X
    26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
    Yohana 17:3X
    3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
    Mathayo 28:20X
    20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
    Waebrania 13:5X
    5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
    1 Petro 1:2X
    2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
    2 Wakorintho 2:13, 14X
    13 sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia. 14 Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
    Yohana 6:47X
    47 Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
    Mathayo 1:21X
    21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
    Matendo 4:12X
    12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
    2 Wakorintho 5:19X
    19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
    Tito 3:4X
    4 Lakini wema wake Mwokozi wetu Mungu, na upendo wake kwa wanadamu, ulipofunuliwa, alituokoa;
    Waefeso 5:23X
    23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
    Wafilipi 3:20X
    20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
    Tito 3:6X
    6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
    Wakolosai 1:27X
    27 ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu
    Yohana 14:6X
    6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
    1 Wakorintho 1:30X
    30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
    Wafilipi 4:7X
    7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
    1 Wakorintho 8:4-6X
    4 Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu. 5 Kwa maana ijapokuwa wako waitwao miungu, ama mbinguni ama duniani, kama vile walivyoko miungu mingi na mabwana wengi; 6 lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo.