Mwanadamu na Asili yake

Utangulizi


Mwanamume na mwanamke waliumbwa wakiwa na sura ya Mungu binafsi wakiwa na uwezo na uhuru wa kufikiri na kutenda. Japo waliumbwa huru, kila mtu katika umoja wote wa mwili, akili na roho, walimtegemea Mungu kwa uhai, kuvuta pumzi na mengineyo yote. Wakati wazazi wetu walipomkaidi Mungu, sura ya mwumbaji iliharibiwa na wakawa watu wa kufa. Uzao wao hushiriki hali hii ya mwanadamu aliyeanguka na matokeo yake yote. Huzaliwa wakiwa na unyonge na kuelekea kutenda dhambi. Lakini Mungu katika Kristo, aliupatanisha ulimwengu kwa nafsi yake na kwa roho yake akarejeza kwa watu wenye hali ya kufa taswira ya Mwumbaji. Walioumbwa kwa utukufu wa Mungu, wameitwa kumpenda Yeye, kupendana wao kwa wao na kutunza mazingira.” (Mw. 1:26,27, 2:7, Zab.8: 4- 8, Mdo. 17:24-28, Mw. 3:4, 6-9, 15 -19, 24 Zab. 51:5, Rum 5:12-17, 2 Cor. 5:19, 20, Zab. 50:10, 1 Yoh. 4:7, 8)

Asili ya Mwanadamu

Wazo la kumuumba mwanadamu lilitoka kwa Mungu (Mwa. 1:26)

Na wakati anamuumba, alitekeleza wazo lake kwa kuumba watu wawili, mtu mume na mtu mke, akawaita jina lao Adamu. (Mw. 1:27; 5:1, 2)

Mwanadamu aliumbwa kwa udongo na pumzi (Mw. 2:7)

Vitu viwili vilitengeneza mtu, udongo na pumzi ya uhai. Kilichopatikana kutokana na mwunganiko wa udongo na pumzi kimeitwa nafsi hai, yaani kama tungekuwa tunafanya hesabu, udongo + pumzi ya uhai = nafsi hai. Nafsi hai haiwezi kuwa nafsi hai ikiwa kimojawapo kati ya udongo au pumzi ya uhai kitaondolewa. Kwa hiyo, nafsi hai ni kitu kisichoweza kugawanyika ili kila kipande kibaki na maisha yake )yanayojitegemea peke yake. (cf. Mhu. 12:7)

Aliumbwa kwa sura ya Mungu (Mwa.1:26)

Viumbe vingine vilikuwa kwa jinsi zake (Mwa.1:2, 24, 25). Lakini mwanadamu alikuwa kwa mfano wa Mungu. Na Luka anasema, Adamu ni mwana wa Mungu (Luk.3:38)

Mwanadamu ana hadhi ya juu.

Aliumbwa akiwa na hadhi ndogo kuliko malaika lakini alipewa kusimamia uumbaji wa Mungu. (Mwa. 1:28; Zab. 8:4-9)

Umoja wa wanadamu.

Wote tulianzia kwa Adamu. Mungu alifanya kila taifa la wanadamu kutoka mmoja (Mdo.17:26). Kwa kosa la Adamu wote tumeanguka dhambini na kwa tendo la Yesu, wote twaweza kuokolewa (Rum.5:12, 19; 1Kor.15:21, 22)

Umoja wa Asili ya Mwanadamu (Mwa.2:7)

Udongo:

Tafsiri ya udongo haina shida. Ni sehemu ya ardhi.

Pumzi ya Uhai. (Mwa.2:7).

Wakati Mungu alipobadili maada ya dunia kuwa kiumbe hai, alipulizia pumzi ya uhai. Alipulizia pumzi ya uhai, pumzi za Mwenyezi (Ayu.33:4), cheche ya uhai.

Mwanadamu - Nafsi Hai

Hesabu ya Maandiko iko wazi. Udongo jumlisha pumzi ya Mungu ni sawa na nafsi hai. Siyo wanadamu pekee waliopewa pumzi ya uhai. Nafsi hai hujumuisha pia wanyama wa baharini, vitambaavyo, na wanyama (Mwa.1:20, 24; 2:19). Siyo kwamba mwanadamu akapokea roho, bali akawa nafsi (roho) hai.

Umoja usiogawanyika

Mwanadamu ni kiumbe kimoja kisichogawanyika. Je, kuna uhusiano gani baina ya nafsi na roho?

1. Maana ya Biblia ya Nafsi.

Katika Agano la Kale, neno la kiebrania lililotafsiriwa nafsi ni nephesh. Ndivyo Mw. 2:7 inavyosema mtu akawa nafsi hai. Kwa jinsi hiyo hiyo kila mtoto mchanga anapozaliwa, nafsi hai huongezeka. Kwa hiyo, nephesh siyo sehemu ya mwanadamu hai bali ni mwanadamu mzima. Anavyokufa binadamu vivyo hivyo na mnyama (Mwa.7:20–23) Wakati wa Nuhu vilikufa viumbe vyote isipokuwa Nuhu na waliobaki ndani ya safina. Kwa kuwa roho (nephesh) ndiyo nafsi hai, roho nayo inakufa (Ez.18: 4).

Katika Agano Jipya lililoandikwa Kigiriki, neno litumikalo kwa nafsi ni psuche. Hutumika kwa wanadamu na wanyama (Uf. 16:3) “Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu, kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.” Kwingine roho ina maana ya uhai (Mat. 2:20, 6:25, 16:25). Kwingine roho inamaanisha watu (Mdo. 7:14, 27:37, Rum. 13:11Pet.3:20) Hutumika kwa nafsi (Mt. 12:17. 2Kor.12:15) Na kwingine humaanisha hisia (Mk.14:34Luk. 2:35) au akili (nia) (Mdo 14:2, Filipi 1:27) au moyo (Ef. 6:6) Katika yote haya, lengo ni kuhitimisha kwamba psuche (roho) haina hali ya kutokufa bali ina hali ya kufa(Uf. 16:3)

2. Maana ya Pumzi ya Uhai

Neno ruach lililotafsiriwa pumzi, hupatikana kwenye Agano la Kale mara 377. Kufuatana na Ayubu 33:4, ni pumzi ya Mungu inayotia uhai, Inaitwa upepo, roho au pumzi (Mw. 8:1) Na kila chenye uhai, Hutumika kuonyesha hali ya kuwa mzima wenye nguvu (Amu. 15:19). Hutumika wakati mwingine kuonyesha ujasiri (Yosh. 2:11) hasira au kukosa uvumilivu (Amuz. 8:3). Pia huonyesha hadhi (Isa. 54:6), tabia adilifu (Ez. 11:19) “Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, name nitawapa moyo wa nyama.”

Kwa maana ya upepo au pumzi, hakuna tofauti kati ya binadamu na mnyama kwenye kifo (Mh. 3:19 -21). Roho humtoka mwanadamu akifa Zab. 146:4 na humrudia Mungu Mh. 12:7 (Angalia pia Ay. 34:14). Ruach hutumika mara nyingi kumaanisha Roho ya Mungu (Isa. 63:10). Hakuna kwenye Agano la Kale ambako roho (ruach) imepata kuishi kwa kujitegemeaNje ya mwili.

Katika Agano jipya, neno lililo na maana ya ruach (Kiebrania) ya agano la kale ni pneuma (Kigiriki) – kupuliza, kupumua. Kama ilivyo kwa ruach, hakuna chochote ndani ya mwanadamu chenye kuweza kuishi nje ya mwili.

Roho/Moyo (pneuma) imetumika pia kuonyesha mtizamo – (Rum. 8:15, 1 Kor 4:21, 22; Rum. 1:7, 1Yoh.4:6) na hali mbali mbali za kibinadamu kama katika (Gal. 6:1, na Rum. 12:11). Pneuma hutoka mtu anapokufa (Luk. 23:46, Mdo. 7:59). Kama ruach, pneuma pia inatumika tunaposema Roho ya Mungu (1Kor.2:11, 14, Ef.4:30, Ebr.2:41Pet.1:12, 2Pet. 1:21).

3. Muungano wa mwili, moyo na roho

a) Muungano wa viwili

Biblia haisemi uhusiano uliopo baina ya mwili, moyo na roho. Wakati mwingine nafsi na roho hutumika kwa kubadilishana “moyo wangu wamwadhimisha Bwana, roho yangu imemfurahia” (Luk. 1: 46, 47). Mara moja, Yesu amemsema mwanadamu kuwa ni mwili na roho (Mt.10:28). Mahali pengine, Paulo anamwona binadamu kuwa ni mwili na roho (1Kor.7:34)

b) Muungano wa vitatu.

Paulo ambaye alipata kumzungumza mwanadamu kuwa wa muungano wa viwili, amesema kwenye 1Thes.5:23 kuwa mwanadamu ana nafsi, roho na mwili. Hapa, roho yaweza kuwa kanuni ya juu ya akili inayowasiliana na Mungu (Rum. 8:16). Kufanywa upya nia, hutubadilisha (Rum.12:1, 2)

c) Muungano usiogawanyika.

Mwili, moyo na roho hutenda kazi kwa kushirikiana ikionesha hali ya mtu kiroho, kiakili na kimwili.

Mwanadamu katika Sura ya Mungu (Mwa.1:27 Ina maana gani?)

Aliumbwa kwa mfano wa Mungu.

Malaika ambao kama Mungu ni Roho (Yoh.4:24; Ebr.1:7, 14). Lakini huonekana katika umbo la kibinadamu (Mwa.18:1-19:22; Dan. 9:21; Luk.1:11-38; Mdo.12:5-10). Je, roho yaweza kuwa na mwili wa kiroho? (cf. 1Kor.15:44). Biblia inasema Musa, Haruni, Nadabu, Abihu na wazee sabini waliona sehemu ya mwili wa Mungu (Kut.24:9-11; Kut.33:20-23). Danieli alimwona Mzee wa Siku akihukumu (Dan.7:9, 10). Kristo anaelezewa kuwa ni mfano wa (taswira ya) Mungu asiyeonekana (Kol.1:15) na chapa ya nafsi ya Mungu (Ebr.1:3). Maelezo yanaelekea kupendekeza kuwa Mungu ni nafsi yenye umbo. Mwanadamu aliumbwa kwa hadhi ndogo kuliko malaika (Ebr.2:7) yamaanisha alikuwa na hali ya kiroho na kiakili. Alikuwa mkamilifu (Mh.7:29) akiwa mwenye haki na mtakatifu (cf. Efe.4:24) na alikuwa sehemu ya uumbaji ambayo Mungu aliitamka ni njema sana (Mwa.1:31). Alikuwa na uhuru wa kuonyesha upendo ulio tabia ya Mungu (1Yoh.4:8) akilenga kufikia upendo kwa Mungu kwa moyo wote, roho yote na nguvu zote na upendo kwa wengine kama nafsi yake (Mt.22:36-40).

Aliumbwa ahusiane na watu wengine.

Siyo vema mtu huyu awe peke yake (Mwa.2:18) na hivyo kuna mahusiano yanaoingia kutokana na familia, jamii na hata taifa. (Mdo.17:26)

Aliumbwa Kuwa Wakili wa Mazingira

Akiwa mtawala wa ndege wa angani, wanyama na nchi (Mwa.1:26) ni wakili kwa niaba ya Mungu. Daudi alisema, Mungu alimtawaza juu ya kazi zake (Zab.8:4-9).

Aliumbwa kumfuata Mungu

Japokuwa ni wanadamu, tumeitwa kumwiga Mungu. Amri ya nne, inasema tumwige Mungu kufanya kazi sita, na sabato tupumzike (Kut.20:8-11).

Aliumbwa akiwa na hali ya kutokufa yenye sharti

Hali ya mwanadamu ya kutokufa ilitegemea utii wake kwa amri ya Mungu (Mwa.2:16, 17) na alipokosea, hakuweza kuwa na hali hiyo tena (Mwa.3:19, 22, 24).

Kuanguka dhambini

Asili ya Dhambi:

Ikiwa Mungu aliumba kitu chema (Mwa.1:31), dhambi ingeweza kuanzia wapi?

1. Mungu na Asili ya Dhambi

Biblia husonda kwamba Mungu ni Mtakatifu (Isa.6:3). Hakuna ukengeufu ndani yake kwani “kazi yake ni kamilifu, njia zake zote ni haki, ni wa uaminifu asiye na uovu” (Kumb.32:4). Mungu asidhaniwe kutenda udhalimu wala uovu (Ayu.34:10). Haiwezekani kumjaribu Mungu kwa maovu, wala yeye hamjaribu mtu (Yak.1:13). Mungu huchukia dhambi (Zab.5:4; 11:5). Uumbaji wa Mungu kwa asili ulikuwa mwema (Mwa.1:31). Badala ya kuwa chanzo cha dhambi, yeye ni chanzo cha wokovu kwa hao wanaomtii (Ebr.5:9).

2. Mwanzilishi wa Dhambi

Mungu angeliweza kuzuia dhambi kama angeumba roboti, yaani viumbe visivyo na uhuru wa kuamua. Kwa kuumba viumbe huru ina maana alikabiliwa na hatari ya maamuzi yaliyo kinyume na mapenzi yake. Bahati mbaya Lusifa, malaika wa ngazi ya juu aliingiwa kiburi (Eze.28:17; cf 1Tim.3:6). Kwa kutokuridhika na nafasi yake (Yud. 6) , alianza kutamani nafasi ya Mungu (Isa.14:12-14). Kwa kutamani kushika nafasi ya Mungu, malaika huyu alianza kupanda mbegu za kutokuridhika na akapata wafuasi. Vita ikatokea, (sasa malaika huyu anaitwa) Shetani akafukuzwa mbinguni yeye pamoja na malaika wenzake. (Ufu.12:4, 9-12).

3. Asili ya dhambi kwa Mwanadamu

Pasipo kuzuiwa na kufukuzwa kwake mbinguni, Shetani alitaka wengine pia wamwasi Mungu. Aliingia katika bustani ya Edeni akiwa na umbo la nyoka na akamshawishi Hawa kula matunda ya mti uliokatazwa. (Mwa.3:4, 5) Hawa alishawishika akala, akampelekea na mumewe naye akala. (Mwa.3:6). Hivyo dhambi ikaangia duniani (Rum.5:12).

Athari za Dhambi

Athari za haraka

Kufumbuliwa macho kuliwafanya Adamu na Hawa waone aibu (Mwa.3:7). Badala ya kufanana na Mungu kama walivyoahidiwa na Shetani, waliogopa wakajaribu kujificha (Mwa.3:7-8). Mahusiano ya ndoa yaliharibika kwa Adamu kulaumu uwepo wa Hawa (Mwa.3:12) na Hawa kulaumu uwepo wa nyoka (Mwa.3:13). Matamshi ya laana, yalifanya nyoka atembee kwa tumbo (Mwa.3:14), mwanamke kuzaa kwa uchungu na kutawaliwa na mwanaume (Mwa.3:16), kulaaniwa ardhi, kuwepo miimba na michongoma na kazi za jasho (Mwa.3:17-19). Kusisitiza kuwa sheria yake haibadiliki, Mungu alisema “kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi”. (Mwa.3:19). Alitekeleza hukumu yake kwa kukata mawasiliano ya moja kwa moja (Mwa.3:8), kuwafukuza watoke Edeni na kuwazuilia wasile matunda ya mti wa uzima (Mwa.3:23, 24). Hivyo, Adamu na Hawa na uzao wao wakawa watu wa kufa. (Mwa.3:22).

Tabia ya dhambi

Maelezo mengi ya Maandiko Matakatifu, hueleza kuwa dhambi ni uovu, pale viumbe huru wanapochagua kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu (Mwa.3:1- 6; Rum.1:18-22).

Maana ya dhambi

a) Maana ya dhambi

Maana ya kibiblia ya dhambi inajumuisha uasi (1Yoh.3:4), mtu kushindwa kutenda vema wakati anajua (Yak.4:17) na kutokufanya matendo kwa imani (Rum.14:23). Dhambi haina kutokuhusika na upande wowote “asiye nami yu kinyume changu” (Mt. 12:30). Kutokumwamini ni dhambi (Yoh.16:9). Dhambi ni dhambi, kwamba ni amri moja imevunjwa au nyingi (Yak.2:10).

b) Dhambi huhusisha mawazo na matendo

Mara nyingi dhambi husemwa kuhusu matendo. Lakini Kristo alisema dhambi huhusisha mawazo pia. (Kut.20:13 cf. Mt.5:21, 22; Kut.20:14 cf Mt. 5:27, 28)

c) Dhambi na hatia

Dhambi huleta hatia na hatia huleta hukumu (Rum.3:19). Isipothibitiwa, itaharibu, mwili, akili, moyo na roho. Hatimaye italeta mauti. (Rum.6:23). Kinachoharibu dhambi ni msamaha (Mt.6:12). Kwa waliolemewa na mzigo wa dhambi Yesu amealika wakapumzike kwake. (Mt. 11:28).

d) Kinachothibiti dhambi

Dhambi huwa ndani ya kinachoitwa na Biblia moyo, au kama tujuavyo, ni nia. Kutoka moyoni, huchipua mambo ya uzima (Mith.4:23). Ni mawazo ya mtu ndiyo hutia unajisi (Mt.15:19). Ni kwa moyo, mtu mzima huvutiwa kutenda maovu (Yer.17:9).

1. Athari za dhambi kwa Mwanadamu

Athari za dhambi ya Adamu na Hawa kwa mwanadamu zilikuwa kubwa. Mwana wao wa kwanza aliua. Uzao wao mara moja ulidharau ndoa na kuanza mitala, na haikuchukua muda mrefu dunia ikajaa dhuluma (Mwa.4:8, 23; 6:1-5, 11-13).

  1. Hali ya dhambi kwa wanadamu wote Uzao wa Adamu huchangia asili ya dhambi ya Adamu (Mwa.5:1, 2). Daudi anasema hakuna aliye hai mwenye haki (Zab.143:2; cf 14:3). Hakuna asiyetenda dhambi (1Fal.8:46). Nani awezaye kusema mie ni msafi (Mith.20:9; Mh. 7:20). Agano jipya nalo lasema: wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum.3:23). Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya (1Yoh.1:8).
  2. Hali ya dhambi hurithiwa au humkuta mtu baadaye? Katika Adamu wote wanakufa (1Kor.15:22). Kwa dhambi ya mtu moja, wote dhambi iliingia duniani, ikaleta mauti kwa kuwa wote wametenda dhambi (Rum.5:12). Hakuna awezaye kutoa kitu safi kutoka katika uchafu (Ayu.14:4). Daudi asema alizaliwa kwenye dhambi…(Zab.51:5). Nia ya mwili ni uadui dhidi ya Mungu… wasio wa Mungu hawawezi kumpendeza (Rum.8:7, 8). Kabla ya kuongoka, ni wana wa ghadhabu (Efe.2:3).
  3. Kuondosha tabia ya dhambi. Hakuna juhudi binafsi itakayoondoa dhambi (Yer.13:23; Yoh.15:5). Atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Yesu ametuhakikishia akituweka huru, tutakuwa huru kweli kweli. (Yoh.8:36). Twaweza kutenda mema tukikaa ndani yake (Yoh.15:4, 5). Hata mtume Paulo alisema hawezi kutenda jema, akajililia nani atamwokoa na mwili wa mauti? (Rum.7:15, 19, 20, 22-24). Paulo hatimaye anakiri nguvu ya kimbingu inahitajika kukomesha dhambi (Rum.7:25; 8:1). Nguvu ya kushinda dhambi ni karama ya Mungu inayobadilisha. (Efe.2:1, 3, 8-10). Kuzaliwa kiroho hubadili maisha (Yoh.1:13; Yoh.3:5) kiasi kwamba twaweza kusema juu ha kuzaliwa upya (2Kor.5:17). Kuwa kiumbe kipya hata hivyo hakuondoi uwezekano wa kufanya dhambi (1Yoh.2:1).

4. Uibukaji na anguko la Mwanadamu.

Tangu uumbaji Shetaji amejitahidi kuhafifisha imani ya wanadamu kwenye Maandiko Matakatifu. Wakristo wengi waliipokea nadharia ya uibukaji na kuiingiza kwenye mafundisho.
  1. Mtazamo wa Biblia wa mwanadamu na uibukaji. Biblia inakataa tafsiri inayofanya kitabu cha Mwanzo kuwa mifano au vielelezo wa hali nyingine. Waandishi wa Biblia wenyewe hutafsiri Mwanzo 1 – 11 kuwa historia ya kawaida. Adamu, Hawa, Nyoka na Shetani wanaonekana kuwa wahusika katika pambano kuu. (Ayu.31:33; Mh.7:29; Mt.19:4, 5; Yoh.8:44; Rum.5:12, 18, 19; 2Kor.11:3; 1Tim.2:14; Ufu.12:9).
  2. Kalvari na Uibukaji. Kalvari hupinga uibukaji. Ikiwa hapakuwa na anguko, kwa nini Yesu ahitajike kufa kwa ajili ya mwanadamu?
  3. Kufanyika Mwili na Uibukaji. Ikiwa Mungu aliweza kufanya muujiza wa kumfanya Yesu afanyike mwili, angeshindwaje kumfanya Adam katika ile nafasi ya kwanza?
  4. Je, Mwanadamu amekuwa wa miaka mingi? Iko imani kwamba mwanadamu akipewa wakati wa kutosha, ataondokana na matatizo yake. Hata hivyo, kwa kile kinachoitwa maendeleo ya kisayansi, dunia imekuwa eneo hatari kuliko wakati uliopita. Hivyo mwanadamu anahitaji mwokozi nje ya uanadamu ili aokolewe.

Miali ya Matumaini

Kupungukiwa mwanadamu ni kukubwa hata walimsulubisha mwumbaji wao. Maneno ya mwanadamu kuwa chini ya malaika bali ametawazwa juu ya kazi za mikono ya Mungu ni ya kweli kabisa. (Zab.8;5, 6 cf. Ebr.2:7). Pamoja na anguko bado hadhi ya uanadamu iko juu. Daudi alishangalia, Ee Mungu, jinsi lilivyo tukufu jina lako. (Zab.8:9)

Agano la Neema

Baada ya kutenda dhambi, Adamu na Hawa walikuwa wadhambi, wasioweza kumpinga Shetani. Je, wangeweza kuwa huru au waliachwa wapotee?

Agano lilitolewa wakati wa Anguko.

Kabla Mungu hajatamka adhabu kwa Adamu na Hawa, aliwapa matumaini kwa kutangaza agano la neema. “nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wake na uzao wako; huo utakuponda kinywa, na wewe utamponda kisigino”. (Mwa.3:15). Wanaokubali neema ya Mungu wataujua uadui na kwa imani watashiriki ushindi wa Kristo Kalvari.

Agano Lilianzishwa Kabla ya Uumbaji

Agano la neema halikuanzishwa baada ya mwanadamu kuanguka. Alituchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tuwe watakatifu…wanawe kwa njia ya Yesu Kristo. (Efe.1:4-6; 2Tim.9). Kujitoa Yesu kulijulikana kabla ya misingi ya ulimwengu. (1Pet.1:20). Agano lilijengwa kwenye ahadi na kiapo cha Mungu mwenyewe (Ebr.6:18). Yesu alikuwa amana ya agano (Ebr.7:22). Si malaika au mwanadamu, angeweza kutimiza madai ya sheria ya Mungu iliyovunjwa, isipokuwa Yesu (Rum.5:12-21; 1Kor.15:22).

Yesu siyo tu amana, bali pia mtendaji wa agano. Alikuja kutenda mapenzi ya Baba yake (Yoh.6:38 cf. 5:30, 36). Mapenzi ya Baba ni amwaminiye Mwana apate uzima wa milele (Yoh.6:40). Uzima wa milele ni kumjua Baba na Yesu (Yoh.17:3).

Mwisho wa huduma ya Yesu duniani alisema, nimeimaliza kazi (Yoh.17:4). Msalabani Yesu alipaza sauti akisema, “Imekwisha”. (Yoh.19:30).

Agano Kufanywa Upya

Wanadamu walikataa agano kabla na baada ya gharika (Mwa.6:1-8; 11:1-9). Mungu alipotoa agano tena, alilifanya na Ibrahimu (Mwa.22:18 cf. 12:3; 18:18). Ibrahimu alikuwa mwaminifu kwa masharti ya agano (Mwa.15:6). Pamoja na kujengwa kwenye neema, agano pia liliegemea kuitambua sheria ya Mungu (Mwa.17:1; 26:5). Imani ya Ibrahimu ilikuwa makini hadi akaitwa baba wa imani (Rum.4:11). Ni kielelezo cha haki kwa imani (Rum.4:2, 3; Yak.2:23, 24). Baraka inaenda kwa uzao wa Ibrahimu wenye imani sawa naye (Gal.3:7). Kila mtu duniani aweza kuokolewa kwa sharti la kuwa ndani ya Kristo, na kuwa uzao wa Ibrahimu (Gal.3:29). Kwa mtazamo wa Mungu, agano la Sinai vilevile lilikuwa agano la neema kwa Ibrahimu lililofanywa upya (Ebr.9:1). Lakini Waisraeli walipotosha kuwa agano la matendo (Gal.4:22-31).

Agano Jipya

Baadaye sehemu ya Maandiko huzungumzia agano jipya lililo bora zaidi. Halifanyi hivyo kwa sababu agano la milele lilibadilishwa, ila (1) kutokana na Waisraeli kutokuwa waaminifu, agano la milele limepotoshwa na kuwa mfumo wa matendo. (2) liliambatana na ufunuo mpya wa upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo na (3) halikutimia hadi lilipokamilishwa msalabani kwa damu ya Kristo. (Dan.9:27; Luk.22:20; Rum.15:8; Ebr.9:11-12). Agano hili lafanya mtu kuzaliwa upya, na kuwezesha utii wa amri za Mungu kutoka moyoni (Yer.31:33). Hiyo ndiyo haki ya Kristo inayofanya mtu kuzaa matunda ya roho, upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili uaminifu, upole, kiasi (Gal.5:22, 23)
×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Mwanzo 1:26, 27X
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 2:7X
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Zaburi 8:4-8X
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
Matendo 17:24-28X
24 Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono; 25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. 26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao; 27 ili wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasa-papasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na kila mmoja wetu. 28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
Mwanzo 3:4, 6-9X
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. 7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone. 9 Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Zaburi 51:5X
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Warumi 5:12-17X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; 14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. 15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.
2 Wakorintho 5:19X
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Zaburi 50:10X
10 Maana kila hayawani ni wangu, Na makundi juu ya milima elfu.
1 Yohana 4:7, 8X
7 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Mwanzo 1:26X
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:27X
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Mwanzo 5:1, 2X
1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya; 2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
Mwanzo 2:7X
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Mhubiri 2:7X
7 Nami nikanunua watumwa na wajakazi, nikawa na wazalia nyumbani mwangu; tena nikawa na mali nyingi za ng'ombe na kondoo, kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu;
Mwanzo 1:26X
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:2, 24, 25X
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. 25 Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Luka 3:38X
38 wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.
Mwanzo 1:28X
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Zaburi 8:4-9X
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini. 9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Matendo 17:26X
26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
Warumi 5:16, 19X
16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
1 Wakorintho 15:21, 22X
21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
Mwanzo 2:7X
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Mwanzo 2:7X
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Ayubu 33:4X
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
Mwanzo 1:20, 24X
20 Mungu akasema, Maji na yajawe kwa wingi na kitu kiendacho chenye uhai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu. 24 Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
Mwanzo 2:19X
19 Bwana Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Mwanzo 2:7X
7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Mwanzo 7:20-23X
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano. 21 Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi, na ndege, na wanyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu, na kila kitambaacho chenye kutambaa juu ya nchi, na kila mwanadamu; 22 kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu. 23 Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.
Ezekieli 18:4X
4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.
Ufunuo 16:3X
3 Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Mathayo 2:20X
20 akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto.
Mathayo 6:25X
25 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
Mathayo 16:25X
25 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona.
Matendo 7:14X
14 Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano.
Matendo 27:37X
37 Na sisi tuliokuwa ndani ya merikebu tulipata watu mia mbili na sabini na sita.
Warumi 13:1X
1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.
1 Petro 3:20X
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Mathayo 12:17X
17 ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
2 Wakorintho 12:15X
15 Nami kwa furaha nyingi nitatapanya, tena nitatapanywa kwa ajili ya roho zenu. Je! Kadiri nizidivyo kuwapenda sana, ninapungukiwa kupendwa?
Marko 14:34X
34 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
Luka 2:35X
35 Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi.
Matendo 14:2X
2 Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.
Wafilipi 1:27X
27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;
Waefeso 6:6X
6 wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
Ufunuo 16:3X
3 Na huyo wa pili akakimimina kitasa chake juu ya bahari, ikawa damu kama damu ya mfu, na vitu vyote vyenye roho ya uhai katika bahari vikafa.
Ayubu 33:4X
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
Mwanzo 8:1X
1 Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
Waamuzi 15:19X
19 kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu;
Waamuzi 8:3X
3 Mungu amewatia hao wakuu wa Midiani, Orebu na Zeebu, mikononi mwenu; na mimi nilipata kufanya nini kama mlivyofanya ninyi? Ndipo hasira zao walizokuwa nazo juu yake zikatulia aliposema maneno hayo.
Isaya 54:6X
6 Maana Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
Ezekieli 11:19X
19 Nami nitawapa moyo mmoja, nami nitatia roho mpya ndani yao; nami nitauondoa moyo wa kijiwe katika miili yao, nami nitawapa moyo wa nyama;
Mhubiri 3:19-21X
19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. 20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena. 21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
Zaburi 146:4X
4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Mhubiri 12:7X
7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Ayubu 34:14X
14 Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;
Isaya 63:10X
10 Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
Warumi 8:15X
15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.
1 Wakorintho 4:21X
21 Mnataka vipi? Nije kwenu na fimbo, au nije katika upendo na roho ya upole?
Warumi 1:7X
7 kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
Wagalatia 6:1X
1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.
Warumi 12:11X
11 kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
Luka 23:46X
46 Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu.
Matendo 7:59X
59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu.
1 Wakorintho 2:11, 14X
11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Waefeso 4:30X
30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
Waebrania 2:4X
4 Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.
1 Petro 1:21X
21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.
2 Petro 1:21X
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Luka 1:46, 47X
46 Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, 47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
1 Wakorintho 7:34X
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
1 Wathesalonike 5:23X
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
Warumi 8:16X
16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
Warumi 12:1, 2X
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Mwanzo 1:27X
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Yohana 4:24X
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Waebrania 1:7, 14X
7 Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto. 14 Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Mwanzo 1:1-19, 22X
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. 4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza. 5 Mungu akaiita nuru Mchana, na giza akaliita Usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. 6 Mungu akasema, Na liwe anga katikati ya maji, likayatenge maji na maji. 7 Mungu akalifanya anga, akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga; ikawa hivyo. 8 Mungu akaliita lile anga Mbingu. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya pili. 9 Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, ili pakavu paonekane; ikawa hivyo. 10 Mungu akapaita pale pakavu Nchi; na makusanyiko ya maji akayaita Bahari; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. 12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu. 14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; 15 tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. 16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi 18 na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. 19 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. 22 Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
Danieli 9:21X
21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.
Luka 1:11-38X
11 Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. 12 Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13 Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14 Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. 15 Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. 16 Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. 17 Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. 18 Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje neno hilo? Maana mimi ni mzee, na mke wangu ni mkongwe wa siku nyingi. 19 Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema. 20 Na tazama! Utakuwa bubu, usiweze kusema, mpaka siku ile yatakapotukia hayo, kwa sababu hukuyasadiki maneno yangu; nayo yatatimizwa kwa wakati wake. 21 Na wale watu walikuwa wakimngojea Zakaria, wakastaajabia kukawia kwake mle hekaluni. 22 Alipotoka hali hawezi kusema nao, walitambua ya kuwa ameona maono ndani ya hekalu, naye aliendelea kuwaashiria akakaa bubu. 23 Ikawa siku za huduma yake zilipokuwa zimetimia akaenda nyumbani kwake. 24 Hata baada ya siku zile mkewe Elisabeti alichukua mimba akatawa miezi mitano, akisema, 25 Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana katika siku zile alizoniangalia ili kuniondolea aibu yangu mbele ya watu. 26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 38 Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.
Matendo 12:5-10X
5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake. 6 Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza. 7 Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi. 8 Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate. 9 Akatoka nje, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni kweli yaliyofanywa na malaika; bali alidhani kwamba anaona maono. 10 Na walipopita lindo la kwanza na la pili, wakaja hata mlango wa chuma wa kuingilia mjini, ukawafungukia wenyewe. Wakatoka nje, wakapita katika njia moja; mara malaika akamwacha.
1 Wakorintho 15:44X
44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.
Kutoka 28:4X
4 Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Kutoka 33:20-23X
20 Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 21 Bwana akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; 22 kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; 23 nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.
Danieli 7:9, 10X
9 Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. 10 Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.
Wakolosai 1:15X
15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
Waebrania 1:3X
3 Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Waebrania 2:7X
7 Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Mhubiri 7:9X
9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Waefeso 4:24X
24 mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Mwanzo 1:31X
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
1 Yohana 4:8X
8 Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Mathayo 24:36-40X
36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 38 Kwa kuwa kama vile siku zile zilizokuwa kabla ya Gharika watu walivyokuwa wakila, na kunywa, wakioa na kuolewa, hata siku ile aliyoingia Nuhu katika safina, 39 wasitambue, hata Gharika ikaja, ikawachukua wote, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu. 40 Wakati ule watu wawili watakuwako kondeni; mmoja atwaliwa, mmoja aachwa;
Mwanzo 2:18X
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Matendo 17:26X
26 Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja, wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;
Mwanzo 1:26X
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Zaburi 8:4-8X
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie? 5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake. 7 Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
Kutoka 20:8-11X
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Mwanzo 2:16, 17X
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Mwanzo 3:19, 22, 24X
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. 22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; 24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Mwanzo 1:31X
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Isaya 6:3X
3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
K. Torati 32:4X
4 Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili.
Ayubu 32:4X
4 Basi huyo Elihu alikuwa anangoja ili anene na Ayubu, kwa sababu hao wengine walikuwa wazee kuliko yeye.
Zaburi 4:5X
5 Toeni dhabihu za haki, Na kumtumaini Bwana.
Zaburi 11:5X
5 Bwana humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.
Mwanzo 1:31X
31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.
Waebrania 5:9X
9 naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii;
Ezekieli 28:17X
17 Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
1 Timotheo 3:6X
6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi.
Yuda 6X
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.
Isaya 14:12-14X
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! 13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. 14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
Ufunuo 12:4, 9-12X
4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. 10 Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. 11 Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. 12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.
Mwanzo 3:4, 5X
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Mwanzo 3:6X
6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Warumi 5:12X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Mwanzo 3:7X
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
Mwanzo 3:7, 8X
7 Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo. 8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
Mwanzo 3:12X
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Mwanzo 3:13X
13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala.
Mwanzo 2:13X
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.
Mwanzo 3:16X
16 Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mwanzo 3:17-19X
17 Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3:19X
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3:8X
8 Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.
Mwanzo 3:23, 24X
23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. 24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Mwanzo 3:22X
22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Mwanzo 3:1-6X
1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? 2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; 3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. 4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Warumi 1:18-22X
18 Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. 19 Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. 20 Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; 21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. 22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
1 Yohana 3:4X
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
Yakobo 4:7X
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
Warumi 14:23X
23 Lakini aliye na shaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.
Mathayo 12:30X
30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.
Yohana 16:9X
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
Yakobo 2:10X
10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
Kutoka 20:13X
13 Usiue.
Mathayo 5:21, 22X
21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Kutoka 20:14X
14 Usizini.
Mathayo 5:27, 28X
27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Warumi 3:19X
19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;
Warumi 6:23X
23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Mathayo 6:12X
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Mathayo 11:28X
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mithali 4:23X
23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Mithali 15:19X
19 Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.
Yeremia 17:9X
9 Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?
Mwanzo 4:8, 23X
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, Twende uwandaniIkawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua. 23 Lameki akawaambia wake zake, Sikieni sauti yangu, Ada na Sila; Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu; Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha; Kijana kwa kunichubua;
Mwanzo 6:1-5, 11-13X
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.
Mwanzo 5:1, 2X
11 Dunia ikaharibika mbele za Mungu, dunia ikajaa dhuluma. 12 Mungu akaiona dunia, na tazama, imeharibika; maana kila mwenye mwili amejiharibia njia yake duniani. 13 Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Zaburi 143:2X
2 Wala usimhukumu mtumishi wako, Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.
Zaburi 14:3X
3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.
1 Wafalme 8:46X
46 Ikiwa wamekutenda dhambi, (maana hakuna mtu asiyetenda dhambi), hata ukawaghadhibikia, ukawatia katika mikono ya adui zao, wawachukue mateka mpaka nchi ya adui zao, iliyo mbali au iliyo karibu;
Mithali 20:9X
9 Nani awezaye kusema, Nimesafisha moyo wangu; Nimetakasika dhambi yangu?
Mhubiri 7:20X
20 Bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.
Warumi 3:23X
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
1 Yohana 1:8X
8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.
1 Wakorintho 15:22X
22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
Warumi 5:12X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Zaburi 51:5X
5 Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
Warumi 8:7, 8X
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii. 8 Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Waefeso 2:3X
3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Yeremia 13:23X
23 Je! Mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza, ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema, ninyi mliozoea kutenda mabaya.
Yohana 15:5X
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Yohana 8:36X
38 Niliyoyaona kwa Baba ndiyo niyanenayo; nanyi vivyo hivyo mliyoyasikia kwa baba yenu ndiyo myatendayo.
Yohana 15:4, 5X
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Warumi 7:15, 19, 20, 22-24X
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 22 Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, 23 lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. 24 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?
Warumi 7:25X
25 Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.
Warumi 8:1X
1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Waefeso 2:1, 3, 8-10 X
1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; 3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Yohana 1:13X
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
1 Yohana 2:1X
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Ayubu 31:33X
33 Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;
Mhubiri 7:29X
29 Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.
Mathayo 19:4, 5X
4 Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, 5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
Yohana 8:44X
44 Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa huo.
Warumi 5:12, 18, 19X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki.
2 Wakorintho 11:3X
3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.
1 Timotheo 2:14X
14 Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
Ufunuo 12:9X
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Zaburi 8:5, 6X
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima; 6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Waebrania 2:7X
7 Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
Zaburi 8:9X
9 Wewe, MUNGU, Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote!
Mwanzo 3:15X
15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Waefeso 1:4-6X
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
2 Timotheo 1:9X
9 ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele,
1 Petro 1:20X
20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu;
Waebrani 6:18X
18 ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;
Waebrania 7:22X
22 basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Warumi 5:12-21X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; 13 maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; 14 walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja. 15 Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 16 Wala kadiri ya yule mtu mmoja aliyefanya dhambi si kadiri ya kile kipawa; kwa maana hukumu ilikuja kwa njia ya mtu mmoja ikaleta adhabu; bali karama ya neema ilikuja kwa ajili ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. 17 Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. 18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. 20 Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi; 21 ili kwamba, kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.
1 Wakorintho 16:22X
22 Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maran atha.
Yohana 6:38X
38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Yohana 3:30-36X
30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua. 31 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote. 32 Yale aliyoyaona na kuyasikia ndiyo anayoyashuhudia, wala hakuna anayeukubali ushuhuda wake. 33 Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia muhuri ya kwamba Mungu ni kweli. 34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo. 35 Baba ampenda Mwana, naye amempa vyote mkononi mwake. 36 Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Yohana 6:40X
40 Kwa kuwa mapenzi yake Baba yangu ni haya, ya kwamba kila amtazamaye Mwana na kumwamini yeye, awe na uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.
Yohana 17:3X
3 Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Yohana 17:4X
4 Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.
Yohana 19:30X
30 Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
Mwanzo 6:1-8X
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. 3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. 4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa. 5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.
Mwanzo 11:1-9X
1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja. 2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko. 3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. 4 Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 Bwana akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko Bwana akawatawanya waende usoni pa nchi yote.
Mwanzo 22:18X
18 na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.
Mwanzo 12:3X
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 18:18X
18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
Mwanzo 15:6X
6 Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.
Mwanzo 17:1X
1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu.
Mwanzo 26:5X
5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
Warumi 4:2, 3X
2 Kwa maana ikiwa Ibrahimu alihesabiwa haki kwa ajili ya matendo yake, analo la kujisifia; lakini si mbele za Mungu. 3 Maana maandiko yasemaje? Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa haki.
Yakobo 2:23, 24X
23 Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu. 24 Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Wagalatia 3:7X
7 Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.
Wagalatia 3:29X
29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Waebrania 9:1X
1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia.
Wagalatia 4:22-31X
22 Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 23 Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi. 24 Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri. 25 Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika pamoja na watoto. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 27 Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. 28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa. 30 Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe, kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa mwungwana. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Danieli 9:27X
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
Luka 22:20X
20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.
Warumi 15:8X
8 Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
Waebrania 9:11-12X
11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele.
Yeremia 31:33X
33 Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema Bwana; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Wagalatia 5:22, 23X
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,