Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo kwa ajili ya ustawi wa wote kanisani na wa wanadamu. Zikitolewa kwa nguvu za Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila mshiriki kama apendavyo Yeye, karama hizi hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajika na kanisa katika kutimiza kazi iliyoagizwa kimbingu. Kulingana na Maandiko Matakatifu, karama hizi ni pamoja na huduma kama vile imani, kuponya, unabii, kuhubiri, kufundisha, utawala, upatanisho, huruma, na huduma ya kujinyima na upendano wa kusaidia na faraja kwa watu. Baadhi ya washiriki wameitwa na Mungu na kukirimiwa na Roho kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, utume na huduma ya kkufundisha inayohitajika hasa katika kuwapa zana washiriki kwa ajili ya huduma, kulijenga kanisa hata likomae kiroho, na kukuza umoja wa imani na kumjua Mungu. Wakati washiriki wanapozitumia karama hizi za Roho kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya mivuto ya uharibifu wa mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuzi utokao kwa Mungu, na kujengwa imara katika imani na upendo.” (Rum.12:4-8;
1Kor.12:11-13, 27, 28; Efe.4:8, 11-16; Mdo.6:1-7; 1Tim.3:1-3; 1Pet.4:10, 11)
Maneno aliyosema Yesu kabla ya kupaa mbinguni yangebadili historia. “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” (Mk.16:15). Ulimwenguni mwote…? Kwa kila kiumbe…? Wanafunzi wangefikiri kuwa ni kazi isiyowezekana. Kristo hali akijua hali yao kuwa hawajiwezi, aliagiza wasitoke Yerusalemu bali waingoje “ahadi ya Baba”. Ndipo alipowahakikishia kuwa “mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria na hata mwisho wa nchi.” (Mdo.1:4, 8). Baada ya Yesu kupaa, wanafunzi walitumia muda mwingi kwa maombi. Umoja na unyenyekevu vilichukua nafasi ya kutofautiana na wivu vilivyotia doa wakati wao wakiwa na Yesu. Wanafunzi walikuwa wameongoka. Uhusiano wao karibu na Yesu na umoja uliotokea, vilikuwa muhimu kwa kujazwa Roho Mtakatifu. Kama Kristo alivyotiwa mafuta na Roho Mtakatifu afanye utume wake (Mdo.10:38), wanafunzi nao walipokea ubatizo wa Roho Mtakatifu (Mdo.1:5) kuwawezesha kushuhudia. Siku waliyopokea Roho Mtakatifu, walibatiza watu elfu tatu. (Angalia Mdo.2:41).
Karama za Roho Mtakatifussss
Kristo alifafanua karama za Roho Mtakatifu kwa mfano. “Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.” (Mt.25:14, 15).Mtu anayesafiri kwenda mbali inamwakilisha Kristo. Watumishi wa mtu ni wafuasi wake ambao “wamenunuliwa kwa thamani” (1Kor.6:20)- “damu ya thamani ya Kristo (1:Pet.1:19).
Yesu amewakomboa ili watumike na “hawako hai tena kwa kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa anjili yake Yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.” (2Kor.5:15). Kristo ametoa mema kwa kila mtumishi kwa kadiri ya uwezo wake na kila mtu “kazi yake” (Mk.13:34). Pamoja na karama na uwezo mbalimbali, mema haya huwasilisha karama maluum zinazotolewa na Roho Mtakatifu. Kwa maana maalum, Kristo aligawa karama hizi kanisani siku ya Pentekoste. “Alipopaa juu… aliwapa wanadamu vipawa” . Hivyo “kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. (Efe.4:7, 8). Roho Mtakatifu ndiye Mtendaji, “akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye” (1Kor.12:11).
Makusudi ya Karama za Kiroho
Roho Mtakatifu humpatia uwezo wa kipekee mshiriki, na kumwezesha kulisaidia kanisa litimize utume wake.
Umoja ndani ya Kanisa
Kanisa la Korintho halikupungukiwa karama yoyote (1Kor.1:4, 7). Ila washiriki wake walitofautiana na kugombana kama watoto kuwa ni karama ipi iliyo muhimu kuliko nyingine. Kufuatia migawanyiko ndani ya kanisa, Paulo aliwandikia asili halisi ya karama hizi. Karama za kiroho, ni karama za neema. Kutoka kwa Roho mmoja, huja “tofauti za karama” ambazo huleta “tofauti za huduma” na “tofauti za kutenda kazi”. Lakini Paulo anasisitiza kuwa ni “Mungu yeye yule azitendaye kazi zote katika wote” (1Kor. ambazo huleta “tofauti za huduma” na “tofauti za kutenda kazi”. Lakini Paulo anasisitiza kuwa ni “Mungu yeye yule azitendaye kazi zote katika wote” (1Kor.12:4-6).
1. Jinsi zitendavyo kazi.
Paulo anatumia mwili wa mwanadamu kuelezea umoja katika tofauti za karama. Mwili una viungo vingi, ambavyo kila kimoja huchangia ustawi wake. “Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alviyotaka.” Hakuna kiungo kinachoweza kukiambia kiungo kingine, “sina haja na wewe”. “Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi, vyahitajiwa zaidi. Vile viungo vidhaniwavyo havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visvyo na uzuri, vina uzuri zaidi. (1Kor.12:21-24). Viungo vilivyo vinyonge huhitaji ulinzi maalum. Twaweza kutembea pasipo mkono au mguu, lakini hatuwezi kutembea pasipo mapafu, maini au moyo. Huwa tunatoa nyuso na mikono yetu watu waone, lakini viungo vingine tunavisitiri kwa mavazi. Mungu anakusudia kwamba mgawanyo wa karama za roho kuzuia faraka na kuleta roho ya kuungana na kutunzana. Kama kiungo kimoja kikiugua, viungo vyote vitauugua navyo, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho. (1Kor.12:25, 26). Baada ya kuziorodhesha karama, Paulo anahitimisha kwamba “Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kasha miujiza, kasha karama za kuponya wagonjwa na masaidiano, na maongozi na aina za lugha.” (1Kor.12:28). Kwa sababu si kila mshiriki atakuwa na karama zote, tumeitwa kuzitaka karama zilizo kuu. (1Kor.12:31).
2. Kipimo muhimu
Karama za Roho hazitoshelezi zenyewe peke yake. Iko njia iliyo bora (1Kor.12:31). Karama za Roho zitapita Yesu atakaporudi mara ya pili. Tunda la Roho ni la kudumu milele. Tunda la Roho huja na hali bora ya upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema wote na haki na kweli ambavyo upendo huja navyo (Gal.5:22, 23; Efe.5:9). Unabii, kunena kwa lugha na ufahamu vitapotea, lakini imani, tumaini na upendo vitadumu, na lililo kubwa katika hayo ni upendo. (1Kor.13:13).
Upendo huu ambao Mungu hutoa (kwa Kigiriki agape), ni upendo unaojinyima na kutoa upendo kwa kitu au mtu anayependwa, upendo ambao hukua kutokana na heshima ya vilivyo bora vilivyomo ndani ya mtu/kitu. Karama zisizo na upendo huleta faraka na migogoro kanisani. Kwa hiyo njia bora ni kuufuata upendo, na kutaka sana karama za rohoni. (1Kor.14:1).
Kuishi kwa utukufu wa Mungu
Katika waraka kwa Warumi, Paulo anazungumzia karama za roho na kuwaita waumini wapate kuishi kwa utukufu wa Mungu (Rum.11:36 – 12:2). Anatumia kielelezo cha mwili kuonyesha utofauti wa viungo na huduma (fungu la 3-6). Katika sura ya 12, anaorodhesha: unabii, huduma, kufundisha, kuonya (kutia moyo), ukarimu, uongozi (usimamizi), na kurehemu. Kama katika Wakorintho, Paulo anamalizia kwa kanuni kuu ya upendo (fungu la 9). Petro anazungumzia karama za roho kwa kuangalia mwisho unaokaribia (1Pet.4:7). Umuhimu wake ni kuwa watu wazitumie karama kabla wakati haujaisha. Kila moja kadiri alivyopokea karama aitumie kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu (1Pet.4:10). Kama Paulo, anasema karama hizi siyo kwa kujivunia bali kwa bali kwa utukufu wa Mungu (1Pet. 4:11). Pia alihusisha upendo na karama za roho. (1Pet.4:8).
Kukua kwa Kanisa
Paulo katika hoja yake ya tatu na ya mwisho kuhusiana na karama za roho, alisihi waumini kuishi maisha yanayostahili wito wao walioitiwa. Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. (Efe.4:1-3). Karama za kiroho huchangia kuimarika kwa umoja ambao unasaidia Kanisa kukua. Kila mshiriki amepokea “neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo” (Efe.4:7).
Kristo mwenyewe “alitoa wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, kata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo. (Efe. 4:11-13).
Huduma hizi huimarisha kanisa na kuliongezea uwezo wake wa kinga “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujaja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.” (Efe.4:14, 15).
Hatimaye, katika Kristo, huduma hizi huleta umoja na ustawi wa kanisa. “Katika Yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.” (Efe. 4:16). Kukua huwa kwa aina mbili; kwanza; kuongezeka washiriki na kuongezeka kwa karama za kiroho kwa mshiriki moja moja. Tena, upendo ni sehemu ya wito, kwa kuwa kila mshiriki atatumia karama zake kwa upendo.
Athari za Karama za Kiroho
Huduma moja
Maandiko hayatetei wazo kwamba wachungaji wahudumu na washirki wapashe joto mabenchi wakisubiri kulishwa. Wote wachungaji na washiriki ni watu wa miliki ya Mungu (1Pet.2:9). Wote wameitwa kuutayarisha ulimwengu ili kumpokea mwokozi arudipo. (Mt.28:19, 20; Ufu.14:6-12).
Jukumu la Viongozi wa Kiroho
Fundisho la Karama za kiroho huweka jukumu la kufundisha washiriki kwa viongozi wa kiroho ili washiriki wafanye iliyo kazi yao. Mafanikio ya mpango wa Mungu kwa kanisa hutegemea utayari na uwezo wa wachungaji kuwafundisha washiriki kutumia talanta walizopewa na Mungu.
Karama na Utume
Mungu hutoa karama za kiroho kulifaidia mwili wote ambao ni kanisa na siyo tu mshiriki anayezipokea. Kadhalika kanisa halipokei karama kwa ajili yake tu ila kulisaidia kutimiza utume ambao Mungu amelipa.
Umoja katika kutofautiana
Baadhi ya wakristo hujaribu kuwafanya wengine wafane nao. Huo ni mtazamo wa kibinadamu wala siyo mpango wa Mungu. Karama zimetolewa tofauti tofauti kwa kufaidiana. Katika Kristo, jiwe kuu la pembeni, “jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.” (Efe.2:21)
Kushuhudia - kusudi la karama
Waumini hupokea karama tofauti ni ishara kuwa kila moja ana huduma yake iliyo tofauti. Hata hivyo bado mshiriki anapaswa kuikiri imani yake akishuhudia yale Mungu aliyomtendea. Makusudi ya karama kwa ujumla wake ni kumfanya mshiriki ashuhudie.
Kushindwa kutumia karama
Waumini ambao wanashindwa kutumia karama siyo tu kwamba karama zao zinapotea bali wanahatarisha fursa yao kuupata uzima wa milele. (Mt.25:26-30)
Kuzitambua Karama za Kiroho
Ili washiriki wafanikiwe kwenye utume wa Kanisa, wanapaswa kuzitambua karama zao. Kuzitambua karama za kiroho kwapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
Maandalizi ya Kiroho
Mitume waliomba kwa umakini ili wapate kufaa kusema Neno litakalowavuta wenye dhambi kwa Kristo.Waliondoa tofauti zao na matamanio yao ya kuwa wakubwa. Twapaswa kuendelea kuupokea ubatizo wa Roho Mtakatifu tumsihi atupatie hekima kuzitambua karama tulizo nazo. (Yak.1:5)
Kujifunza Maandiko
Kujifunza Agano Jipya kwa maombi kutafanya akili zetu zitambue karama tulizonazo na tunazoweza kuzitumia kwa utukufu wa Mungu. Ni jukumu letu pia kuamini Mungu amempatia kila moja wetu angalau karama moja kwa utumishi wake.
Kuwa tayari kwa kile Mungu anachotupatia
Hatumtumii Roho bali ni Mungu ndiye atendaye kazi ndani yetu, “kutaka kwetu, na kutenda kwetu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.” (Filp.2:13).
Kuthibitishwa na Kanisa
Kwa kuwa Mungu ndiye atoaye karama kujenga kanisa lake, twaweza kutarajia hatimaye uthibitisho wa karama zetu kutokea kwenye maamuzi ya mwili wa Kristo wala siyo hisia zetu wenyewe.
Warumi 12:4-8X 4 Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; 5 Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. 6 Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; 7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; 8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
1 Wakorintho 12:11-13, 27, 28X 11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 27 Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
Waefeso 4:8, 11-16X 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Matendo 6:1-7X 1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku. 2 Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. 3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; 4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. 5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; 6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao. 7 Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.
Matendo 3:1-3X 1 Basi Petro na Yohana walikuwa wakikwea pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tisa. 2 Na mtu mmoja aliyekuwa kiwete toka tumboni mwa mamaye alichukuliwa na watu, ambaye walimweka kila siku katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aombe sadaka kwa watu waingiao ndani ya hekalu. 3 Mtu huyu akiwaona Petro na Yohana wakiingia hekaluni aliomba apewe sadaka.
1 Petro 4:10, 11X 10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Marko 16:15X 15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Matendo 1:4, 8X 4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Matendo 1:5X 5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.
Matendo 2:41X 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Mathayo 25:14, 15X 14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. 15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
1 Wakorintho 6:20X 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
1 Petro 1:19X 19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
2 Wakorintho 5:15X 15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
Marko 13:34X 34 Mfano wake ni kama mtu mwenye kusafiri, ameiacha nyumba yake, amewapa watumwa wake amri, na kila mtu kazi yake, naye amemwamuru bawabu akeshe.
Waefeso 4:7, 8X 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.
1 Wakorintho 12:11X 11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
1 Wakorintho 1:4, 7X 4 Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; 7 hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo;
1 Wakorintho 12:4-6X 4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
1 Wakorintho 12:21-24X 21 Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi. 22 Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi. 23 Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana. 24 Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;
1 Wakorintho 12:25, 26X 25 ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe. 26 Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
1 Wakorintho 12:28X 28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
1 Wakorintho 12:31X 31 Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.
Wagalatia 5:22, 23X 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Waefeso 5:9X 9 kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
1 Wakorintho 13:13a href="#close" title="Close" class="close">X 13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
1 Wakorintho 14:1X 1 Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.
36 Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Warumi 12:1-2 1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
1 Petro 4:7X 7 Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
1 Petro 4:10X 10 kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu.
1 Petro 4:11X 11 Mtu akisema, na aseme kama mausia ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
Waefeso 4:1-3X 1 Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; 2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3 na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
Waefeso 4:7X 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.
Waefeso 4:11-13X 11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
Waefeso 4:14, 15X 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.
Waefeso 4:16X 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
1 Petro 2:9X 9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Mathayo 28:19, 20X 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Ufunuo 14:6-12X 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji. 8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. 9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, 10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake. 12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Waefeso 2:21X 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
Mathayo 25:26-30X 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
Yakobo 1:5X 5 Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.
Wafilipi 2:13X 13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
1 Wakorintho 12:1X 1 Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.