Kanisa

Utangulizi


Kanisa ni jumuiya ya waumini waliokubali kumkiri Yesu kama mwokozi na Bwana wao. Kwa kuunganika na watu wa Mungu katika Agano la Kale, tumeitwa kutoka ulimwenguni na tunaungana pamoja kwa ibada, ushirika, kufundisha Neno, kusherehekea Meza ya Bwana, katika utumishi kwa wanadamu na katika kutangaza injili duniani kote. Kanisa hupokea mamlaka yake kutoka kwa Kristo ambaye ni Neno aliyefanyika mwili, na katika Maandiko Matakatifu, ambayo ni Neno lililoandikwa. Kanisa ni familia ya Mungu iliyotengenezwa kwa agano. Kanisa ni mwili wa Kristo, jumuia ya imani ambayo Kristo mwenyewe ndiye Kichwa (Kiongozi). Kanisa ni bibi arusi ambaye Kristo alimfia ili apate kumtakasa na kumsafisha. Katika kurudi kwake kwa ushindi, atajiwasilishia kwake mwenyewe likiwa kanisa tukufu, aminifu kwa vizazi vyote, kile ambacho damu yake ilikinunua, likiwa halina doa wala kunyanzi bali takatifu lisilo na waa. (Mw. 12:3, Mdo. 7:38, Efe. 4:11-15, 3:8-11, Mt.28:19,20; Mt 16:13-20; Mt 18:18; Efe. 2:19-22; Efe 1:22,23, Efe 5:23-27, Kol.1:17,18)

Maana ya Kanisa Kibiblia

Kwenye Biblia, neno la Kigiriki lililotafsiriwa kanisa ni ekklesia, likimaanisha kuitwa ili kuondoka/kutoka. Kitabu kiitwacho Septuagint yaani tafsiri ya Kigiriki ya Agano la Kale iliyotumiwa nyakati za Yesu, hutafsiri neno la kiebrania qahal iliyomaanisha mkutano, kusanyiko, jamii. (Kumb.9:10, Kumb 18:16; 1Sam.17:47, 1Waf.8:14, 1Nya.13:2). Matumizi ya maana ya kanisa yalipanuka kwenye Agano Jipya ambako maana zifuatazo zinaonekana: -

  1. Waumini wanaokutana kuabudu katika mahali fulani maalum (1Kor. 11:18; 14:19, 28)
  2. Waumini wanaoishi katika eneo mojawapo kijiografia (1Kor.16:1, Gal.1:2 1Thes.2:14)
  3. Kundi la waumini katika nyumba ya mtu (1Kor.16:19, Kol.4:15, Filem. 2)
  4. Makundi ya Makusanyiko ya waumini kwenye eneo mojawapo kijiografia (Mdo. 9:31)
  5. Kundi linalojumuisha waumini wote ulimwenguni (Mt.16:18; 1Kor.10:32; 12:28; cf. Efe. 4:11-16)
  6. Jamii ya waumini waaminifu wote ulimwenguni – duniani na mbinguni (Efe. 1:20-22; Filip. 2:9-11)

Chimbuko la Kanisa

Biblia hulionyesha kanisa kuwa ni taasisi ya kimbingu, ikiliita Kanisa la Mungu (Mdo.20:28), 1Kor.1:2). Yesu aliwekeza mamlaka yake ndani ya Kanisa (Mt. 18:17,18). Twaweza kutambua mizizi ya Kanisa katika Agano la Kale na vielelezo vya Agano Jipya.

Mizizi ya Kanisa

Agano la Kale linadhihirisha kwamba kanisa ni kundi lenye mpangilio la watu wa Mungu. Tangu awali familia zenye kumcha Mungu tangu Adamu, Seti, Nuhu, Shemu na Ibrahimu ziliutunza ukweli. Mungu alitoa ahadi nzito na hatimaye hii nyumba ya Mungu ilikuwa taifa: na jamaa zote zote za dunia watabarikiwa (Mwa. 12:1-3)

Taifa alilolitoa Misri liliitwa Kanisa llililokuwa Jangwani (Mdo. 7:38). Washiriki wake wa Kanisa walitambulika ‘ufalme wa makuhani na taifa takatifu (Kut.19:6), Watakatifu wa Mungu (Kumb.28:9 c/f Law.26:12), Kanisa lake. Aliwaweka Palestina, mahali ambako mabara matatu ya Afrika, Ulaya na Asia hukutana lengo likiwa kuwaita wote waingie (Isa.56:7). Pamoja na uangalizi wa Mungu, Israeli waliendelea kuabudu miungu mingine, kujitenga kiubaguzi, utaifa, kiburi na kujiangalia wenyewe, wakashindwa kutimiza makusudi ya Mungu.

Katika siku za Yesu, Israeli walipata upendeleo wa kufikiwa na Masihi aliyetarajiwa kuwafungua kwenye utumwa wa kujitumainia nafsi. Kwa kumsulibisha Yesu, ilidhihirika jinsi Israeli walivyooza ndani yao. Walipopaza sauti hatuna mfalme ila Kaisari (Yoh. 19:15), walikataa Mungu asitawale juu yao. Kwa kushindwa Israeli, Mungu alianzisha taifa jingine, kanisa jingine, ambalo lingetimiza makusudi yake. (Mt. 21:41,43).

Kanisa katika Agano jipya linaundwa na Wayahudi waumini na watu wa Mataifa mengine (Gal.3:26-29). Wayahudi wasiomwamini Yesu siyo watoto wa Mungu tena (Rum.9:6-8). Mataifa wanaomkubali Mungu wanafananishwa na mzabibu mwitu ulipandikizwa kwenye mzabibu mwema (Rum.11:17-25). Matawi yanaonywa kushikamana na Mungu wasije wakakatiliwa mbali (Rum.11:16-18). Tofauti na Kanisa kwenye Agano la Kale, Kanisa la Agano Jipya halijifungamanishwi na taifa moja, bali limepangiliwa kuwa la Ulimwengu mzima (Mt.28:19)

Vielelezo vya Agano Jipya Kuhusu Kanisa

1. Kanisa kama Mwili:

Kanisa kama mwili ni kielelezo kinachosisitiza umoja wa Kanisa na mahusiano baina ya washiriki. Msalaba huwapatanisha waumini katika mwili moja (Efe. 2:16). Kwa njia ya Roho Mtakatifu hubatizwa katika mwili moja (1Kor.12:13). Mwili unaosemwa hapa ni wa Yesu Kristo (Efe.1:22, 23). Washiriki ni viungo kwenye mwili wa Kristo (Efe.5:30). Kristo ndiye huhuisha mwili wake. Yeye ndiye kichwa (Kol.1:18) kiongozi wa Kanisa (Efe.5:23.)

2. Kanisa kama Hekalu:

Kanisa ni hekalu, maskani ambako Roho Mtakatifu hukaa. (1Kor.3:9-16, Efe.2:20). Hekalu hili liko hai, kwa kuwa Kristo ni jiwe lililo hai na washiriki mawe yaliyo hai ambayo hufanya nyumba hai. (1Pet.2:4-6). Hekalu halijakamilika, linaendelea kujengwa (Efe.2:22) na zana bora zatakiwa kulijenga ili listahimili majaribu hata hukumu (1Kor.3:12-15). Kielelezo cha hekalu husisitiza utakatifu kwa kuwa atayeliharibu ataharibiwa (1Kor.3:17). Hakuna ushirika baina ya Kristo na Beliari (2Kor. 6:14, 16).

3. Kanisa kama Bibi Arusi:

Kanisa husemwa kuwa Bibi Arusi wa Bwana Harusi Yesu Kristo. Bwana asema nitakuposa uwe wangu milele (Hosea 2:19), …mimi ni mume wenu (Yer.3:14). Paulo anarudia kielelezo hiki kwa kusema nalimposea Kristo bikira safi (Kol. 1:18, 22-23). Upendo wa Kristo kwa kanisa ni mkubwa kwani alilazimika kufa kwa ajili yake(Efe.5:25) na kwa kafara yake kulisafisha (Efe.5:26) ni sala yake litakaswe kwa neno (Yoh.17:17) ili hatimaye liwe safi na lisilo na mawaa (Efe.5:27).

4. Kanisa kama Yerusalemu iliyo juu:

Biblia huita jiji la Yerusalemu Sayuni. Humo, Bwana anakaa na watu wake (Zab.9:11), na wokovu hutokea (Zab.14:7, 53:6). Ni furaha ya dunia yote (Zab.48:2). Agano jipya hutambua jiji la Yerusalemu la juu mbinguni (Gal.4:26) na wakazi wa Yerusalemu hiyo wana makazi na uraia wa mbinguni (Wafil. 3:20). Wakazi ni wana wa ahadi, waliozaliwa kwa roho (Gal.4:28, 29;5:1), hawajitahidi kuhesabiwa haki kwa matendo ya sharia (Gal.4:22,26,31; Gal 5:4) bali kwa imani. Wanatambua kwamba imani itendayo kwa upendo ndiyo huwapa uraia (Gal. 5:5, 6). Waliofika hapo, wako kwenye maskani ya Mungu yenye malaika maelfu na majina yao yameandikwa kuwa ni wenyeji (Ebr.12:22, 23).

5. Kanisa kama Familia:

Kanisa lililoko mbinguni na duniani huzingatiwa kuwa ni familia (Efe.3:15). Kujiunga na familia hii hutokana na kuzaliwa upya (Yoh.3:8) au kwa kuasiliwa (Rum. 8:14-16, Efe.1:4-6). Kwa njia ya imani katika Kristo na ubatizo, hawatakuwa watumwa tena bali wana wa Baba (Gal.3:26-4:7). Ni wa nyumba ya Mungu (Efe.2:19) na jamaa ya waaminio (Gal.6:10). Washiriki wa familia humwita Mungu ‘Baba’ (Gal.4:6) na hujitambua kuwa ndugu – kaka na dada (Yak.2:15, 1Kor.8:11, Rum.16:1). Ni kweli kutokana na huduma yake, Paulo alileta wengi kwa Kristo hata akasema yeye ni baba yao (1Kor.4:15) aliowahubiria watoto wake (1Kor.4:4, Efe.5:1) hata hivyo, kawaida ya msingi ya kanisa ni kujumuika kwa ushirika (fellowship) katika injili (Wafil. 1:5), kwa kujumuika na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (1Yoh.1:3, 1Kor. 1:9; 2Kor.13:14) pamoja na washiriki wengine (1Yoh.1:3, 7). Mfano wa Kanisa kama familia hukazia wajibu wa kupendana, kuthaminiana na mahali ambako watu huhitajiana na talanta hukuzwa. Washiriki wanaotofautiana bado waweza kupeana misaada.

6. Kanisa kama Nguzo na Msingi wa Ukweli:

Kanisa la Mungu ni nguzo na msingi wa ukweli (1Tim.3:15). Hulinda ukweli kutokana na mashambulizi ya adui. Kukitokea fundisho jipya, lapaswa kulinganishwa na maandiko (Isa.8:20). Washiriki wote wapaswa kukubaliana na uamuzi uliosimama katika Biblia kwa kuwa kwa washauri, huja wokovu. (Mith.11:14). Kupitia huduma yake, kanisa huwa chumvi na nuru ya dunia (Mat.5:13-15).

7. Kanisa kama Jeshi: linalo pambana na lililoshinda

Kanisa ni jeshi linalopambana na giza “Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho”(Efe.6:12). Wakristo wapaswa ikuvaa silaha ili waweze kushindana siku ya uovu itakapokuja na wakiisha kufanya yote, kusimama. (Efe.6:13). Maadui wako ndani nan je (Mdo.20:29,30; 1Tim.4:2). Pamoja na kuwapo vitani, bado kanisa lina kasoro zisizo ndogo, ndani yake alikuja adui akapanda magugu akaenda zake (Mt.13:24, 25) na hivyo kuna magugu na ngano yanayoendelea kukua pamoja (Mt.13:29, 30). Vita ya adui wa nje haijakoma, kwa kuwa shetani anaendelea kusumbua (Uf.12:12, 17). Hata hivyo Kristo ataingilia kati na kuokoa kila aliyeandikwa kwenye kitabu chake (Dan.12:1). Yesu amehakikisha kwamba atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka (Mt.24:13). Kristo atakaporejea mara ya pili Kanisa lililoshinda litatokea “kwa kuwa atajiletea Kanisa tukufu lisilo na doa wala kunyanzi au waa lo lote, bali takatifu lisilo na hatia” (Efe.5:27)

Muundo na Majukumu ya Kanisa

Kanisa linaloonekana na Kanisa lisiloonekana

Maneno ya linaloonekana na lisiloonekana hutumika kutofautisha hali mbili za kanisa juu ya dunia. Vielelezo vilivyotumika, huzungumzia kanisa linaloonekana.

Kanisa linaloonekana

Kanisa linaloonekana ni kanisa la Mungu lililojipanga kwa ajili ya huduma. Hutimiza agizo la Yesu la kupeleka injili kwa kila kiumbe (Mt. 28:18-20) na hutayarisha watu kwa ujio wa Yesu wa utukufu (Efe.5:27). Mashahidi wa kweli wa Yesu watafanya kama yeye alivyofanya “‘Roho wa Bwana yu juu Yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwaletea maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubalika.” Luka 4:18,19)

Kanisa lisiloonekana

Kanisa lisiloonekana vile vile hujulikana kama kanisa la ulimwengu wote, huundwa na watu wote wa Mungu kwenye ulimwengu wote, likijumuisha washiriki walioko kwenye kanisa linaloonekana na wengine wengi ambao wameifuata kwa uaminifu nuru waliyopokea (1Yoh.1:9). Hapa liko kundi ambalo halikupata kusikia habari za Yesu bali ndani ya mioyo yao, wakiongozwa na Roho Mtakatifu, wanatii maagizo ya torati (Rum.2:14). Kuwepo kwa kanisa lisiloonekana kunadhihirisha kwamba Mungu huabudiwa katika roho na kweli (Yoh.4:23). Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Mungu huongoza washiriki wa Kanisa lisiloonekana waingie katika Kanisa linaloonekana. “Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.” (Yoh.10:16). Ni katika kanisa linaloonekana tu, ndipo wanapoweza kupata utimilifu wa ukweli, upendo na ushirika (Efe.4:4-16). Paulo alipojiunga na Kanisa linaloonekana, alipewa kulihudumia (Mdo.9:10-22). Hivyo wanapojiunga, huungana kutimiza utume wa Kristo (Uf.14:12, 18:4, Mt. 24:14). Kanisa lisiloonekana vilevile limeunganisha kanisa la mbinguni na duniani (Efe.1:22, 23) na kanisa lililojificha wakati wa mateso (Uf.12:6, 14)

Muundo

Agizo la Yesu la kupeleka injili kwa ulimwengu wote, limejumuisha kuwatunza wale waliopokea neno. (Mt.28:18,19). Kwa kuwa Mungu siyo wa machafuko bali wa amani (1Kor.14:33), Kanisa linapaswa kuwa na muundo rahisi, lakini wenye kutosheleza.

Washiriki wa Kanisa:

Waongofu wakishakukamilisha sifa kadhaa, huwa washiriki wa jumuiya ya waumini. Ushiriki hujumuisha kukubali aina ya mahusiano baina ya watu wengine, Mamlaka ya Siasa (Serikali, Bunge na Mahakama) pamoja na Mungu.

a) Sifa ya kuwa mshiriki:

Wanaotaka kuwa washiriki lazima wamkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wao, watubu dhambi na kubatizwa (Mdo.2:36-41 cf. 4:10-12). Wanapaswa kuzaliwa mara ya pili na kukubali agizo la Yesu la kuwafanya mataifa kuwa wanafunzi (Yoh.3:3,5 na Mt. 28:18-20).

b) Usawa na Utumishi:

Kwa kuzingatia tangazo la Yesu, washiriki wote ni ndugu (Mt.23:8) na wanafursa ya kutumikiana (Mt.23:11). Mahusiano ya washiriki wao kwa wao yanapaswa kufuata kielelezo cha Yesu.

c) Ukuhani wa waumini wote:

Ukuhani wa Walawi ulikoma Yesu alipoanza ukuhani halisi mbinguni (Ebr.8 - 9). Sasa Kanisa limekuwa ukuhani wa kifalme (1Pet.2:5). “Lakini ninyi ni taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu la Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa Zake Yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru Yake ya ajabu.”(1Pet.2:9)

d) Utii kwa Mungu na kwa Serikali:

Biblia hutambua mkono wa Mungu kuhusika kuanzisha mamlaka za kiutawala wa kidunia na huwataka waumini kuziheshimu kwa kulipa kodi, hofu na heshima (Rum.13:4, 7). Katika mtazamo wao kwa mamlaka ya kitaifa, waumini huongozwa na kanuni ya Yesu, kwamba “Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari na Mungu yaliyo ya Mungu (Mt.22:21). Ikiwa Serikali itaamua kuingilia amri ya Mungu, mtume alisema “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu” (Mdo 5:29).

Majukumu Makuu ya Kanisa:

Kanisa liliundwa ili kuijulisha dunia utukufu wa Mungu. Ni kanisa linaloonekana tu, ndilo linaloweza kutimiziza jukumu hilo.

a) Ibada na kuhimizana:

Katika historia yote, kanisa ni chombo cha Mungu kukusanya waumini kwa ibada kwenye siku za sabato. “Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi ya kukutana, tuhimizane sisi kwa sisi kadri tuonavyo siku ile inakaribia.” (Ebr.10:25 cf. 3:13)

b) Ushirikiano wa Kikristo:

Kwa njia ya Kanisa, mahitaji ya ushirikiano wa kikristo hukamilishwa. Kushiriki kueneza Injili (Wafil. 1:5) hupita mahusiano mengine yote kwani hutufanya tufahamiane sisi kwa sisi na pia tumjue Mungu.(1Yoh.1:3, 6, 7)

c) Kufundisha Maandiko:

Yesu alilipa Kanisa funguo za ufalme (Mt.16:19). Hizi funguo ni maarifa ya kuingia ufalme wa Mungu (Luk.11:52). Maneno ya Yesu ni roho na uzima kwa wanaoyapokea (Yoh.6:68). Yakihubiriwa, yana mamlaka ya kufunga na kufungua kadiri msikilizaji anavyopokea. Hivyo neno ni harufu ya mauti pia ni harufu nzuri iletayo uzima (2Kor.2:16). Yesu alijua umuhimu ya Neno litokalo kwenye kinywa cha Mungu (Mt.4:4) na ameagiza kwenda kulifundisha ili watu walishike (Mt.28:19,20)

d) Kusimamia uendeshaji wa desturi za Kanisa:

Kanisa ni nyenzo ya kuendesha huduma ya ubatizo na kumpokea mshiriki kanisani. (Mt.28:19, 20 cf. Mk.16:16) Pia, huendesha huduma ya kuoshana miguu pamoja na Meza ya Bwana (Yoh. 13:12-14, Luk. 22:17-20)

e) Kutangaza injili ulimwenguni pote:

Jukumu kubwa ambalo kanisa limepewa ni kuhubiri injili iwe ushuhuda (Mt.24:14) kwa kuwezeshwa na ubatizo wa Roho Mtakatifu. Injili yajumuisha kukumbushana kujiandaa na ujio wa Yesu ( 1Kor.1:7, 8; 2Pet.3:14; Uf.3:14-22; 14:5) na kwa wanadamu wengine (Uf.14:6-12; 18:4)

Uongozi wa Kanisa

Baada ya Yesu kupaa, uongozi wa Kanisa uliachwa kwenye mamlaka ya Mitume. Jambo lao la kwanza ilikuwa kumteua mtume mwingine kuchukua nafasi ya Yuda (Mdo.1:15-26). Kanisa lilipokuwa, ilikuwa vigumu kuhubiri neno na wakati huo huo kuhudumu mezani. Hivyo waliteua waumini wengine kuhudumu mezani (Mdo. 6:1-4). Mashemasi wawili kati ya saba, Stefano na Filipo walijulikana kwa uhodari wao kuhubiri (Mdo. 7 & 8). Kanisa lilipopanuka Asia na Ulaya, Wazee waliwekewa mikono kuongoza makanisa (Mdo. 14:23). Mgogoro mkubwa ulipoanza, umuhimu wa kuwa na halmashauri kuu ya kanisa ulionekana, misimamo ya pande zinazosigana ilizungumzwa na kuamuliwa (Mdo.15:1-29). Maamuzi yalifikiwa kwa uwakilishi wa pande zote zinazohusika (Mdo.15:22, 25). Hivyo kadiri ya mahitaji yalivyojitokeza, Mungu aliongoza kazi yake na Uongozi wa Kanisa ambao ukifutwa leo, utalinda kanisa kutokana na uasi na kuwezesha kutimiza jukumu lake kuu.

Kanuni za Biblia za Uongozi wa Kanisa

1. Kristo ni Mkuu wa Kanisa:

Uongozi wa Kristo unatokana na huduma yake ya upatanisho. Tangu alipomshinda Shetani msalabani, alipewa mamlaka mbinguni na duniani (Mt.28:18). Mungu ameweka yote chini ya miguu ya Yesu (Efe. 1:22, cf. Wafil. 2:10, 11). Na kwa hiyo Kristo ndiye Bwana wa Mabwana na Mfalme wa Wafalme (Uf.17:14). Kristo pia ni kiongozi wa Kanisa kwa kuwa Kanisa ni mwili wake (Efe.1:23, Kol.1:18). Viungo vya mwili wake ndio washiriki wa Kanisa (Efe.5:30). Wanapaswa kuwa na muunganiko wa karibu kwa kuwa kutokana na Kristo, kanisa hulishwa na kufungamanishwa pamoja (Kol. 2:19).

2. Kristo ndiye chanzo cha mamlaka yote ya Kanisa:

Kristo amedhihirisha mamlaka yake kwa Kanisa kwa (a) kuanzisha kanisa (Mt. 16:18), (b) kuanzisha desturi ambazo kanisa lapaswa kuzisimamia (Mt.26:26-30, Mt. 28:19, 20; 1Kor.11:23-27; Yoh.13:1-17); (c) kuachia kanisa mamlaka ya kutumia Jina lake (Mt.16:19; Mt. 18:15-18Yoh. 20:21-23) (d) Kulipatia Kanisa Roho Mtakatifu aliongoze (Yoh. 15:26; 16:13-15) (e) Kugawa karama ndani ya kanisa yaani mitume, waalimu, manabii na nyinginezo ili kuukamilisha mwili wake (Efe. 4:7-13)

3. Maandiko Matakatifu yana mamlaka ya Kristo:

Pamoja na Kristo kuongoza kanisa kwa Roho Mtakatifu, Maandiko Matakatifu ndicho kiwango pekee cha shughuli za Kanisa. Washiriki wanapaswa kuyatii Maandiko kwa kuwa ndiyo sheria katika uhalisi wake. Desturi, tamaduni, mapokeo yote ya kibinadamu yanapaswa kutiishwa kwa maandiko. (2Tim.3:15-17).

4. Mamlaka ya Kristo na Maofisa wa Kanisa:

Kristo hutumia mamlaka yake kupitia watumishi wake walioteuliwa, lakini kamwe hahamishii kwao mamlaka yake. Hakuna Ofisa wa Kanisa aliye na uhuru wa kutenda apendavyo zaidi ya Kristo na Neno lake.

Maofisa wa Kanisa katika Agano Jipya

Agano Jipya linataja vyeo viwili vya uongozi wa Kanisa – Wazee na Mashemasi. Sifa maalum za kimaadili na za kiroho zimetajwa kwa wanaopaswa kuchaguliwa kushika nafasi hizo. Kanisa linatambua utakatifu wa madaraka ya vyeo hivyo na ndiyo maana huwawekea mikono (Mdo. 6:6; Mdo 13:2, 3; 1Tim.4:14; 5:22)

Wazee wa Kanisa:

(a) Mzee ni nani?

Wazee, kwa kigiriki presbuteros au Maaskofu (episkopos) ndio maofisa wa ngazi ya juu wa Kanisa. Mzee ni kuwa na umri mkubwa ikimaanisha madaraka na heshima. Cheo cha Mzee wa Kanisa kinafananishwa na cha Msimamizi wa Sinagogi. Neno Askofu humaanisha msimamizi. Paulo hutumia Mzee au Askofu kwa kubadilishana akilinganisha wazee na wasimamizi au maaskofu. (Mdo. 20:17, 28; Tit. 1:5, 7). Wazee husimamia Makanisa. Kwa kuwa Mitume nao walijiita Wazee (1Pet. 5:1; 2Yoh.1; 3Yoh.1) hudokeza kwamba walikuwako Wazee wa Kanisa mahalia na wale wanaozuru makanisa kwa ratiba. Aina zote za wazee ni wachungaji wa makutano ya kikanisa.

(b) Sifa za Mzee:

Ili mtu apate sifa za kuwa Mzee lazima asiwe na lawama, mume wa mke moja, mwenye kiasi, tabia njema, ambaye hakuongoka karibuni asije akajikwaa (1Tim.3:1-7; cf. Tit. 1:5-9). Kabla ya kuchaguliwa, mtu anapaswa kuonyesha sifa za uongozi, kwa kusimamia nyumba yake mwenyewe (1Tim. 3:15). Kwa umuhimu wa madaraka ya Uzee, Paulo alionya wasiwekewe mikono upesi (1Tim.5:22).

(c)Majukumu na mamlaka ya Mzee:

Mzee ni kiongozi wa kiroho (Mdo. 20:28). Hujumuisha kuwasaidia walio wanyonge (Mdo. 20:35), akiwaonya wanaopotea (1Thes.5:12), na kuwa chonjo na mafundisho yanayoweza kusambaratisha kundi (20:29-31). Wazee wanapaswa kuishi maisha yanayoweza kuigwa na waumini wengine (Ebr. 13:7; 1Pet.5:3) na kuonyesha mfano wa ukarimu (Mdo. 20:35).

(d)Mtazamo wa waumini kwa Wazee:

Kwa kiwango kikubwa, uongozi wa kanisa hufanikiwa kutokana na utii wa washiriki kwa viongozi. Hivyo waumini wameitwa kuwapa heshima (1Thes. 5:12). Watiini wale ambao wanajitaabisha kwa ajili yenu (Ebr. 13:17 cf. 1Pet.5:5). Wanahimizwa kufuata mwenendo wa kikristo wa viongozi wao (Ebr. 13:7), wakiepuka masengenyo “usikubali mashtaka dhidi ya Mzee ila kwa mashahidi wawili au watatu” (1Tim. 5:19)

Mashemasi wa Kiume na wa Kike:

Neno shemasi kwa kigiriki diakonos humaanisha mtumishi au msaidizi. Mashemasi waliwekwa kusaidia ili mitume wadumu katika sala na huduma ya neno (Mdo. 6:4). Ingawa mashemasi waliwekwa kuangalia ustawi wa washiriki, hawakubaki nyuma kupeleka injili (Mdo. 6:8; 8:5-13, 26-40). Shemasi wa kike anasomeka kwenye Rumi 6:1. Kama walivyo Wazee, Mashemasi nao huchaguliwa kwa kufaa kwao kwa maadili na kiroho (1Tim.3:8-13).

Nidhamu ya Kanisa

Kristo alilipa Kanisa mamlaka ya kusimamia nidhamu. Anatarajia Kanisa kutekeleza misingi ya nidhamu inapobidi ili kudumisha wito mtwa ukuhani wa kifalme na taifa takatifu (Mt.18:15-18; 1Pet. 2:5, 9). Kanisa linawajibika kushughulikia washiriki wake wanaoasi. Kristo analisifu kanisa la Efeso kwa kutochukuliana na wabaya (Uf. 2:2), anayakemea makanisa ya Pergamo na Thiatira kwa kuvumilia uzushi na zinaa (Uf. 2:14, 15, 20).

Kushughulika na makosa binafsi

Mtu moja akimkosea mwenzake, (Mt. 18:15-17), Kristo anashauri aliyekosewa, kumwendea aliyekosa na kushauriana naye abadilike tabia. Akishindwa kuelewana baada ya mashahidi, Kanisa hujulishwa ili kuliangalia jambo husika. Litakalofungwa au kufunguliwa na Kanisa, hukubalika mbinguni (Mt. 18:18).

Kushughulika na makosa ya wazi

Pamoja na kwamba wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu (Rum. 3:23) makosa ya wazi na uasi huliabisha kanisa. Kumwondoa mtu kwenye ushirika huondoa chachu ambayo ingeharibu vyote. (1Kor.5:4, 5, 7) Msichangamane na mzinzi, mwenye kutamani, mwenye kuabudu sanamu, mtukanaji mlevi au mnyang’anyi. Mwondoeni aliye mbaya miongoni mwenu. (1Kor.5:11,13)

Kushughulika na anayejitenga:

Wanaojitenga kwa kufanya fitina na kujikwaza wapaswa kuepukwa (Rum. 16:17). Jitengeni nao, jihadharini msimhesabu kuwa adui ila mwonyeni kama ndugu (2Thes. 3:6, 14, 15). Anayeonywa na kuendelea na msimamo wake hukataliwa (Tit. 3:10, 11).

Kurejesha wakosaji wanaotubu:

Kanisa halipaswi kuwadharau, kuwapuuza au kuwasusia waliotengwa. Juhudi yapaswa kufanywa ili kuwarejesha.(2Kor.2:6-10). Ni katika kuwarejesha wadhambi ndipo uwezo, utukufu na rehema za Mungu hudhihirika. Kwa sasa Kristo kwa njia ya Kanisa anaalika kila mtu aje apate kuwa mwanafamilia (Uf. 3:20).

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Mwanzo 12:3X
3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Matendo 7:38X
38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Waebrania 4:15X
15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
Waebrania 3:8-11X
8 Msifanye migumu mioyo yenu, Kama wakati wa kukasirisha, Siku ya kujaribiwa katika jangwa, 9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arobaini. 10 Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu; 11 Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.
Mathayo 28:19,20X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 16:13-20X
13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani? 14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii. 15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani? 16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. 17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni. 18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. 20 Ndipo alipowakataza sana wanafunzi wake wasimwambie mtu ye yote ya kwamba yeye ndiye Kristo.
Mathayo 18:18X
18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Waefeso 2:19-22X
19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. 22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Waefeso 1:22,23X
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Waefeso 5:23-27X
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. 24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. 25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; 26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; 27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Wakolosai 1:17,18X
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
K. Torati 9:10X
10 Bwana akanipa zile mbao mbili za mawe zimeandikwa kwa kidole cha Mungu; na juu yake yameandikwa maneno mfano wa yote aliyosema nanyi Bwana mle mlimani toka kati ya moto siku ya mkutano.
K. Torati 18:16X
16 Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.
1 Samweli 17:47X
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
1 Wafalme 8:14X
14 Mfalme akageuza uso wake, akawabariki mkutano wote wa Israeli; na mkutano wote wa Israeli wakasimama.
1 M. Nyakati 13:2X
2 Daudi akawaambia jamii yote ya Israeli, Likiwa jema kwenu, tena likiwa limetoka kwa Bwana, Mungu wetu, na tutume watu huku na huku mahali pote kwa ndugu zetu waliosalia katika nchi yote ya Israeli, ambao pamoja nao makuhani na Walawi wamo ndani ya miji yao yenye viunga, ili wakusanyike kwetu;
1 Wakorintho 11:18X
18 Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu nasadiki;
1 Wakorintho 14:19, 28X
19 lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha. 28 Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
1 Wakorintho 16:1X
1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
Wagalatia 1:2X
2 na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia;
1 Wathesalonike 2:14X
14 Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;
1 Wakorintho 16:19X
19 Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao.
Wakolosai 4:15X
15 Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
Filemoni 2X
2 na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.
Matendo 9:31X
31 Basi kanisa likapata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Mathayo 16:18X
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
1 Wakorintho 10:32X
32 Msiwakoseshe Wayahudi wala Wayunani wala kanisa la Mungu,
1 Wakorintho 12:28X
28 Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha.
Waefeso 4:11-16X
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Waefeso 1:20-22X
20 aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; 21 juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia; 22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
Wafilipi 2:9-11X
9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. 11 Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono;
Matendo 20:28X
28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako.
1 Wakorintho 1:2X
2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.
Mathayo 18:17,18X
17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Mwanzo 12:1-3X
1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Matendo 7:38X
38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.
Kutoka 19:6X
6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
K. Torati 28:9X
9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
M. Walawi 26:12X
12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
Isaya 56:7X
7 Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Yohana 19:15X
15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.
Mathayo 21:41,43X
41 Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya; na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake. 43 Kwa sababu hiyo nawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake.
Wagalatia 3:26-29X
26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
Warumi 9:6-8X
6 Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. 7 Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali, Katika Isaka wazao wako wataitwa; 8 yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazao.
Warumi 11:17-25X
17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe. 19 Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi. 20 Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope. 21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe. 22 Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali. 23 Na hao pia, wasipokaa katika kutokuamini kwao, watapandikizwa; kwa kuwa Mungu aweza kuwapandikiza tena. 24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe? 25 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii, ili msijione kuwa wenye akili; ya kwamba kwa sehemu ugumu umewapata Israeli, mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili.
Warumi 11:16-18X
16 Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika. 17 Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake, 18 usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
Mathayo 28:19X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Waefeso 2:16X
16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
1 Wakorintho 12:13X
13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.
Waefeso 1:22, 23X
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo 23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Waefeso 5:30X
30 Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
Wakolosai 1:18X
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Waefeso 5:23X
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
1 Wakorintho 3:9-16X
9 Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu. 10 Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake. 11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. 15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto. 16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Waefeso 2:20X
20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
1 Petro 2:4-6X
4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima. 5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
Waefeso 2:22X
22 Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
1 Wakorintho 3:12-15X
12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. 15 Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto.
1 Wakorintho 3:17X
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
2 Wakorintho 6:14, 16X
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Hosea 2:19X
19 Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
Yeremia 3:14X
14 Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema Bwana; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
Wakolosai 1:18, 22-23X
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 22 katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; 23 mkidumu tu katika ile imani, hali mmewekwa juu ya msingi, mkawa imara; msipogeuzwa na kuliacha tumaini la Injili mliyosikia habari zake, iliyohubiriwa katika viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu; ambayo mimi Paulo nalikuwa mhudumu wake.
Waefeso 5:25X
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
Waefeso 5:26X
26 ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
Yohana 17:17X
17 Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
Waefeso 5:27X
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Zaburi 9:11X
Mwimbieni Bwana akaaye Sayuni, Yatangazeni kati ya watu matendo yake.
Zaburi 14:7X
7 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Zaburi 53:6X
6 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Zaburi 48:2X
2 Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
Wagalatia 4:26X
2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba.
Wafilipi 3:20X
20 Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;
Wagalatia 4:28, 29X
28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi. 29 Lakini kama vile siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomwudhi yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo na sasa.
Wagalatia 5:1X
1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Wagalatia 4:22,26,31X
22 Kwa maana imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. 26 Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. 31 Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
Wagalatia 5:4X
4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.
Wagalatia 5:5, 6X
5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. 6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
Waebrania 12:22, 23X
22 Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, 23 mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika,
Waefeso 3:15X
15 ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa,
Yohana 3:8X
8 Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
Warumi 8:14-16X
14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;
Waefeso 1:4-6X
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Wagalatia 3:26-4:7X

Wagalatia 3:26-29

26 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. 27 Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. 28 Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. 29 Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.

Wagalatia 4:1-7

1 Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, angawa ni bwana wa yote; 2 bali yu chini ya mawakili na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba. 3 Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia. 4 Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, 5 kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana. 6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba. 7 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu.
Waefeso 2:19X
19 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
Wagalatia 6:10X
10 Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.
Wagalatia 4:6X
6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Yakobo 2:15X
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,
1 Wakorintho 8:11X
11 Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
Warumi 16:1X
1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
1 Wakorintho 4:15X
15 Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.
1 Wakorintho 4:4X
4 Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.
Waefeso 5:1X
1 Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa;
Wafilipi 1:5X
5 kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi.
1 Yohana 1:3X
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
1 Wakorintho 1:9X
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
2 Wakorintho 13:14X
14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
1 Yohana 1:3, 7X
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
1 Timotheo 3:15X
15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
Isaya 8:20X
20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
Mithali 11:14X
14 Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.
Mathayo 5:13-15X
13 Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. 15 Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani.
Waefeso 6:12X
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Waefeso 6:13X
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
Matendo 20:29,30X
29 Najua mimi ya kuwa baada ya kuondoka kwangu mbwa-mwitu wakali wataingia kwenu, wasilihurumie kundi; 30 tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawaandamie wao.
1 Timotheo 4:2X
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
Mathayo 13:29, 30X
29 Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo. 30 Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
Ufunuo 12:12, 17X
12 Kwa hiyo shangilieni, enyi mbingu, nanyi mkaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule Ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi, akijua ya kuwa ana wakati mchache tu. 17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Danieli 12:1X
1 Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako; na kutakuwa na wakati wa taabu, mfano wake haukuwapo tangu lilipoanza kuwapo taifa hata wakati uo huo; na wakati huo watu wako wataokolewa; kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.
Mathayo 24:13X
13 Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.
Waefeso 5:27X
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Mathayo 28:18-20X
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Waefeso 5:27X
27 apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Luka 4:18,19X
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
1 Yohana 1:9X
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Warumi 2:14X
14 Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe.
Yohana 4:23X
23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 10:16X
16 Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Waefeso 4:4-16X
4 Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. 5 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6 Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? 10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. 11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Matendo 9:10-22X
10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; 12 naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. 13 Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; 14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. 15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. 16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. 17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18 Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa; 19 akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu. 21 Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewaharibu walioliitia Jina hili huko Yerusalemu? Na hapa alikuwa amekuja kwa kusudi hilo, awafunge na kuwapeleka kwa wakuu wa makuhani? 22 Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.
Ufunuo 14:12X
12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
Ufunuo 18:4X
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Mathayo 24:14X
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
Waefeso 1:4-6X
4 kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5 Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake. 6 Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa.
Ufunuo 12:6, 14X
6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini. 14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
Mathayo 28:18,19X
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
1 Wakorintho 14:33X
33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.
Matendo 2:36-41X
36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.
Matendo 4:10-12X
10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu. 11 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. 12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Yohana 3:3,5X
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. 5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Mathayo 28:18-20X
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. 19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 23:8X
8 Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu.
Mathayo 23:11X
11 Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.
Waebrania 8 - 9X

Waebrania 8

1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. 6 Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. 7 Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la pili. 8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; 9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu. 11 Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, Na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; Kwa maana wote watanijua, Tangu mdogo wao hata mkubwa wao. 12 Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. 13 Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.

Waebrania 9

1 Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia. 2 Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, Patakatifu. 3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu, 4 yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; 5 na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja. 6 Basi, vitu hivi vikiisha kutengenezwa hivyo, makuhani huingia katika hema hiyo ya kwanza daima, wakiyatimiza mambo ya ibada. 7 Lakini katika hema hiyo ya pili kuhani mkuu huingia peke yake, mara moja kila mwaka; wala si pasipo damu, atoayo kwa ajili ya nafsi yake na kwa dhambi za kutokujua za hao watu. 8 Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo hema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama; 9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, 10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya. 11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. 13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; 14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? 15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele. 16 Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. 18 Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. 19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote, 20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na Mungu. 21 Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo. 22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. 23 Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo. 24 Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu; 25 wala si kwamba ajitoe mara nyingi, kama vile kuhani mkuu aingiavyo katika patakatifu kila mwaka kwa damu isiyo yake; 26 kama ni hivyo, ingalimpasa kuteswa mara nyingi tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu; lakini sasa, mara moja tu, katika utimilifu wa nyakati, amefunuliwa, azitangue dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake. 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu; 28 kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi; atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu.
1 Petro 2:5X
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
1 Petro 2:9X
9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Warumi 13:4, 7X
4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu. 7 Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Mathayo 22:21X
21 Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Matendo 5:29X
29 Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Waebrania 10:25X
25 wala tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane; na kuzidi kufanya hivyo, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.
Waebrania 3:13X
13 Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
Wafilipi 1:5X
5 kwa sababu ya ushirika wenu katika kuieneza Injili, tangu siku ile ya kwanza hata leo hivi.
1 Yohana 1:3, 6, 7X
3 hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo. 6 Tukisema ya kwamba twashirikiana naye, tena tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatuifanyi iliyo kweli; 7 bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Mathayo 16:19X
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Luka 11:52X
52 Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Yohana 6:68X
68 Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
2 Wakorintho 2:16X
16 Wakamwambia, Angalia, wako hapa pamoja nasi watumishi wako watu hamsini walio hodari; waende, twakuomba, wamtafute bwana wako; isiwe labda roho ya Bwana imemtwaa na kumtupa juu ya mlima mmoja, au katika bonde moja. Akasema, Msiwatume.
Mathayo 28:19,20X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Mathayo 28:19, 20X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Marko 16:16X
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
Yohana 13:12-14X
12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi.
Luka 22:17-20X
17 Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18 Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. 19 Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.
Mathayo 24:14X
14 Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.
1 Wakorintho 1:7, 8X
7 hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; 8 ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Petro 3:14X
14 Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ili mwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake.
Ufunuo 3:14-22X
14 Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu. 15 Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. 17 Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. 18 Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona. 19 Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu. 20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. 21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi. 22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.
Ufunuo 14:5X
5 Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa.
Ufunuo 14:6-12X
6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
Ufunuo 18:4X
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
Matendo 1:15-26X
15 Siku zile akasimama Petro kati ya hao ndugu (jumla ya majina ilipata mia na ishirini), akasema, 16 Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi, katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu; 17 kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. 18 (Basi mtu huyu alinunua konde kwa ijara ya udhalimu; akaanguka kwa kasi akapasuka matumbo yake yote yakatoka. 19 Ikajulikana na watu wote wakaao Yerusalemu; hata konde lile likaitwa kwa lugha yao Akeldama, maana yake, konde la damu.) 20 Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa, Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; 21 Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, 22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi. 23 Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. 24 Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, 25 ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. 26 Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.
Matendo 6:1-4X
1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku. 2 Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. 3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili; 4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.
Matendo 7 - 8X

Matendo 7

1 Kuhani Mkuu akasema, Je! Mambo hayo ndivyo yalivyo? 2 Naye akasema, Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Ibrahimu, alipokuwa katika Mesopotamia, kabla hajakaa Harani, 3 akamwambia, Toka katika nchi yako na katika jamaa zako, ukaende hata nchi nitakayokuonyesha. 4 Ndipo alipotoka katika nchi ya Wakaldayo, akakaa Harani, akatoka huko baada ya kufa babaye, Mungu akamhamisha mpaka nchi hii mnayokaa ninyi sasa. 5 Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto. 6 Mungu akanena hivi, ya kwamba wazao wake watakuwa wageni katika nchi ya watu wengine, nao watawafanya kuwa watumwa wao, na kuwatenda mabaya kwa muda wa miaka mia nne. 7 Na lile taifa watakaowafanya watumwa nitawahukumu mimi, alisema Mungu; na baada ya hayo watatoka, nao wataniabudu mahali hapa. 8 Akampa agano la tohara; basi Ibrahimu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu. 9 Wale wazee wetu wakimwonea wivu Yusufu, wakamwuza aende Misri. Mungu akawa pamoja naye, 10 akamtoa katika dhiki zake zote, akampa fadhili na hekima mbele ya Farao, mfalme wa Misri; naye akamfanya awe mtawala juu ya Misri na nyumba yake yote. 11 Basi kukawa njaa katika nchi yote ya Misri na Kanaani, na dhiki nyingi, wala baba zetu hawakupata chakula cha kuwatosha. 12 Hata Yakobo aliposikia ya kwamba huko Misri kuna nafaka, akawatuma baba zetu mara ya kwanza. 13 Hata safari ya pili Yusufu akajitambulisha kwa ndugu zake, jamaa ya Yusufu ikawa dhahiri kwa Farao. 14 Yusufu akatuma watu akamwita Yakobo babaye na jamaa zake wote pia, watu sabini na watano. 15 Basi Yakobo akashuka mpaka Misri; akafa yeye na baba zetu; 16 wakachukuliwa mpaka Shekemu wakazikwa katika kaburi lile, ambalo Ibrahimu alilinunua kwa kima cha fedha kwa wana wa Hamori, huko Shekemu. 17 Basi wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu ulipokuwa unakaribia, wale watu wakazidi na kuongezeka sana huko Misri, 18 hata mfalme mwingine akainuka juu ya Misri, asiyemfahamu Yusufu. 19 Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi. 20 Wakati huo akazaliwa Musa, naye alikuwa mzuri sana, akalelewa muda wa miezi mitatu katika nyumba ya babaye. 21 Hata alipotupwa, binti Farao akamtwaa, akamlea awe kama mwanawe. 22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. 23 Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli. 24 Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. 25 Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu. 26 Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana? 27 Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu? 28 Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri jana? 29 Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko. 30 Hata miaka arobaini ilipotimia, malaika wa Bwana akamtokea katika jangwa la mlima wa Sinai katika mwali wa moto, kijitini. 31 Musa alipouona, akastaajabia maono yale, na alipokaribia ili atazame, sauti ya Bwana ikamjia, 32 Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akatetemeka, asithubutu kutazama. 33 Bwana akamwambia, Vua viatu miguuni mwako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu. 34 Yakini nimeona mateso ya watu wangu waliomo Misri, nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka niwatoe. Basi sasa, nitakutuma mpaka Misri. 35 Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti. 36 Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini. 37 Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. 38 Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi. 39 Mtu huyo baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali, na kwa mioyo yao wakarejea Misri, 40 wakamwambia Haruni, Tufanyie miungu, watakaotutangulia; maana huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui lililompata. 41 Wakafanya ndama siku zile, wakaleta dhabihu kwa sanamu ile, wakafurahia kazi za mikono yao. 42 Basi Mungu akaghairi, akawaacha ili waliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Je! Mlinitolea mimi dhabihu na sadaka Miaka arobaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli? 43 Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli. 44 Ile hema ya ushahidi ilikuwa pamoja na baba zetu jangwani, kama alivyoagiza yeye aliyesema na Musa, ya kwamba aifanye sawasawa na mfano ule aliouona; 45 ambayo baba zetu, kwa kupokezana, wakaiingiza pamoja na Yoshua katika milki ya Mataifa wale, ambao Mungu aliwafukuza mbele ya baba zetu, mpaka siku za Daudi; 46 aliyepata fadhili mbele za Mungu, naye aliomba ampatie Mungu wa Yakobo maskani. 47 Lakini Sulemani alimjengea nyumba. 48 Ila Yeye aliye juu hakai katika nyumba zilizofanywa kwa mikono, kama vile asemavyo nabii, 49 Mbingu ni kiti changu cha enzi, Na nchi ni pa kuwekea miguu yangu; Ni nyumba gani mtakayonijengea? Asema Bwana, 50 Au ni mahali gani nitakapostarehe? Si mkono wangu uliofanya haya yote? 51 Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo. 52 Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua; 53 ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike. 54 Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. 55 Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. 56 Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. 57 Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, 58 wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. 59 Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema, Bwana Yesu, pokea roho yangu. 60 Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.

Matendo 8

1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. 2 Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 3 Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. 4 Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno. 5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. 6 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. 7 Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. 8 Ikawa furaha kubwa katika mji ule. 9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. 10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. 14 Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana; 15 ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu; 16 kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu. 17 Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. 18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, 19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu. 20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali. 21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu. 22 Basi, tubia uovu wako huu, ukamwombe Bwana, ili kama yamkini, usamehewe fikira hii ya moyo wako. 23 Kwa maana nakuona u katika uchungu kama nyongo, na tena u katika kifungo cha uovu. 24 Simoni akajibu, akasema, Niombeeni ninyi kwa Bwana, yasinifikilie mambo haya mliyosema hata moja. 25 Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria. 26 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. 27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu. 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.
Matendo 14:23X
23 Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Matendo 15:1-29X
1 Wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. 2 Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. 3 Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. 4 Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. 5 Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa. 6 Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo. 7 Na baada ya hoja nyingi Petro akasimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. 8 Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; 9 wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. 10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. 11 Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao. 12 Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa. 13 Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni. 14 Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. 15 Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa, 16 Baada ya mambo haya nitarejea, Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, Nami nitaisimamisha; 17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana, Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao; 18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele. 19 Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; 20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. 21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi. 22 Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao, 23 Mitume na ndugu wazee, kwa ndugu zetu walioko Antiokia na Shamu na Kilikia, walio wa Mataifa; Salamu. 24 Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbua kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, ambao sisi hatukuwaagiza; 25 sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26 watu waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 27 Basi tumewatuma Yuda na Sila, watakaowaambia wenyewe maneno yayo hayo kwa vinywa vyao. 28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, 29 yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.
Matendo 15:22, 25X
22 Basi ikawapendeza mitume na wazee na kanisa lote kuwachagua watu miongoni mwao na kuwapeleka Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba; nao ni hawa, Yuda aliyeitwa Barsaba, na Sila, waliokuwa watu wakuu katika ndugu. Wakaandika hivi na kupeleka kwa mikono yao, 25 sisi tumeona vema, hali tumepatana kwa moyo mmoja, kuwachagua watu na kuwapeleka kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,
Mathayo 28:18X
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Waefeso 1:22X
22 akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo
Wafilipi 2:10, 11X
10 ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 11 na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
Ufunuo 17:14X
14 Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.
Waefeso 1:23X
23 ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Wakolosai 1:18X
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote.
Wakolosai 2:19X
19 wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu.
Mathayo 16:18X
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 26:26-30X
26 Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu 27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu. 30 Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.
Mathayo 28:19, 20X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; 20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
1 Wakorintho 11:23-27X
23 Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 25 Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. 26 Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. 27 Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.
Yohana 13:1-17X
1 Basi, kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu, hali akijua ya kuwa saa yake imefika, atakayotoka katika ulimwengu kwenda kwa Baba, naye ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo. 2 Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, moyo wa kumsaliti; 3 Yesu, hali akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu, 4 aliondoka chakulani; akaweka kando mavazi yake, akatwaa kitambaa, akajifunga kiunoni. 5 Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. 6 Hivyo yuaja kwa Simoni Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? 7 Yesu akajibu, akamwambia, Nifanyalo wewe hujui sasa; lakini utalifahamu baadaye. 8 Petro akamwambia, Wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, Kama nisipokutawadha, huna shirika nami. 9 Simoni Petro akamwambia, Bwana, si miguu yangu tu, hata na mikono yangu na kichwa changu pia. 10 Yesu akamwambia, Yeye aliyekwisha kuoga hana haja ila ya kutawadha miguu, bali yu safi mwili wote; nanyi mmekuwa safi, lakini si nyote. 11 Kwa maana alimjua yeye atakayemsaliti; ndiyo maana alisema, Si nyote mlio safi. 12 Basi alipokwisha kuwatawadha miguu, na kuyatwaa mavazi yake, na kuketi tena, akawaambia, Je! Mmeelewa na hayo niliyowatendea? 13 Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. 14 Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi. 15 Kwa kuwa nimewapa kielelezo; ili kama mimi nilivyowatendea, nanyi mtende vivyo. 16 Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. 17 Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda.
Mathayo 16:19X
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Mathayo 18:15-18X
15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Yohana 20:21-23X
21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23 Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.
Yohana 15:26X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Yohana 16:13-15X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
Waefeso 4:7-13X
7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8 Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. 9 Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? 10 Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. 11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;
2 Timotheo 3:15-17X
15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.
Matendo 6:6X
6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.
Matendo 13:2, 3X
2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.
1 Tmotheo 4:14X
14 Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee.
1 Timotheo 5:22X
22 Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.
Matendo 20:17, 28X
17 Toka Mileto Paulo akatuma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. 28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Tito 1:5, 7X
5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; 7 Maana imempasa askofu awe mtu asiyeshitakiwa neno ,kwa kuwa ni wakili wa MUNGU;asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake,asiwe mwepesi wa hasira,asiwe mlevi wala mgomvi,asiwe mpenda mapato ya aibu.
1 Petro 5:1X
1 Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye;
2 Yohana1:1X
1 Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli;
3 Yohana 1:1X
1 Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
1 Timotheo 3:1-7X
1 Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. 2 Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; 3 si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; 4 mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) 6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 7 Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.
Tito 1:5-9X
5 Walakini mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. 6 Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili; 7 wapenda kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti. 8 Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali; 9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu wa haki, bali waasi, na wasio wataratibu, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
1 Timotheo 3:15X
15 Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
1 Timotheo 5:22X
22 Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.
Matendo 20:28X
28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Matendo 20:35X
35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
1 Wathesalonike 5:12X
12 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;
Waebrania 13:7X
7 Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
1 Petro 5:3X
3 Wala si kama wajifanyao mabwana juu ya mitaa yao, bali kwa kujifanya vielelezo kwa lile kundi.
Matendo 20:35X
35 Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea.
1 Wathesalonike 5:12X
12 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;
Waebrania 13:17X
17 Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi.
1 Petro 5:5X
5 Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Waebrania 13:7X
7 Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao.
1 Timotheo 5:19X
19 Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.
Matendo 6:4X
4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.
Matendo 6:8X
8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.
Matendo 8:5-13, 26-40X
5 Filipo akatelemka akaingia mji wa Samaria, akawahubiri Kristo. 6 Na makutano kwa nia moja wakasikiliza maneno yale yaliyosemwa na Filipo walipoyasikia na kuziona ishara alizokuwa akizifanya. 7 Kwa maana pepo wachafu wakawatoka wengi waliopagawa nao, wakilia kwa sauti kuu; na watu wengi waliopooza, na viwete, wakaponywa. 8 Ikawa furaha kubwa katika mji ule. 9 Na mtu mmoja, jina lake Simoni, hapo kwanza alikuwa akifanya uchawi katika mji ule, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa. 10 Wote wakamsikiliza tangu mdogo hata mkubwa, wakisema, Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu. 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mwingi kwa uchawi wake. 12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. 13 Na yeye Simoni mwenyewe aliamini akabatizwa, akashikamana na Filipo; akashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendeka. 26 Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. 27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu. 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.
Warumi 6:1X
1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
1 Timotheo 3:8-13X
8 Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu. 9 wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. 10 Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. 11 Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. 12 Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. 13 Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
Mathayo 18:15-18X
15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. 18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
1 Petro 2:5, 9X
5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
Ufunuo 2:2X
2 Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo;
Ufunuo 2:14, 15, 20X
14 Lakini ninayo maneno machache juu yako, kwa kuwa unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki atie ukwazo mbele ya Waisraeli, kwamba wavile vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na kuzini. 15 Vivyo hivyo wewe nawe unao watu wayashikao mafundisho ya Wanikolai vile vile. 20 Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.
Mathayo 18:15-17X
15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. 16 La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. 17 Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Mathayo 18:18X
18 Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Warumi 3:23X
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
1 Wakorintho 5:4, 5, 7X
4 Katika jina la Bwana wetu Yesu, ninyi mkiwa mmekusanyika pamoja na roho yangu, pamoja na uweza wa Bwana wetu Yesu; 5 kumtolea Shetani mtu huyo, ili mwili uadhibiwe, ili na roho iokolewe katika siku ya Bwana Yesu. 7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;
1 Wakorintho 5:11,13X
11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang'anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye. 13 Lakini hao walio nje Mungu atawahukumu. Ninyi mwondoeni yule mbaya miongoni mwenu.
Warumi 16:17X
17 Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao.
2 Wathesalonike 3:6, 14, 15X
6 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu. 14 Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari; 15 lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Tito 3:10, 11X
10 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; 11 ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
2 Wakorintho 2:6-10X
6 Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; 7 hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. 8 Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. 9 Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. 10 Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo,
Ufunuo 3:20X
20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.