Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yake ana kutokufa, atawapa waliokombolewa wake uzima wa milele. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya kutojifahamu kwa watu wote. Wakati Kristo, ambaye ni uzima wetu, atakapoonekana, wenye hai waliofufuliwa na wenye haki walio hai watabadilishwa na kupewa miili ya utukufu na hivyo kunyakuliwa kwa pamoja na kumlaki Bwana wao. Ufufuo wa pili, ambao ni ufufuo wa waovu, utatokea mika elfu moja baadaye.” (Rum.6:23;1Tim.6:15, 16;Mhu.9:5, 6;Zab.146:3, 4;Yoh.11:11-14;Kol.3:4;1Kor.15:51-54;1Thes.4:13-17;Yoh.5:28, 29Ufu.20:1-10)
Jeshi la Wafilisti liliingia Shunem, likaweka kambi na kujiandaa kuipiga Israel. Hali yake ikiwa mbali na ushindi, Mfalme Sauli alipanga Jeshi lake kwenye Mlima Gilboa. Wakati uliopita, uhakika wa uwepo wa Mungu ulimwezesha Sauli kuongoza Israeli dhidi ya maadui yake pasipo hofu. Bali aligeuka akaacha kumtumikia BWANA, na Mfalme mwasi alipojaribu kuulizia kwa BWANA juu ya matokeo ya vita, Mungu alikataa kuwasiliana naye.
Hofu korofi ya matokeo ya vita yasiyojulikana ilimwelemea Sauli kwa uzito. Kama Samweli angekuwako hapa. Lakini Samweli alikuwa amekufa na asingeweza kumshauri. Au angeweza? Akitambua aliko mchawi aliyeokoka katika misako yake iliyopita, Mfalme mrefu aliinama kuulizia matokeo ya vita itakayopiganwa kesho. Aliomba, “Nipandishie Samweli.” Katika tukio hilo, mwanamke aliona “roho akipanda kutoka kwenye nchi”. Huyu ‘roho’ alimwambia Mfalme mwovu kuwa siyo tu Israeli watashindwa vita ila pia, yeye na mwanae watakufa vitani. (1Samweli 28).
Utabiri uliotolewa ulitimia. Je, hivi ni kweli roho ya Samweli ndiyo iliyotoa unabii? Inawezekanaje, mchawi anayelaumiwa na Mungu awe na nguvu kwenye ‘roho’ ya Samweli – nabii wa Mungu? Ni wapi Samweli alikotokea, katika nchi? Kifo kilikuwa kimemtendea nini Samweli? Kama siyo roho ya Samweli iliyoongea na Sauli, ni nani basi? Hebu tutazame jinsi Biblia inavyofundisha juu ya kifo, kuwasiliana na wafu na ufufuo.
Hali ya Kutokufa na Mauti (Kifo)
Kutokufa ni hali au ubora wa kutofikiwa na kifo. Watafsiri wa Maandiko walitumia neno kutokufa kutafsiri neno la Kigiriki athanasia “kutokufikwa na kifo – deathlessness” aphtharsia “kutokuharibika”. Je, mambo haya yanahusika vipi na mwanadamu?
Kutokufa.
Maandiko Matakatifu hufunua kwamba Mungu wa milele ana hali ya kutokufa. (1Tim.1:17). Kwa kweli, Yeye peke yake ana hali ya kutokufa. (1Tim.6:16). Hakuumbwa, anaishi mwenyewe pasipo kuwezeshwa na hana mwanzo wala mwisho. (Angalia somo la Utatu Mtakatifu).
Hakuna mahali popote katika Maandiko ambako kutokufa inatajwa kuwa hali ambayo mwanadamu anayo, au nafsi yake, au roho yake inayo. Maneno nafsi na roho hupatikana kwenye Biblia zaidi ya mara 1600 na kote hakuna ambako maneno husika yameambatana na hali ya kutokufa au kutokuharibika. (Angalia somo la Mwanadamu na Asili Yake).
Tofauti na Mungu, mwanadamu ana hali ya kufa. Maandiko hulinganisha hali hiyo na “mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. (Yak.4:14). Ni ‘kiwiliwili, upepo upitao wala haurudi.” (Zab.78:39). Mwanadamu “huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe. (Ayu.14:2). Mungu na mwanadamu hutofautiana sana. Mungu hana mwisho, mwanadamu ana ukomo. Mungu hapatikani na mauti, mwanadamu hufa. Mungu ni wa milele, mwanadamu ni wa kupita.
Hali ya Kutokufa yenye Masharti
Katika Uumbaji, Mungu alimfanya “mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai.” (Mwa.2:7). Habari ya uumbaji hudhihirisha kuwa mwanadamu alipata uhai wake kutoka kwa Mungu.(cf. Mdo.17:25, 28;Kol.1:16,17). Ukweli unaoonekana kwa maelezo haya ni kwamba kutokufa yaani uzima wa milele siyo hali aliyo nayo mwanadamu bali ni karama ya Mungu. (Rum.6:23).
Mungu alipowaumba Adamu na Hawa, aliwapa uhuru wa kuchagua. Wangeweza kuchagua kutii au kutokutii, lakini kuendelea kuwa hai, kulitegemea utii unaoendelea kupitia uwezo wa Mungu. Kwa hiyo, kuwa kwao na kutokufa (uzima wa milele), kulitegemea kutimiza masharti. Mungu kwa uangalifu mkubwa, alitaja masharti husika. “Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakayokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” (Mwa.2:17).
Mauti (Kifo) Mshahara wa Dhambi.
Akipinga onyo la Mungu kwamba kutokutii kutaleta kifo, Shetani alidai “Hakika hamtakufa.” (Mwa. 3:4). Lakini baada ya kutokutii, Adamu na Hawa waligundua kuwa mshahara wa dhambi kwa uhalisi ni “mauti” (Rum.6:23). Hukumu yao ilibeba maneno haya: “kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”(Mwa.3:19).
Baada ya hukumu, Mungu alizuilia wanandoa wenye dhambi wasiufikie Mti wa Uzima wasije wakala matunda yake na kuishi milele. (Mwa.3:22). Kitendo chake kiliweka wazi kwamba kutokufa ambako kuliahidiwa kutokana na utii kulipotea kwa sababu ya dhambi. Sasa wamekuwa watu wenye hali ya kufa, na kwamba watakufa. Kwa sababu Adamu asingeweza kurithisha uzao wake hali ambayo hana, “hivyo mauti ikawafikia watu wote, kwa sababu wote wamefanya dhambi.” (Rum.5:12).
Ni rehema ya Mungu tu ndiyo iliyowafanya Adamu na Hawa wasife mara moja baada ya dhambi. Mwana wa Mungu alikuwa amejitolea kutoa uhai wake ili kwamba mwanadamu awe na fursa nyingine. Yeye ni “Mwanakondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.“ (Uf. 13:8).
Tumaini kwa Mwanadamu
Pamoja na kwamba wanadamu huzaliwa wakiwa na hali ya kufa, Biblia huhimiza watafute kutokufa. (Angalia kwa mfano (Rum. 2:7). Yesu Kristo ndiye chanzo cha kutokufa. “Bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Rum. 6:23 cf. 1Yoh. 5:11). Kristo Yesu alibatili mauti na kufunua uzima na kutokuharibika. (2Tim.1:10).”Kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.” (1Kor.15:22). Kristo mwenyewe alisema sauti yake itafungua makaburi na kufufua wafu. (Yoh.5:28, 29).
Kama Kristo asingelikuja, hali ya mwanadamu ingekosa matumaini na waliokufa wangepotea milele. (Yoh.3:16). Kwa hiyo, imani kwa Kristo siyo tu inamwepushia mwanadamu adhabu ya kifo ila pia inampatia zawadi yenye thamani kuu ya kutokufa.
Kristo alituletea kutokufa kupitia nuru ya injili. (2Tim.1:10). Paulo anathibitisha kwamba Maandiko Matakatifu yaweza kutuhekimisha hata kupata uzima wa milele. (2Tim.3:15). Wanaoikataa injili, hawatapokea kutokufa.
Kupokea kutokufa
Wakati wa kupokea kutokufa umesimuliwa na Paulo. “Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatulala sote, lakini sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.” (1Kor.15:51-54). Hii huweka wazi kuwa Mungu hatatupatii kutokufa wakati tunapokufa, badala yake atatupatia kutokufa wakati parapanda itakapolia, ndipo mwili wa kufa, utapovaa kutokufa. Ni kweli Yohana husema kwamba tunapompokea Yesu tunapata uzima wa milele (1Yoh.5:11-13). Utimilifu wa kupokea uzima wa milele utatokea siku Yesu akirejea mara ya pili. Hapo ndipo tutabadilishwa kutoka wa kufa kuwa wa kutokufa na wa kuharibika kuwa wa kutokuharibika.
Asili ya Mauti (Kifo)
Ikiwa mauti ni kukoma kuwa uhai (uzima), Biblia inasemaje kuhusu hali ya mtu aliyekufa? Kuna umuhimu gani kwa wakristo kufahamu jambo hili?
Mauti (Kifo) ni usingizi
Mauti (kifo) siyo maangamizi kamili bali ni hali ya kutokuwa na fahamu kwa muda wakati mtu anasubiri ufufuo. Biblia kwa kurudia rudia huiita hali hiyo usingizi.
Likielezea vifo vya wafalme wa Israeli, Agano la Kale linasema kifo cha Daudi, Sulemani, na wafalme wengine na Yuda kuwa wamelala na baba zao. (1Fal.2:10; 11:43; 14:20, 31; 15:8;2Nyak.21:1; 26:23); n.k. Ayubu alikiita kifo usingizi (Ayu. 14:10-12), kama Daudi (Zab.13:3) Yeremia (Yer.51:39, 57) na Danieli (Dan. 12:2).Agano Jipya hutumia msemo huo pia. Akielezea hali ya binti Yairo ambaye alikuwa amekufa, Kristo alisema kuwa amelala (Mt.9:24;Mk.5:39). Alimwelezea Lazaro aliyekufa kwa namna hiyo hiyo (Yoh.11:11-14). Mathayo aliandika, “ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala” (Mt.27:52) wakitoka makaburini mwao baada ya kufufuka (Mt.27:53). Akielezea kuuawa Stefano, Luka aliandika akisha kusema haya, “akalala”. (Matendo.7:60). Paulo na Petro pia walikiita kifo usingizi. (1Kor. 15:51,52;1Thes.4:13-17;2Pet.3:4).
Kwa nini usingizi ni kielelezo kizuri kuelezea kifo?
Maelezo ya Biblia kama usingizi yanafaa kwa asili yake kwa kuwa kuna kufanana kwa kifo na usingizi.
1. Waliolala hawana ufahamu. “lakini wafu hawajui neno lolote” (Mh.9:5).
2. Katika usingizi, hakuna kufikiri. “Pumzi yake hutoka… siku hiyo mawazo yake yapotea” (Zab.146:4)
3. Usingizi huwa ukomo wa kazi za siku. “kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe” (Mhu. 9:10).
4. Usingizi hututenga na walio macho na matendo yao. “Wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua.” (Mhu.9:6).
5. Usingizi wa kawaida hufanya hisia kutokutenda kazi. “Mapenzi yao, na machukio yao, na husuda yao imepoa yote pamoja. (Mhu.9:6).
6. Kwenye usingizi, watu hawawezi kumsifu BWANA. “Sio wafu wamsifuo BWANA, wala wowote washukao kwenye kimya.”
7. Usingizi hutangulia kabla ya kuamka. “”saa yaja ambayo waliomo makaburini wataisikia sauti yake; nao watatoka."(Yoh. 5:28,29)
Mtu kurudi Mavumbini
Kuelewa kinachotokea mtu akifa, twapaswa kuelewa kinachomfanya binadamu. (Angalia somo la Mwanadamu na Asili yake). Kwenye uumbaji wa mwanadamu, mwungano wa mavumbi ya ardhi (udongo) na pumzi ya uhai vilimfanya nafsi hai (Mwa.2:7). Katika kifo, kinyume chake hutokea: mavumbi ya ardhi yakiondolewa pumzi ya huai hufanya mfu asiye na ufahamu (Zab.146:4). Yaliyomtengeneza mwanadamu hurudi yalikotoka. (Mwa.3:19). Roho haina uhai nje ya mwili, wala hakuna andiko linalodokeza kuwa katika mauti nafsi (ambayo huitwa roho) huishi kama kitu hai. Kwa ukweli, “roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa.” (Eze.18:20).
Wafu wako wapi?
Agano la Kale linapaita mahali walipo wafu kuwa ni sheol (Kiebrania) na Agano Jipya hades (Kigiriki). Katika Maandiko, maana rahisi ya sheol (kuzimu) ni kaburi. Maana ya hades ni sawa na maana ya sheol.
Wafu wote huenda mahali hapo. (Zab.89:48), wema kwa waovu. Yakobo alisema atamshukia mwanawe hata kuzimu (Mwa.37:35). Ardhi ilipofunguka, iliwameza Kora pamoja na wenzake hadi kwenye sheol (Hes.16:30). Sheol hupokea mtu mzima. Kristo alipokufa, alizikwa kaburini (hades) lakini katika Ufufuo, nafsi yake iliacha kaburi hades (Mdo.2:27,31) au sheol. (Zab.16:10). Daudi alipomshukuru Mungu kwa uponyaji, anashuhudia kuwa aliokolewa kutoka kwenye sheol (kuzimu/kaburi). Kaburi siyo mahali pa ufahamu. Kwa kuwa kifo / mauti ni usingizi, wafu watabaki pasipo kuwa na ufahamu hadi hades (kuzimu) kutakapotoa wafu wake. (Uf.20:13).
Roho kumrudia Mungu
Ijapokuwa mwili hurudi udongoni, roho humrudia Mungu. (Mh.12:7). Hili ni jambo linalotokea kwa wote, wema kwa waovu. Wengi wamedhani kwamba fungu hili la Biblia huhakikisha kwamba kipo kipengele ndani ya mwanadamu kinachoendelea kuishi baada ya kufariki. Lakini katika Biblia, neno roho (Kwa Kiebrania ruach au Kigiriki pneuma), haimaanishi kitu kizima chenye akili kinachoweza kuishi peke yake pasipo mwili. (Angalia somo la Mwanadamu na Asili yake). Kufuatana na Sulemani, katika kifo, hakuna tofauti ya roho za wanyama na za wanadamu, wote huenda pamoja. (Mh.3:19-21). Anachomaanisha kuwa kinamrudia Mungu ni ile kanuni, cheche ya uhai. (Mwa.2:7).
Kupatana kwa Maandiko
Watu waaminifu ambao hawajajifunza kwa makini Biblia, hawajafahamu kwamba kifo ni usingizi hadi mtu atakapofufuliwa. Wanadhani kwamba yako mafungu yanayohakikisha wazo la mtu kuwa na hali nyingine ya uhai. Kujifunza kwa makini huhitimisha kwamba kifo hufanya kukoma kwa ufahamu (uhai).
Imani ya Kuongea na Wafu (Spritualism)
Ikiwa wafu hawana ufahamu, je, wanaongea na wafu huwa wanaongea na nani? Kila aliye mwaminifu atakubali kwamba baadhi ya matukio yanayodaiwa kwamba wafu wanaongea, ni ya hila. Lakini mengine hayana maelezo. Kuna nguvu zinazopita nguvu za asili isiyo ya kawaida iliyoungana na imani ya kuongea na wafu. Biblia hutufundisha nini kuhusiana na jambo hili?
1. Msingi wa Imani ya Kuongea na Mizimu (Wafu)
Imani ya kuongea na wafu imeanzia kwenye uongo wa awali wa Shetani kwa Hawa. “Hakika hamtakufa” (Mwa.3:4). Maneno hayo yalikuwa hubiri la kwanza juu ya kutokufa kwa roho (nafsi). Katika ulimwengu wa leo, ziko jamii nyingi za kidini zinazorudia kosa hilo. Kwa wengi, ile hukumu kwamba roho itendayo dhambi itakufa (Eze.18:20) imebadilishwa na kuwa “roho hata ikitenda dhambi itaendelea kuishi milele.”
Imani ya kwamba watu waliokufa wana fahamu, imewaandaa Wakristo wengi kukubali imani ya kuongea na mizimu. Kwa kutumia uwongo huo, Shetani na malaika zake (Ufu.12:4, 9) wameanzisha namna ya mawasiliano na wafu. Wakati mwingine hutoa utabiri, na utabiri huo unapotimia, huanza kuaminika kwenye jamii. Ndipo uwongo wake unapohesabika ni jambo la hakika hata kama unapingana na Biblia au Sheria ya Mungu. Kwa kuondosha kizuizi cha uovu, Shetani anao utawala huru unaoongoza wanadamu mbali na Mungu na kwenye uharibifu wa hakika.
2. Onyo dhidi ya Imani ya Kuongea na Mizimu
Hakuna moja apaswaye kudanganywa na imani ya kuongea na wafu. Biblia kwa uwazi hufunua kwamba madai yake ni uwongo. Kama tunavyojua, tayari Biblia inatuambia kwamba wafu hawajui lolote na kwamba wako makaburini pasipo na ufahamu.
Biblia pia hukataza jaribio lolote la kuwasiliana na wafu au roho za kidunia. Husema wote ambao hudai kuwasiliana na wafu kwa uhalisi huwa wanawasiliana na pepo wachafu au roho za mashetani. Bwana asema vitendo hivyo ni machukizo na wowote ambao wangehusika navyo walipaswa kuadhibiwa kifo.(Law.19:31; 20:27 cf.Kumb.18:10,11). Isaya anaelezea vema upumbavu wa imani ya kuongea na wafu. “Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao pana asubuhi”. (Isa.8:19, 20). Kwa hakika, ni mafundisho ya Biblia tu ndiyo yatakalinda Waksristo dhidi ya uwongo huu wa kutisha.
3. Matukio Yanayojitokeza ya Imani ya Kuongea na Wafu
Biblia inayo kumbukumbu za imani ya kuongea na wafu – kutokea kwa wachawi wa Farao na wachawi, waganga na wasihiri wa Ninawi na Babeli na wachawi na waaguzi wa Israeli na kuwahukumu wote hao. Biblia inasema: “Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.” (1Sam.28:6). Kwa hiyo, Mungu hakuwa na sehemu ya kilichotokea Endori. Sauli alidanganywa na pepo lililojifanya nabii Samweli; kamwe hakumwona Samweli halisi. Alichoona mchawi kilikuwa umbo la mzee wakati Sauli alihihesabu na kuhitimisha kwamba ni Samweli. (1Sam.28:14).
Ikiwa tutaamini kwamba kilichoonekana ni Samweli, lazima tujiandae kuamini kwamba wachawi, wasihiri, waganga, wanajimu, wapiga bao wanaweza kuwaita watakatifu waliokufa popote walipo baada ya kufa. Pia lazima tuamini kwamba Samweli wa Mungu aliishi akiwa na ufahamu ndani ya nchi, kwa sababu mwanaume mzee aliinuka “kutoka kwenye nchi.” (fungu la (13,).
Mazungumzo yaliyofanyika yalimkatisha tama Sauli wala hayakumpa tumaini. Siku iliyofuata, alijiua. (1Sam.28:19). Kama angekuwa sahihi, tungehitimisha kwamba baada ya kufa, Sauli mkaidi na Samweli mwenye haki waliishi pamoja. Badala yake inatulazimu kuhitimisha kwamba malaika mwovu alileta matukio ya kudanganya katika mazingira haya.
4. Udanganyifu wa mwisho
Wakati uliopita, matukio yaliyojitokeza ya Imani ya Kuongea na Wafu yalijibana kwenye ulimwengu wa uchawi, lakini siku hizi, imaini ya kuongea na wafu inabeba taswira ya “Kikristo” ili idanganye ulimwengu wa kikristo. Kwa kukiri kumkubali Yesu na Biblia, Imani ya Kuongea na Wafu (mizimu) imekuwa adui wa hatari kwa waumini.Matokeo yake ni ya pole pole na yanadanganya. Kupitia imani hiyo, Biblia hutafsiriwa kwa namna ambayo hupendeza moyo usiofanywa upya, wakati maonyo na ukweli muhimu yakifanywa hayana athari yoyote. Upendo unakuwa tabia kuu ya Mungu, lakini huhafifishwa kwa mambo ya hisia, ikiwekwa tofauti ndogo baina ya mema na mabaya. Hukumu ya Mungu, chuki yake kwa dhambi, madai ya sheria yake takatifu yanaepukwa. Watu wanafundishwa kutazama amri kumi kama iliyo ya maana. Hadithi za kichawi chawi, huteka fikra na kuwangoza watu kuikataa Biblia kama msingi wa imani yao.
Kupitia njia hiyo, mema na mabaya yanafanywa kuhusiana, na kila mtu au hali, au utamaduni unakuwa kanuni ambayo ni kanuni ya kuishi kwayo ya kile kinachohesabika kuwa ni “kweli.” Kwa uhalisi, kila mtu anakuwa mungu, akitimiza ahadi ya Shetani kwamba “mtakuwa kama miungu” (Mwa.3:5.
Mbele yetu iko “saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.” (Ufu.3:10). Karibu, Shetani atatumia miujiza mikubwa na maajabu katika juhudi yake ya mwisho kuudanganya ulimwengu. Akizungumzia jambo hili, nabii Yohana anasema “Naliona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uwongo. Hizo ndizo roho za mashetani zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu.” (Ufu.16:13, 14 cf. 13:13, 14).
Ni wale tu wanaolindwa na uwezo wa Mungu, mawazo yao yakijikita kwenye kweli ya Maandiko Matakatifu, wakiyakubali kwamba ndiyo mamlaka pekee, wataweza kuokoka. Wengine wote hawana ulinzi nao watazolewa na uwongo huu.
Mauti ya Kwanza na Mauti ya Pili
Mauti ya pili ni adhabu ya mwisho ya wenye dhambi wasiotubu – wote ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima - itakayotolewa baada ya miaka 1,000 (Angalia somo la Miaka Elfu). Kwa mauti ya pili hakuna ufufuo. Kwa maangamizi ya Shetani na wasio haki, dhambi inaondoshwa, na kifo chenyewe kinaharibiwa.(1Kor.15:26;Ufu.20:14; 21:8). Kristo ametuhakikishia kwamba “yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. (Ufu.2:11). Kwa msingi wa Maandiko kwamba mauti ya pili ni adhabu kwa dhambi, twaweza kuhesabu kwamba mauti ya kwanza ni ile impatayo kila mwanadamu isipokuwa wale ambao watakuja kubadilishwa siku Yesu akirudi, uzoefu tulioupokea kutoka uasi wa Adamu. Ni kawaida inayotokana na kuendelea kuharibika kwa sababu ya dhambi.
Ufufuo
Ufufuo ni kurejeshewa uhai, pamoja na ukamilifu wa kuwapo na nafsi, baada ya kufa. Kwa kuwa wanadamu hupatwa na mauti, lazima uwepo ufufuo ikiwa watakuwa na uhazi baada ya kaburi. Kwenye Agano la Kale na Agano Jipya, wajumbe wa Mungu walieleza tumaini lao kwa ufufuo. (Ayu.14:13-15; 19:25-29;Zab.49:15; 73:24;Isa.26:19; 1Kor.15). Tumaini la ufufuo ambalo tunao ushahidi wake wa kutosha, hututia shime kutazamia maisha bora ng’ambo ya ulimwengu wa sasa, ambako sote twakabiliwa na kifo.
Ufufuo wa Kristo
Ufufuo wa wenye haki waliokufa kuvaa kutokufa unafanana kwa karibu na ufufo wa Kristo, kwa sababu ni Kristo aliyefufuka ndiye hatimaye atafufua wafu. (Yoh.5:28, 29).
1. Umuhimu wake
Nini kingetokea ikiwa Kristo asingekuwa amefufuka? Paulo anafanya mhutasari wa matokeo: a. kusingekuwa na maana kuihubiri injili. ”tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure.” B. Kusingekuwa na msamaha wa dhambi: “na kama Kristo hakufufuka…mngalimo katika dhambi zenu. (1 Wakorintho 15:17). c. Kusingekuwa na maana kumwamini Yesu. “Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure.” d. Kusingekuwa na kufufuliwa wafu. “Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema hakuna kiyama ya wafu?” (fungu la 12). e. Kusingekuwa na tumaini ng’ambo ya kaburi. “Ikiwa Kristo hakufufuka…na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.” (1kor.15:17, 18).
2. Ufufuo wa mwili
Kristo aliyetoka kaburini alikuwa Yesu yuleyule aliyeishi hapa katika mwili. Sasa ana mwili uliovikwa utukufu, lakini bado ni mwili ule ule. Ulikuwa mwili halisi kiasi ambacho wengine hawakuona tofauti.(Luk.24:13-27;Yoh.20:14-18). Yesu mwenyewe alikana kwamba siyo roho au pepo. Akiongea na wanafunzi wake, alisema: “Tazameni mkono yangu na miguu yangu, ya kuwa mimi ni mwenyewe” (Luk.24:39). Kuthibitisha kwamba ana umbo halisi baada ya kufufuka, pia alikula pamoja nao. (fungu la 43).
3. Athari yake
Ufufuo ulikuwa na athari ya kuwasisimua wanafunzi. Ulibadili kikundi cha watu wanyonge na waoga kuwa mitume mashujaa wakiwa tayari kufanya lolote kwa ajili ya Bwana wao. (Fil.3:10,11; Mdo. 4:33). Utume walioufanya yakiwa matokeo ya ufufuo, ulitikisa dola ya Rumi na ukapindua ulimwengu. (Mdo.17:6).
Ilikuwa ni uhakika wa kufufuka kwa Kristo ndio ulioleta hoja na uwezo wa kuhubiri injili. (cf. Fil.3:10, 11). Petro anazungumzia ufufuo wa Yesu kuwa ulileta tumaini la uzima (1Pet.1:3). Mitume walijihesabu kwamba wamewekwa wakfu kuhubiri ufufuo. (Mdo.1:22), na mahubiri yao yalikuwa kwenye msingi kuwa ufufuo wa Yesu wa Masihi ulitabiriwa (Mdo.2:31). Ilikuwa ufahamu wao binafsi kuhusu ufufuo kulikowapa uwezo wa kushuhudia kwa nguvu kufufuka kwa Yesu. (Mdo.4:33). Mitume walivutia upinzani wa Viongozi wa Kiyahudi walipofundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu. (Mdo.4:2). Aliposhtakiwa mbele ya Baraza la Wayahudi (Sanhedrin), Paulo alipaza sauti kwamba ni kwa sababu ya tumaini lake la ufufuo wa wafu kwamba anahukumiwa. (Mdo.23:6; cf. 24:21). Kwa Warumi, Paulo aliandika kamba Yesu Kristo ali “dhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu … kwa ufufuo wa wafu.” (Rum.1:4). Kwenye ubatizo, alieleza Mkristo anakiri imani yake katika ufufuo wa Kristo. (Rum.6:4, 5).
Fufuo Mbili
Kristo alifundisha kwamba kwa ujumla ziko fufuo mbili: “ufufuo wa uzima” kwa wenye haki na “ufufuo wa hukumu” kwa wasio haki. (Yoh.5:28, 29;Mdo. 24:15). Miaka 1,000 inatenganisha fufuo mbili hizi. (Ufu.20:4, 5).
1. Ufufuo wa uzima
Wanaofufuliwa kwenye ufufo wa kwanza wameitwa “heri na mtakatifu” (Ufu.20:6). Hawatapata mauti ya pili katika ziwa la moto mwisho wa miaka 1,000. (Ufu.20:14). Ufufuo wa uzima na kutokufa (Yoh.5:29;1Kor.15:52,53) utafanyika Yesu akija mara ya pili. (1Kor.15:22,23; 1Thes.4:15-18). Wale watakaopata ufufuo huu hawatakufa tena. (Luk.20:36). Wataungana na Kristo milele.
Mwili uliofufuliwa utakuwaje? Kama Kristo mfufuka alivyokuwa, watakatifu watakuwa na miili halisi. Na kama Kristo alivyofufuka, mwenye utukufu, ndivyo watakatifu watakavyokuwa. Paulo alisema kwamba Kristo ataubadili “mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu.” (Filp. 3:21). Anauita mwili wa sasa kuwa usio na utukufu na wa kuharibika na ule wa ufufuo kuwa mwili wenye utukufu na mwili wa kiroho; wa kwanza kuwa wenye kufa na kuharibika na wa pili usiokufa wala usioharibika. Badiliko kutoka kufa kwenda kutokufa litafanyika kwa kufumba na kufumbua katika ufufuo. (1Kor.15:42-54).
2. Ufufuo wa hukumu
Wasio haki watafufuliwa kwenye ufufuo wa kiujumla wa pili, utakaofanyika baada ya miaka1,000. (Angalia somo la Miaka 1,000). Ufufuo huu unaendelea kwenye hukumu ya mwisho na waovu kuadhibiwa. (Yoh.5:29). Ambao majina yao hayamo kwenye Kitabu cha Uzima watafufuliwa wakati huo na “kutupwa kwenye ziwa la moto” na kupokea mauti ya pili. (Ufu.20:14, 15).
Wangeweza kuepuka mwisho mbaya wa namna hii. Kwa lugha isiyokosewa, Maandiko Matakatifu huwakilisha njia ya Mungu ya kuoka. “Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu. Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa enyi nyumba ya Israel? Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini mkaishi.” (Eze.18:30-32)
Kristo anaahidi kwamba “yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. (Ufu.2:11). Watakaomkubali Yesu na wokovu anaouleta watapata furaha isiyo kifani siku akirudi kwa kishindo. Katika furaha isiyofifia, watatumia umilele wakiwa washirika wa Bwana na Mwokozi wao.
===Mwisho wa somo====
Mafungu ya Biblia yanayodhaniwa Kuelezea Wafu wako Hai
Yapo mafungu katika Biblia ambayo hutafsiriwa vibaya hata kudhania wafu wana hali ya kutokufa na hivyo wanadamu walio hai wanaweza kufanya maombi, au kutekeleza sharti la mhubiri wa injili ili hao waliokufa warejee kwenye hali ya mwili unaoonekana tena. Mafungu husika yameonyeshwa na kupewa maelezo yake.
Maelezo ya Mafungu
1.Mwa. 35:18 “Ikawa hapo katika kutoa roho yake” Hii ina maana katika nyakati za pumzi ya mwisho za uhai wake alimwita mtoto Benoni.
2.1Fal.17:21,22 “Nakusihi roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake” Mungu alipojibu ombi hili kwa kumfufua mtoto wa mwanamke wa Sarepta, kanuni ya uhai ilitumika. Siyo mwili wala roho iliyokuwa na uhai peke yake, bali vilipoungana, mtoto alifufuka.
3. Kuonekana kwa Musa kwenye mlima aliobadilika Yesu. (Mt.16:28-17:3). Yesu alikuwa ameahidi baadhi ya wanafunzi wake hawatakufa hadi wamwone katika utukufu. Na hapo,
fursa ndogo ilitolewa kwa Petro, Yohana na Yakobo. Kwenye mlima, alitokea Musa aliyekufa zamani (Kumb.34:5, 6) na Eliya aliyepaa (2Fal.2:11). Musa na Eliya wanawakilisha jamii ya wanadamu watakaobadilishwa kuurithi ufalme wa milele. Kwamba wapo watakaokufa kabla ya kufufuliwa na kubadilishwa na wapo watakaobadilishwa pasipo kufa na kunyakuliwa. Yuda ana ushahidi kwamba Musa alifufuliwa kwenye ufufuo wa pekee (Yud. 9). Baada ya Mikaeli kushindana na Ibilisi, Ibilisi alishindwa na Musa akafufuliwa. Ufufuo wa Musa, hauungi mkono kutokufa kwa roho bali ufufuo wa mwili.
4. Kuishi ni Kristo na kufa ni faida… ninasongwa katika mambo mawili, ninatamani nikakae na Kristo maana ni vizuri sana. (Filp.1:21, 23). Je, Paulo alitegemea kuingia mbinguni mara moja baada ya kufa kwake? Hapana. Paulo amezungumzia somo la wafu kwa upana wake. Kwenye waraka mwingine aliandika “waliokufa katika Kristo”, katika ujio wa Kristo watafufuliwa kwanza. (1Thes.4:16). Ndipo walio hai na waliofufuliwa watanyakuliwa ili kumlaki Bwana hewani. (fungu la 17). Na kwamba ni nafsi, mwili na roho ndivyo vitakavyokuwa na Kristo (1 Thes. 5:23).
5.1 Pet. 3:18-20 na 4:6 Petro anaposema kuwa Yesu alikwenda kuhubiri walio kifungoni, ieleweke kuwa dunia yote inahesabika iko kuzimu cf Mt. 11:23. Biblia hufundisha wokovu hutafutwa wanadamu wakiwa hai, siyo wakishakufa.
6.Ebr. 11:4, Habili atanenaje wakati akiwa marehemu? Ni kwamba matendo yake aliyotenda akiwa hai, yaani kutoa sadaka zinazokubalika kwa Mungu, hata kama amekufa, yameacha kielelezo ambacho kinafundisha walio hai.
7.Ufunuo 6:9 – 11 Yohana alikuwa anaona sinema yenye fundisho la kiroho. Hakuwa anatazama mbinguni jinsi ilivyo kwa uhalisi. Kanuni za kutafsiri Ufunuo haitupatii sisi wasomaji mamlaka ya kujitungia tafsiri zetu (2 Pet. 1:20) Kinachosemwa hapa ni kwamba mtazamo unabadilika kutoka uangamivu na vifo ambavyo watakatifu hukabiliana navyo hadi kwenye wanachostahili watakatifu wenyewe.
8.Luka 23:43 Yesu alipokufa, hakupaa mbinguni moja kwa moja. Alibaki duniani baada ya kufufuka kwa siku kadha wa kadha. Siku ya kwenda mbinguni, alipaa peke yake wingu akiwa mtu moja, hakuna maelezo kuwa mwizi aliyeungama alikwenda naye. (Mdo. 1:9-11). Hivyo, kinachosemwa na fungu ni kuwa ahadi ya uzima ilitolewa siku ile wakiwa wote msalabani.
Kisa cha Tajiri (mara nyingi huitwa Dives) na maskini Lazaro (Luk. 16:19 – 31)
Wayahudi walikuwa na utaratibu wa kutumia mifano kwenye simulizi zao. Kwa mfano, katika Waamuzi 9:7-15 ikilinganishwa na 2 Wafalme14:9, utasoma miti inaongea. Hakuna mtu atakayetumia mafungu ya mifano hiyo kuthibitisha kwamba miti huongea. Mfano wa Tajiri na Maskini Lazaro ulikuwa mfano maarufu wa wafu wanaoongea nyakati za Yesu. Kisa ni miongoni mwa mifano iliyotolewa kuwalenga mafarisayo (Luk. 15:2). Mafarisayo walipomwona Yesu anakula na kunywa pamoja na walio na dhambi, walinung’unika, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na kula nao. Hivyo Yesu akawapa mifano ya kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea na Baba mwenye watoto wawili (wengine mnakiita kisa cha mwana mpotevu). Lengo la Yesu lilikuwa kuwaonyesha mafarisayo upendo wa Mungu kwa mwenye dhambi. Na ndiyo maana alisisitiza kuna furaha mbinguni kwa mwenye dhambi atubuye. (Luka 15:7, 10)
Baada ya hayo akafundisha wanafunzi wake, juu ya uwakili. (Luk. 16:1-13). Alipomaliza, mafarisayo waliokuwa wanasikiliza alichokuwa anafundisha wanafunzi wake walimdhihaki. Mafarisayo hao walikuwa wakiamini maskini ni maskini kwa sababu wamelaaniwa na matajiri ni matajiri kwa sababu wamebarikiwa. Na kwa hiyo, kule kuwa maskini ilihesabika katika jamii kuwa ni mapigo ya Mungu kwa mwanadamu mwenye dhambi. Na utajiri ilikuwa ni alama ya kubarikiwa na Mungu. Wakati watu wa kawaida walifurahia mafundisho ya Yesu (Mk. 12:37), mafarisayo walikuwa wakikasirika (Luk. 15:2). Na kwa mafarisayo, Yesu alikuwa na ujumbe kuwa Ole wenu... wanafiki kwa kuwa mnaufunga mlango wa ufalme wa mbinguni, ninyi wenyewe hamuingii na mnawazuia wanaotaka kuingia (Mt. 23:13). Dhihaka ya mafarisayo Luk. 16:14 -18 ilifanya mfano wa Tajiri na maskini Lazaro utolewe. Maelezo ya Hukumu itakavyokuwa ni kwamba:
Biblia hufundisha kuwa maamuzi kwa ajili ya kuokolewa hufanyika mtu akiwa hai na kwamba rehema hufungwa mtu akifa:
Hivyo watu wanapokufa, hawapati ijara zao bali hubaki makaburini hadi Yesu atakapokuja kuwafufua na kuwapa ijara zao. (Yoh. 5:28, 29, Uf. 22: 12,1Thes. 4:13-17)
Maelezo ya kisa cha tajiri na Lazaro ni ya kufikirika
Watu wanapokufa, miili yao huzikwa na pumzi hurudi ilikotoka. (Mh. 12:7) Katika kisa, yanaonekana macho, kifua, kiu inayokatwa kwa tone lililo katika kidole, ulimi, ni mwili au roho? Hivi ni kifua cha Ibrahimu ndicho alikowekwa maskini au Ibrahimu mzima mzima alionekana? Ikiwa kila mtakatifu huwekwa kwenye kifua cha Ibrahimu, hivi Ibrahimu ana kifua chenye ukubwa gani hata kutosha kubeba watakatifu wote! Ibrahimu alikufa, vipi aonekane? Ukubwa wa shimo una utata: Ni jembamba kuruhusu watu waweze kuonana na kusemezana lakini lina kina kirefu hata mtu asiweze kuruka kutoka kwenye hadhi moja hadi nyingine.
Mafundisho yatokanayo na mfano wa tajiri na maskini Lazaro
Mibaraka ya duniani kwa uhalisi wake siyo yakini ni ya kupita. Tajiri alikufa akaacha utajiri wake na maskini alikufa, akatengana na umaskini wake.
Walio matajiri huwajibika siyo tu kwa yale watendayo bali pia kwa yale wasiyofanya kwa utajiri wao. Huyu tajiri alikuwa mwema akaruhusu maskini kula makombo ya mezani pake, lakini alikuwa na nafasi ya kuinua hali ya maskini iwe bora zaidi, jambo ambalo hakufanya.
Maisha tuliyo nayo ndiyo nafasi pekee tuliyonayo kwa ajili ya maandalizi ya ufalme ujao.
Angalia, iliombwa ruhusa aliyekufa apate nafasi ya kuwa hai kwa muda mfupi, lakini haikutolewa.
Uchoyo, na ubinafsi, matumizi mabaya ya utajiri humnyima mtu sifa ya kuurithi ufalme wa milele wa Mungu. Tajiri hakutengwa na Ibrahimu kwa kuwa alikuwa tajiri, bali kwa sababu hakutumia utajiri wake kuwapunguzia maumivu wasio na mali.
Mafundisho ya Biblia yatosha kutufanya wenye hekima hata kupata wokovu. Kunyimwa ruhusa ya kwenda kuhubiri walio hai kulipewa maelezo kwamba walio hai wasipowasikiliza Musa na manabii nao watapotea.
Warumi 6:23X 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Timotheo 6:15X 15 Kwa maana wengine wamekwisha kugeuka na kumfuata Shetani.
Mhubiri 9:5, 6X 5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Zaburi 146:3, 4X 3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake. 4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Yohana 11:11-14X 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.
Wakolosai 3:4X 4 Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.
1 Wakorintho 15:51-54X 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
1 Wathesalonike 4:13-17X 13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Yohana 5:28, 29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Ufunuo 20:1-10X 1 Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. 2 Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; 3 akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache. 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu. 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu. 7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake; 8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari. 9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala. 10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.
1 Samweli 28X 1 Ikawa siku zile hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao waende vitani, ili kupigana na Israeli. Naye Akishi akamwambia Daudi, Jua hakika ya kuwa wewe utatoka pamoja nami jeshini, wewe na watu wako. 2 Naye Daudi akamwambia Akishi, Vema, sasa utajua atakayoyatenda mtumishi wako. Naye Akishi akamwambia Daudi, Haya basi! Mimi nitakufanya wewe kuwa mlinda kichwa changu daima. 3 Basi Samweli alikuwa amefariki dunia, nao Israeli wote walikuwa wamemwomboleza, na kumzika huko Rama, ndani ya mji wake mwenyewe. Tena Sauli alikuwa amewaondolea mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi. 4 Nao Wafilisti wakakusanyika, wakaenda kufanya kambi huko Shunemu; naye Sauli akawakusanya Waisraeli wote, nao wakapiga hema katika Gilboa. 5 Basi alipowaona hao majeshi ya Wafilisti, huyo Sauli akaogopa, na moyo wake ukatetemeka sana. 6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii. 7 Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori. 8 Basi Sauli akajigeuza, na kuvaa mavazi mengine, kisha akaenda, yeye na watu wawili pamoja naye, wakamfikilia yule mwanamke usiku; akasema, Tafadhali unibashirie kwa utambuzi, ukanipandishie yeye nitakayemtaja kwako. 9 Yule mwanamke akamwambia, Angalia, unajua alivyofanya Sauli, jinsi alivyowakatilia mbali hao wenye pepo wa utambuzi na wachawi katika nchi; mbona basi wanitegea tanzi uhai wangu, ili kuniua? 10 Naye Sauli akamwapia kwa Bwana, akasema, Aishivyo Bwana, haitakupata adhabu yo yote kwa jambo hili. 11 Ndipo yule mwanamke aliposema, Je! Ni nani nitakayekupandishia? Naye akasema, Nipandishie Samweli. 12 Hata yule mwanamke alipomwona Samweli alilia kwa sauti kuu; na yule mwanamke akamwambia Sauli, akasema, Mbona umenidanganya? Kwa kuwa wewe ndiwe Sauli. 13 Mfalme akamwambia Usiogope; waona nini? Yule mwanamke akamwambia Sauli, Naona mungu anatoka katika nchi. 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia. 15 Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje. 16 Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako? 17 Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi. 18 Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo. 19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti. 20 Mara Sauli akaanguka chini kifulifuli, akaingiwa na hofu kuu kwa sababu ya maneno hayo ya Samweli, wala hakuwa na nguvu yo yote; kwa maana hakula chakula mchana kutwa, wala usiku kucha. 21 Ndipo yule mwanamke akamwendea Sauli, akamwona ya kuwa yeye ametaabika sana, akamwambia, Angalia, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako, nami nimeutia uhai wangu mkononi mwangu, nami nimeyasikiliza maneno yako uliyoniambia. 22 Basi sasa, tafadhali, wewe uisikilize sauti ya mjakazi wako, nikakuandalie ngaa mkate kidogo; ukale, ili upate nguvu, utakapokwenda zako. 23 Lakini yeye alikataa, akasema, Mimi sitaki kula. Ila watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha; naye akaisikiliza sauti yao. Basi akainuka hapo chini, akaketi juu ya kitanda. 24 Naye yule mwanamke alikuwa na ndama aliyenona nyumbani; akafanya haraka kumchinja; akatwaa na unga, akaukanda, akafanya mkate wa mofa kwa unga huo; 25 kisha akamwandalia Sauli na watumishi wake; wakala. Ndipo wakaondoka, wakaenda zao usiku ule.
1 Timotheo 1:17X 17 Sasa kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.
1 Timotheo 6:16X 16 ambaye yeye peke yake hapatikani na mauti, amekaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hakuna mwanadamu aliyemwona, wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye hata milele. Amina.
Yakobo 4:14X 14 walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka.
Zaburi 78:39X 39 Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi.
Ayubu 14:2X 2 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
Mwanzo 2:7X 7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Matendo 17:25, 28X 25 wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote. 28 Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.
Wakolosai 1:16,17X 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye.
Warumi 6:23X 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Mwanzo 2:17X 17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Warumi 6:23X 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Mwanzo 3:19X 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3:22X 22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;
Warumi 5:12X 12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Ufunuo 13:8X 8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Warumi 2:7X 7 wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika, watapewa uzima wa milele;
Warumi 6:23X 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
1 Yohana 5:11X 11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe.
2 Timotheo 1:10X 10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
1 Wakorintho 15:22X 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.
Yohana 5:28, 29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
Yohana 3:16X 16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
2 Timotheo 1:10X 10 na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Kristo Yesu; aliyebatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika, kwa ile Injili;
2 Timotheo 3:15X 15 na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
1 Wakorintho 15:51-54X 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
1 Yohana 5:11-13X 11 Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwanawe. 12 Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. 13 Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
1 Wafalme 2:10X 10 Basi Daudi akalala na babaze, akazikwa mjini mwa Daudi.
1 Wafalme 11:43X 43 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.
1 Wafalme 14:20X 43 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.
1 Wafalme 15:8X 8 Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.
2 M. Nyakati 21:1X 1 Yehoshafati akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; akatawala Yehoramu mwanawe mahali pake.
2 M. Nyakati 26:23X 23 Basi Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze katika konde la kuzikia la wafalme; kwa kuwa walisema, Huyu ni mwenye ukoma. Na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake.
Ayubu 14:10-12X 10 Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? 11 Kama vile maji kupwa katika bahari, Na mto kupunguka na kukatika; 12 Ni vivyo mwanadamu hulala chini, asiinuke; Hata wakati wa mbingu kutokuwako tena, hawataamka, Wala kuamshwa usingizini.
Zaburi 13:3X 3 Ee Bwana, Mungu wangu, uangalie, uniitikie; Uyatie nuru macho yangu, Nisije nikalala usingizi wa mauti.
Yeremia 51:39, 57X 39 Wakiingiwa na ukali, nitawafanyizia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema Bwana. 57 Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, maliwali wake, na maakida wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, Bwana wa majeshi, ambaye jina lake ni Bwana.
Danieli 12:2X 2 Tena, wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.
Mathayo 9:24X 24 akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana.
Marko 5:39X 39 Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu.
Yohana 11:11-14X 11 Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha. 12 Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. 13 Lakini Yesu alikuwa amenena habari ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa ananena habari ya kulala usingizi. 14 Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa.
Mathayo 27:52X 52 makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala;
Mathayo 27:53X 53 nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.
Matendo 7:60X Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
1 Wakorintho 15:51,52X 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
1 Wathesalonike 4:13-17X 13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
2 Petro 3:4X 4 na kusema, Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake? Kwa maana, tangu hapo babu zetu walipolala, vitu vyote vinakaa hali iyo hiyo, tangu mwanzo wa kuumbwa.
Mhubiri 9:5X 5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.
Zaburi 146:4X 4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Mhubiri 9:10X 10 Lo lote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.
Mhubiri 9:6X 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Mhubiri 9:6X 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua.
Yohana 5:28,29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Mwanzo 2:7X 7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Zaburi 146:4X 4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Mwanzo 3:19X 19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Ezekieli 18:20X 20 Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
Zaburi 89:48X 48 Ni mwanamume gani atakayeishi asione mauti, Atakayejiokoa nafsi yake na mkono wa kuzimu?
Mwanzo 37:35X 35 Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.
Hesabu 16:30X 30 Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana
Matendo 2:27,31X 27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. 31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Ufunuo 20:13X 13 Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Mhubiri 12:7X 7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mhubiri 3:19-21X 19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili. 20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena. 21 Ni nani ajuaye kama roho ya binadamu huenda juu, na kama roho ya mnyama huenda chini?
Mwanzo 2:7X 7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Ezekieli 18:20X 4 Tazama, roho zote ni mali yangu; kama vile roho ya baba ni mali yangu, ndivyo ilivyo roho ya mwana mali yangu; roho ile itendayo dhambi itakufa.
Ufunuo 12:4, 9X 4 Na mkia wake wakokota theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi. Na yule joka akasimama mbele ya yule mwanamke aliye tayari kuzaa, ili azaapo, amle mtoto wake. 9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
M. Walawi 19:31X 31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
K. Torati 18:10,11X 10 Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, 11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.
Isaya 8:19, 20X 19 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai? 20 Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.
1 Samweli 28:6X 6 Lakini Sauli alipouliza kwa Bwana, Bwana hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.
1 Samweli 28:14X 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:14X 14 Naye akamwuliza, Ni mfano wa nini? Akajibu, Ni mzee anazuka; naye amefunikwa vazi. Basi Sauli akatambua ya kwamba ndiye Samweli mwenyewe, akainama uso wake mpaka nchi, akasujudia.
1 Samweli 28:19X 19 Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israeli mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwapo pamoja nami; tena Bwana atawatia jeshi la Israeli pia mikononi mwa Wafilisti.
Mwanzo 3:5X 5 kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Ufunuo 3:10X 5 Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe, wala sitalifuta kamwe jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitalikiri jina lake mbele za Baba yangu, na mbele ya malaika zake.
Ufunuo 16:13, 14X 13 Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14 Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
Ufunuo 13:13, 14X 13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu. 14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
1 Wakorintho 15:26X 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.
Ufunuo 20:14X 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
Ufunuo 21:8X 8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Ufunuo 2:11X 11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Ayubu 14:13-15X 13 Laiti ungenificha kuzimuni, Ukanilinda kwa siri, hata ghadhabu zako zitakapopita, Na kuniandikia muda ulioamriwa, na kunikumbuka! 14 Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie. 15 Wewe ungeita, nami ningekujibu; Ungekuwa na tamaa ya kazi ya mikono yako.
Ayubu 19:25-29X 25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi. 26 Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi, Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; 27 Nami nitamwona mimi nafsi yangu, Na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine. Mtima wangu unazimia ndani yangu. 28 Kama mkisema, Jinsi tutakavyomwudhi! Kwa kuwa shina la jambo hili limeonekana kwake; 29 Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.
Zaburi 49:15X 15 Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
Zaburi 73:24X 24 Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu.
Isaya 26:19X 19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
1 Wakorintho 15X 1 Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, 2 na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. 3 Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; 4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko; 5 na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake. 9 Maana mimi ni mdogo katika mitume, nisiyestahili kuitwa mitume, kwa sababu naliliudhi Kanisa la Mungu. 10 Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami. 11 Basi, kama ni mimi, kama ni wale, ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini. 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu? 13 Lakini kama hakuna kiyama ya wafu, Kristo naye hakufufuka; 14 tena kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure. 15 Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. 16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. 19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. 20 Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. 21 Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja. 24 Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu. 25 Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake. 26 Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti. 27 Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo. 28 Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote. 29 Au je! Wenye kubatizwa kwa ajili ya wafu watafanyaje? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao? 30 Na sisi, kwa nini tumo hatarini kila saa? 31 Naam, ndugu, kwa huku kujisifu kwangu niliko nako juu yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu, ninakufa kila siku. 32 Ikiwa, kwa jinsi ya kibinadamu, nalipigana na hayawani wakali kule Efeso, nina faida gani? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa. 33 Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema. 34 Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe. 35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? 36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; 37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo; 38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake. 39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki. 40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali. 41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota. 42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda. 55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako? 56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Yohana 5:28, 29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
1 Wakorintho 15:17X 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu.
1 Wakorintho 15:12X 12 Basi, ikiwa Kristo anahubiriwa ya kwamba amefufuka katika wafu, mbona baadhi yenu husema kwamba hakuna kiyama ya wafu?
1 Wakorintho 15:17, 18X 17 Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. 18 Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.
Luka 24:13-27X 13 Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. 14 Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. 15 Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. 16 Macho yao yakafumbwa wasimtambue. 17 Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. 18 Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? 19 Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; 20 tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. 21 Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; 22 tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, 23 wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. 24 Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. 25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! 26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? 27 Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
Yohana 20:14-18X 14 Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! 15 Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari. 16 Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu. 17 Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. 18 Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati.
Luka 24:39X 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo.
Wafilipi 3:10,11X 10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
Matendo 4:33X 33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
Matendo 17:6X 6 na walipowakosa, wakamkokota Yasoni na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika huku nako,
Wafilipi 3:10, 11X 10 ili nimjue yeye, na uweza wa kufufuka kwake, na ushirika wa mateso yake, nikifananishwa na kufa kwake; 11 ili nipate kwa njia yo yote kuifikia kiyama ya wafu.
1 Petro 1:3X 3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;
Matendo 1:22X 22 kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.
Matendo 2:31X 31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.
Matendo 4:33X 33 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.
Matendo 4:2X 2 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu.
Matendo 23:6X 6 Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu.
Matendo 24:21X 21 isipokuwa kwa ajili ya sauti hii moja, nilipolia nikisimama katikati yao, na kusema, Kwa ajili ya ufufuo wa wafu ninahukumiwa mbele yenu hivi leo.
Warumi 1:4X 4 na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu;
Warumi 6:4, 5X 4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake;
Yohana 5:28, 29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Matendo 24:15X 15 Nina tumaini kwa Mungu, ambalo hata hao nao wanalitazamia, ya kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, wenye haki na wasio haki pia.
Ufunuo 20:4, 5X 4 Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai, wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu. 5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
Ufunuo 20:6X 6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
Ufunuo 20:14X 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.
Yohana 5:29X 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
1 Wakorintho 15:52,53X 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
1 Wakorintho 15:22,23X 22 Kwa kuwa kama katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa. 23 Lakini kila mmoja mahali pake; limbuko ni Kristo; baadaye walio wake Kristo, atakapokuja.
1 Wathesalonike 4:15-18X 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Luka 20:36X 36 wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.
Wafilipi 3:21X 21 atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
1 Wakorintho 15:42-54X 42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; 43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu; 44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko. 45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. 46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. 47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. 48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. 49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni. 50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika. 51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika, 52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. 53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. 54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
Yohana 5:29X 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Ufunuo 20:14, 15X 14 Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. 15 Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ezekieli 18:30-32X 30 Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu. 30 Basi, nitawahukumu ninyi, nyumba ya Israeli, kila mmoja kwa kadiri ya njia zake, asema Bwana MUNGU. Rudini, mkaghairi, na kuyaacha makosa yenu yote; basi hivyo uovu wenu hautakuwa uharibifu wenu. 31 Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote mliyoyakosa; jifanyieni moyo mpya na roho mpya; mbona mnataka kufa, enyi nyumba ya Israeli? 32 Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini, mkaishi.
Ufunuo 2:11X 11 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Mwanzo 35:18X 18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
1 Wafalme 17:21,22X 20 Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe. 21 Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.
28 Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.
Mathayo 17:1-3
1 Na baada ya siku sita Yesu akawatwaa Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, akawaleta juu ya mlima mrefu faraghani; 2 akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru. 3 Na tazama, wakatokewa na Musa na Eliya, wakizungumza naye.
K. Torati 34:5, 6X 5 Basi Musa, mtumishi wa Bwana, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la Bwana. 6 Akamzika bondeni, katika nchi ya Moabu, kukabili Beth-peori; lakini hapana mtu ajuaye kaburi lake hata leo.
2 Wafalme 2:11X 11 Ikawa, walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli.
yuda 1:9X 9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.
Wafilipi 1:21, 23X 21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. 23 Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo maana ni vizuri zaidi sana;
1 Wathesalonike 4:16X 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
1 Wathesalonike 5:23X 23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Petro 3:18-20X 18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, 19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri; 20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
Mathayo 11:23X 23 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Waebrania 11:4X 4 Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Ufunuo 6:9 – 11X Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao. 10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi? 11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao
2 Petro 1:20X 20 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.
Luka 23:43X 43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
Matendo 1:9-11X 9 Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi. 10 Basi palikuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. 11 Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Luka 16:19 – 31X 19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, 21 naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. 22 Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. 23 Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. 24 Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. 26 Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. 27 Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, 28 kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. 29 Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. 30 Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. 31 Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.
Waamuzi 9:7-15X 7 Kisha walipomwambia huyo Yothamu, yeye akaenda, akasimama juu ya kilele cha kilima cha Gerizimu, akapaza sauti yake, akapiga kelele, na kuwaambia, Nisikieni mimi, enyi watu wa Shekemu, ili kwamba Mungu naye apate kuwasikia ninyi. 8 Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu. 9 Lakini huo mzeituni ukaiambia, Je! Niache mafuta yangu, ambayo kwangu mimi watu wamheshimu Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti? 10 Kisha miti ikauambia mtini, Njoo wewe, utawale juu yetu. 11 Lakini huo mtini ukaiambia, Je! Niuache utamu wangu, na matunda yangu mazuri, niende nikayonge-yonge juu ya miti? 12 Kisha miti ikauambia mzabibu, Njoo wewe, utawale juu yetu. 13 Huo mzabibu nao ukaiambia, Je! Niiache divai yangu, ambayo humfurahisha Mungu na wanadamu, ili niende nikayonge-yonge juu ya miti? 14 Ndipo hiyo miti yote ikauambia mti wa miiba, Njoo wewe, utawale juu yetu. 15 Huo mti wa miiba ukaiambia miti, Kwamba ninyi mwanitia mafuta niwe mfalme juu yenu kwelikweli, basi njoni mtumaini kivuli changu; na kwamba sivyo, na utoke moto katika mti wa miiba na kuiteketeza mierezi ya Lebanoni.
2 Wafalme 14:9X 9 Naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ulituma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni, kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Luka 15:2X 2 Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
Luka 15: 7, 10X 7 Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu. 10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.
Luka 16: 1-13X 1 Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. 2 Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena. 3 Yule wakili akasema moyoni mwake, Nifanyeje? Maana, bwana wangu ananiondolea uwakili. Kulima, siwezi; kuomba, naona haya. 4 Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao. 5 Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? 6 Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. 7 Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini. 8 Yule bwana akamsifu wakili dhalimu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru. 9 Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. 10 Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. 11 Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? 12 Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Marko 12:37X 37 Daudi mwenyewe asema ni Bwana; basi amekuwaje mwanawe? Na mkutano mkubwa walikuwa wakimsikiliza kwa furaha.
Luka 15:2X 2 Mafarisayo na waandishi wakanung'unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
Mathayo 23:13X 13 Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.
Luka 16:14 -18X Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki. 15 Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu. 16 Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. 17 Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati. 18 Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini
Mathayo 16:27X 27 Kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Warumi 2:6X 6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake;
Waebrania 9:27X 27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Ufunuo 22:12X 12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Luka 23:43X 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Mathayo 26:29X 29 Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Mathayo 6:20X 20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
Yohana 14:2, 3X 2 Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali. 3 Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
Mathayo 10:28X 28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Mathayo 5:22X 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.
Yohana 5:29X 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Mathayo 23:33X 33 Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?
Marko 3:29X 29 bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele,
Yohana 5:28, 29X 28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. 29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Ufunuo 22: 12X 12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
1 Wathesalonike 4:13-17X 13 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Mhubiri 12:7X 7 Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.