19. Sheria ya Mungu

Utangulizi


Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimeunganishwa katika Amri Kuimi na zilifuatishwa katika maisha ya Kristo. Nazo zinadhihirisha upendo na mapenzi ya Mungu, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti kwa watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ni msingi wa agano la Mungu na watu na kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu zinadhihirisha dhambi na kuamsha haja ya kumpata Mwokozi. Wokovu ni kwa neema, na si kwa matendo, lakini matunda yake ni utii kwa Amri Kumi. Utii huu hukuza tabia ya Kikristo na huwa na matokeo ya ustawi. Ni ushuhuda wa upendo wetu kwa Bwana na wajibu wetu kwa wanadamu wenzetu. Utii wa imani hudhihirisha uwezo wa Kikristo katika kubadilisha maisha, na hivyo kuimarisha ushuhuda wa Kikristo. (Kut. 20:1-17;
Kutoka 20:1-17X
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. 8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 13 Usiue. 14 Usizini. 15 Usiibe. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
Zab. 40:7,8,
Zaburi 40:7,8X
7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) 8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Mat. 22:36-40,
Zaburi 40:7,8X
7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,) 8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Kumb. 28:1-14;
K. Torati 28:1-14;X
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. 13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya; 14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
Mat. 5:17-20;
Mathayo 5:17-20X
17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. 19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Ebr.8:8-10;
Waebrania 8:8-10X
8 Maana, awalaumupo, asema Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, Nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda agano jipya; 9 Halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, Katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, Mimi nami sikuwajali asema Bwana. 10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.
Yoh. 15:7-10;
Yohana 15:7-19X
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8 Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. 9 Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11 Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13 Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15 Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. 16 Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 17 Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana. 18 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19 Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.
Efe. 2:8-10;
Waefeso 2:8-10X
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. 10 Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
1Yoh.5:3;
1 Yohana 5:3X
3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
Rum. 8: 3, 4;
Warumi 8:3,4X
3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 4 ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.
Zab. 19:7-14).
Zaburi 19:7-14X
7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. 8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru. 9 Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa. 10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. 11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi. 12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri. 13 Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. 14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.

Macho yote yalielekea mlima. Kilele chake kilikuwa kimefunikwa na wingu zito lilioendelea kuwa jeusi hadi mlima wote ukazingirwa kwa usiri. Radi ilipiga kutoka gizani wakati ngurumo ziliposikika na kuakisiwa. “Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi kwa sababu BWANA alishuka katika moto; na ule moshi wa tanuu, mlima wote ulitetemeka sana. Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana; Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti” (Kut. 19: 18, 19).

Kutoka 19:18,19X
18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana. 19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.
Ufunuo wa Mungu ulitisha sana kiasi kwamba Waisraeli wote walitetemeka.” Mungu alipotoa amri zake Sinai, hakujidhihirisha tu kwamba ni Mtawala bali pia ni Mkombozi (Kut. 20:2).
Kutoka 20:2X
2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Ni Mwokozi ambaye hawaiti Israeli peke yake bali pia wanadamu wote (Mh. 12:13).
Mhubiri 12:13X
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Soma Kut. 20:1-17).
Kutoka 20:1-7X
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.

Asili ya Sheria ya Mungu

Sheria ya Mungu ni ya kimaadili, ya kiroho na yenye kubeba kanuni zinazojitosheleza.

'

Kuakisi tabia ya Mtoa Sheria

Kama alivyo Mungu, Sheria yake nayo ni kamilifu na ushuhuda wake ni safi (Zab.19:7, 8)

Zaburi 19:7,8X
7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima. 8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru.
, Sheria ni takatifu, ya haki na njema (Rum. 7:12)
Warumi 7:12X
12 Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
. Amri ni kweli na haki (Zab. 119: 151, 172).
Zaburi 119:151, 172X
151 Ee Bwana, Wewe U karibu, Na maagizo yako yote ni kweli. 152 Tokea zamani nimejua kwa shuhuda zako, Ya kuwa umeziweka zikae milele. 153 Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako. 154 Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako. 155 Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako. 156 Ee Bwana, rehema zako ni nyingi, Unihuishe sawasawa na hukumu zako. 157 Wanaonifuatia na watesi wangu ni wengi, Lakini sikujiepusha na shuhuda zako. 158 Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako. 159 Uangalie niyapendavyo mausia yako, Ee Bwana, unihuishe sawasawa na fadhili zako. 160 Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele. 161 Wakuu wameniudhi bure, Ila moyo wangu unayahofia maneno yako. 162 Naifurahia ahadi yako, Kama apataye mateka mengi. 163 Nimeuchukia uongo, umenikirihi, Sheria yako nimeipenda. 164 Mara saba kila siku nakusifu, Kwa sababu ya hukumu za haki yako. 165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza. 166 Ee Bwana, nimeungojea wokovu wako, Na maagizo yako nimeyatenda. 167 Nafsi yangu imezishika shuhuda zako, Nami nazipenda mno. 168 Nimeyashika mausia yako na shuhuda zako, Maana njia zangu zote zi mbele zako. 169 Ee Bwana, kilio changu na kikukaribie, Unifahamishe sawasawa na neno lako. 170 Dua yangu na ifike mbele zako, Uniponye sawasawa na ahadi yako. 171 Midomo yangu na itoe sifa, Kwa kuwa unanifundisha mausia yako. 172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, Maana maagizo yako yote ni ya haki.

Sheria ya Maadili

Sheria huonyesha mwenendo wa mfuasi wa Mungu anavyopaswa kuenenda. Kuacha kutii, huhesabika ni uasi. (1Yoh. 3:4)

1 Yohana 3:4X
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.

Sheria ya kiroho

Sheria ni ya kiroho (Rum. 7:14)

Warumi 7:14X
14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.
. Kwa hiyo ni wale waliojawa Roho Mtakatifu ndio wanaoweza kuitii (Yoh. 15:4;
Yohana 15:4X
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Gal. 5:22, 23)
Wagalatia 5:22,23X
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
. Ni roho wa Mungu ndiye atuwezeshaye kuyafanya mapenzi yake (Mdo. 1:8,
Matendo 1:8X
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Zab. 51:10-12)
Zaburi 51:10-12X
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu 11 Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. 12 Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
. Tunapokaa na Yesu, tunapewa uwezo wa kuzaa kwa utukufu wake (Yoh. 15:5)
Yohana 15:5X
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
. Sheria za kibinadamu huhusu matendo machache, bali sheria ya Mungu ni pana mno (Zab. 119:96)
Zaburi 119:96X
96 Nimeona ukamilifu wote kuwa na mwisho, Bali agizo lako ni pana mno.
. Katika hotuba ya Yesu ya Mlimani, Yesu alikazia hali ya kiroho ya Sheria ya Mungu kwamba dhambi huanza kwa kunuia kutoka moyoni (Mt. 5:21, 22, 27, 28;
Mathayo 5:21,22,27,28X
21 Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu. 22 Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. 27 Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; 28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Mk. 7:21-23)
Marko 7:21-23X
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Sheria Chanya

Sheria inaposema usi inaamanisha unatakiwa kutenda jambo chanya. Kwa mfano, usiue (Kut. 20:13)

Kutoka 20:13X
13 Usiue.
ina sehemu chanya yenye kumaanisha kukuza/kulinda uhai. Tunaitwa kuitazama sheria kwamba Mungu, kwa wema wake amefunua kanuni bora za haki zinazowazuilia watu wake mabaya yatokanayo na kumwasi.

Sheria Rahisi

Amri kumi kwa uzito wake ni rahisi. Ni fupi kiasi ambacho hata mtoto mdogo aweza kuzikariri na zinapenya kiasi kwamba hudhihirisha kila dhambi. Hakuna siri katika sheria ya Mungu. Wote wanaweza kweli ibebazo. “Mtu mwenye akili hafifu aweza kuzitambua kanuni zake na aliye mjinga aweza kuendesha maisha yake hata akafanyiza tabia inayofuatana na viwango vya kimbingu.”1SM p235.

Sheria ya Kanuni

Amri kumi ni muhtasari wa wa kanuni zote njema zinazotumika kwa wanadamu wote na kwa nyakati zote. Maandiko hutudai “mche Mungu na kuzitii amri zake, kwa kuwa hii ndiyo impasayo mtu (Mh. 12:13)

Mhubiri 12:13X
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
.Maneno ya maagano (Kut.34:28)
Kutoka 34:28X
28 Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
yamegawanywa kwenye sehemu mbili kama yalivyoandikwa kwenye mbao mbili za mawe (Kumb. 4:13). Amri nne za kwanza (Kut. 20:1-11),
Kutoka 20:1-11X
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. 8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
zinaelekeza wajibu wa mwanadamu kwa Mungu na sita za mwisho (Kut. 20:12-17)
Kuotka 20:12-17X
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 13 Usiue. 14 Usizini. 15 Usiibe. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako.
zinaelekeza wajibu wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake. (Mt. 22:36-40;
Mathayo 22:36-40X
36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Luk. 10:27;
Luka 10:27X
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.
Kumb. 6:4,5;
K. Torati 6:4,5X
4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.
Law. 19:18)
M. Walawi 19:18X
18 Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.
Amri ya kwanza yataka tumwabudu Mungu wa kweli peke yake, ya pili inazuia ibada ya sanamu, ya tatu inazuia watu kudhihaki jina la Mungu na ya nne inaita wanadamu kuikumbuka sabato ya Bwana na kumtambulisha Mungu kuwa muumba wa mbingu na nchi. Amri ya tano yawaita watoto kuwatii wazazi wao, (Kumb. 4:6-9; 6:1-7)
K.Torati 4:6-9; 6:1-7X
6 Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili. 7 Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama Bwana, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? 8 Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo. 9 Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako; 1 Na hii ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki; 2 upate kumcha Bwana, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe. 3 Sikiza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama Bwana, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali. 4 Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. 5 Nawe mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; 7 nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
, ya sita hulinda maisha kwamba ni matakatifu, ya saba huingiza usafi na kulinda mahusiano ya ndoa, ya nane yalinda mali. Ya tisa hulinda ukweli na ya kumi inaenda kwenye mzizi wa mahusiano ya kibinadamu kwa kukemea kutamani ya mwanadamu mwingine.

Sheria ya Pekee

Amri kumi ni tofauti kwa kuwa zilisemwa na Mungu mwenyewe zikasikika na taifa lote (Kumb. 5:22)

K. Torati 5:22X
22 Haya ndiyo maneno ambayo Bwana aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.
na pia ziliandikwa kwa chanda cha Mungu juu ya mbao mbili za mawe na kutunzwa kwenye sanduku la agano (Kut. 31:18;
Kutoka 31:18X
18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.
Kumb. 10:2)
K. Torati 10:20X
20 Mche Bwana, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.
. Kuwasaidia Waisraeli kuzitumia sheria, Mungu aliwapa kanuni za ziada kuimarisha mahusiano yake na wao. Baadhi yake zinahusu mambo ya kijamii (Sheria ya kuongoza nchi), zingine zilihusu usimamizi wa ibada (Sheria za Kafara). Mungu aliwapa sheria hizi Waisraeli kwa kupitia Musa aliyeziandika kwenye kitabu cha sheria kilichowekwa kando ya sanduku la agano (Kumb. 31:25, 26)
K. Torati 31:25,26)X
24 Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la agano la Bwana akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.
na siyo ndani ya Sanduku la Agano kama amri 10. Hizi sheria zilijulikana kama Kitabu cha Sheria cha Musa (Yosh. 8:31;
Yoshua 8:31X
31 Kama Musa, mtumishi wa Bwana, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa Bwana, na kuchinja sadaka za amani.
Neh. 8:1, 2;
Nehemia 8:1,2X
1 Na watu wote wakakusanyika kama mtu mmoja katika uwanja uliokuwa mbele ya lango la maji; wakamwambia Ezra, mwandishi, akilete kitabu cha torati ya Musa, Bwana aliyowaamuru Israeli. 2 Naye Ezra, kuhani, akaileta torati mbele ya kusanyiko, la wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
2Nyak. 25:4)
2 M. Nyakati 25:4X
4 Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya sawasawa na hayo yaliyoandikwa katika torati, katika kitabu cha Musa, kama Bwana alivyoamuru, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.
au kwa urahisi, Sheria za Musa2 Wafalme 23:25
(2Waf.23:25;X
25 Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.
2Nyak. 23:18).
2 M. Nyakati 23:18X
18 Yehoyada akauamuru usimamizi wa nyumba ya Bwana chini ya mkono wa makuhani Walawi, aliowagawa Daudi nyumbani mwa Bwana, ili wazisongeze sadaka za kuteketezwa za Bwana, kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, kwa kufurahi na kuimba, kama alivyoamuru Daudi.

Sheria ya Furaha

Sheria ya Mungu hutia moyo nguvu. Mtunga Zaburi alisema napenda sheria yako na ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa na pia sheria yako ni furaha yangu (Zab. 119: 97, 127,143)

Zaburi 119:97,127,143X
97 Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. 127 Ndiyo maana nimeyapenda maagizo yako, Kuliko dhahabu, naam, dhahabu iliyo safi. 143 Taabu na dhiki zimenipata, Maagizo yako ni furaha yangu.
. Kwa wale wanaompenda Mungu, amri zake siyo nzito (1Yoh. 5:3)
1 Yohana 5:3X
3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
. Kwa wenye dhambi, wanaona sheria inahuzunisha kwa kuwa nia ovu haiwezi kumtii Mungu (Rum. 8:7)
Warumi 8:7X
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
.

Makusudi ya Sheria

Mungu alitoa sheria yake kwa watu ili kuwajaza mibaraka tele na kuwaongoza wapate kuingia kwenye mahusiano naye yenye kuokoa. Madhumuni maalumu ya sheria ni: -

1. Hufunua mapenzi ya Mungu kwa Wanadamu

Kama maelezo ya tabia ya Mungu na mapenzi yake kwa wanadamu, sheria hudhihirisha nia yake na makusudi yake kwa wanadamu. Hudai utii mkamilifu, atakayetii yote akakosea juu ya moja, anakuwa amekosea juu ya yote (Yak. 2:10)

Yakobo 2:10X
10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.
. Utii wa sheria kama kanuni ya maisha ni muhimu kwa wokovu wetu, Kristo mwenyewe alisema “kama ukitaka kuingia mbinguni, zishike amri” (Mt. 19:17)
Mathayo 19:17X
17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
. Utii unawezekana tu kwa uwezo wa Roho wa Mungu.

2. Ni msingi wa Agano la Mungu

Musa alipoandika Sheria na maelezo mengine, aliita Kitabu cha Agano (Kut. 20:1-24:8)

Kutoka 20:1-24X
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. 3 Usiwe na miungu mingine ila mimi. 4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. 5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. 7 Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure. 8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa. 12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako. 13 Usiue. 14 Usizini. 15 Usiibe. 16 Usimshuhudie jirani yako uongo. 17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako. 18 Watu wote wakaona umeme na ngurumo na sauti ya baragumu, na ule mlima kutoka moshi; na watu walipoona hayo wakatetemeka, wakasimama mbali. 19 Wakamwambia Musa, Sema nasi wewe, nasi tutasikia, bali Mungu asiseme nasi, tusije tukafa. 20 Musa akawaambia watu, Msiogope, maana Mungu amekuja ili awajaribu, na utisho wake uwe mbele yenu, ili kwamba msifanye dhambi. 21 Basi hao watu wakasimama mbali, naye Musa akalikaribia lile giza kuu Mungu alipokuwapo. 22 Bwana akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli hivi, Ninyi wenyewe mmeona ya kuwa nimenena nanyi kutoka mbinguni. 23 Msifanye miungu mingine pamoja nami; miungu ya fedha, wala miungu ya dhahabu, msijifanyie. 24 Utanifanyia madhabahu ya udongo, nawe utatoa dhabihu zako juu yake; sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani, kondoo zako, na ng'ombe zako, kila mahali nitakapotia ukumbusho wa jina langu, hapo ndipo nitakapokujilia na kukubarikia.
. Baadaye aliziita Amri Kumi Mbao za Agano (Kumb. 9:9 cf. 4:13)
K. Torati 9:9 cf. 4:13X

K. Torati 9:9

9 Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano Bwana alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.

K. Torati 4:13

13 Akawahubiri agano lake, alilowaamuru kulitenda, yaani, zile amri kumi; akaziandika juu ya mbao mbili za mawe.

3. Ni kipimo cha Hukumu

Kama ilivyo tabia yake, Sheria ya Mungu nayo ni haki (Zab. 119:172)

Zaburi 119:172X
172 Ulimi wangu na uiimbe ahadi yako, Maana maagizo yako yote ni ya haki.
. Kila moja wetu atahukumiwa kwa sheria (Mh. 12:13, 14 cf.
Mhubiri 12:13,14X
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
cf. Yak. 2:12)
Yakobo 2:12X
12 Semeni ninyi, na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ya uhuru.
. Dhamiri za wanadamu hutofautiana. Zingine ni nyonge, na zingine zimenajisiwa, ovu au zimeunguzwa na pasi ya moto (1Kor.7:12;
1 Wakorintho 7:12X
12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.
Tit. 1:15;
Tito 1:15X
15 Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.
Ebr. 10:22;
Waebrania 10:22X
22 na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.
1Tim. 4:2)
1 Timotheo 4:2X
2 kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;
. Dhamiri zetu hutuambia tutende haki, lakini hazituambii haki yenyewe ni ipi. Hivyo sheria ndiyo kipimo cha hukumu.

4. Huonyesha Dhambi

Bila amri kumi, watu hawawezi kuuona utakatifu wa Mungu, hatia yao na hitaji la kutubu. Sheria ni kama kioo (Yak. 1:23-25)

Yakobo 1:23-25X
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. 24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. 25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
na wanaoitazama huona kasoro za tabia zao na kuona tunavyowajibika kwa Mungu (Rum. 3:19)
Warumi 3:19X
19 Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu;
. Sheria hutufanya tuitambue dhambi (Rum. 3:20)
Warumi 3:20X
20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
kwa sababu dhambi ni uasi (1Yoh. 3:4)
1 Yohana 3:4X
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
. Kama sheria isingekuwapo, tusingejua dhambi (Rum.7:7)
Warumi 7:7X
7 Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
.

5. Hutuongoza kuongoka

Sheria ya Mungu ni zana cha Roho Mtakatifu kutuongoza kutubu. Sheria ya Mungu ni kamilifu, huuburudisha moyo (Zab. 19:7)

Zaburi 19:7X
7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.
. Sheria ni kiongozi kutuleta kwa Kristo ili tuhesabiwe haki (Gal. 3:24)
Wagalatia 3:24X
24 Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.
. Kama kioo kisivyoweza kuondoa uchafu, sheria hutufanya tuhitaji chemchemi iliyofunguliwa (Zek. 13:1)
Zekaria 13:1X
1 Katika siku hiyo watu wa nyumba ya Daudi, na wenyeji wa Yerusalemu, watafunguliwa chemchemi kwa dhambi na kwa unajisi.
na kusafishwa na damu ya Mwana Kondoo (Uf.7:14).

6. Hutupatia Uhuru wa Kweli

Atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi (Yoh. 8:34)

Yohana 8:34X
34 Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
. Nitakwenda panapo nafasi, kwa sababu nimejifunza kutii (Zab. 119:45)
Zaburi 119:45X
45 Nami nitakwenda panapo nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
. Yakobo aliita Sheria ya Mungu Sheria ya Kifalme, sheria ya Uhuru (Yak. 2:8; 1:25)
Yakobo 2:8; 1:25X

Yakobo 1:8

8 Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vema.

Yakobo 1:25

25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
. Yesu anapotualika, hutuita kuchukua mzigo mwepesi na nira laini (Mt. 11:28, 29)
Mathayo 11:28, 29X
28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
na hiyo hutupa raha. Palipo na Roho wa Mungu, kuna uhuru (2Kor.3:17)
2 Wakorintho 3:17X
17 Basi <Bwana> ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.
.

7. Hukinga maovu na huleta Baraka

Kuongezeka makosa ya jinai, udhalimu, kukosekana uadilifu, na kuongezeka uovu ambako kumeijaa dunia kwa sasa kunatokana na kudharau Amri Kumi. Wakati sheria hii inapokubaliwa, hukinga dhambi, hukuza matendo mema na huwa njia ya kuimarisha haki. Haki huinua taifa (Mith. 14:34; 16:12)

Mithali 14:34; 16:12X

Mithali 14:34

34 Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.

Mithali 16:12

12 Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki.
. Wale wanaokataa kutii amri za Mungu hawawezi kuikwepa laana (Mith. 3:33; cf.
Mithali 3:33X
33 Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.
cf. Law. 26;,
M. Walawi 26X
1 Msifanye sanamu yo yote, wala msijisimamishie sanamu ya kuchonga, wala mnara, wala msiweke jiwe lo lote lililochorwa katika nchi yenu ili kulisujudia; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 2 Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi Bwana. 3 Kama mkienda katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya; 4 ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa maongeo yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama. 6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu. 7 Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga. 8 Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia, na watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga. 9 Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi. 10 Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya. 11 Nami nitaiweka maskani yangu kati yenu; wala roho yangu haitawachukia. 12 Nami nitakwenda kati yenu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu. 13 Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawaendesha mwende sawasawa. 14 Lakini msiponisikiza, wala hamtaki kuyafanya maagizo hayo yote; 15 nanyi mkizikataa amri zangu, na roho yenu ikichukia hukumu zangu, hata ikawa hamtaki kuyafanya maagizo yangu yote, bali mwalivunja agano langu; 16 mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila. 17 Nami nitauelekeza uso wangu kinyume chenu, nanyi mtapigwa mbele ya adui zenu; hao wawachukiao watatawala juu yenu; nanyi mtakimbia wakati ambao hapana awafukuzaye. 18 Tena ikiwa baada ya hayo hamtaki kunisikiza, ndipo nitawaadhibu zaidi mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 19 Nami nitakivunja kiburi cha uwezo wenu; nami nitazifanya mbingu zenu kuwa kama chuma, na nchi yenu kuwa kama shaba; 20 na nguvu zenu mtazitumia bure; kwa kuwa nchi yenu haitazaa mazao yake, wala miti ya nchi haitazaa matunda yake. 21 Nanyi ikiwa mwaenenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo. 22 Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza muwe wachache hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa. 23 Tena kama hamtaki kurejezwa upya kwangu mimi kwa mambo haya, bali mwaendelea kunishikia kinyume; ndipo mimi nami nitaendelea kuwashikia ninyi kinyume; 24 nami nitawapiga, naam mimi, mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 25 Nami nitaleta upanga juu yenu, utakaopatiliza kisasi cha hilo agano; nanyi mtakutanishwa ndani ya miji yenu; nami nitaleta tauni kati yenu; nanyi mtatiwa mkononi mwa adui. 26 Hapo nitakapovunja tegemeo lenu la mkate, wanawake kumi wataoka mikate yenu katika tanuu moja, nao watawapa mikate yenu tena kwa kupima kwa mizani; nanyi mtakula, lakini hamtashiba. 27 Tena ikiwa baada ya hayo yote hamtaki kunisikiza, bali mwaenenda kwa kunishikia kinyume; 28 ndipo nami nitakwenda kwa kuwashikia ninyi kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu. 29 Nanyi mtakula nyama ya miili ya wana wenu, na nyama ya miili ya binti zenu mtaila. 30 Nami nitapaharibu mahali penu palipoinuka, na kuziangusha sanamu zenu za jua, nami nitaitupa mizoga yenu juu ya mizoga ya sanamu zenu; na roho yangu itawachukia. 31 Nami nitaifanya miji yenu iwe maganjo, na mahali penu patakatifu nitapatia ukiwa; wala sitasikia harufu ya manukato yenu yapendezayo. 32 Nami nitaitia hiyo nchi ukiwa; na adui zenu watakaokaa huko wataistaajabia. 33 Nanyi nitawatapanya-tapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo. 34 Hapo ndipo nchi itakapozifurahia Sabato zake, wakati itakapokuwa hali ya ukiwa, nanyi mtakapokuwa katika nchi ya adui zenu; ndipo nchi itakapopumzika, na kuzifurahia Sabato zake. 35 Wakati wote itakapokuwa na ukiwa, itapumzika; ni hayo mapumziko ambayo haikuwa nayo katika Sabato zenu, hapo mlipokaa katika nchi hiyo. 36 Tena hao wa kwenu watakaobaki, nitawatilia woga mioyoni mwao, katika hizo nchi za adui zao; na sauti ya jani lililopeperushwa itawakimbiza; nao watakimbia, kama mtu akimbiavyo upanga; nao wataanguka hapo ambapo hapana afukuzaye. 37 Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu. 38 Nanyi mtaangamia kati ya mataifa, na nchi ya adui zenu itawameza. 39 Na watu wa kwenu watakaobaki watafifia kwa ajili ya uovu wao, katika hizo nchi za adui zenu; tena watafifia kwa ajili ya uovu wa baba zao, pamoja nao. 40 Nao wataukiri uovu wao, na uovu wa baba zao, katika maasi yao waliyoasi juu yangu, tena ya kuwa kwa sababu wameendelea kunishikia kinyume, 41 mimi nami nimeendelea kuwashikia kinyume wao, na kuwatia katika nchi ya adui zao; lakini hapo, kama mioyo yao isiyokuwa tohara ikinyenyekea, nao wakubali adhabu ya uovu wao; 42 ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Ibrahimu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo. 43 Nchi nayo itaachwa na wao, nayo itazifurahia Sabato zake, itakapokuwa ukiwa pasipokuwa na wao; nao wataikubali adhabu ya uovu wao; kwa sababu, naam, ni kwa sababu wamezikataa hukumu zangu, na roho zao zimezichukia amri zangu. 44 Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wao; 45 lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano la baba zao, niliowaleta watoke katika nchi ya Misri mbele ya macho ya mataifa, ili kwamba niwe Mungu wao; mimi ndimi Bwana. 46 Hizi ni amri na hukumu na sheria, Bwana alizozifanya kati ya yeye na hao wana wa Israeli katika huo mlima wa Sinai kwa mkono wa Musa.
Kumb. 28)
K. Torati 28X
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. 13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya; 14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia. 15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata. 16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani. 17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia. 18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo, 20 Bwana atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo. 21 Bwana atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki. 22 Bwana atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa hari ya moto, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie. 23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma. 24 Bwana atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie. 25 Bwana atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huko na huko katika falme zote za duniani. 26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza. 27 Bwana atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa. 28 Bwana atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni; 29 utakwenda kwa kupapasa-papasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa. 30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake. 31 Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang'anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo zako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa. 32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako. 33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima; 34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona. 35 Bwana atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa. 36 Bwana atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe. 37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza Bwana. 38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila. 39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu. 40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika. 41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani. 42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo. 43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini. 44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia. 45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; 46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele; 47 kwa kuwa hukumtumikia Bwana, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; 48 kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta Bwana juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza. 49 Bwana atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake; 50 taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana; 51 naye atakula uzao wa ng'ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala maongeo ya ng'ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza. 52 Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa Bwana, Mungu wako. 53 Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa Bwana, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako. 54 Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye; 55 hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote. 56 Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatirisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake, 57 na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako. 58 Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, Bwana, MUNGU WAKO; 59 ndipo atakapofanya Bwana mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana. 60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe. 61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha torati hii, atakutia nayo Bwana juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa. 62 Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako. 63 Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi Bwana juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi Bwana juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki. 64 Bwana atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe. 65 Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; 66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; 67 asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona. 68 Bwana atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena po pote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.
. Kanuni hizi zina matokeo hata katika wakati wetu sasa.

Kudumu kwa Sheria

Kwa kuwa Amri Kumi, sheria ya maadili ni mwakisio wa tabia ya Mungu, kanuni zake siyo za muda mfupi au zinazohusiana na mazingira ila ziko kama zilivyo, zisizobadilika na zenye kusimama kwa wanadamu wote kwa nyakati zote.

Sheria kabla ya Sinai

Sheria imekuwapo kwa muda mrefu kabla ya kutolewa Amri Kumi kwa Wana wa Israeli. Kama sivyo, dhambi isingekuwapo kabla ya Sinai, kwa kuwa dhambi ni uasi (1Yoh.3:4)

1 Yohana 3:4X
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
.

Kwa kuwa Lusifa na malaika wake walitenda dhambi, hiyo hutupatia ushahidi wa kuwepo kwa sheria kabla ya uumbaji (1Pet. 2:4)

1 Petro 2:4X
4 Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
. Adamu na Hawa walipoumbwa kwa sura ya Mungu, alifanyiza amri zake ndani ya mioyo yao na kwa kuasi kwao, dhambi iliingia kwa wanadamu (Rum. 5:12)
Warumi 5:12X
12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
. Baadaye, Mungu alimsema Ibrahimu kwamba alizitii amri zake na kuzitenda (Mw.26:5)
Mwanzo 26:5X
5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
Musa alizifundisha Amri za Mungu kwa Waisraeli kabla ya kufika Sinai (Kut. 18:16)
Kutoka 18:16X
16 wakiwa na neno, hunijilia; nami naamua kati ya mtu na mwenziwe, nami nawajuvisha amri za Mungu, na sheria zake.
Ukijifunza kitabu cha Mwanzo, utagundua kwamba amri za Mungu zilijulikana kabla ya kutolewa kwenye mlima Sinai.

Sheria kwenye Mlima Sinai

Wakiwa utumwani Misri, Waisraeli hawakumtambua Mungu wa kweli (Kut. 5:2)

Kutoka 5:2X
2 Farao akasema, Bwana ni nani, hata niisikilize sauti yake, na kuwapa Israeli ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana, wala sitawapa Israeli ruhusa waende zao.
kwa kuwa waliishi katikati ya ibada ya sanamu na ufisadi. Kwa sababu hiyo walipoteza ufahamu wa utakatifu, usafi, na kanuni za kimaadili. Hadhi yao ya kuwa watumwa, iliwanyima nafasi ya kuabudu. Kuitikia kilio chao, Mungu alikumbuka agano lake na Ibrahimu na kuwaokoa kutoka kwenye tanuru la moto (Kumb.4:20)
K. Torati 4:20X
20 Bali Bwana amewatwaa ninyi, na kuwatoa katika tanuu ya chuma, katika Misri, mpate kuwa watu wa urithi kwake, kama mlivyo leo hivi.
na kuwaleta kwenye nchi ambayo wangetii amri na sheria yake (Zab. 105:43-45)
Zaburi 105:43-45X
43 Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. 44 Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; 45 Ili wazishike amri zake, na kuzitii sheria zake. Haleluya.
. Mungu akatoa amri zake moja kwa moja kwa sababu ya uovu (Gal. 3:19)
Wagalatia 3:19X
19 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.
ili dhambi ionekane kwamba ni mbaya(Rum. 7:13)
Warumi 7:13X
13 Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno.
.

Sheria ya Mungu kabla ya Kurudi kwa Yesu

Biblia huonyesha kwamba kabla ya Kristo kurejea, sheria ya Mungu itashambuliwa na Shetani na kufikia kilele chake. Atawaongoza watu wengi wasimtii Mungu (Uf. 12:9)

Ufunuo 12:9X
9 Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
. Akitumia mamlaka ya mnyama, atautaka ulimwengu umwabudu mnyama badala ya Mungu (Uf. 13:3, 12)
Ufunuo 13:3,12X
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule. 12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
.

1. Kushambuliwa sheria

Danieli sura ya 7 huonyesha mamlaka yenye kushambulia sheria ya Mungu kama Pembe Ndogo. Wasomaji wa Biblia wamezitambua falme za sura hii kuwa ni Babeli, Umedi/Uajemi, Ugiriki na Rumi. Pembe kumi ni falme kumi zilizotokea baada ya dola ya Rumi kuanguka mwaka 476BK. Maono ya Danieli yanasimama kwenye Pembe ndogo ambayo inatesa watakatifu, inanena kinyume chake aliye juu na kuazimu kubadili majira na sheria. (Dan.7:25)

Danieli 7:25X
25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
. Mamlaka hii itaendelea hadi Kristo atakaporejea. Maono yanakwisha kwa uthibitisho kwamba Mungu ataingilia kati na kuihukumu na kuingamiza Pembe Ndogo (Dan. 7:11, 26-28)
Danieli 7:11,26-28X
11 Nikatazama wakati huo; kwa sababu ya sauti ya yale maneno makubwa iliyoyasema ile pembe; nalitazama hata mnyama yule akauawa, mwili wake ukaharibiwa, akatolewa ateketezwe kwa moto. 26 Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele. 27 Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii. 28 Huu ndio mwisho wa jambo lile. Nami, Danieli, fikira zangu zilinifadhaisha, na uso wangu ulinibadilika; lakini naliliweka jambo hilo moyoni mwangu.
.

2. Watakatifu watailinda Sheria

Utii wa sheria utawatambulisha watakatifu kabla ya Kristo hajarejea mara ya pili. Wanazishika amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu (Uf. 12:17;

Ufunuo 12:17X
17 Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Uf. 14:12)
Ufunuo 14:12X
12 Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.
. Katika kujiandaa kuja kwake Yesu, watahubiri injili wakiwaalika wengine kumwabudu BWANA kama mwumbaji. (Uf. 14:6, 7)
Ufunuo 14:6, 7X
6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, 7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
. Wale watakaomwabudu kwa upendo, hawataona amri za Mungu kuwa ni nzito (1Yoh. 5:3)
1 Yohana 5:3X
3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
.

3. Hukumu za Mungu na Sheria

Hukumu ya Mungu ya mapigo saba ya mwisho kwa wasiotii inaanzia kwenye hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni (Uf. 15:5)

Ufunuo 15:5X
5 Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa;
. Israeli walilijua vema kwamba ni ile hema ambayo Musa aliifanya (Hes. 1:50, 53; 17:8; 18:2)
Hesabu 1:50, 53; 17:8; 18:2X

Hesabu 1:50, 53

50 lakini uwaweke Walawi wawe juu ya maskani ya ushahidi, na juu ya vyombo vyake vyote, na juu ya vitu vyake vyote; wao wataichukua hiyo maskani, na vyombo vyake vyote; nao wataitumikia, na kupanga hema zao kwa kuizunguka maskani pande zote. 53 Lakini Walawi watapanga hema zao kuizunguka maskani ya ushahidi pande zote, ili zisiwe hasira juu ya mkutano wa wana wa Israeli; kisha Walawi wataulinda ulinzi wa hiyo maskani ya ushahidi.

Hesabu 17:8

8 Ilikuwa siku ya pili yake, Musa akaingia ndani ya hema ya ushahidi; na tazama, ile fimbo ya Haruni iliyokuwa kwa nyumba ya Lawi ilikuwa imechipuka, imetoa michipukizi, na kuchanua maua; na kuzaa malozi mabivu.

Hesabu 18:2

2 Na ndugu zako nao, kabila ya Lawi, kabila ya baba yako, uwalete karibu pamoja nawe, ili waungwe nawe, na kukuhudumia; bali wewe na wanao pamoja nawe mtakuwa mbele ya hema ya ushahidi.
. Iliitwa hivyo kwa sababu ilibeba sanduku la ushuhuda (Kut. 26:34)
Kutoka 26:34X
34 Nawe utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana.
, ambalo lilikuwa na mbao za ushuhuda (Kut. 31:18)
Kutoka 31:18X
18 Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.
. Kwa hiyo amri kumi ni ushuhuda kwa wanadamu juu ya mapenzi Mungu (Kut. 34:28, 29)
Kutoka 34:28, 29X
28 Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi. 29 Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu amesema naye.
. Hata hivyo Ufunuo 15:5
Ufunuo 15:5X
5 Na baada ya hayo nikaona, na hekalu la hema ya ushuhuda mbinguni lilifunguliwa;
inasema sanduku la ushuhuda lililoko mbinguni.

Hii ni kwa sababu Musa aliambiwa atengeneze nakala ya hekalu lililokuwa mbinguni(Ebr. 9:23)
(Waebrania 9:23;X
Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.
Ebr. 8:1-5),
Ebr. 8:1-5X
1 Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, 2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. 3 Maana kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angekuwa juu ya nchi, asingekuwa kuhani; maana wako watoao sadaka kama iagizavyo sheria; 5 watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
. Amri Kumi halisi zimetunzwa pale. Kwamba hukumu ya mwisho itatokana na wanadamu kutomtii Mungu, kunafanya amri za Mungu kuwa za kuendelea daima. Kitabu cha ufunuo pia kinaonyesha kwamba hekalu la mbinguni lilifunguka na Sanduku la Agano likaonekana. (Uf. 11:19)
Ufunuo 11:19X
19 Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana.
. Hekalu la duniani lilikuwa na sanduku la ushuhuda lenye amri za agano (Kut. 34:27; cf.
(Kut. 34:27; cf.X
27 Bwana akamwambia Musa, Andika maneno haya; kwa kuwa mimi nimefanya agano nawe, na pamoja na Israeli, kwa mujibu wa maneno haya.
Hes. 10:33;
Hesabu 10:33X
33 Basi wakasafiri kutoka penye mlima wa Bwana safari ya siku tatu; na sanduku la agano la Bwana likatangulia mbele yao mwendo wa siku tatu, ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.
Kumb. 9:9)
K. Torati 9:9X
9 Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano Bwana alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.
. Hivyo ni dhahiri kwamba hukumu ya Mungu ya mwisho itahusu Sanduku la Agano lake lenye Amri zake asilia mbinguni (Uf. 11:18)
Ufunuo 11:18X
18 Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.

Sheria na Injili

Wokovu ni karama inayotufikia kwa neema kwa njia ya imani, siyo kwa matendo ya sheria (Efe. 2:8)

Waefeso 2:8X
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
. Siyo tendo la sheria wala juhudi hata kama inasifiwa sana, wala siyo matendo mema, yawe mengi au machache, ya kujinyima au vinginevyo kwamba yaweza kumtakasa mwenye dhambi.(Tit. 3:5;
Tito 3:5X
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu;
Rum. 3:20)
Warumi 3:20X
20 kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.
. Maandiko matakatifu yanaelezea uhusiano wa sheria na injili, kila kimoja, kikishikilia kingine.

Sheria na Injili kabla ya Sinai

Adam na Hawa walipotenda dhambi, walijua nini ni hatia, hofu na hitaji. (Mwa. 3:10).

MWanzo 3:10.X
10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Mungu aliwapa walichohitaji, kurejesha mahusiano yake na wao pasipo kutangua sheria yake. Injili ni kwamba mzao wa mwanamke ndiye atakayeleta ushindi dhidi ya dhambi (Mwa. 3:15)
Mwanzo 3:15X
15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
. Kwa kuamini kwamba kifo cha mnyama kiliwaondolea dhambi, walikubali kafara ya Kristo atakayekuja kuwafia, na kwamba wokovu wao ni kwa neema peke yake. Injili ndilo agano alilofanya Mungu na aliowachagua (Mw. 12:1-3; 15:4, 5; 17:1-9)
Mwanzo 12:1-3; 15:4, 5; 17:1-9X

Mwanzo 12:1-3

1 Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; 2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; 3 nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.

Mwanzo 15:4, 5

4 Nalo neno la Bwana likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5 Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Mwanzo 17:1-9

1 Abramu alipokuwa mtu wa miaka tisini na kenda, Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu, ukawe mkamilifu. 2 Nami nitafanya agano langu kati ya mimi na wewe, nami nitakuzidisha sana sana. 3 Abramu akaanguka kifudifudi. Mungu akamwambia, akasema, 4 Mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi, 5 wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Ibrahimu, kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi. 6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, nami nitakufanya kuwa mataifa, na wafalme watatoka kwako. 7 Agano langu nitalifanya imara kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako. 8 Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao. 9 Mungu akamwambia Ibrahimu, Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako.
. Mara nyingi iliambatana na sheria (Mw.18:18, 19; 26:4, 5)
Mwanzo 18:18, 19; 26:4, 5X

Mwanzo 18:18, 19

18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? 19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake.

Mwanzo 26:4, 5

4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. 5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
. Amana ya agano ni Mwana wa Mungu aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. (Uf. 13:8)
Ufunuo 13:8X
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
. Neema ya Mungu ilianza kutenda kazi mara dhambi ilipoingia. Mtunga Zaburi anasema, “Bali fadhili za BWANA zina wamchao, Tangu milele, hata milele--- Maana wale walishikao agano lake, na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye (Zab. 103: 17,18)
Zaburi 103: 17, 18X
17 Bali fadhili za Bwana zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana; 18 Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.
.

Sheria na Injili Sinai

Utangulizi wa Sheria unamtambulisha Mungu akiwa mkombozi (Kut.20:1)

Kutoka 20:1X
1 Mungu akanena maneno haya yote akasema,
. Baada ya kuitoa Sheria, Mungu aliagiza Israeli wajenge madhabahu na kumtolea kafara ili wapatanishwe na Mungu na kupokea mibaraka yake (Kut. 24:9 mpaka 31:18). Wakati Amri Kumi ziliwekwa ndani ya Sanduku la Agano, kitabu cha sheria za maadhimisho kiliwekwa kando ya Sanduku kuwa ushuhuda (Kumb. 31:26)
K. Torati 31:26X
26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.
.

Sheria na Injili Baada ya Msalaba

Kama wakristo wengi walivyoona, kifo cha Kristo kiliondosha sheria ya maadhimisho na kuimarisha sheria ya maadili. Ushahidi ni kama ifuatavyo: -

1. Sheria ya Maadhimisho

Kristo alipokufa, alitimiza alama za kuashiria kwa unabii juu ya mfumo wa kafara. Mfano ulikutana na kitu halisi. Kabla Yesu hajazaliwa, ilitabiriwa kwamba atakomesha mfumo wa kafara (Dan. 9:27)

Danieli 9:27X
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.
. Siku aliyokufa, pazia la hekalu liliraruliwa toka juu hadi chini kuonyesha kukoma umuhimu wa ibada za kafara za hekalu la duniani (Mt. 27:51)
Mathayo 27:51X
51 Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;
. Ingawa Sheria ya Maadhimisho ilitimiza kusudi muhimu kabla ya Kristo, baada ya Yesu kufa msalabani, ilibakia kuwa kivuli cha mambo yajayo (Ebr. 10:1)
Waebrania 10:1X
1 Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
. Iliwekwa kwa kipindi kifupi hadi wakati wa matengenezo (Ebr. 9:10;
Waebrania 9:10X
10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
Gal. 3:19)
Wagalatia 3:19X
19 Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.
hadi Kristo alipokufa kama kafara halisi.

Kifo cha Yesu kilikomesha mamlaka ya mfumo wa kafara na kuugongomelea mslabani (Kol. 2:14, cf.

Wakolosai 2:14X
14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;
, cf. Kumb. 31:26)
K. Torati 31:26X
26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako.
. Hivyo haikuwa muhimu kuendelea kutoa kafara zisizosafisha nia tena (Ebr. 10:4; 9:9; 14)
Waebrania 10:4; 9:9-14X

Waebrania 10:4

4 Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

Waebrania 9:9-14

9 ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, 10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya. 11 Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, 12 wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. 13 Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; 14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
.

Hakuna haja tena ya Sheria ya Madhimisho ihusuyo vyakula, vinywaji, na maadhimisho ya Pasaka, Pentekoste, miezi mipya wala sabato za sikukuu. (Kol. 2:16; cf.
Wakolosai 2:16X
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
; cf. Ebr. 9:10)
Waebrania 9:10X
10 kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya.
ambavyo vilikuwa vivuli vya mambo yajayo (Kol. 2:17)
Wakolosai 2:17X
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Kama Wayahudi walivyotafsiri, Sheria ya Maadhimisho ilikuwa kikwazo, chenye kutenga Wamataifa hivyo Kifo cha Kristo kilivunja kiambaza na kuunda familia moja iliyoungana katika mwili moja kupitia msalaba (Efe. 2:14-16)
Waefeso 2:14-16X
14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. 15 Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. 16 Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.

2. Amri Kumi na Msalaba

Kifo cha Yesu kilikomesha sheria ya maadhimisho na kuimarisha mamlaka ya Amri ya Maadili – Amri Kumi. Waumini wanakuwa watumishi wa haki na siyo watumwa wa dhambi (Rum. 6:14)

Warumi 6:14X
14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
. Hivyo Wakristo hawatii Amri za Mungu ili waokolewe, badala yake wanatii amri kwa sababu wamekwisha kuokolewa. Hawaoni haja ya kutenda dhambi hata kama neema iliyowaokoa ni kubwa (Rum.6:1)
Warumi 6:1X
1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?
Hakuna hukumu kwao kwa sababu wanatembea katika roho (Rum. 8:1)
Warumi 8:1X
1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
.

Utii wa Sheria

Watu hawawezi kwa nguvu zao wenyewe kujipatia wokovu. Wokovu hupatikana kwa njia ya neema ya Mungu peke yake (Ef.2:8)

Waefeso 2:8X
8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
. Hata hivyo, utii wa sheria ni matunda kwamba tumeokolewa kwa neema (Tit. 2:11, 12)
tito 2:11, 12X
11 Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
.

Kristo na Sheria

Kristo aliziheshimu sana Amri Kumi. Ndiye aliyezitoa Sinai akiwa Mimi Niko (Yoh. 8:58;
Yohana 8:58X
58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
Kut.31:4)
Kutoka 31:4X
4 ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,
na utume wake ilikuwa kuitukuza Sheria(Isa.42:21)
Isaya 42:21X
21 Bwana akapendezwa, kwa ajili ya haki yake, kuitukuza sheria, na kuiadhimisha.
. Maneno ya Zaburi yanaonyesha nia ya Yesu juu ya Sheria “Kuyafanya mapenzi yako Ee Mungu wangu ndiyo furaha yangu; Naam sheria yako imo moyoni mwangu (Zab. 40:8)
Zaburi 40:8X
8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
. Aliianzisha imani iliyojali madai ya Amri za Mungu. Paul anauliza, je twaibatilisha torati kwa ajili ya hayo? Na anajibu la, badala yake tunaithibitisha (Rum. 3: 31)
Warumi 3:31X
31 Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.
. Yesu alimjibu kijana tajiri kwamba ikiwa anataka kuupata uzima wa milele, zishike amri (Mt. 19:17)
Mathayo 19:17X
17 Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
. Na ndiye aliyefundisha kwamba wasiofanya mapenzi ya Baba yake, hawataruhusiwa kuingia kwenye ufalme wa mbinguni (Mt. 7:21-24)
Mathayo 7:21-24X
21 Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23 Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;

Yeye mwenyewe aliitii sheria na akaatuusia, amin nawaambia yodi moja wala nukta moja haitaondoka kwenye torati hata yote yatimie (Mt. 5:18)
Mathayo 5:18X
18 Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng'ambo.
Akafundisha kwamba msingi wa Sheria ni upendo, kwa Mungu na kwa jirani (Mt. 22:36-40)
Mathayo 22:36-40X
36 Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. 38 Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. 39 Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. 40 Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
. Ndiye aliyesema anatoa amri mpya, ya kupendana (Yoh. 13:34)
Yohana 13:34X
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
na akaagiza mpendane, kama mimi nilivyowapenda ninyi (Yoh. 15:12)
Yakobo 15:12X
12 Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.
. Utii huonyesha upendo wetu kwa Mungu “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” (Yoh. 14:15)
Yohana 14:15X
15 Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu (Yoh. 15:10)
Yohana 15:10X
10 Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
. Vivyo hivyo, tukiwapenda watu wa Mungu, huwa tunampenda Mungu (1Yoh. 2:3)
1 Yohana 2:3X
3 Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.
. Hatutaweza lolote tusipokaa ndani yake (Yoh. 15:4, 5)
Yohana 15:4, 5X
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. . Kwa kweli maisha yetu yatakuwa yamesulubiwa pamoja na Kristo (Gal. 2:20)
Wagalatia 2:20X
20 Nimesulibiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.
na sheria yake itaandikwa mioyoni mwetu (Ebr. 8:10)
Waebrania 8:10X
10 Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israeli Baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao, Nao watakuwa watu wangu.

Baraka ya Kutii

Utii hukuza tabia ya kikristo na huleta afya, na kutufanya tukue hata tufanane na Kristo (1Pet. 2:2;

1 Petro 2:2X
2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
2Kor. 3:18)
2 Wakorintho 3:18X
18 Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
. Mabadiliko haya, ni ushuhuda mwema kwa nguvu ya Kristo. Heri wanaomtii Mungu (Zab. 119:1)
Zaburi 119:1X
1 Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
, wanaotafakari sheria yake mchana na usiku (Zab. 1:2)
Zaburi 1:2X
2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
. Baraka za utii ni nyingi: -

(1)kupata hekima (Zab. 119:98, 99),
Zaburi 119:98, 99X
98 Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote. 99 Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo.
(2) amani (Zab. 119:165;
Zaburi 19:165X
165 Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
Isa. 48:18)
Isaya 48:18X
18 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
, (3) haki (Kumb. 6:25;
K. Torati 6:25X
25 Tena itakuwa haki kwetu, tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya Bwana, Mungu wetu, kama alivyotuagiza.
Isa. 48:18)
Isa. 48:18)X
18 Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
(4) moyo safi na adilifu (Mith. 7:1-5)
Mithali 7:1-5X
1 Mwanangu, yashike maneno yangu, Na kuziweka amri zangu akiba kwako. 2 Uzishike amri zangu ukaishi, Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako. 3 Zifunge katika vidole vyako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. 4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. 5 Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
, (5) ufahamu wa ukweli (Yoh. 7:17)
Yohana 7:17X
17 Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
, (6) kulindwa na maradhi (Kut. 15:26)
Kutoka 15:26X
26 akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
, (7)maisha marefu (Mith. 3:1, 2; 4:10, 22)
Mithali 3:1, 2; 4:10, 22X

Mithali 3:1, 2

1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. 2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.

Mithali 4:10, 22

10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.

Mithali 4:10, 22

10 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. 22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
na (8) uhakika kwamba sala zitajibiwa (1Yoh. 3:22;
1 Yohana 3:22X
22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
Zab. 66:18)
Zaburi 66:18X
18 Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.

Mungu anapotualika tumtii, ametupatia ahadi nyingi (Law. 26:3-10;
M. Walawi 26:3-10X
3 Kama mkienda katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyafanya; 4 ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake, na nchi itazaa maongeo yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake. 5 Tena kupura nafaka kwenu kutaendelea hata wakati wa kuvuna zabibu, na kuvuna zabibu kutaendelea hata wakati wa kupanda mbegu; nanyi mtakula chakula chenu na kushiba, na kuketi katika nchi yenu salama. 6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala wala hapana atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu. 7 Nanyi mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele zenu kwa upanga. 8 Na watu watano wa kwenu watawafukuza watu mia, na watu mia wa kwenu watawafukuza watu elfu kumi; na adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga. 9 Nami nitawaelekezea uso wangu, na kuwapa uzazi mwingi, na kuwaongeza; nami nitalithibitisha agano langu pamoja nanyi. 10 Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya.
Kumb. 28:1-12)
K. Torati 28:1-12X
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
. Tunapomtii, tunakuwa tunu kwake na hutupa ukuhani wa kifalme (Kut.19:5, 6; cf.
Kutoka 19:5, 6X
5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, 6 nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
; cf. 1Pet. 2:5, 9)
1 Petro 2:5, 9X
5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu; 6 tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya; 7 akamwokoa Lutu, yule mwenye haki aliyehuzunishwa sana na mwenendo wa ufisadi wa hao wahalifu; 8 maana mtu huyu mwenye haki akikaa kati yao, kwa kuona na kusikia, alijitesa roho yake yenye haki, siku baada ya siku, kwa matendo yao yasiyo na sheria; 9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
tukiinuliwa kuliko mataifa kwa kuwa ni kichwa na siyo mkia (Kumb. 28:1, 13)
K. Torati 28:1, 13X
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani; 2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako. 3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani. 4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako. 5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga. 6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo. 7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. 8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako. 9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake. 10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. 11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa. 12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe. 13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728