Mungu Roho Mtakatifu

Utangulizi


Mungu Roho Mtakatifu wa milele alikuwa mtendani pamoja na Baba na Mwana katika Uumbaji, katika Yesu kufanyika mwili na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa Maandiko Matakatifu. Alijaza maisha ya Yesu Kristo na uwezo. Huwavuta na kuasadikisha wanadamu; na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Alipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hueneza karama za Roho kwa kanisa., na kuwapa uwezo wa kumshuhudia Kristo, na kwa ulinganifu na Maandiko Matakatifu hongoza katika kweli yote.” (Mwa.1:1, 2; Luk.1:35; 4:18; Mdo.10:38; 2Pet.1:21; 2Kor.3:18; Efe.4:11, 12; Mdo. 1:8; Yoh.4:16-18, 26; 15:26, 27; 16:7-13)

Ijapokuwa kusulubiwa kuliwachanganya, kuwanyong’onyeza, na kuwatisha wafuasi wa Kristo, ufufuo ulileta asubuhi katika maisha yao. Kristo alipovunja vifungo vya kifo, ufalme wa Mungu ulileta nuru katika mioyo yao. Sasa moto usiozimika uliwaka mioyoni mwao. Tofauti ambazo wiki chache zilizopita zilileta kuta za vipingamizi, ziliyeyuka. Waliungamiana makosa wao kwa wao na kufungua mioyo yao kikamilifu kumpokea Yesu, mfalme wao aliyepaa. Umoja wa kundi hili ambalo awali lilikuwa limetawanyika, uliongezeka kadiri walivyotumia wakati wao katika maombi. Siku moja isiyosahaulika, walipokuwa wakimsifu Mungu, ndipo kelele za ngurumo za mvua ya dhoruba ilipowafikia. Kana kwamba mwako ulio mioyoni mwao unaonekana, miale ya moto iliwashukia kila moja wao. Kama moto unaowaka, Roho Mtakatifu aliwafikia.

Wakiwa wamejazwa Roho Mtakatifu wafuasi hawa hawakuweza kuficha upendo wao wa dhati na furaha yao katika Yesu. Kwa hamu kubwa na kwa uwazi, walianza kuhubiri habari njema za wokovu. Wakishangazwa kwa sauti, umati wa watu ukaliendea jengo walimokuwamo. Wakiwa wamechanganyikiwa na kujawa mshangao, walisikia Wagalilaya wakisema habari njema za Yesu katika lugha zao wenyewe. “Hatuelewi”, baadhi yao walisema, wengine wakajaribu kupenyeza uvumi, “wamelewa”. “Siyo hivyo”, Petro akapaza sauti yake mbele ya umati, “sasa ni saa tatu za asubuhi, haiwezekani kukawa na kulewa”. Mlichosikia na kukiona kikitokea ni kwa sababu Yesu Kristo aliyefufuka ameinuliwa na kuketi mkono wa kuume wa Mungu na amegawa Roho Mtakatifu. (Mdo. 2).

Roho Mtakatifu ni Nani?

Biblia hufunua kuwa Roho Mtakatifu ni nafsi na siyo nishati isiyo nafsi. Kauli kama “ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi” (Mdo.15:28), hufunua kuwa waumini wa awali walimwona Yeye kuwa nafsi. Kristo naye alimtaja kuwa ni nafsi “atanitukuza mimi kwa kuwa atatwaa katika yangu na kuwapasha habari” (Yoh.16:14). Maandiko yakielezea Utatu Mtakatifu, humtaja Roho Mtakatifu kuwa nafsi (Mt.28:19; 2Kor.13:14). Roho Mtakatifu ni nafsi kwa kuwa hushindana (Mwa.6:3), hufundisha (Luk.12:12), husadikisha (Yoh.16:8), huendesha shughuli za kanisa (Mdo. 13:2), husaidia kuombea (Rum.8:26), huvuvia (2Pet.1:21) na kutakasa (1:1:2). Matendo haya, hayafanywi na nguvu ya Mungu bali na Nafsi ya Roho Mtakatifu.

Roho Mtakatifu Kwa Uhalisi ni Mungu

Maandiko Matakatifu humhesabu Roho Mtakatifu kuwa ni Mungu. Petro alimwambia Anania ‘kwa kumwambia uwongo Roho Mtakatifu alikuwa hamwambii uongo mwanadamu bali Mungu’ (Mdo. 5:3, 4). Yesu aliitaja dhambi isiyosameheka kuwa ni ya kumkufuru Roho Mtakatifu (Matt.12:31, 32). Hili litakuwa kweli ikiwa tu, Roho Mtakatifu ni Mungu.

Biblia huzielezea sifa za Uungu kwa Roho Mtakatifu. Ni uzima “Roho wa uzima” (Rum.8:2). Ni Kweli – “Roho wa Kweli” (Yoh.16:13), upendo wa Roho (Rum.15:30), na Roho Mtakatifu wa Mungu (Efe.4:30), huonesha upendo na utakatifu ni sehemu ya asili yake.

Roho Mtakatifu hupatikana wakati wote na mahali pote. Hugawa karama za roho kadiri apendavyo (1Kor.12:11). Yupo wakati wote. “Atakaa na watu wake milele” (Yoh.14:16). Hakuna ambaye aweza kukwepa mvuto wake (Zab.139:7-10). Roho Mtakatifu anajua yote kwa sababu aweza kuyachunguza mafumbo ya Mungu kwa sababu anayajua (1Kor.2:10, 11).

Kazi za Mungu pia zinahusishwa na Roho Mtakatifu. Uumbaji na ufufuo vinamhusisha Yeye (Ayu. 33:4). “Waipeleka Roho yako, wanaumbwa, (Zab.104:30). Roho aliyemfufua Kristo katika wafu, ataihuisha miili iliyo katika hali ya kufa. (Rum.8:11). Ni Mungu apatikanaye wakati wote ndiye angeweza kutenda muujiza wa wa kumleta Mungu Kristo kwa mwanadamu - Mariam. Siku ya Pentekoste, Roho alimfanya Mungu–Mwanadamu pekee Yesu, aweze kupatikana katika ulimwengu wote kwa wanaopenda kumpokea. Roho Mtakatifu yuko sawa na Baba na Yesu katika kanuni ya ubatizo (Mt.28:19) na katika baraka ya mitume (2Kor.13:14) na katika kufunua karama za roho (1Kor.13:14).

Roho Mtakatifu na Utatu Mtakatifu

Tangu milele Mungu Roho Mtakatifu aliishi katika Utatu Mtakatifu akiwa wa tatu. Pamoja na kuwa sawa, kuna mgawano wa majukumu katika Utatu Mtakatifu. (Angalia somo la Mungu Mwana). Ukweli kumhusu Roho Mtakatifu hueleweka vema kupitia Yesu Kristo. Matendo yake katika historia, humwelekea Kristo katika utume wa wokovu. Alihusika katika kuzaliwsa kwa Yesu (Luk.1:35). Alithibitisha utume wake katika ubatizo (Mt.3:16, 17) and kuleta mafao ya kafara ya Kristo na ufufuo kwa wanadamu (Rum.8:11). Anaoneka kuwa Mtekelezaji. Baba alipomtoa Yesu kwa ulimwengu (Yoh.3:16), Roho aliwezesha mimba ifanyizwe (Mt.1:18-20), akaufanya mpango utekelezeke. Kuhusika kwa Roho katika Uumbaji, kunaonekana kwa kuweko kwake tangu mwanzo (Mwa.1:2). Asili ya uhai na kuudumisha kunategemea utendaji wake. (Ayu.34:14, 15; cf. 33:4). Tunauona utendaji wa Roho katika watu binafsi, anapowaumba wawe watoto wa Mungu.

Roho Aliyeahidiwa

Tuliumbwa ili Roho Mtakatifu apate maskani katika miili yetu (1Kor.3:16). Adamu na Hawa walijitenga na Edeni na Roho akaaye ndani, hadi Mungu akasema wakati wa gharika “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele (Mwa.6:3). Katika Agano la Kale aliwapatia baadhi ya watu kufanya kazi maalum (Hes.24:2; Amu.6:34; 1Sam.10:6). Nyakati kadhaa huwa ndani ya watu (Kut. 31:3; Isa. 63:11). Pasipo shaka waumini wana ufahamu wa kuwapo kwake, hata hivyo ilitabiriwa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu kwa wote wenye mwili (Yoe.2:28), wakati ambao udhihirisho wa Roho utaleta enzi mpya.

Wakati ulimwengu ulipokuwa kwenye mikono ya mnyang’anyi umwagaji wa Roho Mtakatifu ulipaswa kusubiri. Akionyesha utume wa Kristo, Yohana Mbatizaji alisema kuwa Yesu atabatiza kwa Roho Mtakatifu (Mt.3:11). Injili hazisemi kuwa Yesu alibatiza kwa Roho. Lakini kabla ya kifo chake, Yesu aliahidi wafuasi wake kuwa atamwomba Baba awapatie Msaidizi mwingine, akae nao milele, Roho wa Kweli. (Yoh.14:16, 17). Je, ubatizo ulipatikanamsalabani? Hapana. Ni mpaka baada ya kufufuka kwake ndipo alipowapa Roho Mtakatifu (Yoh.20:22).

Aliwaambia wasubiri Yerusalemu, hadi wapatiwe uwezo (Luk.24:49). Roho aliyepokewa, angewezesha wafuasi kuwa mashahidi hadi mwisho wa nchi. (Mdo.1:8). Yohana alidokeza Roho hakutolewa kabla ya Yesu kutukuzwa (Yoh.7:39). Enzi mpya ilianza baada ya Yesu kuketi mkono wa kuume wa Mungu. Petro alisema, alimwaga Roho Mtakatifu (Mdo.2:33) kwa waliotazamia kwa hamu kutimizwa kwa jambo hili wakiwa wamoja (Mdo.1:5, 14). Katika siku ya Pentekoste, siku hamsini tangu Kalvari, enzi mpya ilianza: “Kukaja ghafla toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu, ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote, waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” (Mdo.2:2-4). Utume wa Yesu na Utume wa Roho Mtakatifu havikuingiliana. Ujazo wa Roho Mtakatifu haukutimilika kwa kiwango kikamilifu hadi Yesu alipokamilisha utume wake. Na kwa upande mwingine, Yesu alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Mt.1:8-21), alibatizwa na Roho Mtakatifu (Mk.1:9, 10), Aliongozwa na Roho (Luk.4:1), alitenda miujiza kwa Roho Mtakatifu (Mt.12:24-32), akajitoa mwenyewe Kalvari kwa Roho Mtakatifu (Ebr.9:14, 15) na kwa sehemu, alifufuliwa na Roho Mtakatifu (Rum.8:11). Yesu alikuwa wa kwanza kujazwa kwa ujazo wote, Roho Mtakatifu. Na ukweli wa ajabu ni kwamba, Yuko tayari kumjaza yeyote Roho wake, mtu anayemhitaji kwa bidii.

Utume wa Roho Mtakatifu

Usiku kabla ya kifo cha Kristo, maneno yake kuhusu kuondoka kwake katika kipindi kifupi kijacho, yaliwafanya wanafunzi wake wafadhaike. Haraka aliwaahidi kuwapa Roho Mtakatifu na hatawaacha yatima. (Yoh.14:18)

Asili ya Utume

Agano Jipya humdhihirisha Roho Mtakatifu katika njia maalum. Anaitwa Roho wa Yesu (Mdo.16:7), Roho wa Mwana (Gal.4:6), Roho wa Mungu (Rum.8:9), Roho wa Kristo (Rum.8:9; 1Pet.1:11) na Roho wa Yesu Kristo (Fil.1:19). Ni nani aliyeanzisha utume wa Roho Mtakatifu, ni Yesu Kristo au Mungu Baba?

Yesu alipodhihirisha asili ya utume wa Roho Mtakatifu kwa ulimwengu uliopotea, alitaja vyanzo viwili. Kwanza kwa Baba (14:16; cf 15:26). Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni ahadi ya Baba (Mdo.1:4). Pili, Yesu alijirejea Yeye kama chanzo. Nitamtuma kwenu (Yoh.16:7). Hivyo Roho Mtakatifu alitoka kwa Baba na kwa Yesu.

Utume wake kwa Ulimwengu

Twaweza kukubali Ubwana wa Kristo kwa kupitia Roho Mtakatifu pekee (1Kor.12:3). Twahakikishiwa kwa Roho Mtakatifu kuwa Nuru ya Kweli yamwangazia kila mtu ajaye ulimwenguni (Yoh.1:9). Utume wake ni kusadikisha ulimwengu juu ya dhambi na haki na hukumu (Yoh.16:8). Kwanza anatusadikisha dhambi kubwa ya kutomwamini Yesu (Yoh.16:9). Pili Roho hutushurutisha tuipokee haki ya Kristo. Tunapotubu twazaliwa upya kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu (Yoh.3:5). Sasa maisha yetu huwa mapya kwa kuwa tumekuwa maskani ya Roho Mtakatifu.

Utume wake kwa Waumini

Wingi wa mafungu ya Biblia kuhusu utendaji wa Roho Mtakatifu unahusiana na uhusiano wake na watu wa Mungu. Mvuto wake wa kutakasa (1Pet.1:2) lakini haiwezekani kuendelea kuwa naye pasipo kutimiza masharti kadha wa kadha. Petro anasema Mungu amemtoa Roho kwa wale wanaoendelea kumtii (Mdo. 5:32). Hivyo waumini wanaonywa wasije wakampinga, wakamhuzunisha, wakamzima Roho Mtakatifu. (Mdo7:51, Efe.4:30; 1Thes.519).

1. Husaidia waumini:

Alipomtambulisha Roho, Kristo alisema atakuwa Msaidizi (Yoh.14:16). Tunaonywa tusitende dhambi na kama tukitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba. (1Yoh.2:1). Hivyo, Roho hutuongoza kwa Kristo na neema yake. Hiyo ndiyo maana huitwa Roho wa neema (Ebr.10:29). Ndiye anayefanya neema iokoayo ya Kristo ipate matumizi kwa wanadamu. (1Kor.15:10; 2Kor.9:14; Yak.4:5, 6).

2. Huleta ukweli wa Kristo:

Kristo alimwita Roho Mtakatifu Roho wa Kweli (Yoh.14:17; 15:26; 16:13). Jukumu lake jingine ni kutukumbusha aliyotuambia Kristo (Yoh.14:26) na kutuongoza kwenye kweli (Yoh.16:13). Ujumbe wake unamshuhudia Kristo (Yoh.15:26). Pia humtukuza Kristo kwa kuwa hutwaa ya Kristo na kutupasha habari (Yoh.16:13, 14)

3. Huleta kuwepo kwa Kristo:

Yesu alisema ni bora aondoke ili Roho aje (Yoh.14:16, 17; Yoh. 16:17). Akiwa katika umbo la kibinadamu, Yesua asingeweza kupatikana mahali pote na wakati wote. Aliahidi kutokutelekeza watu wake (Ebr.13:5; Mt. 28:20). Kwa kutambua ukweli huo, Roho amepewa jina ambalo halijapata kutumika kwenye Agano la Kale, Roho wa Kristo (Filp.1:19). Kwa njia ya Roho Mtakatifu, Baba na Mwana hufanya maskani kwa wanadamu (Yoh.14:23)

4. Hongoza Shughuli za Kanisa:

Kwa kuwa Roho Mtakatifu ndiye Msaidizi wa Kristo, ndiye aliongozaye Kanisa. Alihusika wakati wa Mitume, kwa kuomba na kufunga wakachagua Wamishenari (Mdo.13:1-4). Waliochaguliwa walikuwa wamejawa na Roho (Mdo.13:9, 52). Matendo yao yalithibitiwa na Roho (Mdo.16:6, 7). Paulo alionya Wazee wa Kanisa kuwa walichaguliwa na Roho (Mdo.20:28). Roho Mtakatifu alitatua mgogoro wa kanisa, “Imempendeza Roho Mtakatifu na sisi…” (Mdo.15:28).

5. Hulipa Kanisa Karama maalum:

Roho Mtakatifu huwajaza watu wa Mungu karama maalum. Katika Agano la Kale, aliwajaa watu wa Mungu na kutenda maajabu (Amu.3:10; 6:34; 11:29; nk) na uwezo wa kutabiri (Hes.11:17, 25, 26; 2Sam.23:2). Roho alimjia Sauli na Daudi walipotiwa mafuta (1Sam.10:6,10; 16:13). Kwa watu wengine Roho aliwapa ujuzi maalum (Kut.28:3; 31:3; 35:30-35). Katika Kanisa la Awali, Roho Mtakatifu aligawa karama kadiri alivyoona yeye inafaa ili kazi ya utume itendeke na kulinufaisha kanisa zima (Mdo.2:38; 1Kor.12:7-14; Efe.4:11, 12) na kukamilisha utume wa injili (Mdo.1:8).

Hujaa kwenye mioyo ya Waumini:

Kwa swali la Paulo, je mlipokea Roho Mtakatifu mlipobatizwa, jibu la la, lilimfanya kuwabatiza na waliobatizwa walijawa Roho Mtakatifu. (Mdo.19:2, 6). Yesu alizungumzia umuhimu wa kubatizwa kwa maji na kwa Roho (Yoh.3:5). Kabla ya kupaa, aliagiza ubatizo unapofanywa, ufanywe kwa Jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (Mt.28:19). Petro anasema Roho Mtakatifu hupokewa wakati wa ubatizo (Mdo.2;38), jambo ambalo linathibitishwa na Paulo. (Efe.518). Roho hutubadilisha, tufanane na Mungu (Tit.3:5, 6). Roho ni muhimu katika maisha ya kikristo na pasipo yeye hatutaweza kufanya lolote. (Yoh.15:5).

×0001020304050607080910111213141516171819202122232425262728
Mwanzo 1:1, 2X
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Luka 1:35X
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Luka 4:18X
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
Matendo 10:38X
38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
2 Petro 1:21X
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
2 Wakorintho 3:18X
8 je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?
Waefeso 4:11, 12X
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
Matendo 1:8X
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Yohana 4:16-18X
16 Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. 17 Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; 18 kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.
Yohana 15:26, 27X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27 Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.
Yohana 16:7-13X
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; 10 kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. 12 Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. 13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Matendo 2X
1 Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. 2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka. 5 Na walikuwako Yerusalemu Wayahudi wakikaa, watu watauwa, watu wa kila taifa chini ya mbingu. 6 Basi sauti hii iliposikiwa makutano walikutanika, wakashikwa na fadhaa, kwa kuwa kila mmoja aliwasikia wakisema kwa lugha yake mwenyewe. 7 Wakashangaa wote, wakastaajabu wakiambiana, Tazama, hawa wote wasemao si Wagalilaya? 8 Imekuwaje basi sisi kusikia kila mtu lugha yetu tuliyozaliwa nayo? 9 Warparthi na Wamedi na Waelami, nao wakaao Mesopotamia, Uyahudi na Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia na Pamfilia, Misri na pande za Libia karibu na Kirene, na wageni watokao Rumi, Wayahudi na waongofu, 11 Wakrete na Waarabu; tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu. 12 Wakashangaa wote wakaingiwa na shaka, wakiambiana, Maana yake nini mambo haya? 13 Wengine walidhihaki, wakisema, wamelewa kwa mvinyo mpya. 14 Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu. 15 Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana; 16 lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli, 17 Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. 19 Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. 20 Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. 21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. 22 Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua; 23 mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua; 24 ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao. 25 Maana Daudi ataja habari zake, Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote, Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike. 26 Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini. 27 Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu; Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu. 28 Umenijuvisha njia za uzima; Utanijaza furaha kwa uso wako. 29 Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo. 30 Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi; 31 yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu. 32 Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. 33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia. 34 Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume. 35 Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako. 36 Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37 Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. 42 Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali. 43 Kila mtu akaingiwa na hofu; ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. 44 Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja, na kuwa na vitu vyote shirika, 45 wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. 46 Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe, 47 wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
Matendo 15:28X
28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima,
Yohana 16:14X
14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Mwanzo 1:2X
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
2 Wakorintho 13:14X
14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.
Mwanzo 6:8X
8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.
Luka 12:12X
12 kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
Yohana 16:8X
8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Matendo 13:2X
2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
Warumi 8:6X
6 Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
2 Petro 1:21X
21 Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
1 Petro 1:2X
2 kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.
Matendo 5:3, 4X
3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
Mathayo 12:31, 32X
31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. 32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Warumi 8:2X
2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti.
Yohana 16:13X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Warumi 15:30X
30 Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu;
Waefeso 4:30X
30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
1 Wakorintho 12:11X
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.
Yohana 14:16X
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Zaburi 139:7-10X
7 Niende wapi nijiepushe na roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako? 8 Kama ningepanda mbinguni, Wewe uko; Ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko. 9 Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; 10 Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika.
2 Wakorintho 10, 11X

2 Wakorintho 10

1 Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu; 2 naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili. 3 Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 4 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 5 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 6 tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia. 7 Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi. 8 Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika; 9 nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. 10 Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu. 11 Mtu kama huyo na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo. 12 Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. 13 Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu. 14 Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo; 15 wala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, yaani, katika taabu za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu, na kupata ziada; 16 hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa. 17 Lakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana. 18 Maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye, bali yeye asifiwaye na Bwana.

2 Wakorintho 11

1 Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami. 2 Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi. 3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. 4 Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! 5 Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu. 6 Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu. 7 Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira? 8 Naliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi. 9 Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda. 10 Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. 11 Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua. 12 Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi. 13 Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 15 Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 16 Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo. 17 Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu. 18 Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu. 19 Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha. 20 Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni. 21 Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri. 22 Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 23 Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. 24 Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 25 Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; 26 katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; 27 katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. 28 Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote. 29 Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe? 30 Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu. 31 Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo. 32 Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata; 33 nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake.
Ayubu 33:4X
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
Zaburi 104:30X
30 Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.
Warumi 8:11X
11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Mathayo 28:19X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
2 Wakorintho 11:14X
14 Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.
1 Wakorintho 12:4-6X
4 Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. 5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. 6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Luka 1:35X
35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Mathayo 6:16, 17X
16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
Warumi 8:11X
11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Yohana 3:16X
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Mathayo 1:18-20X
18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Mwanzo 1:2X
2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Ayubu 34:14, 15X
14 Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake; 15 Wenye mwili wote wataangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
Ayubu 33:4X
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
1 Wakorintho 3:16X
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Mwanzo 6:3X
3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Hesabu 24:2X
2 Balaamu akainua macho yake akawaona Israeli wamekaa kabila kabila; roho ya Mungu ikamjia.
Waamuzi 6:34X
34 Lakini roho ya Bwana ikaja juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata.
1 Samweli 10:6X
6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine.
Kutoka 31:3X
3 nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
Isaya 63:11X
11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?
Yoeli 2:28X
28 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;
Mathayo 3:11X
11 Kweli mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba; bali yeye ajaye nyuma yangu ana nguvu kuliko mimi, wala sistahili hata kuvichukua viatu vyake; yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Yohana 14:16, 17X
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 20:22X
22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Luka 24:29X
29 Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao.
Matendo 1:9X
9 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
Yohana 7:39X
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Matendo 2:33X
33 Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.
Matendo 1:5, 14X
5 ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache. 14 Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake.
Matendo 2:2-4X
2 Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. 3 Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. 4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.
Mathayo 1:8-21X
8 Asa akamzaa Yehoshafati; Yehoshafati akamzaa Yoramu; Yoramu akamzaa Uzia; 9 Uzia akamzaa Yothamu; Yothamu akamzaa Ahazi; Ahazi akamzaa Hezekia; 10 Hezekia akamzaa Manase; Manase akamzaa Amoni; Amoni akamzaa Yosia; 11 Yosia akamzaa Yekonia na ndugu zake, wakati wa ule uhamisho wa Babeli. 12 Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli; 13 Zerubabeli akamzaa Abihudi; Abihudi akamzaa Eliakimu; Eliakimu akamzaa Azori; 14 Azori akamzaa Sadoki; Sadoki akamzaa Akimu; Akimu akamzaa Eliudi; 15 Eliudi akamzaa Eleazari; Eleazari akamzaa Matani; Matani akamzaa Yakobo; 16 Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo. 17 Basi vizazi vyote tangu Ibrahimu hata Daudi ni vizazi kumi na vinne; na tangu Daudi hata ule uhamisho wa Babeli ni vizazi kumi na vinne; na tangu ule uhamisho wa Babeli hata Kristo ni vizazi kumi na vinne. 18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. 20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Marko 1:9, 10X
9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. 10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;
Luka 4:1X
1 Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,
Mathayo 12:24-32X
24 Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo. 25 Basi Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, hufanyika ukiwa; tena mji au nyumba yo yote ikifitinika juu ya nafsi yake, haitasimama. 26 Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? 27 Na mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, je! Wana wenu huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo hao ndio watakaowahukumu. 28 Lakini mimi nikitoa pepo kwa Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. 29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 31 Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa. 32 Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao.
Waebrania 9:14, 15X
14 basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai? 15 Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Warumi 8:11X
11 Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu.
Yohana 14:18X
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
Matendo 16:7X
7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
Wagalatia 4:6X
6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
Warumi 8:9X
9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
Warumi 8:9X
9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.
1 Petro 1:11X
11 Wakatafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao, ambaye alitangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwako baada ya hayo.
Wafilipi 1:19X
19 Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo;
Yohana 14:16X
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Yohana 15:26X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Matendo 1:4X
4 Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu;
Yohana 16:7X
7 Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.
1 Wakorintho 12:3X
3 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
Yohana 1:9X
9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
Yohana 16:8X
8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
Yohana 16:9X
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
Yohana 5:3X
3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, wakingoja maji yachemke.
Yohana 16:9X
9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
Matendo 5:32X
32 Na sisi tu mashahidi wa mambo haya, pamoja na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wote wamtiio.
Matendo 7:51X
51 Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo.
Waefeso 4:30X
30 Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.
1 Wathesalonike 5:19X
19 Msimzimishe Roho;
Yohana 14:16X
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
1 Yohana 2:1X
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
Waebrania 10:29X
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
1 Wakorintho 15:16X
16 Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka.
2 Wakorintho 9:14X
14 Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu.
Yakobo 4:5, 6X
5 Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? 6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Yohana 14:17X
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 15:26X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Yohana 16:13X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 14:26X
26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Yohana 16:13X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Yohana 15:26X
26 Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Yohana 16:13, 14X
13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
Yohana 14:16, 17X
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Yohana 16:17X
17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Waebrania 13:5X
5 Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.
Mathayo 28:20X
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Wafilipi 1:19X
19 Maana najua ya kuwa haya yatanigeukia kuwa wokovu wangu, kwa sababu ya kuomba kwenu, na kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo;
Yohana 14:23X
23 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.
Matendo 13:1-4X
1 Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa mfalme Herode, na Sauli. 2 Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. 3 Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao. 4 Basi watu hao, wakiisha kupelekwa na Roho Mtakatifu wakatelemkia Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini hata Kipro.
Matendo 13:9, 52X
9 Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, 52 Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
Matendo 16:6, 7X
6 Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. 7 Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,
Matendo 20:28X
28 Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Matendo 15:28X
28 Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima,
Waamuzi 3:10X
10 Roho ya Bwana ikamjilia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kwenenda vitani, naye Bwana akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.
Waamuzi 6:34X
34 Lakini roho ya Bwana ikaja juu yake Gideoni; naye akapiga tarumbeta; na Abiezeri walikutanika na kumfuata.
Waamuzi 11:29X
29 Ndipo roho ya Bwana ikamjilia juu yake Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni.
Hesabu 11:17, 25, 26X
17 Nami nitashuka niseme nawe huko, nami nitatwaa sehemu ya roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao; nao watachukua mzigo wa watu hawa pamoja nawe, ili usiuchukue wewe peke yako. 25 Ndipo Bwana akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena. 26 Lakini watu wawili walisalia kambini, jina la mmoja aliitwa Eldadi, na jina la wa pili aliitwa Medadi; na roho ile ikawashukia; nao walikuwa miongoni mwao walioandikwa, lakini walikuwa hawakutoka kwenda hemani; nao wakatabiri kambini.
2 Samweli 23:2X
2 Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu.
1 Samweli 10:6, 10X
6 na roho ya Bwana itakujilia kwa nguvu, nawe utatabiri pamoja nao, nawe utageuzwa kuwa mtu mwingine. 10 Basi, walipofika Gibea, tazama, kikosi cha manabii wakakutana naye; kisha roho ya Mungu ikamjilia kwa nguvu, naye akatabiri kati yao.
1 Samweli 16:13X
13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.
Kutoka 28:3X
3 Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.
Kutoka 31:3X
3 nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,
Kutoka 35:30-35X
30 Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli, Angalieni, Bwana amemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda; 31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina; 32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba, 33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina. 34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani. 35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
Matendo 2:38X
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
1 Wakorintho 12:7-14X
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana. 8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; 9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; 10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; 11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. 12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja. 14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
Waefeso 4:11, 12X
11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
Matendo 1:8X
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Matendo 19:2, 6X
2 akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 6 Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri.
Yohana 3:5X
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Mathayo 28:19X
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Matendo 2:38X
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Waefeso 5:18X
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
Tito 3:5, 6X
5 si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa kwa pili na kufanywa upya na Roho Mtakatifu; 6 ambaye alitumwagia kwa wingi, kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu;
Yohana 15:5X
5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.