Picha ya Maandiko

Mafundisho Makuu ya Biblia

Mafundisho ya Biblia ni seti ya mada za msingi katika Biblia, zinazotusaidia kuelewa kile Biblia inachofundisha katika ujumla wake. Mada hizi za Biblia husaidia kueleza ukweli wa msingi kuhusu Mungu, mwanadamu, na wokovu kwa namna iliyopangiliwa vizuri. Mafundisho haya yanachukuliwa kuwa ya muhimu sana katika Imani ya Kikristo kwa kuwa yanatoa mfumo wa kuielewa tabia ya Mungu, uhusiano wetu na Yeye, na kuonesha njia ya uzima wa milele. Mafundisho yote ya Biblia yanaweza kuainishwa katika mada au mafundisho au imani 28 za msingi, ambazo zimegawanyika katika mafundisho makuu sita ya Biblia ambayo ni: Mungu, Mwanadamu, Wokovu, Kanisa, Maisha ya Kikristo, na Matukio ya Siku za Mwisho 

Fundisho Kuhusu Mungu

Mafundisho haya yanafundisha kuhusu namna Mungu anavyowasiliana na mwanadamu na kumuonesha asili Yake, sifa Zake, na matendo yake makuu kama Muumbaji na Mkombozi. Fundisho hili hueleza namna Mungu anavyotaka tufahamu jinsi alivyo mkuu na kuitambua mamlaka Yake kama mamlaka ya juu kabisa. Imani za Msingi katika mafundisho haya ni:

  • Maandiko Mtakatifu
  • Utatu Mtakatifu
  • Mungu Baba
  • Mungu Mwana
  • Mungu Roho Mtakatifu

  • Fundisho Kuhusu Mwanadamu

    Fundisho hili hufafanua chimbuko la mwanadamu, likieleza kuanza kwa dhambi duniani na madhara yake. Linaonesha kusudi la ubinadamu na hitaji la ukombozi. Linafafanua namna Biblia inavyoeleza juu ya utambulisho wa binadamu na kuweka msingi wa wajibu wa kimaadili. Imani za Msingi ndani ya Fundisho hili ni pamoja na:

  • Uumbaji
  • Asili ya Mwanadamu

  • Fundisho Kuhusu Wokovu

    Fundisho hili hueleza mchakato wa ukombozi ulivyo likifafanua umuhimu wa kifo na ufufuo wa Yesu Kristo. Hapa ndipo tunapojifunza sehemu ya neema na imani katika kuutafuta uzima wa milele. Fundisho hili hufafanua jinsi Mungu anavyowapatanisha wanadamu na Yeye Mwenyewe. Imani za msingi katika fundisho hili ni:

  • Pambano Kuu
  • Maisha, Kifo na Ufufuo wa Kristo
  • Uzoefu wa Wokovu
  • Kukua Katika Kristo

  • Fundisho Kuhusu Kanisa

    Fundisho hili linafafanua na kueleza namna ya kulitambua Kanisa la Mungu, na utume wa Kanisa. Hapa tunajifunza namna Biblia inavyofafanua suala la la ibada, na kuelekeza namna Mungu anavyoliagiza Kanisa lake kuisambaza Injili. Fundisho hili linawasaidia waumini kuelewa wajibu wao katika mpango wa Mungu wa Wokovu. Imani za msingi katika mafundisho haya ni:

  • Kanisa
  • Masalio na Utume Wake
  • Umoja katika Mwili wa Kristo
  • Ubatizo
  • Meza ya Bwana
  • Karama za Kiroho na Huduma
  • Karama ya Unabii

  • Fundisho Kuhusu Maisha ya Kikristo

    Fundisho hili huwawaongoza watu kuishi huki wakiwa na utii kwa Mungu. Husisitiza utakatifu, upendo, na tabia bora inayompendeza Mungu. Ni fundisho linaloonyesha jinsi ya kutumia kanuni za kibiblia katika maisha ya kila siku. Imani za msingi katika mafundisho haya ni:

  • Sheria ya Mungu
  • Sabato
  • Uwakili
  • Mwenendo wa Kikristo
  • Ndoa na Familia

  • Fundisho Kuhusu Mambo ya Mwisho

    Fundisho hili linahusu mambo ya nyakati za mwisho, kurudi kwa Kristo, na hukumu ya mwisho. Fundisho hili huwahimiza na kueleza namna watu wanavyoweza kubaki wakiwa waaminifu huku wakitarajia uzima wa milele. Imani za msingi zinazozungumzia mambo ya mwisho ni:

  • Huduma ya Kristo katika Patakatifu pa Mbinguni
  • Kuja kwa Yesu Mara ya Pili
  • Mauti (Kifo) na Ufufuo
  • Milenia na Mwisho wa Dhambi
  • Dunia Mpya